Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Msanii wa muziki wa bongo fleva anayefanya vizuri katika soko la muziki na wimbo wake wa Dume Suruali Dume kaptula Khamis Mwijuma ‘Mwana FA’ amesema ilimchukua muda sana kupata jina la wimbo huo.
Mwana FA amesema hayo alipokuwa akizungumza na globu ya jamii juu ya namna alivyoweza kurekodi wimbo huo katika mazingira magumu ya kurudia rudia.
“hii nyimbo niliifanya mara ya kwanza lakini nikaiona haipo sawa ndipo nikaamua kumshirikisha mwanadada Vanessa Mdee kutokana na staili yake ya uimbaji” amesema FA.
Amesema ni mara nyingi sana amekuwa akirudi studio kwa ajili ya kurekebisha mstari mmoja wa shairi kuhakikisha kuwa anapata wimbo wenye ubora.
FA amemaliza kwa kusema kuwa ni vyema msanii ukatambua mashabiki wako nini wanataka kuliko kwenda kwenda studio kila siku kuleta mziki wa bigijii