Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Sensei Rumadha Fundi aka Romi (3rd Dan black belt) mtaalamu wa kujivunia

$
0
0
 Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi  (pichani) hatuwezi kulikwepa. Yeye  ni Mtanzania mwenye makazi yake huko Texas, nchini Marekani. 
Kabla ya kujikita huko Romi  alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale Zanaki jijini Dar es salaam chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), akiwa mmoja wa vijana wadogo wateule wa mwalimu huyo aliyebuni kundi maalumu la vijana hodari wa mchezo huo, kwa jina Bomani Brigade.

Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi huko Okinawa nchini Japan, Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga.

Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji, akiwa  ni mwalimu wa karate na yoga mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana na mwenye nidhamu.

Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni. Ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo na kadhalika  wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.
Sensei Rumadha Fundi 'Romi' (3rd Dan black belt),  akiwajibika katika semina ya karate katika Dojo ya Sugarland, Texas, nchini Marekani katika semina ya walimu wa karate (ma-sensei)  chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>