Na Rhoda Ezekiel Kigoma
KATIKA kuelekea siku ya Wanawake Duniani, Baafha ya Wanawake Mkoani Kigoma Wamewaomba Wanaume Mkoani humo kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanawake kwa kuwaachia majukumu ya kuzihudumia familia zao, hali inayosababisha Watoto wengi kukosa elimu na wanawake kushindwa kufikia Malengo yao ya kujikomboa na umasikini.
Akizungumza na Globu ya Jamii ofisini kwake jana, katibu wa umoja wa Wanawake Mkoani Kigoma , Salome Luhinguranya alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi kukimbia familia zao na kuwaachia mzigo wa malezi na kusomesha watoto wanawake wao hali inayo wapelekea wanawake wengi kishindwa kufanikiwa katika biashara zao kuyokana na Mzigo mkubwa unao Walemea.
Luhinguranya alisema Watoto wengi wamekuwa wakikosa elimu Mkoani humo kutokana na matatizo ya Wanajme wengi kuwatelekeza wake zao na familia zao na kwenda kuoa wake wengine hali inayo wapelekea Wanawake kushindwa kuhudumia familia zao kutokana na ufinyo wa mitaji waliyo nayo.
"Kauli mbiu ya Mwaka huu katika maadhimisho ni Tanzania ya Viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko Kiuchumi,kuelekea. Mkoa wa kigoma wanawake wengi wanajishughulisha katika Shughuli mbali mbali na Wengine ni wafanya kazi ,
UWT Mkoa imewahamasisha kuingia kwenye ujasiliamali huo na wanaume wengi wamekuwa Wakiwarudisha Nyuma kutokana na mizigo wanayo waachia , niwaombe wanaume kuepukana na fikra mgando ya kuwanyanyasa wanawake pindi wanapo jishughulisha kwa kuwaachia kulea familia ,
Baba ni kichwa katika familia wanatakiwa kutafuta fedha na kuwasaidia wanawake kulea familia zao ilikuwasaidia watoto kupata elimu na malezi bora", alisema Katibu wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa kigoma.


Baadhi ya akina mama wakijishughulisha na biashara zao mbalimbali za ujasiliamali mkoano Kigoma.