Na Fredy Mgunda,Iringa.
MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji kata hiyo.
Akishudia mchezo wa nusu fainal kati ya timu yaWaandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu tawalawilaya ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Chitinka
Aidha Chitinka aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.

Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.