Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

waziri wa uchukuzi dkt mwakyembe atembelea mataruma yaliyoibiwa.

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mkwakyembe(mwenye tai nyekundu), akiangalia mataruma 35 yaliyoibiwa kutoka katika stesheni ya Reli ya Pugu na kusafirishwa kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuja kuuzwa kama chuma chakavu . Kulia kwa Waziri wa Uchukuzi ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa tai ya mistari).
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba akipata maelezo na mataruma yaliyobiwa kutoka kwa ACP Saada Haji ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi Cha Polisi Reli, wakati walifanya ziara ya kuangalia mataruma ya reli yalyibiwa katika vipindi tofauti tofauti yaliyopo katika eneo la Mivinjeni kurasini. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini Uchukuzi).
 Shehena ya mataruma ya zaidi ya Tani 15 yaliyokamatwa na askari wa kikosi cha reli yakiwa katika eneo la reli Mivinjeni baada ya kukamatwa tarehe 14/2/2013 na dreva wa Lori hilo kukimbia. Waziri wa Uchukuzi na Naibu Waziri wamefanya Ziara katika eneno hilo leo kujionea mzigo wa Mataruma yaliyobiwa katika vipindi tofauti tofauti.
Waziri wa Uchukuzi.Dkt Harrison Mwakyembe (mwenye tai  nyekundu),akipata maelezo kutoka kwa ACP Saada Haji Mkuu wa kikosi cha Polisi (Reli)(aliyevaa hijabu) ya namna wezi wa Mataruma hayo walivyoiba na kukamatwa na askari wake tarehe 14 Februari 2013. Kulia kwa ACP Saada Haji, ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba.

Magunia yaliyotumika kufunikia mataruma ya Reli ambayo yaliibiwa na kusafirishwa kutokea Tabora tarehe 14/2/2012 na kubebwa kwenye Lori la Mizigo la Kampuni ya Unga ya Azania (linaloonekana mbele) kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuuza kama chuma chakavu. Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba wamefanya ziara ya kuangalia mataruma hayo leo mchana jijini Dar es Salaam. Mataruma hayo yamehifadhiwa katika yadi ya Reli iliyoko Mivinjeni Kurasini, Dar es Salaam.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>