JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2012 na kumalizika tarehe 16/11/2012.
Mwaka 2012 kulikuwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, ikiwa ni ongezeko la vituo 117(2.79 %) ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.