TANESCO SIMIYU NA KITENGO CHA MASOKO MAKAO MAKUU WATOA ELIMU KATIKA VIJIJI VINAVYOFADHILIWA NA REA
UTSHEGO BANK TANZANIA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIDIGITALI ZAIDI
TANZANIA ni kati ya nchi ambayo inatumia vema huduma za kidigitali kwenye sekta ya fedha ambapo kwa sasa imekuwa siyo tena mapinduzi tu ya mifumo ya kidigitali bali ni sehemu ya maisha ya kila siku ya huduma za kifedha nchini.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za Letshego Group yenye makao yake makuu nchini Botswana, Andrew Fening katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini kuhusiana na huduma za kibenki za benki hiyo ambapo ilibainisha kuwa Tanzania inaendana na maendeleo ya kidigitali sekta za Fedha huku akitaka kubuniwa kwa njia sahihi zitakazomwezesha mteja kupata huduma kwa ukaribu, uharaka na urahisi.
Akizungumzia kuhusiana na huduma hiyo, alisema itamwezesha mtumiaji kupata huduma za taarifa mbalimbali za mikopo, kufanya mihalamala na kupata huduma nyingine za kifedha kwa haraka.
Alisema:” kutokana na changamoto kadhaa kama vile ugonjwa wa covid kwa sasa kuna uhitaji wa kuja na mikakati kama hii ya kushughulikia huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali ili kuwawezesha wateja kutosongamana wakati wa kupata huduma.
"Kwa sasa wanaweza kupata huduma kwa njia ya simu zao za mkononi au televisheni na tena wakanufaika kwa haraka na ufanisi zaidi huku wakiwa wamejirinda na ndiyo maana Letshego imekuwa karibu zaidi kuwahudumia wateja wake kibunifu.”
Alisema kuwa, benki hiyo itaendelea na utamaduni wake wa kutumia zaidi matumizi ya mifumo ya kidigitali hasa huduma ya LetsGo katika kuwaunganisha wateja wake ili waendelee kufurahia huduma.
Alisema,“Kwa sasa LetsGO platform inaweza kupatikana kupitia simu ya mkononi na tovuti ambapo mteja ataweza moja kwa moja kuingia kwenye akaunti yake na kuendelea kujipatia huduma kama za mikopo, taarifa mbalimbali na huduma nyinginezo kwa Botswana na Nigeria”.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Letshego Tanzania, Andrew Tarimo, alibainisha kuwa muda mfupi ujao wateja wa Taasisi hiyo hapa nchini wataanza kunufaika na ubunifu huo wa kidigitali wa kupitia huduma ya Lets Go ambayo itawaunganisha na wateja wengine Afrika.
“Kwa pamoja tutumie fursa zinazopatikana kwenye huduma hii ya kidigitali ya LetsGo kukua pamoja kwa kuwa ndipo dunia inapoenda na Afrika ya baadaye yenye matumizi bora ya kidigitali inaanza sasa.” alisema Andrew Tarimo.
Walisema kuwa huduma hiyo itaendelea pia kwa nchi nyingine tisa za Afrika huku akibainisha kuwa lengo la huduma hiyo ni kuhakikisha kuwa itatumika kama njia sahihi na salama ya kidigitali kwa taasisi hiyo.
CEO Letshego Bank Tanzania, Andrew Tarimo
Serikali imesisitiza nia yake kuendelea kujenga, kuboresha na mazingira wezeshi kwa NGO's
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao akitoa maelezo mafupi kuhusu Mkutano wa mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Jijini Dodoma katika Mkutano wa Mwaka wa Mashirika hayo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akitoa tuzo kwa mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya mpito ya Uratibu Uchaguzi wa NaCONGO Francis Kiwanga, katika Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (WAMJW)
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali imesisitiza nia yake kuendelea kujenga, kuboresha na mazingira wezeshi kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kufanya kazi kwa ufanisi na kuchochea Maendeleo ya Taifa.
Akifungua Mkutano wa Mwaka wa Mashirika hayo Jijini Dodoma ,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na NGOs katika kuisaidia Serikali ili kuwaletea wananchi Maendeleo.
"Mashirika yanakwenda hatua kwa hatua na Serikali na hata Maendeleo haya tuliyonayo na hapa tulipofika ni kutokana na mchango mkubwa wa Mashirika haya" amesema Waziri Gwajima.
Mhe. Gwajima ameongeza kuwa Mkutano huo ni fursa muhimu ya kujadiliana masuala mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo kuyajengea uwezo Mashirika hayo kuhusu sheria na kanuni zinazoongoza NGOs na Serikali pia kufahamu changamoto na shughuli zinazofanywa na NGOs ili kuwa na uelewa wa Pamoja.
Aidha, Mhe. Gwajima ametoa wito kwa NGOs kuimarika kwa kufanya kazi kwa weledi na uzalendo, kufuata sheria na kanuni zake kwa manufaa ya Taifa na kwamba Serikali ipo tayari kupokea maoni na changamoto kupitia Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaani NaCONGO.
Amesisitiza kuwa, NGOs zifanye kazi kwa uwazi na uwajibikaji kwenye mipango yao ya kila mwaka hususani kuanzia kwenye maeneo wanayofanyia kazi.
