Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Makandarasi waliofutiwa usajili watakiwa kurejesha vyeti, kutofanya kazi

$
0
0
Na Ripota Wetu , Dar es Salaam
Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) imesisitiza kuwa wakandarsi 1110 waliofutiwa usajili hivi karibuni waharuhusiwi kufanya kazi yoyote hapa nchini kwa vile kuendelea kufanya kazi hivyo kutapelekea adhabu kali zaidi za kisheria.
Msajili wa Bodi hiyo, Eng. Boniface Muhegi aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa wale wote waliofutiwa usajili hivi karibuni wanatakiwa kurudisha vyeti vya usajili wao kwenye bodi ya makandarasi kwa sababu kubaki navyo na kuendelea kufanya kazi ni kinyume na sheria.
Akitoa sababu za kufutiwa kwa usajili kampuni hizo alisema kampuni 10 zimefutiwa sababu majina yao yalitumiwa na kampuni nyingine zisizo na sifa; na kampuni 34 kwa kushindwa kutimiza masharti ya usajili katika mamlaka husika.
Alisema kampuni mbili zilishindwa kusimamia vizuri kazi; tano ziliomba zenyewe zifutwe na kampuni 1059 zilishindwa kulipa  ada ya usajili kwa muda unaotakiwa.
Hatua hii ya kufuta usajili wa idadi hii ya makandarasi imepata baraka za kibali toka kwa waziri wa ujenzi, Dkt. John Magufuli.
Alieleza kuwa kwa kampuni 1059 zilizoshindwa kulipa ada zao kwa wakati, wanaweza kulipa ada hiyo na faini ili bodi iweze kuangalia taratibu za kuwarudishia tena usajili wao.
“Kwa mujibu wa sheria mkandarasi aliyefutiwa usajili haruhusiwi kufanya kazi tena…hata kama alikua na kazi anaendelea nayo,” alisema, na kufafanua kuwa waajiri waliokuwa na wakandarasi waliofutiwa usajili wanatakiwa kutafuta wengine kwani wenye sifa zinazotakiwa wako wengi nchini.
Alisema mkandarasi aliyefutiwa usajili na kugundulika anafanya kazi atakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya asilimia 10 ya mradi wote anaoutekeleza.
Alisema bodi kupitia ofisi zake za kanda itaendelea kuwafutia usajili wakandarasi nchini ambao wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Alitoa wito kwa wanaotoa kazi kwa wakandarasi kushirikiana vyema na bodi hiyo kuhakikisha kuwa taratibu zinafuatwa na mafanikio yanapatikana katika sekta ya ujenzi nchini.
Alisema kuanzia mwaka 2000, kampuni za kizalendo zimekuwa zikiimarika na kufanya vizuri na kwamba bodi itaendelea kuzipatia mafunzo na uwezeshaji wa aina mbalimbali katika kiziimarisha na kuzijengea uwezo.
Alisema waajiri wote wanaotumia kazi za wakandarasi nchini wanahitajika kupata ushauri kutoka bodi hiyo ili kupata wakandarasi bora na kupata huduma iliyo bora na salama.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>