Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Mikutano ya kipupwe yaanza rasmi mjini Washington DC

$
0
0
Mikutano ya kipupwe imeanza rasmi mjini Washington DC kuanzia tarehe 15/4/2013 na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi ya 188. Kila kunapokuwa na mikutano ya kipupwe maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta za elimu na binafsi, wanakutana mjini Washington DC kwa mikutano hii ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la Fedha la kimataifa pamoja na kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu akitoa maelekezo kwa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe. Gavana alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha.
Kikao hicho Kikiendelea.
Wajumbe wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo pichani, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dr. Joseph Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Susan Mkapa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya wa Wizara ya Fedha wakisikiliza kwa makini katika kikao hicho pembeni ni Mchumi mwandamizi wa Wizara ya Fedha Bw. Patric Pima.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana Bw. Msafiri Nampesya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw. Paul Mwafongo.Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>