Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119151 articles
Browse latest View live

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUENDESHA SEKTA YA SANAA KIBIASHARA – NAIBU WAZIRI KIHAGE

$
0
0

Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuendesha sekta ya Sanaa kibiashara na kuongeza tija  ikiwa ni pamoja na kuwezesha sekta hii kutumika kama nyenzo ya kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Hayo yamesemwa na  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe Septemba 29, 2021 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Sekta ya Sanaa 2021 ambao lengo lake ni kujadili kwa Pamoja masuala yanayohusu Sekta ya Sanaa kati ya Serikali na wadau ili kufikia lengo la kuifanya sekta hii kuendeshwa kibiashara ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Sanaa Biashara”

“Serikali imejipanga kuweka mazingira wezeshi ya kukuza Sanaa zetu ili kufikia viwango vya kimataifa na kuboresha mbinu na Mikakati ya Utekelezaji wa sera na Sheria za kuimalisha kazi za Sanaa nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sanaa hususani wasanii” amaeeleza Mhe. Exaud Kigahe

Aidha, Mhe. Exaud Kigahe ameeleza kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara ni mdau mkubwa wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwani Sekta ya Sanaa ni kiwanda kinachozalisha bidhaa na huduma za sanaa ambazo zinahitaji mchango mkubwa wa Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuweka sera, sheria, kanuni na miongozo  mbalimbali ya kusimamia uendeshaji wake na kuiendeleza kama inavyofanyika katika Sekta nyingine za kiuchumi hapa nchini.

Kwa upande wake, Dkt. Emmanuel Ishengoma Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaaa wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ameeleza kuwa ili kuendesha Sanaa kibiashara, Serikali imeanzisha mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao utasaidia kuimarisha sekta hiyo kwa kudhamini mafunzo vilevile kutoa mkopo kwa mashariti nafuu ya kusaidia Sanaa na utamaduni na mpaka sasa Serikali imeshatoa billioni moja na milioni mia tano za kuwezesha mfuko huo




 


 


SERIKALI YAPELEKA VIFAA TIBA HOSPITALI YA CHALINZE,RIDHIWANI KIKWETE ASHUKURU

$
0
0

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
 

SERIKALI  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa leo imetimiza ahadi zake zilizotolewa na Rais wa Samiah Suluhu Hassan kwa kupeleka vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani.

Vifaa hivyo vina thamani ya Shilingi Milioni 480 ikiwemo mashine ya Kupiga picha za Mionzi yaani X-Ray, Jokofu la kuhifadhia maiti, mashine za kupimia damu na vifaa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameishukuru Serikali kwa kutekeleza ahadi hii ndani ya muda wa wiki tatu toka kutolewa kwa ahadi.

Wananchi wa Kata hiyo wakiongozwa na wakina mama ambao walikuwa ipokea wameshangilia na huku wazee wakimuombea Mungu amlinde Rais wa nchi yetu.




 

NAWAASA WANANCHI KUACHANA NA IMANI POTOFU NA KUWASIKILIZA WATAALAMU WA AFYA-DC KIBITI.

$
0
0

 NA WAMJW- KIBITI, PWANI.

MKUU wa Wilaya ya Kibiti Kanali. Ahmed Abasi Ahmed ametoa wito kwa wananchi kuachana na Imani potofu zinazotolewa na watu wasio na nia njema kwa wananchi na kuwataka kuwasikiliza zaidi Wataalamu wa afya na viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

Ameyasema hayo leo waati akifungua kikao cha kamati ya Afya ya msingi ya Wilaya Kibiti, chenye lengo la kuhamasisha wananchi kupata Chanjo ya UVIKO-19 kupitia kampeni shirikishi na harakishi inayoongozwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR TAMISEMI.

"Nichukue nafasi hii kuwasisitiza wananchi kuachana na Imani potofu, wawasikilize Wataalamu wa huduma za Afya lakini pia wawasikilize viongozi wilio na dhamana ya kutuongoza katika mapambano haya makubwa ya UVIKO-19 tulionayo" amesema Kanali. Ahmed.

Natambua Serikali imewekeza nguvu kubwa katikati mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa UVIKO-19, na sisi kama Wadau wa vita hii, tuunge mkono jitihada hizi za Serikali ili kushinda dhidi ya vita hii. Alisisitiza.

Aidha, Amesema kuwa, Shirika la Afya Duniani na Wataalamu wa ndani tayari wamethibitisha Chanjo ni salama, haina madhara, hivyo kuwataka kwasikiliza watoa mafunzo kwa makini ili kwenda kuwaelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ili wajikinge dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

"Shirika la Afya Duniani na Wataalamu wetu wameshatuhakikishia Chanjo hii ni salama, haina madhara, hivyo niwaombe tuwasikilize kwa makini Wataalamu wetu waliokuja kutupa mafunzo na tutayojifunza twende tukawaelimishe wananchi wetu ili wajutikeze kwa wingi kupata Chanjo ili wajikinge dhidi ya ugonjwa huo." Amesema.

Mbali na hayo, amesema kuwa, Wilaya hiyo ilianza kuwa na vituo vitatu vya kuchanja baadae kuongezeka mpaka vituo vitano na kuweka wazi kuwa, mpaka sasa vimeongezeka na kufikia vituo zaidi ya hamsini na nne (54), ikiwa ni jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya kuwakinga wananchi dhidi ya UVIKO-19.

Hata hivyo amesema kuwa, pamoja na uwepo wa vituo hivyo bado kasi ya watu kujitokeza kuchanja sio kubwa, hivyo kuwataka wajumbe katika kikao hicho kufuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa ili kuwa na uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa chanjo na kuweza kuwashawishi wananchi kujikinga dhidi ya UVIKO-19 kupitia afua ya Chanjo


 


 


IDARA YA AFYA SHINYANGA YAWATAKA WANACHI KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0



Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.
Idara ya Afya katika Halmashari ya Manispaa ya Shinyanga imewataka Wananchi wote kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kufanya usafi katika makazi yao,kudhibiti utupaji wa taka ovyo, pamoja na kuwa na vyoo Bora na imara.


Wito huo umetolewa na Mratibu wa afya Manispaa ya Shinyanga Bwana Ramadhan Hamimu wakati alipotembelea kata ya Ibinzamata kuhamasisha suala la usafi wa mazingira ambapo amesema Halmashauri hiyo itasimamia na kuhakikisha kila mwananchi anafanya usafi katika makazi yake,ikiwa ni pamoja na kudhibiti utupaji wa taka ovyo. 


Amesema Idara ya afya kwa kutumia sheria na kanuzi za usafi wa mazingira itawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukaidi utekelezaji wa agizo hilo muhimu ambalo limelenga kuweka mazingira yote katika hali ya usafi.


“Kuna mtu anafagia halafu taka anatupa kwenye kiwanja cha mtu mwingine yaani hana sehemu yake ya kuhifadhia taka ukitupa taka kwenye kiwanja siyo chakwako hilo ni kosa la jinai kisheria na ndiyo maana kisheria kama kiwanja cha jirani yako kipo wazi unatakiwa ukisafishe nikikuta kichafu kinamakaratasi nakukamata wewe kwa sababu yeye hayupo hapo kimechafukaje”


Amesisitiza umuhimu wa kila Mwananchi kuwa na Choo bora na imara hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye msimu wa Mvua za Masika ili kudhibiti maonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, na kuhara.


