• ATOA SIKU 10 KWA YEYOTE ANAYEJIHUSISHA NA BIASHARA YA MOVIE, KUDOWNLOAD KAZI ZA WASANII KUACHA MARA MOJA
• BAADA YA SIKU 10, OPARESHENI KUBWA KUANZISHWA JIJI ZIMA KUWABAINI WOTE WANAOFANYA BIASHARA HIYO.
• AFISA BIASHARA KUFANYA TADHMINI YA MADUKA HALALI YA KAZI ZA WASANII WA FILAMU JIJINI NA KUWABAINI WOTE WANAOUZA KAZI FEKI ZA WASANII WAZAWA WA FILAMU.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepiga marufuku kuanzia leo tarehe 06 Aprili, 2017 uuzwaji, uingizwaji na usambazaji wa CD, flash, DVD na filamu za ngono katika mkoa wa Dar es Salaam.
Hali kadhalika Mhe. Makonda ametoa siku kumi kwa wote wanaojihusisha na biashara isiyo halali ya ku-download filamu na kazi za wasanii jijini waache mara moja kwani baada ya siku hizo, ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa bado wanajihusisha na biashara hiyo isiyonufaisha wasanii na Kuzorotesha pato la Taifa.
Mhe. Makonda pia amemuagiza Afisa Biashara wa Mkoa kufanya tathmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi yanayouza mikanda ya filamu kihalali jiji Dar es Salaam.
Mhe. Makonda ametoa maagizo hayo baada ya kutembelewa ofisini kwake na wawakilishi wa wasanii na wasambazaji, watengenezaji wa Filamu jijini Dar es Salaam, ambao walifikisha kilio chao cha kutonufaika na kazi zao za uzalishaji na usambazaji wa filamu nchini kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridhaa yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato!
Wasanii hao wakiongozwa na Jacob Steven - JB, Vicent Kigosi - Ray walimuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati tatizo lao hilo kwa maslahi ya tasnia nzima ya sanaa nchini.
Mkuu wa Mkoa Mh,Paul Makonda akijadiliana jambo na Kamanda Sirro
Kikao kikendelea
RC Makonda akiwa katika picha na Msanii wa Filamu aitwae Rado.