Amesema hatarajii kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya sheria kutoka pande zote za Serikali na Mashirika na kuwe na mifumo ya kujiratibu katika kuisaidia Jamii kutatua changamoto kwa kushirikiana na Jamii zinazowazunguka.
Mhe. Waziri ametumia fursa hiyo pia kuyahimiza Mashirika hayo kushirikiana na watendaji kwenye maeneo yao kuhakikisha elimu ya chanjo ya UVIKO 19 inatolewa kwa kina, ili wananchi wajitokeze kwa hiyari kuchanja.
"Nia ya Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuona Taifa lipo salama kwa kutekeleza afua za kinga ikiwemo chanjo kwa hiyari na dawa ni kuwa na elimu ya kutosha, hivyo Wadau niwakumbushe kushirikiana na wataalamu wa Afya kusimamia na kuwezesha elimu ya kutosheleza kwa wananchi ili suala la hiyari lifanyike" ameongeza Dkt. Gwajima.
Waziri Gwajima pia ametoa tuzo kwa baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyofanya vizuri hasa kwa upande wa kuzalisha ajira nyingi kwa Watanzania yakiongozwa na CCBRT na Marie Stopes.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Dkt. Lilian Badi amempongeza Waziri Gwajima Kwa kufanikisha uchaguzi wa NaCONGO na kusema kuwa ni wakati wa kufungua macho na kuboresha utendaji kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kuongeza Kasi ya Maendeleo.
Awali akiwasilisha maelezo kuhusu Ofisi yake na huduma za uratibu na usajili, Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao amesema lengo la Mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa NGOs na Serikali kwa kujadiliana changamoto zilizopo na namna ya kuzitatua kwa kuzingatia Sheria na Sera zilizopo.
Aidha, Mkutano umelenga kutambua na kujadili mchango wa NGOs katika Maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira ameiomba Serikali kufanya mapitio ya kanuni ya fedha ya NGOs kuwezesha kupata vibali mapema ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
MAWAKILI , OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI WANOLEWA KISHERIA
Mafuzo hayo ya siku mbili yaliyofadhiliwa na kampuni hiyo ya AG ya Dubai yenye makao yake Makuu nchini Uingereza na PLO yameendeshwa na wakurugenzi wa AG, Alex Sarac na Bevan Farmer. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mawakiliwa Serikali wa ofisi ya wakili Mkuu wa serikali.
Akiongea baada ya mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa PLO ambaye ni mshirika Mkuu (Mbia) wa kampuni hiyo ya Ag Amani Tenga amesema, mafunzo hayo yameenda vizuri na wanaimani mawakili wa serikali wameongeza ujuzi.
WALIOKIUKA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA WAKALIA KUTI KAVU
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba, wakifungua ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2020/21, kushoto ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA, Prof. Ninatubu Lema, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba, ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2020/21, kushoto ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akitoa agizo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi na uchunguzi wa kina kwa Taasisi tano zilizofanya vibaya katika shughuli za manunuzi ili kubaini tatizo lililosababisha Taasisi hizo kufanya vibaya kwenye mchakato wa manunuzi baada ya kupokea ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), jijini Dodoma.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Prof. Ninatubu Lema, akieleza mafanikio ya matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao (TANePS), wakati akiwasilisha ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kutoa ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2020/21, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Sera ya Ununuzi wa Umma, Bw. Alex Araba, ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2020/21, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kulia) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA, Prof. Ninatubu Lema wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine kutoka PPRA na Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2020/21, jijini Dodoma.
……………………………………………………
Na: Josephine Majura na Alice Nyange WFM – DODOMA
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufazifanyia ukaguzi na uchunguzi wa kina Halmashauri 4 za Wilaya na Taasisi moja ya Serikali kwa kukiuka Sheria za Ununuzi wa Umma.
Dkt. Nchemba alitoa maagizo hayo baada ya kupokea Ripoti ya Tathimni ya Utendaji ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ya Mwaka wa Fedha 2020/2021, jijini Dodoma.
Dkt. Mwigulu amesema kuwa uchunguzi lazima ufanyike ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watu wote watakaobainika kukiuka taratibu za ununuzi ikiwemo kutoa zabuni nje ya mfumo wa kieletroniki wa TANePS unaotumika kuchakata zabuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma PPRA, Profesa Ninatubu Lema kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA Prof. Marten Lumbanga, Taasisi tano zilizopata wastani hafifu wa kufuata sheria taratibu na kanuni za ununuzi wa umma kuwa ni Halmashauri ya Mji Kondoa, Halmashauri ya Mbogwe, Halmashauri ya Biharamulo, Halmashauri ya Chato na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama.
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kuziandikia waraka Taasisi 172 ambazo zimeunganishwa kwenye Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao (TANePS) watoe sababu za kutotumia mfumo huo katika kufanya ununuzi.
Alizitaka pia Taasisi nunuzi zote kutumia asilimia 30 ya gharama yote ya zabuni zinazotangazwa katika mpango wao wa ununuzi wa mwaka kwa ajili ya kuyawezesha makundi maalumu yakiwemo ya vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu kwa mujibu wa Sheria ya ununuzi.
