Na Rhoda Ezekiel -Globu ya Jamii,Kigoma,
VIONGOZI wa Mikoa na Wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuibua fursa za uwekezaji na kuibua miradi itakayo wawezesha Wananchi kunufaika na ukuaji Wa uchumi katika kuelekea kuwa Nchi ya viwanda ilikuwawezesha Wananchi kuepukana na umasikini .
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Agrey Mwanry ambae pia ni mwenyekiti wa Baraza la uwezeshaji kanda ya ziwa Mkoani kigoma katika Semina ya mafunzo ya uwezeshaji kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya za Kigoma, Kagera , Tabora na Katavi ya kanda ya Mgharibi ambayo iliandaliwa na Baraza la uwezeshaji Taifa iliyo lenga kuwawezesha viongozi kuwajengea uwezo wananchi katika kukuza uchumi.
Mkuu huyo alisema ilikuwawezesha Wananchi kunufaika na uchumi ni lazima Viongozi kushirikiana katika kuibua Fursa za uwekezaji na kuboresha Miundombinu itakayo saidia Wananchi kunufaika na uchumi katika kufanya shughuri zao katika mazingira mazuri na yanayo wavutia katika kuboresha uthamani wa bidhaa Wanazo zalisha.
Mwanry alisema Viongozi kazi yao kubwa ni kuonyesha njia ya maendeleo kwa Wananchi juu ya ukuaji wa kiuchumi, fursa zinazotakiwa kuibuliwa ni pamoja na kila halmashauri kutenga bajeti ya maendeleo ya wananchi kwa Asilimia tano ilikuweza kuwawezesha Wananchi kuepukana na umasikini na kunufaika na Ukiaji wa uchumi.