Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117162

Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Amvisha Cheo Kanali wa JWTZ

$
0
0
Katika hali ambayo haijazoeleka na iliyoonekana kuwa ngeni, Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo alimvisha Cheo Kanali Joseph Bakari aliyepandishwa Cheo hivi karibuni kutoka Luteni kanali.
Hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na  ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania  Mhe. Geofrey Meena, Maafisa wa Ubalozi na wageni wengine ilifanyika karibuni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Berlin nchini Ujerumani.
Akitoa maelezo mafupi kuhusu tukio hilo  Mhe. Balozi Marmo alitanabaisha kuwa kwake ni tukio la kwanza na la aina yake kupewa dhamana hiyo  na kwamba amepokea maelekezo husika kutoka Makao Makuu ya Jeshi kupitia Wizarani. 
Akisoma sehemu ya maelekezo hayo alisema: “ kwa kawaida Afisa anapopanda cheo akiwa nje ya nchi, na  iwapo hataweza kwenda Tanzania kuvalishwa cheo hicho na viongozi husika wa JWTZ, cheo hicho kipya huvishwa na Afisa Mkuu au Balozi wa Tanzania katika Nchi aliyopo”. 
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo na  Acting Colonel Joseph Bakari wakisikiliza maelezo kabla ya hatua ya kumvua cheo cha zamani na kumvika kipya.  Kanali Joseph Bakari ni mwakilishi wa JWTZ katika Sekretarieti ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (International Military Sports Council-CISM) kama Mshauri na msaidizi wa Mkurugenzi wa Michezo katika Baraza hilo katika makao makuu yake Brussels, Ubelgiji.
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akimvisha cheo kipya Colonel Joseph Bakari 
Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akimvisha kofia ya cheo kipya Colonel Joseph Bakari 
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akipikea zawadi maalumu ya  Sekretarieti ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (International Military Sports Council-CISM)  toka kwa Kanali Joseph Bakari wakati wa hafla hiyo

 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kushoto)  Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri (wa pili kulia) Colonel Joseph Bakari na mkewe 
 Tukio hilo la kuvisha Cheo  lilihitimishwa na kuimbwa wimbo wa Taifa wa Tanzania.
 Picha ya pamoja na ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania  Mhe. Geofrey Meena, Maafisa wa Ubalozi na wageni wengine katika hafla fup iliyofanyika karibuni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Berlin nchini Ujerumani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117162

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>