Wataalam wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 05 Machi, 2017 wako katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme pamoja na kukutana na wadau wa nishati jadidifu.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric Company, Alex Andoya (katikati) akielezea maendeleo ya kampuni hiyo katika uzalishaji wa umeme mara baada ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kufanya ziara katika kampuni hiyo, Mbinga mkoani Ruvuma ili kujionea maendeleo ya shughuli zake. Wataalam hao wako katika ziara ya kukagua miradi ya umeme pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam.
Mtaalam kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric Company, Mhandisi Jasper Bubelwa (kulia) akielezea mfumo wa uendeshaji mitambo wa kampuni hiyo
Wataalam wa Nishati Jadidifu, Emillian Nyanda, (wa pili kutoka kulia) na Mhandisi Stephan Kashushura ( wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric Company mara baada ya kumaliza ziara katika kampuni hiyo. Kushoto kabisa ni Fred Tawete kutoka Wizara ya Nishati na Madini