Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi ,Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mafanikio katika kukusanya kodi.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 10.87katika kipindi cha miezi tisa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 kuanzia juni 2016 hadi March 2017.
Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo na kutaja kuwa makusanyo hayo ni ukuaji wa asilimia 9.99 ukilinganisha na makusanyo yaliyopita katika mwaka wa fedha uliopita.
“katika mwezi wa machi 2017 TRA imekusanya trilioni 1.34 ukilinganisha na trilioni 1.31 ya mwezi machi mwaka 2016 ambao ni sawa na ukuaji wa asilimia 2.23 ,mamlaka ya mapato Tanzania inawashukuru walipa kodiwote ambao wameitikia wito wa kulipa kodi ya serikali kwa hiari kila wakati na hivyo kuiwezesha mamlaka kutimiza wajibu wake kisheria”Amesema Kayombo.
Amesema kuwa pamoja na mafanikio tuliyopata katika kipindi cha miezi tisa iliyopita mamlaka kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 na cha miezi mitatu kinachoanza April mpaka juni itaelekeza juhudi zake katika kukusanya kodi mbalimbali.