Na Fadhili Atick Globu ya Jamii Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi mtaa wa Shewa kata ya Mwakibete mkoani Mbeya,na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali zinazo wakabili.
Makala ambaye ametembelea Shule ya Msingi Shewa na kushuhudia msongamano wa wanafunzi, amepongeza wananchi kwa kushiriki ujenzi wa madarasa kupunguza msongamano wa wanafunzi, ambapo halmashauri ya jiji la Mbeya walichangia shilingi milioni 6.3 kuunga Mkono jitihada za wananchi.
Makala ameahidi kufuatilia kwa Karibu ujenzi wa madarasa mpaka yakamilike, kwani wananchi wamekuwa wakichukizwa na baadhi ya watu wachache wanaopita kushawishi wananchi wasichangie
Makala amewaonya wote wanaoshawishi wananchi kutochangia Maendeleo kuacha tabia hiyo mara moja katika na kuamua kuonyesha mfano wa kuchangia milioni moja katika ujenzi wa choo cha Shule msingi shewa
Pia ameagiza Tanesco na Mamlaka ya Maji kushughulikia haraka matatizo ya Umeme na Maji katika mkoa wa Mbeya hili kupunguza kero kwa Wananchi.
Rc Makalla akizungumza na wananchi wa kata ya mwakibete jijini mbeya
Akishangazwa na wingi wa wanafunzi katika shule ya msingi mwakibete ambapo idadi ilionesha wanafunzi ni wengi kuliko madarasa.
Moja kati ya Wakazi wa shewa kata ya mwakibete wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya.
Mmoja wa Wananchi akitoa duku duku lake kwa RC Makala.
Baadhi ya wakazi wa Mwakibete wakifuatilia mkutano huo.