Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117164

Mashindano Ya Taifa Ya Kuogelea Kufanyika Aprili 7 na 8 Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Mashindano ya kutafuta bingwa wa Taifa wa mchezo wa kuogelea yamepangwa kufanyika Aprili 7 na 8 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Heaven of Peace Academy (Hopac) iliyopo Kunduchi Mtongani.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya timu 19 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na visiwani.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alizitaja timu ambazo zinatarajia kushiriki kuwa ni Dar es Salaam Swimming Club, Taliss swimming club, Bluefins, JKT, Morogoro International School, Champions Rise, Braeburn International School na shule ya sekondari ya Makongo.

Timu nyingine ni ISM Leopards, Arusha Swim Club, Mwanza Swim Club, Kennedy School Arusha, Stingrays Swim Club, Tanzania Marines, Hopac Swim Club, Genesis Swim Club, KMKM, Wahoo –IZS na Zanzibar Dolphins.
Waogeleaji hao watashinda katika stali nne ambazo ni freestyle, backstroke, Individual Medley na breaststroke. Pia kutakuwa na mashindano ya ‘relay’ ambayo yatashirikisha waogeleaji wa kike na wa kiume.

“Tunatarajia kuwa na mashindano myenye ushindani mkubwa kutokana na maandalizi ya kila timu, mchezo unakuwa na timu zinazidi kuongezeka, kwa kifupi kuna mwamko mkubwa sana katika mchezo, tunawaomba wadhamini wajitokeze kutusaidia,” alisema Namkoveka.

Alisema kuwa kwa sasa wapo katika maandalizi ya kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha kimataifa na kwa kutumia sheria za shirikisho la mchezo huo duniani, Fina.

“Mashindano yatakuwa ya umri, kutakuwa na umri kati ya miaka 9 -10, 11-12, 13-14, 15-16 ba zaidi ya 17, hakuna muogeleaji atakayeruhusiwa kushiriki katika shindano zaidi ya moja, viongozi wote wa timu watanakiwa kufika kwenye mkutano utakaofanyika Hopac kabla ya mashindano kuanza, mkutano huo utaendeshwa na kamati ya ufundi,” alisema.
Wogeleaji wakishindana katika mashindano yaliyopita ya kuogelea.
Peter Itatiro ‘akikata’ maji katika mashindano yaliyopita ya kuogelea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117164

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>