“Nimesikitika sana baada ya kusikia kwamba kati ya Taasisi 86 mlizozikagua ni Taasisi mbili tu ndizo zilitenga asilimia 30 katika mpango wao wa ununuzi wa mwaka kwa ajili ya makundi maalumu,” alisisitiza Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Mjumbe na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Prof. Ninatubu Lema, alisema kuwa katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 walifanya ukaguzi wa mikataba 8,838 ya ununuzi yenye thamani ya Sh. trilioni 9.2 kutoka Taasisi 86.
Prof. Lema alifafanua kuwa matokeo ya ukaguzi huo yalionesha kuwa Taasisi 130 kati ya 718 zilizounganishwa kwenye mfumo wa Ununuzi wa TANePS hazikuwasilisha mipango yao ya ununuzi kupitia mfumo huo huku Taasisi 208 ziliwasilisha mipango yao kupitia mfumo huo lakini zikachakata zabuni nje ya mfumo hali inayoashiria kuwepo kwa vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, alimhakikishia Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango kwamba atafuatilia maelekezo aliyopewa na kuwawajibisha wale wote watakaobainika kuhusika na ukiukaji wa Sheria ya ununuzi na pia kuangalia uwezo wao wa utendaji kazi na namna ya kuwajengea uwezo.
Alisema kuwa ni muhimu taasisi za umma zikazingatia sheria, taratibu na kanuni za ununuzi wa umma ili kuthaminisha miradi ya maendeleo na fedha zinazotumika kwani sekta ya ununuzi inatumia kiasi kikubwa cha Bajeti ya Serikali ambapo kwa mwaka 2020/2021, bajeti ya ununuzi ilikuwa shilingi trilioni 25 sawa na zaidi ya asilimia 75 ya Bajeti yote ya Serikali.
Bw. Tutuba alisema kuwa Mfumo wa ununuzi wa TANePS unaleta uwazi na uwajibikaji katika ununuzi ili fedha za umma zinazotolewa na Serikali ziweze kuleta manufaa kwa wananchi.
MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA OLE NASHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Marehemu William Ole Nasha mara alipofika nyumbani kwa marehemu Medeli – Jijini Dodoma. (Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango) Septemba 29,2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akimfariji Bi. Asha Mlekwa mke wa marehemu William Ole Nasha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji alipofika nyumbani kwa marehemu Medeli – Jijini Dodoma (Septemba 29,2021)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwafariji watoto wa marehemu William Ole Nasha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, alipofika nyumbani kwa marehemu Medeli – Jijini Dodoma (Septemba 29,2021)
………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiambatana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango hii leo Septemba 29, 2021 amefika nyumbani kwa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Marehemu William Ole Nasha kwaajili ya kutoa pole na kuifariji familia kufuatia kifo cha naibu waziri huyo kilichotokea Septemba 27,2021 nyumbani kwake Medeli Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais ameweka saini katika kitabu cha maombolezo na baadaye kuzungumza na Mke wa Marehemu Bi.Asha Abdallah Mlekwa ambapo amempa pole na kumuomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Baadaye akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani hapo, Makamu wa Rais ametoa pole kwa wote walioguswa na msiba huo. Mamaku wa Rais amemtaja Marehemu William Ole Nasha kama kiongozi aliyekuwa hodari katika kufanya kazi zake na kuzitimiza vema. Amesema ni wazi kwamba wananchi wa Ngorongoro wamepoteza kiongozi shupavu na mwema aliyekuwa akijitoa kuwasaidia.
Aidha Makamu wa Rais amesema ni vema kujifunza juu ya Maisha alioishi Marehemu William Ole Nasha kwani yamejaa mengi yaliomema ambayo vijana wanaweza kujifunza, kuyaishi na baadae kuleta mchango chanya katika jamii
MBEYA KUTENGA BAJETI YA UNYWAJI MAZIWA SHULENI





Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote zilizopo mkoani kwake kutenga bajeti ya maziwa kwa wanafunzi wote wa shule za awali na msingi waliopo mkoani humo.
Homera ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya unywaji maziwa shuleni ulimwenguni ambayo kitaifa imefanyika leo (29.09.2021) mkoani Mbeya amesema kuwa suala la unywaji maziwa shuleni kwa wanafunzi ni la lazima na si hiyari. “Hatuwezi kusubiri wadau tu kila siku wajitoa wakati watoto ni wetu wenyewe hivyo ni lazima wakati wa kupanga bajeti zote za halmashauri zilizopo mkoani Mbeya iwekwe bajeti ya kutekeleza mpango huu na kwa sababu mimi ndo naidhinisha bajeti zote,sitopitisha bajeti yoyote ambayo haina bajeti ya kutekeleza mpango huo” Amesema Homera. Aidha Homera amepongeza juhudi na kazi inayofanywa na Wizara ya mifugo na Uvuvi kupitia bodi ya maziwa kwa kuwa karibu na wadau mbalimbali wa tasnia ya maziwa waliopo mkoani humo ambapo amewataka wasindikaji wote wa maziwa nchini kuendelea kuwekeza katika mkoa huo. “Mimi ninapenda sana wawekezaji na kipekee kabisa niwashukuru ASAS kwa kuamua kuja kujenga kiwanda kikubwa cha maziwa hapa, niwaombe Tanga Fresh na makampuni mengine ya maziwa kufanya hivyo pia ili kuchochea zaidi uwekezaji katika tasnia ya maziwa katika mkoa wa Mbeya” Amesisitiza Homera. Akizungumzia hali ya uwekezaji kwenye tasnia ya maziwa nchini, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Stephen Michael amesema kuwa hadi sasa Tanzania ina jumla ya ng’ombe wa maziwa Mil. 1.2 ambao huzalisha jumla ya lita za maziwa Bil.3.1. “Aidha hadi kufikia Aprili 30 mwaka huu, Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda vya kusindika maziwa vikubwa, vidogo na vya kati 104 na kati ya hivyo 96 ndo vinafanya kazi” Amesema Michael. Akibainisha kuhusu uwezo wa uzalishaji wa viwanda hivyo, Michael amesema kuwa viwanda vilivyopo vina uwezo uliosimikwa wa kusindika lita 865600 kwa siku lakini kutokana na uhaba wa upatikanaji wa malighafi viwanda hivyo vinasindika wastani wa asilimia 24 ya uwezo wake ambao ni sawa na lita 206849 kwa siku. Akielezea kuhusu utekelezaji wa mpango wa unywaji maziwa shuleni, Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini (TDB) Dkt. George Msalya amesema kuwa mpango huo ulianzia mkoani Kilimanjaro mwaka 2007 kwa lengo la kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini kwa kujenga utamaduni huo kuanzia ngazi ya shule ya awali. “ Tunafanya hivi kwa sababu mbali na maziwa kuwa lishe nzuri na kiburudisho kwa watoto, imethibitika kuwa maziwa ni mlo kamili unaoweza kujitosheleza bila kutegemea chakula kingine na ndo chakula pekee chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini” Amesema Dkt. Msalya. Aidha Dkt. Msalya amebainisha kuwa tangu kuanza kwa mpango huo takribani watoto elfu 90 kutoka shule 210 hapa nchini wamepatiwa maziwa ambapo amesema kuwa idadi hiyo imeendelea kupungua kadri miaka inavyoendelea. “ Tunaendelea kufanya jitihada kubwa katika kuwajengea uwezo wanafunzi, wazazi na walezi wao juu ya umuhimu wa maziwa ili kuhakikisha kiwango cha matumizi ya bidhaa hiyo kinaongezeka” amehitimisha Dkt. Msalya. Maadhimisho ya Siku ya unywaji Maziwa mwaka huu yalitanguliwa na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na ugawaji maziwa katika vituo vya afya, mahabusu ya watoto na kwenye vituo vya watoto yatima.
WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA COMORO NCHINI, WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA MASUALA YA ULINZI NA USALAMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Balozi wa Comoro Nchini Tanzania, Dkt..Ahamada El Badaoui, katika kikao kilichojadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika ulinzi na usalama kati ya Serikali ya Tanzania na Comoro. Kikao hicho kilifanyika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimshukuru Balozi wa Comoro Nchini Tanzania, Dkt..Ahamada El Badaoui, kwa kumtembelea ofisini kwake baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyojadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika ulinzi na usalama kati ya Serikali ya Tanzania na Comoro. Kikao hicho kilifanyika jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
DG MPYA REA ATAKA UTENDAJI KAZI WENYE BIDII, MAARIFA NA UADILIFU
Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said (kulia) akipokea Kabrasha lenye taarifa mbalimbali kuhusu REA kutoka kwa Mtangulizi wake, Mhandisi Amos Maganga katika hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi, Dodoma, Septemba 29, 2021.
Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said akizungumza na wafanyakazi wa REA baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Mtangulizi wake Mhandisi Amos Maganga, Septemba 29, 2021 Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (kulia), akimtambulisha rasmi Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said kwa Wafanyakazi wa REA mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi, Septemba 29, 2021 Dodoma.
Mhandisi Amos Maganga akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) – (hawapo pichani), baada ya kukabidhi rasmi Ofisi kwa Mkurugenzi mpya wa REA, Mhandisi Hassan Said, Septemba 29, 2021 Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Said (wa tatu-kulia) na Mtangulizi wake, Mhandisi Amos Maganga (wa tatu-kushoto) baada ya makabidhiano rasmi ya Ofisi Septemba 29, 2021 Dosoma. Wengine pichani ni baadhi ya Wajumbe wa Bodi.
Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiimba wimbo wa ‘Mshikamano Daima’ wakati wa hafla fupi ya kumpokea Mkurugenzi mpya wa REA, Mhandisi Hassan Said na kumwaga Mtangulizi wake Mhandisi Amos Maganga (hawapo pichani), Septemba 29, 2021 Dodoma.
Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Said akipokea shada la maua kutoka kwa mfanyakazi wa REA, Eshimuni James, alipowasili rasmi Makao Makuu ya Ofisi hizo Dodoma, Septemba 29, 2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Elineema Mkumbo akimkaribisha (kwa niaba ya Menejimenti) Mkurugenzi mpya wa REA Mhandisi Hassan Said (kushoto) alipowasili rasmi Makao Makuu ya Ofisi hizo Dodoma, Septemba 29, 2021.
Mapokezi ya Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Said, alipowasili rasmi Makao Makuu ya Ofisi hizo Dodoma, Septemba 29, 2021.
………………………………………………………………………
Na Veronica Simba – REA
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said, amekabidhiwa rasmi Ofisi na Mtangulizi wake, Mhandisi Amos Maganga leo Oktoba 29, 2021 ambapo amewaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii, maarifa na uadilifu.
Mhandisi Said amesema matumaini ya Watanzania, hasa wa vijijini, yanategemea dhamana ambayo REA imepewa.
“Tukitetereka katika kutimiza majukumu yetu, tutafifisha matumaini ya Watanzania wengi ambao wanategemea nishati kama nyenzo ya kubadilisha maisha yao,” amesisitiza.
Aidha, Mkurugenzi huyo mpya wa REA amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini kuwatumikia Watanzania katika wadhifa huo na kuahidi kuwa hatamwangusha.
Vilevile, ametoa pongezi kwa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Kalolo, Mtangulizi wake Mhandisi Maganga pamoja na wafanyakazi wote wa REA kwa kazi nzuri iliyofanyika na kufikia hatua nzuri katika kusambaza nishati vijijini.
“REA ni miongoni mwa Taasisi za Umma ambazo zimefanya kazi kubwa sana na ambazo zimegusa maisha ya wananchi. Huwezi kupata mafanikio kama haya ikiwa hauna Bodi imara na yenye weledi mkubwa, Menejimenti nzuri na wafanyakazi wanaojituma,” amefafanua.
Sambamba na hayo, Mhandisi Said ameomba ushirikiano kutoka kwa Bodi, Menejimenti na Watumishi wote wa REA katika kutekeleza majukumu yake.
Awali, akizungumza baada ya kukabidhi rasmi Ofisi kwa Mkurugenzi mpya, Mtangulizi wake Mhandisi Maganga amemshukuru Mungu, Bodi na Wafanyakazi wote wa REA kwa kumpatia ushirikiano katika kipindi chote alichofanya kazi nao.
Mhandisi Maganga amebainisha kuwa mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya nishati vijijini, yanatokana na ushirikiano mkubwa alioupata kutoka kwao.
Amewataka kumpatia ushirikiano wa aina hiyo, Mkurugenzi mpya huku akibainisha kuwa yeye binafsi anamwamini na anamtambua kama mchapakazi na mwenye uhodari katika utendaji kazi.
Akizungumza kwa niaba ya Bodi, Mwenyekiti Wakili Julius Kalolo amempongeza Mhandisi Hassan kwa kuaminiwa na Rais na kuteuliwa kushika wadhifa huo mkubwa. Amemwahidi kuwa Bodi itampatia ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yake.
Vilevile, amempongeza na kumshukuru Mhandisi Maganga kwa ushirikiano alioutoa kwa Bodi katika kipindi chote alichofanya kazi katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.
Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa niaba ya Menejimenti ya REA na wafanyakazi wote, Kaimu Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti, Mhandisi Elineema Mkumbo, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Grace Sengula pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Tawi la REA, Swalehe Kibwana, wameahidi ushirikiano pamoja na kutekeleza yale yote aliyoyasisitiza Mkurugenzi mpya.
Mhandisi Hassan Said aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa REA kuanzia Septemba 23 mwaka huu akitokea Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) alikokuwa akifanya kazi kama Meneja Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki.
Mdau wa Elimu Hanang achangia mifuko 200 ya Saruji shule ya Msingi Bassotughang.
Mdau wa Maendeleo wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara Clentine Fissoo ameahidi kutoa mifuko 200 ya saruji kwa shule ya msingi Bassotughang kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.
Akizungumza kwenye mahafali ya 22 katika shule hiyo mdau huyo amesema ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na changamoto ya miundombinu ya shule hiyo.
Fissoo ameueleza uongozi wa shule ya msingi kuwasiliana nae muda wowote ili kupatiwa mifuko hiyo ya Saruji.
Hata hivyo amesema kuwepo kwa miundombinu rafiki katika shule hiyo kutaongeza ari ya wanafunzi kusoma na kuongeza ufaulu.
Risala iliyoandaliwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu Antony Marwa imeeleza kuwa shule hiyo ina wanafunzi 589 wakiwemo wavulana 237 na wasichana 352 wakianzia darasa la awali hadi la saba.
Sehemu ya risala hiyo imeendelea kueleza kuwa shule ina upungufu wa miundombinu mbalimbali ambapo ina nyumba nne za walimu kati ya tisa zinavyohitajika, madarasa kumi kati ya 14 yanayopaswa kuwepo,matundu nane ya vyoo vya wanafunzi kati ya 22 yanayohitajika huku nane yaliyopo yakikosa sifa kwa kuwa haajakidhi vigezo husika kwani havina milango na kimo cha paa ni kifupi.
Changamoto nyingine inayoikabili shule hiyo ni ukosefu wa kabati la kuhifadhia vitabu hivyo vitabu kusalia kwenye maboksi na kupelekea kuharibiwa na mchwa na panya. Jumla ya wanafunzi 54 sawa na asilimia 71 wamehitimu elimu yao ya msingi katika shule ya Bassotughang huku 22 asilimia 29 wakishindwa kumaliza darasa la saba kutokana na sababu mbalimbali.
RAIS DKT.MWINYI ASHIRIKI MKUTANO WA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI YA KIKRISTO ZANZIBAR.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini ya Kikristo alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar kwa ajili ya Mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo.[Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiteta na baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kikristo kabla ya Mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo katika Ofisi ya Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Baadhi ya Masister na Viongozi wengine wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo ni miongoni mwa washiriki wa mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar mgeni rasmi alikuwa rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.[Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Baadhi ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.alipokuwa akizungumza na Viongozi hao katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar [Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar [Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar [Picha na Ikulu] 29/09/2021.
Baadhi ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo wakifurahia hotuba iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.alipokuwa akizungumza na Viongozi hao katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar [Picha na Ikulu] 29/09/2021.
RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA UINGEREZA MHE.TONY BLAIR IKULU CHAMWINO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo Sept 29,2021. PICHA NA IKULU.
TRY AGAIN BOSI MPYA SIMBA SC, MO DEWJI ATANGAZA KUKAA PEMBENI
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MWEKEZAJI na Mwanahisa wa Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji (MO Dewji) ametangaza kuachia ngazi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi wa Klabu hiyo badala yake amemtaja Makamu Mwenyekiti, Salim Abdallah (Try Again) kuwa mrithi wake.
MO Dewji ametangaza kuachia nafasi hiyo mapema leo kupitia ukurasa wake rasmi Instagram kwa kuweka kipande kifupi cha video kikimuonesha akitoa kauli hiyo. Amesema amefanya uamuzi huo kutokana na yeye muda mrefu kusafiri nje ya nchi.
“Makubaliano yaliyofikiwa Septemba 21, 2021 tukikubaliana kuwa Mwenyekiti wa Bodi uwepo wake muda wowote katika kuiongoza Klabu ni muhimu, hivyo kwa makubaliano hayo namteua Salim Abdallah kuanzia sasa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC”, amesema MO Dewji.
Pia amesema licha ya kuachia ngazi katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Bodi ataendelea kuwa Mwekezaji na Mwanahisa, amesema na kuahidi ataendelea kuipenda Simba SC hadi siku ya kufa kwa muda wote.
“Katika kipindi cha miaka minne nikiwa Mwenyekiti wa Bodi tumefanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na tumepata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne na kufanya vizuri katika Michuano ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, natoa Shukran kwa Viongozi wa Simba, Wanachama na Mashabiki”, ameeleza MO Dewji.
Hata hivyo, MO Dewji amesema Salim Abdallah (Try Again) ana uzoefu wa kazi hiyo kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano wakiwa wote kama Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, ameahidi kushirikiana naye katika nafasi hiyo sambamba na Uongozi wote wa Simba SC.
RC TABORA ATOA ELIMU JUU YA UMUHIMU WA CHANJO YA UVIKO 19 KATIKA MNADA WA MWISOLE WILAYANI UYUI
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ametoa elimu kwa wakazi wa Kijiji cha Mwisole wilayani Uyui kuhusu umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO 19 na kufanya watu kujitokeza na kupata chanjo katika eneo la Mnada wa Mwisole.
Dkt. Batilda ameendesha zoezi hilo leo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kufikisha elimu kwa wananchi wengi ambao bado hawana uelewa sahihi wa faida ya chanjo ya UVIKO 19.
Amesema viongozi wa Kitaifa wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wameshachanja na wale wa Mkoa wa Tabora na wameshachanjwa na hakuna madhara yoyote waliyopata.
Dkt. Batilda chanjo hiyo salama na inatolewa bure kwa mwananchi yoyote ambayo umri wake unazidi miaka 18 .
“Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan anatupenda sana na ndio maana ametuletea chanjo kwa ajili ya kupambana na ugonjwa UVIKO 19 ambao ni hatari sana …ni vema kwa wale ambao hawajachanjwa wakachangamkia fursa hiyo…na hivi sasa hatuki mfuate chanjo mbali tunawaletea huku mlipo” amesisitiza
Dkt. Batilda amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan inajari sana afya za wananchi wake na ndio maana inajenga miundombinu mbalimbali ambao kwa Mkoa wa Tabora imetoa fedha kwa ajili ya kuongeza Vituo vya Afya vipya viwili.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo amewakumbusha wakazi wa Tabora kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19 kwa kuepuka misongamano,kunawa na maji tiririka na kuvaa barakoa.
Mhudumu wa Afya Kutoka Hospitali ya Wilaya ya Uyui Rahel Mazinge akitoa chanjo ya kujikinga na UVIKO 19 kwa wakazi wa Kijiji cha Mwisole walikuwa katika Mnada wa kila Jumatano.
Mkuu wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (mwenye kipaza sauti) akitoa elimu ya faida ya chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 leo wakati ziara yake katika Mnada uliopo katika Kijiji cha Mwisole wilayani Uyui.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto) akibadilisha mawazo leo na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori(kulia) mara baada ya kumalizika kwa utoaji wa elimu ya umuhimu wa chano ya UVIKO 19 katika mnada uliopo katika Kijiji cha Mwishole.
Picha na Tiganya Vincent
…
932 WACHANJWA CHANJO YA UVIKO19 KWA SIKU MBILI NAMTUMBO
NA YEREMIAS NGERANGERA…..NAMTUMBO
Timu ya wataalamu wa afya ikiongozwa na mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo Lucia Kafumu wanatoa elimu kwa wananchi wa kata na vijiji vya wilaya ya Namtumbo kuhusu umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 na kufanikiwa kuchanja wananchi 932 kwa siku mbili kwa siku ya jumatatu na jumanne ya wiki hii.
Wananchi wa kata ya Likuyu ,kata ya Mgombasi,kata ya kitanda walipatiwa elimu ya ugonjwa wa UVIKO19 kwa kuelezwa nini maana ya ugonjwa huo,dalili za ugonjwa huo ,chanzo cha ugonjwa pamoja na kuelezwa njia sahihi ya kuzuia ugonjwa usilete madhara makubwa kwa wananchi ni kupata chanjo ya UVIKO 19 ambapo wananchi katika kata hizo waliojitokeza kusikiliza elimu kutoka kwa wataalamu wa afya na kukubali kupata chanjo ya UVIKO19.
Kata ya Mgombasi Kijiji cha Nambecha kitongoji cha masimango pekee kilichanja wananchi 74 wote waliohudhuria mkutano huo Kijiji cha mandela Kilichanja wananchi 63 na Kijiji cha Likuyuseka kilichanja wananchi 50 siku ya kwanza huku wananchi wengine wakidai utaratibu huo uendelee kwa kuwa wananchi wengi hawana uwezo wa kusafiri umbali mrefu wa kufuata huduma ya chanjo katika vituo vilivyotengwa na serikali.
Saidi Hashimu mkazi wa Kijiji cha Mandela alihoji wataalamu wa afya sababu ya Watoto chini ya miaka 18 kutochanjwa huku wazazi wake wakihimizwa kuchanjwa na kuwataka wataalamu kumpatia majibu ambayo yanawafanya Watoto hao kutochanjwa.
Kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Godwin Luta pamoja na mambo mengine alimthibitishia bwana Saidi Hashimu kuwa kinga za Watoto waliochini ya miaka 18 ni thabiti na zenye uwezo wa kupambana na virusi kuliko kinga za watu wenye umri Zaidi ya miaka18.
Naye Amina Ngonyani mkazi wa Kijiji cha Mtonya alihoji mtu mwenye magonjwa mengine kama kisukari,BP,UKIMWI na mengineyo hawezi kusumbuliwa baada ya kuchoma chanjo hiyo aliuliza Amina kwa kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Luta ambaye alimjibu hawezi kusumbuliwa na kumtaka kuchukua namba yake ya simu ampigie simu kama atajisikia tofauti alisema Luta.
Timu ya wataalamu wa afya wilaya ya Namtumbo wanaendelea na kuhamasisha wananchi katika kata na vijiji kutoa elimu katika kata zote 21 za wilaya ya Namtumbo kwa kuwahamasisha wananchi hao kuchanja ili waweze kujikinga na UVIKO19 ambapo kwa siku mbili timu hiyo ya wataalamu wa afya wamechanja wananchi 932 katika wilaya ya Namtumbo
BENKI YA NMB YAZINDUA AKAUNTI MPYA 'WEKEZA' ITAKAYOWAWEZESHA WATEJA KUPATA BIMA YA MAISHA BURE
KATIKA kuwakumbusha wateja wao kuweka akiba ya maisha ya baadae, Benki ya NMB leo imezindua akaunti mpya inayoenda kwa jina la Wekeza itakayomuwezesha mteja kuweka akiba ya muda mrefu na kupata riba kubwa.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Mkuu wa Wateja na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi wakati akizindua akaunti hiyo ambapo amesema akaunti hiyo ya wekeza ni ya kwanza kuwahi kutokea nchini ambapo mteja atajitunzia fedha zake kuanzia Sh 250,000 na kupata riba kubwa mpaka 12 kulingana na miaka ambayo mteja anakusudia kuwekeza akiba yake.
Kupitia Wekeza mteja atakapojiandikisha kwenye akaunti hiyo atapata Bima ya Maisha bure na endapo atafariki au kupata ulemavu wa kudumu atalipwa mara Mbili ya akiba yake ambapo kima cha chini kupata bima hiyo ni Sh Milioni Mbili hadi Milioni 50.
Mponzi amesema muda wa kutunza akiba hiyo ni kati ya miaka sita mpaka 20 na riba hulipwa mara mbili kwa mwaka (Juni na Desemba) na Mteja atakuwa na uwezo wa kuongeza akiba kupitia matawi ya NMB, Mawakala wa NMB na NMB Mkononi.
" Hii maana yake ni kuwa, sisi kama benki iliyo salama zaidi nchini na kinara wa ubunifu katika utoaji wa huduma za benki, tunaendelea kuwekeza kimkakati kwenye teknolojia na mtandao wa matawi yetu huku tukiimarisha uwezo wetu wa kuihudumia jamii. Lengo likiwa kuwawezesha wateja kuimarisha zaidi kipato na uchumi wao.
Tunabuni bidhaa zinazowasaidia wateja kuokoa muda na fedha na tunatumia teknolojia ya kisasa zaidi kufanya hivyo. Tunahitaji kila mtu kuzisimamia fedha zake akiwa na uelewa wa kutosha. Wateja watakao ruhusiwa ni wale wenye akaunti binafsi," Amesema Mponzi
Amesema lengo lao ni kupanua wigo wa akaunti zao binafsi ili kuwawezesha wateja wao kuwa na amani zaidi katika kusimamia fedha zao kwani akaunti hii ni kama kibubu chenye faida nyingi ambazo zitamsaidia mteja kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwa matumizi yenye malengo.