“Vyoo tunavyo lakini havina sifa ya kuwa vyoo yaani tumejiwekea sehemu ya kujificha tu lakini siyo vile vyoo ambavyo vinahitajika hapa Manispaa ya Shinyanga kwanza tunaingia msimu wa mvua jana nimetembelea kaya zaidi ya miamoja lakini nimekuta kaya angalau vimeezeka tu ni kaya 23 kaya zingine zote vyoo vyao vikowazi kwa juu ambapo msimu wa mvua unaingia badae vitakuja kutitia ukimfuata mtu anakwambia huu ni msimu wa mvua kimetitia sitokuelewa kabisa nataka choo chako nikikute kimeezekwa na kina mlango hiyo ni lazima kwa hiyo mimi sitaki tufike huko ustaarabu ni kusafisha mazingira,

hakuna kutupa taka ovyo nikikuta taka zimezagaa kwako hilo ni kosa utakamatwa na utapigwa faini ya Shinlingi elfu hamsini(50000) siwatishi nipo kwa ajili ya kulinda afya zenu ili msipate magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu, kuhara na magonjwa mengine”







SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kupokea vifaa saidizi kwa ajili ya wenye ulemavu vilivyotolewa na Taasi ya kutoa huduma ndogo za kifedha (ASA Microfinance Company Limited) katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Septemba 28, 2021 Jijini Dodoma.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ASA Microfinance Company Limited, Muhammad Shah Newaj akitoa salamu za kampuni hiyo kabla ya kukabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu katika Ofisi ya Waziri Mkuu enep la Mtumba Jijini Dodoma.



Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Jacob Mwinula akizungumza katika hafla ya kupokea vifaa saidizi kwa ajili ya wenye ulemavu vilivyotolewa na Taasisi ya kutoa huduma ndogo za kifedha (ASA Microfinance Company Limited)..



Afisa Sheria kutoka kutoka kampuni ya ASA Microfinance Company Limited, Zephania Paul akifafanya jambo wakati wa hafla niyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ASA Microfinance Company Limited, Muhammad Shah Newaj ( wa tatu kulia) akikabidhi vifaa saidizi vya watu wenye ulemavu kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga ( wa nne kulia ) Jijini Dodoma.



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya ASA Microfinance Company Limited wakiwa katika picha ya pamoja na watu wenye ulemavu baada ya makabidhiano hayo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

…………………………………………………………………..

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

SERIKALI imesema inaendelea na utaratibu wa kujenga na kukarabati vyuo vya watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwasaidia wenye ulemavu kupata ujuzi ili kujikomboa kiuchumi.

Akizungumza Jijini Dodoma baada ya kupokea msaada wa vifaa visaidizi kwa ajili ya wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi milioni 13.9 ambavyo ni viti mwendo 55 na fimbo nyeupe 50 za wasioona kutoka kwa Taasisi ya kutoa huduma ndogo za kifedha (ASA Microfinance Company Limited), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anapata haki yake bila vikwazo.

Aliongeza kuwa ipo mikakati madhubuti ya kuhakikisha masuala ya wenye ulemavu yanapewa kipaumbele ikiwemo uboreshwaji wa vyuo ikiwemo Chuo cha Mwanza ambacho ujenzi wake unatarajiwa kukamilika kuanzia mwezi Januari mwakani kuwawezesha vijana kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kufanya shughuli zao za uzalishaji na kushiriki katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

“Kwasasa Wizara inaratibu kwa kasi ujenzi wa vyuo vya watu wenye ulemavu na ufufuaji wa vile ambavyo vipo.Tunaendelea kufanya hivyo katika Chuo cha Yombo Dar es salam, tumezindua Chuo kingine Tabora ambacho kilikuwa kimefungwa kwa miaka 10 na kumalizia ujenzi wa chuo cha kisasa Mkoa wa Tanga,” alisema Naibu Waziri Ummy.

Pia Naibu Waziri huyo alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuendelea kutoa fedha ya elimu bila malipo ambapo watu wenye ulemavu nao hunufaika na mfumo huo huku akieleza kuwa Serikali inatambua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.

“Serikali kupitia bohari kuu ya dawa inaendelea kuagiza mafuta ili kuwakinga dhidi ya saratani ya Ngozi kwa watu wenye ualbino sambamba na kuzitaka Halmashauri kuendelea kutenga fedha za mapato ya ndani kupitia asilimia 10 inayotolewa na kila Halmashauri kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu kwa sababu hii inawasaidia kupambana na umasikini,”alieleza.

Hata hivyo aliishukuru kampuni hiyo kwa moyo wake wa kujitoa na kuiunga mkono serikali katika juhudi za kuwaletea ustawi wananchi wake na kuwahimiza wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuwasaidia watu wenye ulemavu hatua itakayofanya kujiona wana thamani na kutambulika ndani ya jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ASA Microfinance Limited , Muhammad Shah Newaj alieleza kwamba wametoa msaada huo wenye thamani ya Sh. milion 13.9 kama sehemu ya kutambua mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa akisema wana uwezo wa kufanya kazi kama watu wengine endapo watapewa fursa na kuhudumiwa katika mahitaji yao wataendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanaisaidia jamii kuepukana na umaskini.

Naye Afisa Sheria kutoka ASA Microfinance Limited, Zephania Paul alifafanua kwamba vifaa hivyo ni sehemu ya kutoa huduma kwa jamii na awamu hiii ni yapili kufanyika akisema awamu ya kwanza ilifanyika jijini Dar es salaam huku akibainisha kuwa taasisi hiyo ipo katika Mikoa nane ya Tanzania Bara na Zanzibar na hadi sasa wamewafikia wanawake 1,600 na kutoa ajira .

Akitoa shukrani zake mama wa mtoto mwenye ulemavu Martha Mshama aliishukuru serikali kwa kushirikiana na wadau kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu akieleza kuwa kiti alichopewa kitamsaidia kufanya kazi zake kwani awali alikuwa akitumia muda mwingi kuwa karibu na mtoto akihofia kuanguka na kupata madhara.

” Tunaishukuru serikali kwa kutupatia viti mwendo ambapo ni msaada mkubwa kwangu maana nilikuwa nikihofia usalama wa mtoto wangu kuna wakati anaweza kuanguka natakiwa kuwa naye karibu sana lakini sasa walau nitaweza kufanya kazi zangu nawashukuru sana Mungu awabariki,”alishukuru Martha.

Naye Selina Nigangwa (mwenye ulemavu wa miguu) mkazi wa Swaswa aliishukuru serikali kwa kuwapatia msaada huo na kushauri wakati mwingine kutoa viti vya kuendesha kwa kutumia mikono.

“Tunashauri serikali wakati mwingine watoe viti vya kuendesha kwa mikono ili tuweze kuendesha wenyewe bila kumtegemea mtu,” alieleza Selina.

VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUHAMASISHA WATU KUFUNGA NDOA KUKABILIANA NA UTORO,UZURURAJI NA MIMBA ZA UTOTONI

$
0
0

Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESH), Henerico Masasi akifungua kikao cha Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Shilela na Lunguya na Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na TGNP.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Imeelezwa kuwa bado migogoro ya ndoa ni chanzo cha matukio ya ukatili dhidi ya watoto hali inayosababisha watoto kubeba majukumu ya familia na kuchangia utoro wa wanafunzi shuleni, mimba na ndoa za utotoni na uzururaji wa watoto pindi wazazi wao wanapotengana.

Hayo yamebainishwa Jumatano Septemba 29,2021 na Wanavituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya Msalala Mkoani Shinyanga wakati wa kikao cha kutoa Matokeo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA tangu mwezi Julai 2020.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Nitesh Mjini Kahama umehudhuriwa na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa 40 kutoka kata ya Shilela na Lunguya na Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) 25 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Lameck Manyesha amezitaja baadhi ya changamoto wanazoendelea kukabiliana nazo kuwa ni migogoro ya ndoa (kutengana kwa wanandoa) hali inayosababisha watoto kubeba majukumu ya familia na kupelekea utoro wa wanafunzi shuleni, mimba na ndoa za utotoni na uzururaji wa watoto.

“Tunaomba viongozi wa dini wahamasishe wanajamii kufunga ndoa na kuishi vizuri kwani watu waliofunga ndoa wanakuwa na hofu ya Mungu na hawatengani hovyo hovyo kama hawa wanaookotana tu mtaani na kuanza kuishi kama mme na mke matokeo yake wakitengana watoto wanatelekezwa na kuanza kuteseka.

