Mbaraka Yusuf alikunjuka zikiwa zimebaki dakika chache mpira kumalizika na kumchambua beki wa Ruvu Shooting na kuziona nyavu za Ruvu Rooting ambapo mpaka wakati huo Kipa hakuwepo langoni mwake. Ushindi huo wa Kagera Sugar umewapandisha juu nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24. Ligi hii ya Vodacom sasa inaenda mapumziko ya msimu wa kwanza wa 2016/2017. Kipindi cha pili Temu Felix aliisawazishia bao Kagera Sugar na Kisha baadae Seleman Mangoma akapachika bao la pili na kufanya Kagera Sugar waongoze kwa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting.
Seleman Mangoma Kulia baada ya kuziona nyavu za Ruvu Shooting leo
Said Dunga dakika ya 45 kipindi cha kwanza aliifungia bao RUVU SHOOTING na kwenda mapumziko wakiongoza bao 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Waamuzi wa Mtanange kati ya Kagera Sugar v/s Ruvu Shooting wakati wa mapumziko wakitoka Nje ya Uwanja kwenda kwenye mapumziko ya dakika chache kujiandaa na dakika 45 za kipindi cha pili.