NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAKINAMAMA wa kata ya Pangani wanaoishi katika mitaa minne ya Lumumba,Kidimu, Liwale pamoja ma mkombozi katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani wanakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama hivyo kuwalazimu wakati mwingine kuamka usiku wa manane kwa ajili ya kwenda kuchota maji visimani kitu ambacho kinahatarisha usalama wa maisha yao kutokana na mazingira yenyewe kuwepo katika mapori.
Kilio hicho cha wakinamama hao wamekitoa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kufanya ziara yake ya kikazi katika mitaa mbali mbali iliyopo katika kata ya Pangani kwa lengo ya kuweza kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuweza kuzungumza na wananchi ili kubaini changamoto ambazo zinawakabili.
Wakinamama hao akiwemo Maria Benjamini ,Zawadi Ibrahimu,pamoja na Asimu Mendani walisema kuwa wanashindwa kufanya shuguli nyingine za kuleta maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi wa kutafuta maji hivyo wameiomba serikali kupitia mamlaka zinazohusika kuliingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma ya maji.
Kilio cha wakinamama hao kinamgusa na kumwinua Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka na kuamua kumwagiza mbele ya mkutano wa adhara Injinia wa maji katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji kuhakikisha wananchi wa mitaa minne ya Kidimu, Lumumba,miwale pamoja na mkombozi iliyopo kata ya Pnagani wanapata maji ya bomba haraka ili waweze waondokana na adha waliyokuwa wanakabiliana nayo kwa muda mrefu.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata ya Pangani baada ya kufanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.

Baadhi ya wananchi wa kata ya pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji wakimsikiliza Mbunge wakati akiwahutubia katika mkutano wa adhara uliofanyika katika viwanja vya mtaa wa kidimu.

Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi akifafanua jambo kwa wananchi katika mkutano huo uliondaliwa na mbunge ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA