Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117062

KIKAO CHA KAMATI MAALUM CCM LEO.

$
0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, leo (jana) amekiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa..

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM wa Idara ya Itikadi na Uenezi Bi. Waride Bakari Jabu, amesema kikao hicho cha siku moja kilifanyika Afisi Kuu ya CCM, Mjini Unguja.

Ameeleza kwamba pamoja na mambo mengine, kikao kilipokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya Chama hicho, ili waweze kuwania nafasi ya Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, kwa kipindi cha mwaka 2017 - 2022.

“ Kutokana na Chama chetu kuwa Kinara wa Demokrasia wanachama wengi wamejitokeza kuwania nafasi hizo ili waweze kuiwakilisha vyema CCM na serikali inazoziongoza katika Bunge hilo muhimu.

Pia Wana CCM na wananchi kwa ujumla tukumbuke kuwa fursa hizi zisingeweza kujitokeza kama nchi yetu ingekuwa katika mashaka na migogoro, hivyo wito wangu tuendelee kuwa wamoja ili wenzetu waweze kutuwakilisha vyema.”, alisema Bi. Waride.

Kikao hicho kimefanyika kwa kuzingatia Ibara ya 114 (7) (b) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, Toleo la 2012, ambayo inatoa Mamlaka kwa Kamati Maalum ya H/Kuu yaTaifa ya CCM Zanzibar, kupokea na kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu, kwa hatua zinazofuatia.

Bi. Waride amesema jumla ya wana CCM 33, wakiwemo wanawake 7 na wanaume 26, kutoka Mikoa mbali mbali ya Unguja na Pemba, wamejitokeza kuomba waruhusiwe na CCM kugombea nafasi hizo.

Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inapaswa kuwakilishwa na Wabunge tisa (9).

Aidha kikao hicho kilimtambulisha Ndugu. Abdullah Juma Saadalla (Mabodi) aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM hapo Machi 13, mwaka huu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. Aidha, kimeahidi kumpa kila aina ya mashirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake aliyopewa na Chama ipasavyo.

Hata hivyo Kikao pia kimewapongeza kwa dhati wana CCM hasa Vijana waliojitokeza kuomba kugombea nafasi hizo muhimu za Uongozi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hali inayoonyesha kuimarika kwa Demokrasia ndani ya Chama hicho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117062

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>