Na Rhoda Ezekieli Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amepiga marufuku vitendo vya baadhi ya wanaume Mkoani humo kuwadhurumu na kuwatishia kuwafukuza wake zao pindi wanapothubutu kutetea haki zao,badala yake amewataka washirikiane nao kutambua na kuchangamkia fursa za maendeleo zilizopo nchini.
Mkuu huyo wa Mkoa aliitoa kauli hiyo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoani humo ambayo kimkoa yalifanyika katika kijiji cha kinyinya kata ya nyamutukuza wilayani kakonko Mkoani humo .
RC Maganga alisema kuwa pamoja na mambo mengine, wakati umefika kwa wanawake kuamka na kusimamia haki zao ikiwa ni pamoja na kutokukubali kubaki nyuma kwa kuchangamkia fursa hizo zinapozitokeza.
Alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi,Wake wanapo kuwa wakijishughulisha kutafuta fedha ili kuzitunza familia zao, wanawanyang'anya na kwenda kuzitumia kwenye starehe zao, suala ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Wanawake wengi.
Alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi,Wake wanapo kuwa wakijishughulisha kutafuta fedha ili kuzitunza familia zao, wanawanyang'anya na kwenda kuzitumia kwenye starehe zao, suala ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Wanawake wengi.
Katika kuhakikisha suala la kuwa Nchi ya viwanda, ni lazima wanawake kushirikiana na wanaume katika kufanya kazi ili kuongeza kipato katika familia na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa zawadi kwa mmoja wa akina mama aliyejifungua katika kituo cha afya cha Nyanzige,Wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

RC Maganga akiwasikiliza akina mama mbalimbali waliofika katika kituo cha afya cha Nyanzige,Wilayani Kakonko mkoani Kigoma kujipatia matibabu mbalimbali,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala

Akina Mama wakisherehekea siku ya Wanawake hapo jana

RC Maganga akiwa ameongozana na DC wa Kakonko,Kanali Hosea Ndagala wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wajasiliamali,kufuatia bidhaa zao walizozitengeneza.