Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117395

CDEA yawapiga msasa wabunifu wa mavazi na urembo wa Afrika Mashariki kwa ufadhili wa IIDEA 2017

$
0
0
Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ tawi la Afrika Mashariki. 

Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka. 

Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata ufadhili. Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika. 
 
Washiriki ambao ni wabunifu kutoka Afrika Mashariki akiwemo Andrew Kalema, Joyce Gerald (katikati) na Makeke Jocktan wakifuatilia mafunzo hayo.

Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding). Mafunzo hayo ya siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo. 

Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo. Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda. 
 
Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa akitoa takwimu za fashionomics kwa washiriki wa mafunzo hayo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>