Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

WARSHA KUHUSU HALI YA NISHATI JADIDIFU NCHINI TANZANIA 26 MACHi, 2013

$
0
0
Katika nchi ya Tanzania zimekuwepo jitihada nyingi kuongeza upatikanaji na utumiaji wa Nishati jadidifu.Kwa muda mrefu sasa kumekuwa hakuna utaratibu maalum unaoonyesha ukusanywaji wa taarifa juu ya hali halisi ya maendeleo ya sekta ya Nishati jadidifu kama ilivyo katika sekta nyingine mathalani Afya.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Taasisi ya wadau wa nishati Jadidifu nchini Tanzania(TAREA) wameandaa warsha ambayo wadau mbali mbali wa Nishati watabadilishana mawazo juu ya hali halisi ya Teknolojia ya Nishati jadidifu nchini Tanzania hadi kufikia mwezi Disemba 2002

Mwishoni mwa warsha hii,washiriki watatoa maoni yao juu ya mfumo na mbinu za kuendeleza ukusanyaji taarifa kuhusu maendeleo ya Teknolojia ya Nishati jadidifu.

Katika warsha hii COSTECH na TAREA watabadilishana makubaliano ya ushirikiano kati yao juu ya mambo yote yanayohusu utafiti,uhawilishaji na ukuzaji wa teknolojia ya nishati jadidifu.
MKURUGENZI MKUU WA COSTECH DR HASSAN MSHINDA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MAKUBALIANO YA COSTECH NA TAREA KATIKA UTAFITI,UHAWILISHAJI NA UKUZAJI WA TEKNOLOJIA YA NISHATI JADIDIFU.
WASHIRIKI KATIKA WARSHA HIYO.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>