Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga (Wa pili Kulia) akipokea Tisheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group, Sudi Simba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bima mpya ya Afya, inayojulikana kwa jina la Afya Wote, iliyo chini ya Jubilee Insurance, Zurich Group waanzilishi wa Afya Wote Medical Insurance Scheme, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar esSalaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Jubilee Insurance, Rogation Selengia (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Afya Jubilee Insurance, Kenneth Agunda. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Wakionyesha Vipeperushi na fomu zinazoelezea huduma za Bima hiyo, baada ya uzinduzi huo.
Na Ripota wa mafoto Blog, Dar
WITO umetolewa kwa wananchi wa kipato cha chini na kati kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya mpya unaojulikana ‘Afya Wote’, uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga, alisema kuwa uzinduzi wa mfuko huo wenye gharama nafuu ni kimbilio la wanyonge kutokana na kuwajali wananchi wa aina zote.
Aidha alisema kuwa wananchi wataona umuhimu wa mfuko huo pindi wanapopatwa na tatizo la ugonjwa na kwa wakati huo wakawa hawana pesa za kukidhi matibabu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA