Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117365

WANAWAKE WANAOFANYA KAZI MGODI WA BULYANHULU WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA BAISKELI KWA WANAFUNZI WA KIKE NA SHUKA VITUO VYA AFYA

$
0
0

Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8,2017 kwa kutoa zawadi ya baiskeli kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na kuwatembelea na kuwapatia zawadi wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya.

Wanawake hao wametoa zawadi ya baiskeli 10 zikiwemo 8 kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao katika shule ya Sekondari Bulyanhulu na Bugarama na baiskeli mbili kwa ajili ya walimu wa kike walezi wa wanafunzi hao.

Mbali na kutoa zawadi kwa wanafunzi,pia wametembelea kituo cha afya cha Bugarama na Lunguya vilivyopo jirani na mgodi huo kisha kutoa zawadi ya shuka 70 kila kituo na kuwapa wauguzi na wagonjwa sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake,Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo alisema wameamua kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kuwapongeza wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni ili kuwapa ari ya kujifunza zaidi na kuwarahisishia usafiri kufika shuleni.

“Tuwatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu na Bugarama,tumetoa msaada wa baiskeli 10 hivyo kila shule imepata tano ambapo nne kwa ajili ya wanafunzi kike na moja ni kwa ajili ya walimu wa kike kwa kila shule”,alieleza Senkondo.

“Pia tumetoa shuka 140 kwa ajili ya vituo vya afya viwili,Bugarama na Lunguya kisha kugawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa waliopo katika vituo hivyo”,aliongeza Senkondo.

Senkondo alisema wameamua kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kukutana na watoto wa kike na wanawake ili kuwahamisha wanawake katika jamii kushiriki katika shughuli za migodi kwani wanaweza.

Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo wakati wa maadhimisho hayo,ametuletea picha za matukio yaliyojiri mwanzo hadi mwisho…Tazama hapa chini .

Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa wamebeba mtoto aliyezaliwa na Salome Raphael baada ya kumpatia zawadi ya vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno 


Hapa ni katika Kituo cha afya Bugarama kilichopo katikakata ya Bugarama halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.Kituo hiki cha afya kimepewa shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa.Kulia ni Muuguzi katika kituo hicho Mwalushani Mabula akizungumza wakati wa kupokea shuka 70,sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa waliokutwa katika kituo hicho siku ya siku ya wanawake duniani Machi 8,2017

Mwalimu Bumi Mwasalujonja akiwa amebeba juu baiskeli wakati akikabidhiwa na wanawake kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu wakiwa katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri kupata zawadi kutoka kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia dhahabu wa Bulyanhulu uliopo jirani na shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 920 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117365

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>