Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo imevitembelea vituo vya utangazaji vya CLOUDS MEDIA GROUP, ikiwa katika ziara ya kawaida ya kuvitembelea vituo vya utangazaji nchini katika kutoa elimu ya uboreshaji wa maudhui ya utangazaji nchini.
Pichani kushoto ni Ruge Matahaba, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Maudhui ambao ni Mwenyekiti Valerie Msoka, Joseph Mapunda, Abdul Ngalawa. Derek Murusuri Zainabu Mwatawala.