“Pindi wazazi wanapotelezwa wanajikuta wanabeba majukumu ya familia,ikiwemo kulea wadogo zao na wakati mwingine watoto wanajiingiza katika makundi mabaya na wengine kuacha shule na kuanza kufanya biashara ya ngono”,ameeleza Manyesha.

Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya, Meja John amesema wamefanikiwa kupunguza mila na desturi zisizofaa ikiwemo ya Mila ya Ukango ambapo sasa wachezaji wa ngoma hiyo wameacha kutumia lugha za matusi wanapocheza ngoma zao lakini pia sasa wananchi wameacha kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo na sasa pia wanawake wanashiriki kwenye shughuli za uchimbaji madini bila bughudha yoyote.

“Tuliibua choo cha msingi katika shule ya Msingi Lunguya ambacho kilikuwa kibovu. Tukashirikiana na Mwalimu Mkuu na viongozi wa Kijiji na kufanikiwa kujenga matundu 12 ya vyoo (6 kwa ajili ya wasichana na 6 kwa ajili ya wavulana. Pia tumefanikiwa kujengwa kwa choo cha mwalimu Mkuu katika shule hiyo ambapo TGNP imetoa shilingi 600,000 ili kufanikisha ujenzi wa choo hicho”,amesema.

Katika hatua nyingine amesema kata ya Lunguya ina vijiji vitano lakini shule nne za msingi ambazo Madaho, Nyamishiga, Kalole na Kabanda zilizopo hazina walimu wa kike na hakuna vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike tofauti ya kijiji cha Lunguya.

Naye Msaidizi wa Kisheria Phillip Jackson Sesawanga kutoka kata ya Kashishi Halmashauri ya wilaya ya Msalala amesema Wasaidizi wa Kisheria kwa kushirikiana na Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP, wanaendelea kutatua migogoro mbalimbali ya ndoa na ardhi pamoja na kupinga mimba na ndoa za utotoni na kurudisha shuleni watoto wa kike waliokuwa wameachishwa masomo.

Sesawanga ameiomba jamii kuacha kuatamia (kukumbatia) matukio ya ukatili wa kijinsia hivyo watoe taarifa kwa wakati juu ya matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na hata wanaume wanapofanyiwa ukatili wasisite kutoa taarifa.

Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESH), Henerico Masasi amesema kikao hicho kinatoa matokeo na ni kipimo cha kujua ni wapi vituo vya taarifa na maarifa na Wasaidizi wa Kisheria wamefikia katika mapambano ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto tangu waanze kutekeleza mradi huo mwaka 2020 hadi Septemba 2021.

Amesema kazi kubwa ya Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa ni kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia hasa yanayowakumba zaidi wanawake na watoto ili kuongeza ustawi wa wanawake na watoto katika jamii.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESH), Henerico Masasi akifungua kikao cha Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa 40 kutoka kata ya Shilela na Lunguya na Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) 25 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na TGNP Jumatano Septemba 29,2021 katika Ukumbi wa Nitesh Mjini Kahama. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa 40 kutoka kata ya Shilela na Lunguya na Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) 25 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga  wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na TGNP
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa 40 kutoka kata ya Shilela na Lunguya na Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) 25 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga  wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na TGNP.
Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Lameck Manyesha akiwasilisha taarifa ya kituo hicho ambapo amezitaja baadhi ya changamoto wanazoendelea kukabiliana nazo kuwa ni migogoro ya ndoa hali inayosababisha watoto kubeba majukumu ya familia na kupelekea utoro wa wanafunzi shuleni, mimba na ndoa za utotoni na uzururaji wa watoto.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya, Meja John  akielezea mafanikio waliyoyapata kwenye kituo hicho ikiwamo kupunguza mila na desturi zisizofaa ikiwemo ya Mila ya Ukango ambapo sasa wachezaji wa ngoma hiyo wameacha kutumia lugha za matusi wanapocheza ngoma zao.
Msaidizi wa Kisheria Phillip Jackson Sesawanga kutoka kata ya Kashishi Halmashauri ya wilaya ya Msalala akielezea kuhusu ushirikiano unaofanywa na Wasaidizi wa Kisheria  na Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP katika kutatua migogoro mbalimbali ya ndoa na ardhi pamoja na kupinga mimba na ndoa za utotoni na kurudisha shuleni watoto wa kike waliokuwa wameachishwa masomo.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa  wa kata ya Shilela  wakifanya majadiliano kuhusu Matokeo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA.
Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala wakifanya majadiliano kuhusu Matokeo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa  wa kata ya Lunguya  wakifanya majadiliano kuhusu Matokeo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON KATIKA ZIARA YA KAZI YA SIKU NNE NCHINI MALAWI

$
0
0

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wapili kulia) akizungumza na Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Hara (katikati) alipowatembelea leo katika ofisi za Bunge la Malawi Lilongwe nchini Malawi, kushoto ni Naibu Spika wa Pili wa Bunge la Malawi, Mhe. Aisha Adams na Naibu Spika wa kwanza wa Bunge la Malawi, Mhe. Madolitso Kazombo. Naibu Spika Tulia yupo Malawi kwa ziara ya kikazi ya siku nne



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akipatiwa maelezo na Naibu Spika wa kwanza wa Bunge la Malawi, Mhe. Madolitso Kazombo akiwa Jukwaa la Spika alipotembela Bunge la Malawi leo Lilongwe nchini Malawi, Naibu Spika Tulia yupo Malawi kwa ziara ya kikazi ya siku nne



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Hara (katikati) wakimsikiliza Naibu Spika wa kwanza wa Bunge la Malawi, Mhe. Madolitso Kazombo alipowatembelea leo katika ofisi za Bunge la Malawi Lilongwe nchini Malawi, Naibu Spika yupo Malawi kwa ziara ya kikazi ya siku nne



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Hara alipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Lilongwe nchini Malawi, Naibu Spika yupo Malawi kwa ziara ya kikazi ya siku nne, Kulia ni Katibu wa Naibu Spika Tulia, James Sapali



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Hara alipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Lilongwe nchini Malawi, Naibu Spika yupo Malawi kwa ziara ya kikazi ya siku nne



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Hara (katikati) pamoja na Naibu Spika wa Pili wa Bunge la Malawi, Mhe. Aisha Adams alipowatembelea leo katika ofisi za Bunge la Malawi Lilongwe nchini Malawi, Naibu Spika Tulia yupo Malawi kwa ziara ya kikazi ya siku nne

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI IWE AJENDA YA KUDUMU KWENYE VIKAO VYA HALMASHAURI

$
0
0

 

Prisca Ulomi na Faraja Mpina, Dodoma


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amezungumza na wajumbe wa Mkutano wa ALAT unaojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kwenda kutekeleza Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwa kuifanya kuwa ajenda ya kudumu katika mabaraza ya madiwani na vikao vyote vya kisheria vinavyofanyika katika Halmashauri zao

 

Hayo ameyazungumza wakati wa Semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo huo kwa wajumbe wa ALAT jijini Dodoma leo Septemba, 2021 na kuwasisitiza kwenda kudhihirisha wanaweza kutekeleza kwa vitendo kwa sababu dhamira ipo, bajeti ipo na uwezo upo wa kulikamilisha uwekaji wa Mfumo huo

 

Dkt. Kijaji amewataka viongozi hao kwenda kuwashirikisha watendaji wao na waheshimiwa madiwani ambapo watashuka mpaka katika ngazi ya kata,Kijiji, mtaa na kitongoji katika halmashauri zote 184 nchi nzima ili manufaa ya mfumo huo yafahamike kwenye jamii na kuwe na muitikio chanya wa utekelezaji wake

 

Amesema kuwa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi ni mfumo mama wa mifumo yote ya utambuzi tuliyonayo nchini inayoiwezesha Serikali kumfikia mwananchi mahali alipo na mwananchi kuweza kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuchumi na kijamiii kwa kufikishiwa huduma na bidhaa mpaka mahali ambapo mwananchi huyo yupo

 

“Tunapokwenda kurahisisha utoaji wa huduma kupitia Anwani za Makazi na Postikodi inamaanisha hata uchumi wa mwananchi utaenda kukua hivyo wakurugenzi na wenyeviti ambao ndio mnaowahudumia wananchi moja kwa moja mlibebe hili”, alizungumza Dkt. Kijaji

 

Amesema kuwa “Dunia inaelekea kwenye uchumi wa dijitali ambapo biashara na huduma zinatolewa kwa njia ya mtandao na kufikishiwa popote ulipo duniani, nasi tunataka kama nchi tuweze kufikia huko na kwa mapenzi mema ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake ya Awamu ya Sita amesema tunakwenda kuuwezesha mfumo huu kukamilika”.

