Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda, akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sacoma group, Bwana. Sam Ochieng, namna ambavyo bidhaa za Matunda na Mboga mboga kutoka nchini Kenya zinavyopakiwa, kusafirishwa na hatimaye kuuzwa kwenye soko la Spitfield nchini Uingereza, kwa kupitia Jumuiya ya Sacoma. Umoja huo wa Sacoma wenye lengo la kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wa africa ya Mashariki. Mheshimiwa Waziri Mkuu, alifanya ziara kwenye Soko la Spitafields, lililopo Stratford nchini Uingereza, kwa lengo la kujionea shughuli za Jumuiya ya Sacoma inavyoendesha shughuli zake kwenye soko hilo na jinsi ambavyo Jumuiya hiyo imeweza kuwasaidia Wakulima wa Matunda na Mboga kutoka nchini Kenya, kupata soko la kuuza Bidhaa zao hapa nchini Uingereza.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, akiangalia na kupata maelezo ya Ubora wa bidhaa unaotakiwa kupata soko nchini Uingereza. Pichani, mstari wa pili, (kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Ungereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, kwanza (kulia) ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, Uingereza Bwana Yusuf Kashangwa, maofisa wa Ubalozi na Viongozi kutoka Tanzania ambao wameambatana na Waziri Mkuu nchini Uingereza kwenye Mkutano unaofanyika leo ambao unahusu jinsi ya kutokomeza njaa na umuhimu wa Lishe bora kwa Mama na Watoto Duniani (Hunger and Nutrition). Mkutano huo ambao umeandaliwa na Asasi za kiserikali na zisizo za Kiserikali, unakutanisha nchi kubwa Duniani, zijulikanazo kama G8, Wadhamini, Wachangiaji na Watoa misaada kwenye Asasi hizo, zenye lengo la kutokomeza njaa duniani na kusaidia kuwapatia Wamama na Watoto Lishe bora.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Soko la Spitalfields. Kushoto ni Meneja wa Masoko wa Kikundi cha Sacoma, Mama Perez Ochieng - Meneja wa Masoko wa Jumuiya ya Sacoma.