Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na wanachi wa Kata ya Boko NHC wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika Kata hiyo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika Kata hiyo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Boko NHC ,Dk. Alexander Kyaruzi akizungumza wakati wa kukabidhiwa mradi wa maji ya Dawasco Boko leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Dawasco Boko NHC, leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akisaini makubaliano na mwenyekiti wa kamati ya Maji Boko NHC, Dk. Alexander Kyaruzi leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji wa Dawasco Boko NHC, leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.