 

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa Serikali kupitia Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 imeimarisha Mfumo wa Anwani za Kitaifa ambao unamtambulisha kila mwananchi mahali alipo kwa kutumia Anwani za Makazi na Postikodi

 

Amesema kuwa zoezi la kusimika mfumo huo lilizinduliwa rasmi mwaka 2016 na kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Halmashauri zote nchini zinaendelea na utekelezaji wa kusimika mfumo huo

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa Wizara hiyo kupitia kamati tendaji ya kutekeleza Mfumo huo imefanya kazi ya ziada kuhakikisha ajenda ya Mfumo huo inasikika, inaeleweka na inatekelezeka na imejipanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 kila nyumba iwe na Anwani ya Makazi

 

“Sisi kama Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22 tuna bajeti ya Halmashauri 17 tu za kusimika Mfumo wa Anwani za Makazi, lakini kila Mkurugenzi katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa ana bajeti ya kutekeleza Mfumo huu ila utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua hivyo tulikaa na kujipanga kuhakikisha kuwa utekezaji huu unafanyika katika Halmashauri

zote nchi nzima

 

Naye Bi. Elizabeth Mrema akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kuwa Wizara hiyo inajukumu la kutafsiri mipaka ambayo imetangazwa na Serikali na kutengeneza ramani za mikoa, wilaya, viwanja vilivyopimwa na kumilikisha ardhi ambapo takwimu husika ndizo zinazotumika na zinakuwa ndio msingi wa kuwekewa Anwani ya Makazi na Postikodi

 

Naye Katibu wa ALAT Taifa Moses Kaaya ameipongeza Wizara husika kwa kuandaa semina inayohusu kwenda kutekeleza mfumo wa dunia wa Anwani za Makazi na Postikodi na kuwataka wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri kulipa suala hilo umuhimu kwa kuwa ni suala la msingi kwa maendeleo ya  Taifa letu 

Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mateus, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhusu utekelezaji na manufaa ya Anwani za Makazi na Postikodi katika semina iliyofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula akizungumza wakati wa semina kuhusu utekelezaji na manufaa ya Anwani za Makazi na Postikodi katika kwa wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini  iliyofanyika jijini Dodoma 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Festo Dugange akizungumza wakati wa semina kuhusu utekelezaji na manufaa ya Anwani za Makazi na Postikodi katika kwa wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini  iliyofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akizungumza wakati wa semina kuhusu utekelezaji na manufaa ya Anwani za Makazi na Postikodi katika kwa wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini iliyofanyika jijini Dodoma
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Elizabeth Mrema akizungumza wakati wa semina kuhusu utekelezaji na manufaa ya Anwani za Makazi na Postikodi katika kwa wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini iliyofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa ALAT Taifa Moses Kaaya akizungumza wakati wa semina kuhusu utekelezaji na manufaa ya Anwani za Makazi na Postikodi katika kwa wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini iliyofanyika jijini Dodoma
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (wa nne kulia) wakifuatilia semina ya Anwani za Makazi na Postikodi kwa wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini iliyofanyika jijini Dodoma
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (wa nne kulia walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyo baada ya ufunguzi wa semina ya Anwani za Makazi na Postikodi kwa wajumbe wa ALAT inayojumuisha Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini iliyofanyika jijini Dodoma

Baadhi ya wajumbe wa ALAT Taifa wakifuatilia semina ya Anwani za Makazi na Postikodi iliyotolewa kwao na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI; na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliyofanyika jijini Dodoma.




TARAFA YA MIHAMBWE WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA CHANJO CORONA

$
0
0

Na Mwandishi wetu Mihambwe


Wakazi Tarafa ya Mihambwe wamehasika  vilivyo kwa hiyari yao kupata chanjo ya Uviko 19 (Corona) mara baada ya kuelimishwa na huduma kusogezwa jirani na Wananchi.

"Nashukuru sana kupata chanjo ya Corona, niwaombe Watanzania wenzangu tuendane na  Dunia ilivyo, na sidhani kuna Mtanzania ama kiongozi yeyote yule anataka kuwatesa Wananchi. Tuchanje ili kupunguza madhara ya ugonjwa huu." amesema Ndaile Abdallah Ulaya mkazi Kijiji cha Dinyeke

Muuguzi Asha Kasembe amewahimiza akina Mama na Wananchi wote wapate chanjo kwani ni salama na inaimalisha kinga za mwili na kupunguza vifo na  inapunguza makali.

Pia Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameungana na Rais Samia kupambana na ugonjwa huu kwa kuwapa elimu Wananchi, kuwahamasisha na wanaoridhia wanapata chanjo bure.

"Dunia ipo kwenye mapambano ya Uviko 19 nasi Tarafa ya Mihambwe tunaungana na Rais Samia kupambana na ugonjwa huu kwenye vijiji na vitongoji kuwaelimisha, kuwahamasisha na tumeona Watu wengi wamejitokeza kwa hiyari yao kupata kinga kutokana na huduma ya chanjo kuwafikia jirani nao. Nazidi kusisitiza Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa vitakasa mikono, kuepuka mikusanyiko na kupata chanjo ya sindano ya Corona" alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika zoezi hilo Mamia ya Wananchi wamejitokeza kupata chanjo ya Corona na zoezi hilo litakuwa endelevu ndani ya Tarafa ya Mihambwe.






 

Customer Service Week should be the right time to address the Service Gaps

$
0
0
By Godwin Semunyu

Phillip Kotler, a seasoned Marketer, defines customer satisfaction as a ‘feeling of pleasure or disappointment, resulted from equating a product’s performance against expectations. Meaning, when a product or service meets customer expectations, we have positive satisfaction and dissatisfaction when it doesn’t.

If you are thirsty and decide to buy a soft drink, your expectations are at both quenching the thirst and enjoying the flavor. When the drink meets your expectations, you are a satisfied customer. You are likely to recommend it to your peers and make a future repeated purchase. In case of disappointment, a terrible experience creates a “service gap.” You are likely to give bad recommendations, and that will probably be your last purchase.

On average, customers tell nine people about a positive brand experience versus telling 16 people about a negative one. Unsurprisingly, 32% of poorly treated customers will never return. The numbers speak for themselves.

From October 4th to 8th-2021, the world will be celebrating customer service Week to commemorate the importance of customer service and the people who serve and support customers daily. This year, the week is themed “The Power of Service,” paying tribute to changes in dynamics of service offering amidst the pandemic.

In Tanzania, the week has gained popularity in recent years, with organizations engaging in several endeavors, notably staff dancing videos to popular Nigerian or South African tunes with matching attires. It has since become a week of marathons of staff dance videos and social media posts of staff donning a variety of matched attires from vitenge to Gujarat attires. The rivalry is so fierce that one crucial aspect is being left out; the customer. Very little is done to improve service levels and address customers’ pain points.

