Naibu waziri Tamisemi,Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa vyama vya msingi na Ushika kikao ambacho kilitoa azimio la kujitoa Ilulu Union na kuunzisha mchakato wa kuunda chama cha RUNALI UNION.
Baadhi wa wana Ushikia toka Amcos za wilaya za Nachingwea,Liwale na Ruangwa wakiwa katika kikao cha pamoja kuazimia kujitoa katika Ushirka wa ILULU.
Wajumbe 9 waliochaguliwa katika kikao hicho kuanzisha RUNALI Union na kuwezesha chama hicho kusajiliwa ili kianze kazi Msimu ujao wa mauzo ya korosho.
Na Abdulaziz Video-Nachingwea
Vyama 46 kati ya 51 vya msingi na ushirika vya wilaya za Nachingwea,Ruangwa na Liwale,mkoani Lindi vimeazimia kujiondoa kwenye chama kikuu cha ushirika cha mkoa wa Lindi cha Ilulu na kuanzisha mchakato wa kuunda chama kipya cha ushirika cha wilaya hizo kitakachojulikana kwa jina la RUNALI Union.
Uamuzi huo ambao uliozamiwa jana kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu Nachingwea chini ya uenyekiti wa Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa,Kasimu Majaliwa ambapo viongozi vya vyama vya msingi vya wilaya hizo waliridhia kwa kauli moja kuachana na chama hicho cha ushirika cha Ilulu kwa kilichodaiwa kuwa kimeshindwa kuwasaidia wakulima hata kusababisha wakulima wa korosho washindwe kulipwa malipo yao yote ya pili kiasi cha kusababisha uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali za viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na wa Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza kwenye kikao hicho,Naibu waziri Tamisemi Kassim Majaliwa alikitupia lawama chama kikuu cha Ilulu katika uendeshaji wake kiasi cha kusababisha wananchi kuichukia serikali yao kwani viongozi wake si waadilifu kwani wamekuwa wakijikusanyia kiasi kikubwa kupitia ushuru mbalimbali zisizo za lazima ambapo alibainisha kuwa licha ya wakulima kutopata malipo stahili chama cha Ilulu kimejipatia zaidi ya shilingi Bilioni 9.9 huku wakulima wenye wakiangaika kupata malipo ya pili Aidha kufuatia azimio hilo aliwaasa wanaushirika na Maafisa Ushirika wa wilaya hizo kutorubuniwa kipindi cha mchakato wa Kuanzisha mchakato wa Ushirika wa wilaya hizo zilizokusudia kujiondoa huku akiwataka kuomba notisi ya kuitishwa kwa mkutano mkuu wa Ilulu ili vyama hivyo vijiondoe kwa mujibu wa Sheria za Ushirika.
Makamu mwenyekiti chama cha msingi cha Umoja cha wilaya ya Liwale,haguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa mchakato wa Kuanzisha RUNALI alitaja baadhi ya mambo yaliyotajwa kuwa ni chanzo cha kujiondoa kwa vyama hivyo vya wilaya tatu ni ukubwa wa eneo linalohudumiwa na Ilulu jambo linalofanya chama hicho kishindwa kutoa huduma mzuri kwa wanachama wake ucheleweshaji wa vitendea kazi yakiwemo magunia na vitabu kwani Ilulu ndio waliojipa uzabuni pekee wa kusambaza huduma hizo huku akieleza kuwa malengo ya Ushirika unaokusudiwa kuanzishwa yatasaidia kupunguza baadhi ya Gharama zisizo lazima zinazokatwa Amcos mbalimbali wakati wa mauzo ya Mazao.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Bi Agness Hokororo alitoa wito kwa Wanasiasa kuwafikia wakulima na kuwaeleza sababu za kuwepo kwa maendeleo ya wakulima ili kuepukana na ujanja uliokuwa unafanywa na Ilulu kutokana na Makato na upandishaji wa gharama mbalimbali za uendeshaji.
kikao hicho pia kilihudhuriwa na wabunge wa majimbo ya Liwale na Ruangwa na wakuu wa wilaya hizo tatu ambao kwa nyakati tofauti waliitaka kamati ya mpito iliyoundwa wajumbe 9 Chini ya Uratibu wa Maafisa Ushirika wa wilaya hizo kuanzisha mchakato wa usajiri wa RUNALI na kuharakisha zoezi hilo linakamilika haraka iwezekanavyo ili chama hicho kipya kianze kazi ya ununuzi wa zao la korosho nje ya Chama kikuu cha Mkoa ( ILULU) Msimu Ujao.