.jpg)
Mwana FA ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati wa kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu fistula iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square kuelekea siku ya fistula dunaini Mei 23.
Kampeni hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Vodacom na Vodafone ya Uingereza ikiihusisha mikoa mbalimbali.
Balozi huyo amesema ni wazi kwamba wanaume wamekuwa wamiliki wa maamuzi katika jamii huku wakitajwa kuwa nguzo ya familia lakini sifa hizo na mamlaka hayo yatakuwa na dosari kubwa iwapo hawatokuwa pia mstari wa mbele katika kuhakikisha jamii inapata suluhisho la matatizo.