While there’s nothing wrong with the dance videos and matching attires, the jubilations should go concurrently with a focus on improving customer service.

In recent times, there have emerged so many gaps in our service delivery industry that, as customers, we are becoming accustomed to a tradition of being “okay” with poor services. Our expectations have gone so low, to the point that being served satisfactorily is considered a favor and not a right.

Suddenly, it is okay for; staff to demonstrate a lousy attitude, take calls while serving, or drop calls. Response times now vary with moods; companies now send reps with a lack of product knowledge. There are cases of unprofessional interactions, poor telephone etiquette, moody cab drivers, poor packaging that leads to spillage, ridiculous flight delays and cancellations, unregulated lunch breaks, and many other shortfalls.

I can’t be the only one who gets dismayed when, after ordering a cab online, clearly stating my destination and fees on display, then being asked by the driver, “unaelekea Wapi Boss,” then start to negotiate the price.

I constantly attend football matches. However, I don’t recall the last time I ended up sitting on my designated seat. You have to look for any vacant seat. The stewards are just there enjoying the match. They want you to “understand” and be “okay” that someone sat in your seat. Find another seat, Bro. It is okay.

The digitization of the monetary transaction services means most transactions and bills are now executed online. Commonly at one’s mobile phone convenience. All is well until in times of troubleshooting. The reverse transaction times vary from 24-72 hours; why? The journey to migrate customers from the traditional to digital channels has been long and costly. Still, the disappointments and unreliability will give customers reasons to think otherwise.

If you are a frequent local flyer, you will agree that some airlines tend to delay or cancel flights out of the blues. They expect you to “understand” the existence of reasons “beyond” their control. Flights from KIA to JKNIA scheduled for 19:00 hours could be delayed to midnight, just like that.  It is supposed to be okay; it is “just five hours “delay, just like last week or a week before. What’s all the fuss about? Just five hours.

We can look all flashy in our “Amapiano dance” Customer Service Week videos, donning the lavish matched vitenge or Gujarat attires. Still, if nothing is done to improve our service levels and address the service gaps, we could all end up sounding like a broken record.
Happy Customer Service Week.

Vodacom Tanzania Plc yatoa zawadi kwa mshindi wa promosheni ya Tusua Mapene kwa mwezi wa Nane

$
0
0

 

 

Msimamizi wa Maduka ya Vodacom kanda ya Ziwa Maryglory Mtika(kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 10 Vincent Gratus ambaye ni mshindi wa promosheni ya Tusua Mapene kwa mwezi wa Nane, mkazi wa Kabuholo jijini Mwanza Vincent Haule, kwenye hafla iliyofanyika jijini humo jana.


Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua d.light Tanzania yafungua kituo cha huduma kwa wateja na mauzo Makumbusho jijini Dar Es Salam

$
0
0

 



Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora (katikati) akikata utepe kuzindua kituo cha huduma kwa wateja na mauzo cha vifaa vya umeme wa jua vya d.light Makumbusho jijini Dar Es Salaam. Wengine kulia ni Mkurugeni wa d.light Tanzania, Charles Natai na kushoto ni Meneja Biashara d.light kanda ya Pwani , Gasper Mrosso.

Afisa Mauzo mkoa wa Dar Es Salaam, Mosenye Chacha akitoa maelezo kwa Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora jinsi vifaa vya umeme wa jua d.light vinavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho kilichopo Makumbusho jijini Dar Es Salaam.
.Mkurugeni wa Dlight Tanzania, Charles Natai (kushoto) akimkabidhi Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora zawadi ya kifaa kinachotumia umeme wa jua kutoka d.Light Tanzania, Kifaa hichi kinatoa mwanga , kina radio na kina sehemu ya USB kwa ajili ya kuchajia simu, mara baada ya uzinduzi wa kituo hichi kilichopo Makumbusho jijini Dar Es Salaam.
.Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja na mauzo cha vifaa vya umeme wa jua d.light Makumbusho jijini Dar Es Salaam.Wengine kushoto ni Mkurugeni wa d.light Tanzania, Charles Natai na Meneja Biashara d.light kanda ya Pwani , Gasper Mrosso.

Mteja wa d.light, Frank Mchaki akielezea namna vifaa vya umeme wa jua vya d.light vinavyofanya kazi.
 Fundi wa vifaa vya umeme wa jua vya d.light, Idd Ramadhani (kulia) akitoa maelezo kwa Diwani wa kata ya Kijitonyama, Mhe. Mhandisi. Damas Samora namna wanavyojali na kutoa huduma ya ufundi kwa wateja wao mara baada ya kununua vifaa hivyo.

VYAMA VYA WAFANYAKAZI VINA TIJA, VITUMIENI VYEMA- WAZIRI MHAGAMA

$
0
0





Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu , Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) uliofanyika Jijini Dodoma Septemba 29, 2021.



Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) anayemaliza muda wake Bwa. Archie Mntambo akitoa salamu za Chama katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) uliofanyika Jijini Dodoma



Bw. Tumaini Nyamhokya rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) uliofanyika Jijini Dodoma



Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Pendo Berege akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) uliofanyika Jijini Dodoma



Baadhi ya viongozi walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama mkutano uliofanyika Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

……………………………………………………………….

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema Vyama vya Wafanyakazi Nchini vina mchango mkubwa katika upatikanaji wa maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayo Septemba 29, 2021 Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) ambapo alisema Serikali inaendelea kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi na kuboresha miundombinu ili watekeleze majukumu yao kwa weledi na uadilifu.

Alisema ni nia ya Serikali kuhakikisha inaondoa changamoto zilizopo kati ya mwajiri na mwajiriwa huku akihimiza uwepo wa mabaraza ya wafanyakazi mahala pa kazi kama sehemu ya kutafuta ufumbuzi pindi migogoro inapojitokeza kwa kufanya mazungumzo kama daraja la mahusiano mema.

“Ninaamini nia njema ya viongozi wetu hawa Rais Samia Suluhu Hassan, Mkamu wa Rais, Waziri Mkuu na sisi kama wasaidizi wao katika kuwathamini wafanyakazi wa sekta ya umma na binafasi kama mchango mkubwa wa ustawi wa maendeleo ya Taifa letu na niwaombe zile changamoto mnazoona ziko ndani ya uwezo wenu mzifanyie kazi haraka,”alisema Waziri Mhagama.

Pia amemuagiza Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi nchini kuweka utaratibu wa kuandaa mafunzo maalumu kwa Viongozi wa TUGHE kuimarisha chama chao na kutumia fursa hiyo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku akisistiza kufuatwa kwa sheria za uamisho wa viongozi wa wafanyakazi kufuatia baadhi ya watu kujichukulia uamuzi wa kuhamisha viongozi bila kufuata sheria kudhoofisha Chama.

Vilevile amewataka waajiri kuatambua umuhimu wa Vyama vya Wafanyakazi na Viongozi wa Vyama vya wafanyakazi katika maeneo yao kama daraja la kuwaunganisha waajiri na wafanyakazi kuondoa migogoro inayoweza kuepukika na kuheshimu Mabaraza mahala pa kazi.

“Ni kweli kuna baadhi yetu sisi viongozi wa Vyama vya wafanyakazi tunakuwa chanzo cha migogoro badala ya kujenga amani sehemu za kazi niwaase ili tuweze kwenda sawasawa kila mtu atimize wajibu wake ningetamani katika kipindi changu cha uongozi kuona mahusiano ya wafanyakazi na waajiri yanakuwa ya hali ya juu,”alieleza .

Hata hivyo alibainsiha kwamba Serikali itaendelea kufanya marejeo ya sheria za utatuzi wa migogoro kwa kulingalisha sheria ya utumishi wa umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) akisema wajibu wa Serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa wafanyakazi na ipo tayari kupokea maoni katika kuongeza uzalishaji kupitia uwekezaji.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya TUGHE, Archie Mntambo alileeza kwamba hivi sasa Chama hicho kina makakati wa kuboresha utendaji wake kuendana na teknolojia iliopo sasa pamoja na kutenga bajeti ya kuwezesha uwepo wa mfumo huku akisisitiza wanachama kuendeleza amani iliyopo ndani ya chama na demokrasia.

“Tunategemea kuwa na vitega uchumi yakiwemo majengo kuanzia Dodoma na tunatarajia kuwa na kamati ya maadili ya viongozi na wanachama pia kusimamia masuala ya rushwa tuwe na TUGHE safi na imara tunaahidi kuendeleeza amani iliyojengeka kwa thamani kubwa,”alifafanua Mwenyekiti huyo.

Katika hatua nyingine alikipongeza Chama hicho kwa kushiriki vyema katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Homa kali ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona akibainisha kwamba ni ugonjwa ulioikumba Dunia hivyo inahitajika nguvu ya pamoja kukabili maradhi hayo.

Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri nchini Bi.Pendo Berege alipongeza Chama cha TUGHE kwa kuheshimu Katiba na kuamua kufanya uchaguzi huo muhimu unaobeba mustakabali wa chama na Taifa kwa ujumla akiwasihi wajumbe kuchagua viongozi bora.

Mbali na hayo rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA),Tumaini Nyamhokya aliwahimiza wanachama na viongozi wa TUGHE kuepuka mipasuko ndani ya Chama inayosababisha kudorora kwa utendaji kazi hivyo kutumia muda mwingi kutatua migogoro badala ya kutimiza majukumu yao.

Aidha Katibu Mkuu Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Bwa. Hery Mkunda alisema Chama hicho kitaendelea kumuunga mkono Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwaletea wananchi maendeleo na Chama kutumika kama nyenzo ya hamasa kwa wafanyakazi kujituma na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.
 
 

RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA SHIRIKA LA LEGAL SERVICES FACILITY DODOMA

$
0
0


Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility, Lulu Ng’wanakilala akizungumzia programu ya upatikanaji wa haki inayotekelezwa na shirika lake mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kutembelea banda la maonyesho la LSF wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali unaofanyika Jijini Dodoma.



 
 

 

6000 WAPATIWA CHANJO YA COVID - 19 JIJI LA TANGA

$
0
0

 

Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe akizungumza wakati wa semina hiyo
MWAKILISHI wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi kutoka Dodoma Mwita Waibe akizungumza wakati wa semina elekezi kwa watumishi wa Afya Jijini Tanga na waandishi wa Habari kuhusu Ugonjwa wa Covid 19 iliyofanyika Jijini Tanga kulia ni Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga Charles Mkobe

Afisa Afya wa Mkoa wa Tanga  Jumanne Magoma akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo



NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MGANGA Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe amesema kwa mujibu wa takwimu zao mpaka Septemba 27 mwaka huu walikuwa wamechanga chanjo ya Uviko watu 6000.

Mkombe aliyasema hayo  wakati wa semina elekezi kwa watumishi wa Afya Jijini Tanga  na waandishi wa Habari kuhusu Ugonjwa wa Covid 19 iliyofanyika Jijini Tanga

Alisema  kampeni ya Kitaifa ya kuharakisha utoaji wa chanjo ya uviko 19 itasaidia kutokana na kama dunia imekumbwa na janga kubwa na lina madhara makubwa na watu wengi wameungua korona na wengine wamefariki.

Aidha alisema ugonjwa huo umeleta changamoto ya matumizi ya dawa na vifaa tiba na ya kiuchumi maana kabla ya Korona watu walikuwa wanafanya biashara vizuri lakini sasa zimefungwa.

“Madhara ya Korona ni zaidi ya kiafya imegusa ishu za kijamii na kiuchumi na kumekuwa na ongezeo la gharama za vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya hospitali gharama zimepanda mara dufu”Alisema

Alisema ugonjwa huo umeleta mtikisiko mkubwa kwenye jamii  na watu wamekata tamaa wamekuwa ni waoga kuishi

Awali akizungumza Afisa Afya wa Mkoa wa Tanga Magoma alisema mkoa huo chanjo ya Uviko 19 ilikuwa inasua  walipokea dozi 35000 na walianza rasmi Agosti 3 mwaka huu na ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima  ilikuwa ya kusuasua kidogo kutokana na vituo vilivyofunguliwa kuwa vichache .

Alisema wana vituo zaidi ya 300 na vituo ambavyo vilikuwa vinatoa huduma ni 33 huku vituo vitatu kila Halmashauri na baadhi ya maeneo mengine kutoka kituo hadi wananchi walipo inabidi watembee umbali mrefu au wakalale huko karibu na vituo vya jiriani.

“Lakini pia kuchelewa kufikia lengo la uchanjaji na tuna lengo la kutazama mabadiliko walizopewa kumaliza kwenye muda uliowekwa”Alisema

Hata hivyo alisema sababu kubwa ni vituo kuwa mbalimbali na wananchi Lakini suala hilo limefanyiwa kazi na halmashauri hivi sasa zimefungua kliniki za mkoba lakini vituo vinavyotoa bila kujali vya serikali,vya umma au madhehebu ya dini vitakuwa vinatoa chanjo na elimu inaendelea kwa jamii ili kuona umuhimu wa chanjo kuweza kudhibiti ugoinjwa wa Uviko.

Hata hivyo kwa upande wake Mwakilishi  wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi kutoka Dodoma Mwita Waibe amesema hivi sasa Taifa litaendelea kutoa chanjo ya Uviko 19 kwa wananchi wake ili wasiendelee kupata madhara yatokanayo na ugonjwa huo.

Waibe Mwita ambaye pia ni Mkuu wa Msafara uliopo Tanga kuhamasisha suala la chanjo ya UVIKO 19 kwa mkoa wa Tanga Mwita Waibe ambapo alisema madhara hayo ni yaliyojitokeza huko nyuma wakati chanjo haikuwepo.

Alisema Taifa limejiridhisha kwamba chanjo hizo ni salama na hazina madhara ya aina yoyote hivyo wananchi wahakikisha wanajitokeza kupata chanjo hizo.

Aidha alisema wanaendelea kuangalia hali upokeaji umekuwaje na changamoto kubwa kutokana na kwamba mikoa inatofautiana kwa hiyo katika ngazi ya Taifa ikaona ni vizuri kuwafikia wananchi kuanzisha zoezi la kushawisha kuharakisha uhamamsisha kwa wananchi ili waweze kupata uelewa

Alisema wataendelea kufanya utafiti kama serikali kuona uchukuaji wa chanjo na upokeaji  baada muda wanakaona kuna changamoto kubwa ni suala pamoja wapo ni upatikanaji wa chanjo karibu na wananchi na elimu ni changamoto hayo ndio maana wameamua kutengeneza kampeni harakishi kuhakikisha wananchi wanapewa elimu.

“Lakini kuhakikisha chanzo zote zilizokuwa zikitolewa kwenye vituo vichache zinatolewa kwenye vituo vyote vya kutoa huduma ya afya”Alisema

Awali akizungumza Afisa Afya wa Mkoa wa Tanga Magoma alisema mkoa huo chanjo ya Uviko 19 ilikuwa inasua  walipokea dozi 35000 na walianza rasmi Agosti 3 mwaka huu na ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima  ilikuwa ya kusuasua kidogo kutokana na vituo vilivyofunguliwa kuwa vichache .

Alisema wana vituo zaidi ya 300 na vituo ambavyo vilikuwa vinatoa huduma ni 33 huku vituo vitatu kila Halmashauri na baadhi ya maeneo mengine kutoka kituo hadi wananchi walipo inabidi watembee umbali mrefu au wakalale huko karibu na vituo vya jiriani.

