Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117404

MAKAMBA ATOA TAARIFA YA OPERESHENI MAALUM YA UTEKELEZAJI WA KUSITISHA, UZALISHAJI, USAMBAZAJI, UUZAJI NA MATUMIZI YA POMBE KALI KATIKA VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI (VIROBA)

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba). Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi

Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alipozungumza nao na kutoa matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba).
……………………………………………………………………………
Kama mnavyofahamu unywaji wa pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki zimechangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira, kupotea kwa nguvu kazi ya taifa, ajali na vifo zivyosababishwa na unywaji uliokithiri wa pombe hizi, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na kupotea kwa mapato yanayosababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu. 

Madhara haya ndiyo yaliyopelekea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kutoa tamko tarehe 16 Februari, 2017 akiwa Mererani, Mkoani  Manyara kuhusu kusitisha uzalishaji, usambazaji,  uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) kuanzia tarehe 1 Machi 2017; Baadaye tarehe 20/2/2017 na tarehe 28/2/2017 nilitoa maelezo na ufafanuzi kuhusu ufuatiliaji wa agizo hilo.
Ili kutekeleza kwa ufanisi agizo hili serikali imeunda Kikosi Kazi cha Kitaifa kwa ajili ya kuratibu Operesheni Maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya serikali na kuchukua hatua stahiki.
Kikosi Kazi hicho kiko chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, na kinajumuisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Fedha na Mipango,  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi.
Operesheni maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inaendelea kutekelezwa nchini kote  kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na  Wilaya pamoja na Kamati za Mazingira za Mikoa na Wilaya.  Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Makamu wa Rais. 

Majumuisho ya taarifa ya nchi nzima yatafanywa baada ya Kikosi Kazi kuendesha Operesheni maalum katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii inatokana na kuwepo kwa Viwanda vingi na wasambazaji wengi wa Pombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets).
Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu operesheni maalum  katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii ilitokana na kuwepo  kwa viwanda vingi vinavyozalisha pombe kali za aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets)  ambazo hazikidhi vigezo mbalimbali vya Sheria.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117404

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>