Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA SERIKALI YA UINGEREZA NA UJUMBE WAKE

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kulia kwake) aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto kwake) aliyeongozana na ujumbe wake wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013 kwa amazungumzo. Picha na OMR
======= ====== ======
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA
DAR ES SALAAM, MACHI 22, 2013
 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Ijumaa, amekutana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Bwana Mark Simmonds ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo sambamba na masuala mengine akaelezea shukrani zake kwa serikali ya Uingereza kwa kuwa na mahusiano mazuri na Tanzania na kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
 Mheshimiwa Makamu wa Rais aliyekuwa anamuwakilisha Rais katika mapokezi hayo alisema, Tanzania inathamini mchango wa Uingereza katika sekta za elimu na afya na sasa ambapo kampuni za Uingereza hasa British Gas inajihusisha katika utafutaji wa Gesi katika bahari ya kina kirefu Kusini mwa Tanzania. Pia alizungumzia kuhusu mchango wa Uingereza kimataifa hasa katika masuala ya Mazingira na akamueleza Waziri Simmonds kuwa, Uingereza inaweza kusaidia nchi zinazokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa yenyewe kushirikiana na nchi kubwa duniani katika kuhakikisha kuwa zinatimiza wajibu wao katika kulinda mazingira.
 Kwa upende wake Waziri Simmonds yeye alimshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa mapokezi mazuri na kisha akaelezea furaha yake kwa mchango wa Tanzania katika kusaka amani katika nchi za Maziwa Makuu hasa DRC, Madagasca na Zimbabwe na kisha akafafanua kuwa, Tanzania ni mshirika mzuri wa Uingereza na kwamba nchi hii ni mfano wa kuigwa kutokana na ushiriki wake katika kusaidia amani kwa majirani zake sambamba na hatua zake za kuwapatia maendeleo wananchi wake.
 Waziri huyo alibainisha kuwa Uingereza iko tayari kuendelea kusaidia katika suala zima la uwazi na uwajibikaji na hasa katika maeneo ya Kodi na akashauri juu ya kuzidi kuwa na mashirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika shughuli za maendeleo.
Waziri Simmonds anakaa nchini kwa siku mbili na katika mkutano huu na Mheshimiwa Makamu wa Rais alifuatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diana Melrose.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam, Tanzania

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>