Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
ZANZIBAR JUMAMOSI JUNI 15, 2013. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghari Zanzibar Mh. Abdallah Mwinyi Khamizi, amepongeza Ushirikiano wa Jeshi la Polisi na Vikosi vya SMZ Zanzibar na kuzitaka Idara nyingine kuiga mfano huo ili kuweza kutatua matatizo yanayowakabili.
Mh, Abdallah ametoa wito huo leo kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar wakati akiwahotubia wananchi na Askari wa Jeshi la Polisi na Vikosi vya SMZ walioshiriki kwenye matembezi ya pamoja ya kijeshi (Route March).
TC 00:54:00 Mh. Abdallah Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema kwa mfano vikundi kama hivyo vinaweza kushirikishwa katika masuala ya usafi wa mazingira, upandaji wa miti na ustawishaji wa bustani za miti ya vivuli na matunda na mambo mengine kama hayo.
Akizungumzia matembezi hayo, Mh. Abdallah amesema tukio hilo ni kielelezo kuonyesha utayari wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kushirikiana na wananchi kwenye mambo mbalimbali yakiwemo ya kimaendeleo.
Awali Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema madhumuni ya matembezi hayo ni kuonyesha umma kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vina ushirikiano na uwezo mkubwa wa kukabiliana na vitendo vyovyote vya kihalifu.
TC 00:46:43 CP Mussa Ali Mussa, Kamishna wa Polisi Zanzibar
Mbali ya Askari, Wakaguzi na Maafisa wa Jeshi la Polisi, Vikosi vya SMZ vilivyoshiki katika matembezi hayo ni Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), Vyuo Vya Mafunzo (Magereza), Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU), Kikosi cha Valantia (KVZ) pamoja na Vikundi 33 vya Mazoezi kotoka mikoa mitatu ya Unguja.
IMETOLEWA NA INSP. MOHAMMED MHINA, AFISA HABARI MKUU WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR.