Benki ya KCB Tanzania imeendelea kuwekeza kwa wajasiriamali wadogo na wakati kupitia kitengo chake cha “Biashara Club”, kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati yaani (SME) kwa kuwapa huduma za kibenki na huduma endelevu za kimaendeleo kwa wateja wake.
Zaidi ya wanachama 100 wa Biashara Club wamekutana kujifunza jinsi ya kutunza fedha, jinsi ya kufanya kwa vitendo uwekaji wa kumbu kumbu za hesabu , jinsi gani taarifa ya fedha za biashara yako na taarifa za kifedha za mtu binafsi zinavyokusanywa na kukaguliwa, na kwa njia gani taarifa hizi zinapatikana kwenye taasisi za mikopo kupitia taasisi za kifedha.
Kwa kuongezea, maelezo mafupi yalitolewa na Taasisi ya biashara, Viwanda na kilimo Tanzania kuhusu utolewaji na uthibitishwaji wa vyeti halali kwa bidhaa zinazo zalishwa hapa Tanzania, wao wamebobea katika kufanya tafiti mbalimbali nchi nzima kwa kutumia mtandao wao na kuanzisha mfumo maalumu kwa wajasiriamali wadogo na wakati,
kuzisaidia taasisi za wajasiriamali wadogo na wakati, na kuwakutanisha wadau wa misitu kwa pamoja na kufanya ushirika wa biashara kwa wadau na kuwaunganisha wanachama na fursa zilizopo kwa washirika wa kibiashara wa kimataifa. Akiongea kwenye warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KBC, Godfrey Ndalahwa akizungumza machache wakati wa warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam leo. ![]()
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB, Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati (SME) ,Edgar Masatu akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Warsha hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo ya KCB mapema leo jijini Dar.
![]()
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo mapema leo asubuhi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB, Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA