Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117025

Angetile Osiah aitaka Serikali ikae pembeni suala la uchaguzi mkuu TFF

$
0
0
SAKATA la serikali kuikataa katiba ya TFF imechukua sura mpya baada ya katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah kumtaka Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amos Makala kujiweka pembeni na kuacha kuzungumzia masuala ya uchaguzi wa shirikisho hilo.

Angetile aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa Makala alishaonyesha kuwa ana upande anaoupendelea ndio maana alitoa maoni yake kama mdau alipokuwa jimboni kwake Mvomero na alipofika Morogoro mjini akadai lazima Serikali itoe tamko zito.

"Katika suala hili tunamuomba Makala akae mbali ameshaonyesha interest, Waziri (Dk Fenela Mukangara) bado tunaimani naye, tumeomba kikao kifanyike kesho kutwa (kesho) Alhamis na kama itashindikana basi kifanyike baada ya tarehe 13 kwa kuwa hapa katikati kuna vikao vya CAF (Shirikisho la Soka Barani Afrika).

"Serikali sio Wizara peke yake ni pamoja na sisi kwa hiyo ikitoa maagizo itoe yanayotekelezeka sio maelekezo ambayo ni vigumu kutekelezeka."alisema Osiah ambaye pia aliwataka waliopoteza sifa za kuingia TFF kuacha kuongea ongea ovyo kwenye vyombo vya habari kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mpira hali kadhalika kwa waliofungua kesi Mahakamani kupinga mchakato wa uchaguzi.

Akizungumzia kauli hiyo ya Angetile, Makala alisema anaheshimu kauli iliyotolewa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga wiki iliyopita ya kuomba kukutana na Waziri kujadili suala hilo lifike mwisho na kudai kuwa kauli ya katibu huyo wa TFF ni yake binafsi na si msimamo wa shirikisho.

" Angetile anaupande ndio maana mimi nilipotoa maoni yangu kama mdau ilimuathiri yeye na mgombea wake, niliwaudhi, alafu hawezi kusema nikae pembeni wakati michezo ni eneo langu katika kazi, wapende wasipende suala lao mimi ndio ninayelisimamia.

Mapema mwezi uliopita kamati ya rufaa chini ya Idd Mtiginjola ilimuengua mgombea wa nafasi ya urais Jamali Malinzi kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 kwa madai ya kukosa uzoefu, na Naibu Waziri Amos Makala alikaririwa akitoa maoni kama mdau wa michezo alisema ameshtushwa kwa Malinzi kuenguliwa na kudai kamati ya rufaa imenunua dharua kwa gharama ndogo.

"Bila kupepesa macho wala kuumauma maneno, nikiwa mdau wa soka na kuuvua wadhifa wangu wa unaibu waziri, hapa kuna tatizo kwani kamati haijamtendea haki Malinzi," alikaririwa Makalla.

Hata hivyo jana alisisitiza: "Kwa taarifa yao Waziri kasafiri kwa siku 10 nina maelekezo yote ya suala lao hivyo waje nilishasema milango ipo wazi, wasichague nesi wakati wapo leba, kwanza aliyefikisha suala hili kwenye matatizo ni Angetile mwenyewe baada ya kufanya makosa yake ya kiutendaji nilidhani angekaa kimya na kutafakari makosa aliyofanya badala ya kuongea ongea."alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117025

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>