Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Chama Cha TLP,Mh. Augustine Mrema wakati wa Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Chama Cha kuweka na kukopa (saccos) Cha waalimu wa Moshi vijijini.Shughuli hiyo ilifanyika jana kwenye Uwanja wa Chuo kikuu kishiriki Cha ushirika mjini Moshi.
Mmoja wa Wazee wa Kichaga akimvisha Kofia ya kichifu,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Mangi wa Wachagga.
Mangi wa Wachaga Mh. Edward Lowassa akiwa na Kofia na Fimbo ya umangi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali,kuanza kushoto ni Mbunge wa Mkoa wa Kilimanjaro Viti Maalim wanawake, Betty Machangu,Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,January Makamba,Mbunge wa Moshi vijijini,Dr. Cyril Chami,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa jana amefanya maajabu huko Moshi,baada ya kuchangisha zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni Mia mbili,katika Harambee ya Chama Cha kuweka na kukopa (saccos) Cha waalimu wa Moshi vijijini.
Katika Harambee hiyo ya aina yake iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo kikuu kishiriki Cha ushirika mjini Moshi,zaidi ya shilingi milioni 500 zikiwa fedha tasilimu zilipatikana, huku ahadi zikiwa zaidi za milioni 700.
Akihutubia katika Harambee hiyo iliyohudhuliwa na maelfu ya waalimu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh Lowassa alisema ana ndoto kuwa siku si nyingi, umuhimu wa elimu utaonekana, na waalimu wataboreshewa maisha na maslahi yao, shule zitaboreshwa vifaa, na usumbufu wanaoupata wanafunzi kutokana na kurudi nyumbani utakwisha.
Mbunge wa Moshi Jimbo la Vunjo (TLP),Mh. Augustine Mrema alimsifu Lowassa kwa uwezo wake na uchapakazi na akamshukuru wa kujitolea kwake katika shughuli za kijamii.
Lowassa alitawazwa na wazee wa kichagga kuwa Mangi ambapo walimkabidhi silaha na kofia ya kijadi ikiwa ni ishara ya kukabiliana na maadui katika harakati za kuwatumikia Watanzania.
Ifuatayo ni Hotuba ya Mh. Lowassa wakati wa harambee hiyo
Ifuatayo ni Hotuba ya Mh. Lowassa wakati wa harambee hiyo