“Lakini pia kuchelewa kufikia lengo la uchanjaji na tuna lengo la kutazama mabadiliko walizopewa kumaliza kwenye muda uliowekwa”Alisema

Hata hivyo alisema sababu kubwa ni vituo kuwa mbalimbali na wananchi Lakini suala hilo limefanyiwa kazi na halmashauri hivi sasa zimefungua kliniki za mkoba lakini vituo vinavyotoa bila kujali vya serikali,vya umma au madhehebu ya dini vitakuwa vinatoa chanjo na elimu inaendelea kwa jamii ili kuona umuhimu wa chanjo kuweza kudhibiti ugonjwa wa Uviko.



SHIRIKA WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI LA PEACE CORPS LASHEREKEA MIAKA 60 NCHINI TANZANIA

$
0
0

Dar es Salaam –

Shirika Wafanyakazi wa Kujitolea wa Kimarekani la Peace Corps, limesherehekea miaka 60 toka kuwasili kwa wafanyakazi wake wa kujitolea wa kwanza nchini Tanzania kwa hafla fupi iliyofanyika jana jioni na kuhudhuriwa na mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula.

Katika hotuba yake, Waziri Mulamula alisema kuwa madhimisho haya ya miaka 60 ya kuwasili kwa Wafanyakazi wa kwanza wa Kujitolea wa Peace Corps ni kielelezo na hatua muhimu katika ushirikiano kati ya serikali na watu wa Marekani na serikali na watu wa Tanzania.

“Maadhimisho ya leo yanadhihirisha hatua nyingine muhimu katika uhusiano rasmi, wa kihistoria na kirafiki baina ya nchi zetu,” alisema Mulamula.

Rais wa Marekani John F. Kennedy alianzisha Peace Corps mwaka 1961, akiwapa changamoto vijana wa Kimarekani kuhudumia wanadamu wengine kwa kufanya kazi kwa ajili ya amani na maendeleo katika nchi nyingine duniani kote. Kwa sababu ya urafiki wa karibu kati ya Kennedy na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Tanzania (wakati huo ikiitwa Tanganyika) ilichaguliwa kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kabisa duniani kupokea Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps. Tarehe 29 Septemba 1961, Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 50 waliwasili mjini Arusha, Tanzania.

Toka wakati huo, takriban Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 3,200 wamefanya kazi sambamba na wenzao wa Kitanzania katika mikoa 22 nchini, wakifuta ufumbuzi utokanao na jamii zao, kutanzua changamoto katika elimu, afya, kilimo, mazingira na maendeleo ya vijana.

Kwa mujibu wa Waziri Mulamula, wafanyakazi hawa wa kujitolea wamechangia pakubwa katika maendeleo ya Tanzania.

“Tunatoa shukrani kwa Wamarekani waliofanya kazi bila kuchoka na wafanyakazi wenzao wa Kitanzania katika maeneo ya vijijini kabisa katika nchi yetu wakiwa walimu wa hesabu na sayansi katika shule za sekondari, wakufunzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano, viongozi katika miradi ya kutoa elimu ya afya kwa umma na viongozi katika miradi ya mazingira inayolenga kukidhi mahitaji ya msingi kabisa katika ngazi ya kijiji ya usimamizi endelevu wa maliasili. Shukrani ziwaendee viongozi wetu wenye maono, Mwalimu Nyerere na rais John F. Kennedy wa Marekani kuwezesha program hii kuwepo,” alisema Mulamula.

Katika hotuba yake, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright alisisitiza kuwa Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wahaohudumu nchini Tanzania nao pia wamepata mabadiliko chanya kutokana na uzoefu wao huo.

“Baada ya miaka miwili ya kufanya kazi bega kwa bega na wenzao wa Kitanzania, wakila pamoja, wakicheka na kujifunza utamaduni wa kila mmoja wao, wafanyakazi wa kujitolea hubadilika milele na huibeba Tanzania mioyoni mwao popote waendapo,” alisema Balozi Wright.

Aidha, Balozi Wright alitoa shukrani kwa serikali na watu wa Tanzania kwa kuisaidia programu ya Peace Corps katika miongo sita iliyopita.

“Kwa dhati kabisa ninapenda kuwashukuru watu wa Tanzania na Serikali katika ngazi zote kwa msaada mkubwa uliotolewa kwa programu na wafanyakazi wa kujitolea katika miaka hii yote. Ninapenda pia kuzishukuru familia na jamii zilizowapokea na kuishi na wafanyakazi wa kujitolea kwa miaka hii yote. Ni kwa sababu yenu, Wafanyakazi wa kujitolewa waliweza kujifunza kikamilifu na kunufaika na utamaduni na ukarimu wa Kitanzania,” alisema.

Kutokana na changamoto zilizojitokeza kutokana na janga la kidunia la UVIKO 19, hivi sasa hakuna Mfanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps anayehudumu nchini. Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps nchini Tanzania, Stephanie Joseph de Goes alisema kuwa ana matumaini kuwa wafanyakazi wa kujitolea watarejea mwaka 2022.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa barua pepe: DPO@state.gov

MTALAAM MAGONJWA YA AKILI ASHAURI WATANZANIA KUJENGA UELEWA KUHUSU TATIZO LA USONJI KWA WATOTO

$
0
0


Na Khadija Seif, Michuzi TV

WATANZANIA wameshauriwa kujenga uelewa kuhusu  tatizo la usonji kwa watoto ili kutengeza uhusiano mzuri na watoto wenye tatizo hilo kwa lengo la kuwasaidia  katika masuala mbalimbali yakiwemo kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.

Ushauri huo umetolewa leo Septemba 30 mwaka huu na Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Chuo Kikuu  Kishiriki cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Dk.Said Kuganda wakati wa semina ya kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusiana na tatizo hilo.

Ambapo amesema jamii ya watoto wenye usonji wamekuwa na wakikutana na changamoto kutokana na  kuzungukwa na watu wasio na uelewa wa tatizo hilo hali inayopelekea wakati mwingine kutengwa bila sababu.

Ameongeza kutokana na hilo, imekuwa shida kwao kupata matibabu ambayo kama jamii wakiwemo baadhi ya wazazi wangekuwa na elimu juu ya tatizo hilo wangeweza kuwasaidia katika  makuzi yao.

" Chanzo cha tatizo hilo  hakijajulikana, zaidi imeonyesha kuwa wanaopatwa na usonji akili zao hushindwa kutengeneza mahusiano na jamii inayomzunguka na wakati mwingine kuwa na tabia za kujirudia rudia" amesema Dk.Kuganda."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya 'Lukiza Autism Foundation' iliyoandaa semina hiyo, Hilda Nkabe amesema tatizo la usonji ambalo zaidi kuonekana kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano, linahitaji kutolewa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuleta mabadiliko.

Aidha,Nkabe amefafanua kimsingi mtoto mwenye usonji huwa na dalili zinazotofautiana na hivyo wakati mwengine kumsababishia mtoto mwenye tatizo hilo kufanya vitendo vya kumkwaza mtu mwingine jambo ambalo huitaji ukaribu na uelewa wa watu walio karibu naye.

Na katika kujenga uelewa kwa jamii kuhusu tatizo hilo, taasisi yake imeandaa hafla maalumu inayotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine itatumika kutoa elimu na hivyo kuondoa hali ya sintofahamu katika jamii.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya Dk.Mengi Foundation (DRMF) Shimimana Ntuyabaliwe ameeleza kuna haja kwa jamii kutanguliza utu wakati wa kutamka majina ya watu wenye ulemavu kwa lengo la kuweka usawa.

