Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyesimama) akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakati Kamati hiyo ilipotembelea Azam Media jana Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Azam Media Bw.Tido Muhando.
Mkurugenzi wa Azam Media Bw. Tido Muhando (aliyesimama) akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) utendaji kazi wa Chombo hicho wakati Kamati hiyo ilipotembelea Azam Media jana Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Faustine Ndugulile akizungumza jambo kwa Kamati hiyo na uongozi wa Azam Media wakati Kamati ilipotembelea chombo hicho jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Mkurugenzi wa Azam Media Bw. Tido Muhando(hayupo pichani ) wakati Kamati ilipotembelea chombo hicho jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wa kwanza kushoto akizungumza na wasikilizaji wa Uhai Radio wakati Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ilipotembelea studio hizo jana Jijini Dar es Salaam.