Waziri wa Mambo ya Katiba Na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe ameagiza kuwa kuanzia tarehe 1 Mei, 2017 ndoa zote zifungwe baada ya wanaotaka kufunga kuwasilisha kwa vyeti vya kuzaliwa kwanza.
Hivyo, amewataka wananchi wote wanaotarajia kufunga ndoa waanze kutafuta vyeti vya kuzaliwa mapema kwa sababu hawataweza kufunga ndoa kuanzia tarehe 1 Mei, 2017.
Agizo hilo amelitoa kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo tarehe 16/3/2017 akiwa ziarani mkoani Morogoro kukagua utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.