Daktari Bingwa wa afya na Magonjwa ya akili wa hospitali ya Taifa Muhimbili,Said Kuganda akifafanua zaidi katika semina iliyowajumuisja Waandishi Wahabari pamoja na wataalam wa afya ya akili,kuwa Kuna haja ya jamii kupewa Elimu ya uelewa kuhusu Magonjwa ya akili
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza Autism akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa kutoa semina kwa Waandishi Wahabari jijini Dar es salaam huku akiwataka jamii kuelewa jinsi ya kuwasaidia watoto wenye Matatizo ya akili (Usonji)
 Baadhi ya sehemu ya Waandishi Wahabari wakisikiliza kwa umakini semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Lukiza Autism Foundation

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATAJWA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TAIFA

$
0
0

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima kizungumza katika mkutano wa Mashirika yasiyo ya kiserikali leo Jijini Dodoma ambapo uliambatana na semiana elekezi kwa watendaji na wadau wa mashirika hayoWashiriki na wamiliki wa NGOs wakiwa katika mkutano wa mwaka wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma leo.29/30/2021.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakiwa katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Mkutano ukiendelea katika kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete leo Jijini Dododma ambapo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima.


Na.Vero Ignatus,Dodoma

Mkutano mkuu wa mwaka Mashirika yasiyo ya kiserikali unaofanyika jijini Dodoma ukiwa umebeba kauli mbiu isemayo "kuimarisha mchango wa NGOs katika maendeleo ya Taifa" ,umeshirikisha wadau kutoka Tanzania bara na Zanzibar


Akitoa salamu kwa mgeni rasmi muwakilishi wa NGO Bungeni Neema Lugangira alisema kuwa anaiomba serikali kupitia wizara ya afya kuangalia vyema suala la kanuni mpya za NGO kwenye eneo ambalo linataka kabla ya kufanya kazi yeyote kwamba NGO inatakiwa kupata kibali kutoka hazina wizara ya fedha jambo ambalo linachelewesha utekelezaji wa kazi za taasisi husika,kwani wakati mwingine mradi huo unatakiwa kutekelezwa ndani ya miezi sita.

Nashukuru sana kamati ya bunge ya sheria ndogo waliridhia ombi hilo na walitoa maelekezo kwamba wizara iweze kupitia mapendekezo hayo,kipekee nimshukuru sana Spika wa Bunge Job ndugai ambae alikazia umuhimu wa kufanya mapitio ya kanuni hizi kuhakikisha kuwa wanaweka mazingira wezeshi kwa ajili ya ustawi wa taasisi husika,hivyo ni matamanio yangu katika mkutano huu tutapata mwelekeo wa lini kipengele hiki kitapata maboresho ili kiletwe bungeni ili na sisi tuweze kufanya uchakataji na kufanya kazi husika.alisema Neema

Aidha alitoa ombi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba alipokuwa kwenye mkutano wa 76 wa baraza kuu la umoja wa mataifa alielezea dira yake na dhamira yake kwamba tunaongeza nafasi za wanawake kwenye uongozi usawa wa kijinsia na kufikia 50 kwa 50 na jambo hili amakekuwa akilisema mara nyingi

Hivyo ni ombi langu kwa mhe.Rais kwamba tufanye mapitio ya na maboresho ya kanuni za uchaguzi ndani ya ccm na katiba ya CCM ili kuwepo na kipengele kinachoelekeza ya kwamba katika nafasi za wagombea asilimia 30% ya wagombea wawe ni wanawake.

"Mashirika haya yamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo tunayojivunia ya Taifa la Tanzania" alisema Neema.

Hata hivyo ametoa wito kwa mashirika hayo kufanya kazi kwa Ueledi ,Uadilifu pamoja na upande wa serikali uimarike katika kufanya kazi kwa weledi,

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wajumbe wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima, amempongeza mbunge huyo kwa jitihada kubwa alizozifanya kwa nafasi yake bungeni, kwa lengo la kuimarisha utendaji wa Asasi za Kiraia kwa kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji hali inayoonekana kubadili mwelekeo wa utendaji kazi

Akifafanua juu ya masula ya Kodi Bwana Matenus Mallya, amesema Mamlaka ya mapato Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Asasi za Kiraia, wamekuwa wakichangia Pato kubwa Serikalini isipokuwa wengi wamekuwa hawatambui ni mapato yapi wanapaswa kuchangia, mchango mkubwa wa asasi za Kiraia inakwenda moja kwa moja katika ngazi ya Jamii na kupelekea kuongezeka kwa idadi kubwa ya walipakodi wa hiyari.

Kupitia mfumo wa ulipaji Kodi, na usajili wa mlipa Kodi, kwa kila Taasisi ili kuweza kukidhi vigezo ili Asasi zinazofikia muzo ghafi ya zaidi ya 14 milioni kuweza kusajiliwa kwa kupata EFD mashine.

Kuhusu ombi la Charitable status, Bwana Octavian Machenje vigezo anavyotazama Kamishina wa mapto, kinatokana na Sheria ya Kodi ya mapato katika kifungu Cha 64, ambapo Sifa muhimu ni, maudhui ya Katiba, shughuli zinazofanyika katika taasisi pamoja uwanda wa kazi unazozifanya katika taasisi husika.

Akizungumza Utaratibu wa kuingia Nchini kwa wageni wanaokuja kufanya kazi za NGO bwana Amon Kamoga amesema Sheria imeweka utaratibu wa vibali vya mda mfupi kwa siku 90 (visa au Pasi) na muda mrefu kwa zaidi y siku 90 kibali cha ukazi kwa kuangalia vigezo vya shughuli unayokuja kufanya kazi nchini, pamoja na mtu mwenyewe anyeomba kibali kutokana na mahali anapotoka.

Aidha wajumbe wa mkutano wanatarajiwa kukutana na mh Rais Samia Suluhu Hassan ambaye atahutubia mkutano huo wa siku mbili ulioanza na semina elekezi kwa katika masuala mbalimbali.

RAIS SAMIA AONGOZA WATANZANIA KUAGA MWILI WA HAYATI OLE NASHA JIJINI DODOMA

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Watanzania kuaga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Sept 30,2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha wakati wa kuaga mwili wa Naibu Waziri huyo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

PICHA NA IKULU

BENKI YA ABSA TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO KWA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA AT TAAUN.

$
0
0

 

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Melvin Saprapasen (kushoto), akimkabidhi vitanda na magodoro Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya At – Taaun,  Ali Betit kama sehemu ya majukumu ya benki kutoa kwa jamii kufuatia na uhitaji wa shule hiyo baada ya ajali ya moto kuteketeza thamani vikiwemo vitanda na magorodo hivi karibuni. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Morogoro hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha biashara kutoka Benki ya Absa Tanzania Melvin Saprapasen (wa pili kulia), akizungumza kabla hajakabidhi vitanda na magodoro kwa Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya At – Taaun,  Ali Betit (kulia kwake), kama sehemu ya majukumu ya benki kutoa kwa jamii kufuatia na uhitaji wa shule hiyo baada ya ajali ya moto kuteketeza thamani vikiwemo vitanda na magorodo. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Morogoro jana.  
 Meneja Huduma za Kijamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria (kushoto), akitoa salamu za pole kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya At – Taaun kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza vitanda na magodoro ambapo benki hiyo imekabidhi vitanda 15 na magodoro ili kupunguza kero wanazokumbana nazo wanafunzi baada ya ajali hiyo. Ilikuwa ni katika hafla ya kukabidhi msaada huo shuleni hapo, mjini Morogoro, jana.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wasichana ya At – Taaun iliyopo manispaa ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Absa Tanzania na viongozi wa shule hiyo mara baada ya kupokea msaada wa vitanda na magodoro vilivyotolewa na Absa shuleni hapo jana.

Vitanda vilivyotolewa msaada  na Benki ya Absa Tanzania kwa Shule ya Sekondari ya wasicha At – Taaun iliyopo Manispaa ya Morogoro baada uhitaji mkubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo kutokana ajali ya moto iliyoteketeza mali za wanafunzi, vitanda na magodoro hivi karibuni. Picha hii imepigwa wakati wa makabidhiano ya vitanda hivyo shuleni hapo, Morogoro jana.

 

 

Viewing all 119151 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>