Mmoja wa mafundi akiweka mabomba ya maji sawa hili aweze kumwagilia vizuri eneo la uwanja wa Bandari, Temeke, jijini Dar es salaam ambao umepandwa nyasi za kisasa kwa ajili ya mazoezi pamoja na kuchezea mashindano ya soka, yakiwemo ya Ndondo Cup.
Mabomba ya kisasa yakimwagilia maji katika uwanja huo wa Bandari ambao unatarajiwa kuwa wa kisasa katika eneo lake la kuchezea kwa kufanana na uwanja wa Taifa.
Bomba jingine lililopo upande wa mashariki ya uwanja likimwagilia maji.
Jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja huo liliwekwa na balozi wa China Dkt. Lu Younqing
Sehemu ya upande wa goli ambayo imewekwa sawa na kupandwa nyasi za kisasa. Picha na HunphreyShayo wa Globu ya Jamii