
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kufanya kwa vitendo kampeni ya usafi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Sophia Mjema akiwa kaongozana na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mhe. Edward Mpogolo alitembelea kituo cha daladala cha stesheni na kukuta magari mengi ya abiria hayana vikapu vya taka, ambapo wameyatoza takribani magari saba kiasi cha shilingi 50,000 kwa kila moja katika eneo hilo.

Huku kwa upande wa madereva wa bajaji wanaopaki eneo la Soko la Samaki Feri wamepewa onyo na kuombwa kufanya hivyo mara moja kabla hawajachuliwa hatua na mamlaka husika ya Halmashauri hiyo ya Ilala.

Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wafanyabishara wadogo wanaopanga bidhaa zao kandokando ya barabara iliyopo jirani na soko la samaki la Feri kujiandikisha kwa afisa mtendaji na kuondoka eneo hilo mara moja, huku akisema Halmashauri hiyo itawapangia maeneo ya biashara ndani ya soko hilo.