MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wameshindwa kuipiku Simba kileleni baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani kwenye mchezo wa ligi kuu iliyofanyika Machi 5, mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.
Yanga watajilaumu wenyewe kutoka na kushindwa kuzitumia nafasi tatu za wazi za kufunga mabao ikiwemo ya penati iliyotolewa katika dakika ya 33 baada ya beki wa timu ya Mtibwa Sugar Ally Lundega kuunawa mpira eneo la hatari.
Mwamuzi wa mchezo huo Hamedi Kikumbo kutoka Dodoma ,aliamuru ipingwe penati kuelekea langoni mwa timu hiyo na mchezaji Saimon Msuva wa Yanga alipewa jukumu la kupinga penati hiyo. Lakini badala ya kupinga mpira huo kulenga lango la Mtibwa Sugar alijikuta akipaisha juu ya lango la wapinzani wao na kuikosesha timu yake bao hali iliyoamsha shangwe za mashambiki wa Mtibwa Sugar waliopewa ushirikiano na wenzao wa Simba kushangilia kwa nguvu kutokana na kukosa bao hilo.
Katika mchez huo Yanga ilikuwa na nafasi nzuri ya kuweza kuipuku Simba kwa idadi ya mabao endapo mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar ingepata ushindi ili kufikisha pointi 55 sawa na mtani wake wa jadi Simba isipokuwa wangepishana kwa mabao ya kufunga .
Mchezo huo ulikuwa ni wa vuta nikuvute ambapo Yanga iliweza kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza na dakika 15 za kipindi mwisho kwa kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar, lakini ukuta wa Mtibwa Sugar ulikaa imara na kuondoa hatari zote langoni mwao hadi mwisho wa mchezo.
Kikosi cha wachezaji wa timu ya Yanga kabla ya mchezo wao na Mtibwa Suga katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro leo Machi 5, 2017
Kikosi cha wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar , kabla ya mchezo wao na Yanga katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro leo.
![]() |
Jukwaa la mashabiki wa timu ya Yanga wakifuatilia mpira uwanja wa Jamhuri wa Morogoro leo |
![]() |
Mshambuliaji Saimon Msuva wa Yanga akipiga na kukosa penati katika mchezo huo |
Mchezaji wa Yanga Justine Zulu akisongwa na beki wa timu ya Mtibwa Sugar Ally Shomari katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika Machi 5, mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri wa Morogoro, timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana.
Mchezaji wa Yanga , Saimon Msuva akijaribu kuwatoka mabeki wawili wa timu ya Mtibwa Sugar , Ally Makarani ( kushoto) pamoja na Ally Shomari ( kulia) wakati wa mchezo wa ligi kuu uliofanyika Machi 5, mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri wa Morogoro, timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana.
Habari na Picha na John Nditi,
Globu ya Jamii, Morogoro