Globu ya Jamii inatoa taarifa kwa Wenye ndugu waliosafiri kwenye Basi la Abood na Happy Nation kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es salaam,yamepata ajali mlima Kitonga hivi punde,ambapo taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wameeleza kuwa katika ajali hiyo wamejeruhiwa abiria 12.
Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo alieleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi la Abood kukosa breki na kuligonga roli la FM ambalo halikuanguka ila liligonga Fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigongana na basi la Happy Nation na mabasi yote kutumbukia korongoni .

Taarifa rasmi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kamanda Kenedy Komba akiwa eneo la tukio ametihibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kuwa taarifa za awali majeruhi ni 12 na kati ya hao majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi, hakuna vifo vilivyotokea katika ajali hiyo.

Moja ya Lori lililogongwa na kumbukia korongoni