Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 116956

Twanga Pepeta kusindikiza utambulisho Miss Tabata 2013 Pasaka

$
0
0
Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tabata 2013, watatambulishwa siku ya sikukuu Pasaka katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata. 

Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga amesema jana kuwa utambulisho huo utasindikizwa na burudani kababembe kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”. 

Kalinga alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya fainali itakayofanyika Mei. 

Utambulisho wa Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti 5 na Kitwe General Traders na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

 Mratibu huyo alisema warembo 25 wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata. 

Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu. Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael (pichani katikati) ambaye pia ni Miss Ilala.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 116956

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>