Nyumba hizi ambazo tayari zote zimeshauzwa (BOFYA HAPA), ziko eneo la Kibada. Kigamboni Housing Estate ipo Kigamboni katika eneo linalofikika kirahisi, kilomita 17 kutoka Feri. Kigamboni Housing Estate ni mradi wa nyumba 182 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo sehemu za kuchezea watoto na shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vilevile, imezingatia nafasi ya miundombinu kama vile mitaro na umeme.
Kwa mujibu wa tovuti ya shirika hilo, Nyumba hizi zenye vyumba kati ya viwili na vitatu ni mwanzo tu wa miradi mbalimbali inayoendelea nchi nzima. Uzinduzi wa Mradi huu ni chachu na dhamira ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha watanzania wanapata nyumba bora na za kisasa vile vile zikiuzwa kwa bei nafuu. Wanunuzi wa nyumba hizi wataishi kwenye maeneo kwa kuzingatia mfumo wa hati pacha (Unit titles Act 2008). Mfumo huu utawawezesha wakazi kuishi katika utaratibu wakiongozwa na sheria hiyo ambayo imeundwa kulinda maslahi ya kila mnunuzi.
Katika mradi wa Kigamboni Housing Estate, nyumba ya vyumba vitatu ina ukubwa wa 70m
²
huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na ukubwa wa 56m², ambapo
Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwa ajili ya matumizi binafsi ya wakazi ikiwa ni pamoja na maegesho ya magari hadi matatu.