Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Mh. Lowassa akutana na vijana wa Boda Boda jijini Arusha

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana waliojiajiri kwa kufanya biashara ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Boda Boda wa Jijini Arusha wakati alipokutana nao na kuzungumza nao jijini humo hivi karibuni,Mh. Lowassa amesema kuwa Bodaboda ni sera ya CCM ambayo Ina nia ya kusaidia  na kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana.
Waendesha Bodaboda Jijini Arusha wakimsikiliza kwa makini,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Vijana wa Boda Boda wa Jijini Arusha wakati alipokutana nao hivi karibuni.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkoni Vijana wa Boda Boda waliofika kumsikiliza.
Waziri Mkuu Mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa amesema kuwa bodaboda ni sera ya CCM ambayo Ina nia ya kusaidia,kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana hapa nchini.

Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda mkoani Arusha,Lowassa amesema hiyo Ni sera ya CCM kuwakomboa Vijana na kuongeza Kuwa kitendo Cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda Ni Cha mfano KWA wafanyabisharaa wengine nchini

"CCM Ni Chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha,kitendo hiki Cha wafanyabishara wa Arusha Ni kuunga mkono sera ya Chama.

Huku akishangiliwaa kila Mara na waendesha bodabodaa hao, Lowassa alirejelea tahadhari yake kuwa tatizo la ajira Ni bomu linalosubiri kulipuka.

"Tusipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hili, amani itatoweka, na ndiyo maana CCM katika Ilani yake ya Uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu mkutano mkuu pamoja na halmashauri Kuu"alisema.

Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani Mathias Manga ndiyo waliobuni wazo Hilo la kuwaanzishia Mfuko Vijana wa bodaboda.

"Hii Ni Changamoto kubwa KWA wafanyabiashara wengine Nchini wenye mapenzi na nchi yetu,kuiga mfano huu wa kuwasaidia vijana kujiajiri na kuwarejeshea matumaini, kwa kufanya hivi kutaepusha hatari ya kupotea kwa amani"alisema Lowassa ambaye amekuwa akilipigia kelele tatizo la ajira kwa Vijana.

"Kuna msemo usemao, kichwa kikiwa kitupu ni rahisi shetani kuingia,vijana wakiwa hawana ajira ni rahisi kushawishiwa kuingia kwenye vurugu na maandamano yasiyo na maana"alionya na kuingia kuwa Serikali isiachiwe pekee yake jukumu hilo.

KWA upande wake mwenyekiti wa Chama Cha waendesha bodaboda mkoani Arusha Fabian Shayo alimpongeza Mh Lowassa kwa kuwa msemaji mkuu wa tatizo la ajira kwa vijana na kumuomba asikatishwe tamaa na yanayosemwa.

Katika Harambee hilo zaidi ya shillingi millions 84 zilipatikana, huku mh Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia mil 10 na pikipiki 10.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>