" Hili halijaja hivi hivi tu, benki ya NMB imeangalia soko la Tanzania taarifa za wateja wake na kuona kuwa watu wengi hawana tabia ya kuweka akiba kwa muda mrefu, hivyo kuna haja ya kuwaletea akaunti ambayo itawasaidia kuweka akiba," Amesema Mponzi.
Amesema huu ni muendelezo wa huduma ambazo NMB imekuwa ikianzisha ili kusaidia wateja wake kwa kutoa suluhisho la huduma za kibenki hapa nchini.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizindua huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa NMB, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu, Getrude Mallya.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Janet Rwegasila na Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro.
NDEJEMBI AFANIKISHA KUANZA KWA UJENZI WA SEKONDARI KATA YA ZAJILWA
Charles James, Michuzi TV
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma, Deo Ndejembi amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha Sh Milioni 103 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa manne na matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kata ya Zajilwa.
Kiasi hicho cha fedha kitakamilisha ujenzi wa Madarasa hayo pamoja na samani zake kwa maana ya madawati na ambapo pia matundu hayo 10 nane yatakua ya wanafunzi na mawili ya walimu.
Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Zajilwa akiwa kwenye ziara yake ya kuzungumza na wananchi ambapo amewahakikishia kuwa ukamilishaji wa umeme kwa baadhi ya vijiji vya Kata hiyo utaanza Oktoba mwaka huu.
"Nichukue fursa hii kwa niaba yenu kumshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TASAF kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha hizi ambazo zitakwenda kukamilisha madarasa haya manne, matundu 10 ya vyoo na haya madarasa siyo majengo tu yatakua na Viti na Meza, haya yote nimefanya kama Mbunge wenu kuwatua mzigo wa kuchangishana kila siku kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari.
Kupitia fedha hizi tunakwenda kukamilisha ujenzi wa Shule hii ambayo niliahidi kipindi cha kampeni na sasa tunatekeleza, hii ndio kazi ambayo niliwaomba na ni lazima niitekeleze kwa nguvu na kasi," Amesema Ndejembi.
Kuhusu changamoto ya miundombinu ambayo kwa kipindi kirefu imekuepo kwenye Kata hiyo, Ndejembi amesema tayari washapokea Sh Bilioni 1.5 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Barabara hivyo fedha hizo zimeshafika kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Wilaya ya Chamwino na tayari mkandarasi ameshaanza kazi.
"Kipekee nimpongeze Rais Samia kwa kutupatia kiasi hicho cha fedha ambacho alitoa kwa majimbo yote nchini, hivyo Mimi baada ya TARURA kunishirikisha nikasema sasa ni wakati Tarafa hii ya Itiso ambayo Zajilwa Iko ndani yake kumaliza changamoto hiyo ya Barabara.
Kwa kusema hivyo tayari mkandarasi yupo kazini tunaanza kutengeneza njia panda,itapita hapa Zajilwa kuelekea Gwandi na kutokea Haneti ni Barabara nzuri ambayo itapitika kwa nyakati zote haya yote ni matokeo ya fedha ambazo tumepatiwa na Rais wetu Samia tunamshukuru sana," Amesema Ndejembi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma, Deo Ndejembi akizungumza na wananchi wa Kata ya Zajilwa alipokua Kwenye ziara yake ya kukagua miradi na kuzungumza nao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi akizungumza na wananchi wake wa Kata ya Zajilwa alipofika kuzungumza nao.
Wananchi kutoka vijiji vya Kata ya Zajilwa Wilayani Chamwino wakimsikiliza Mbunge wao ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi leo akiwa kwenye ziara ya kuzungumza nao.
Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akizungumza na wananchi wa Kata ya Zajilwa jimboni kwake.
Tunakuja na Muongozo wa Matumizi ya Fedha za Uendeshaji wa Halmashauri - Waziri Ummy
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa-Alata
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
SERIKALI iko kwenye mchakato wa kuangalia gharama za uendeshaji wa halmashauri zote Nchini ili kuja na muongozo wa matumizi ya Fedha za uendeshaji wa halmashauri.
Haya yameelezwa jijini hapa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kufunga mkutano wa Jumuiya ya Tawala za
mitaa unaojumuisha mameya,wenyeviti wakurugenzi wa halmashauri, miji, manispaa na majiji.
Mhe. Ummy alibainisha hayo kufuatia ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mamlaka za Mitaa Mhe. Murshid Ngeze ambaye aliiomba Serikali kuangalia mgawanyo wa fedha za mapato ya ndani kwa Uendeshaji wa Halmashauri na zile zinazopelekwa kwenye Utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Alisema kutokana na mgawanyo huo imekuwa vigumu Kwa halimashauri kujiendesha hasa kwa zile Halmashauri zenye mapato madogo.
Akifafanua, Mhe. Ummy amesema maelekezo ya kupeleka asilimia 40 Kwa halmashauri zenye mapato kidogo na asilimia 60 kwa halmashauri zinazokusanya zaidi ya Sh bilioni 5 utaendelea kutekelezwa na kusimamiwa.
Hata hivyo, alisema kamati inayoongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI inapitia na kuangalia tena gharama za Uendeshaji katika halmashauri zote zenye mapato makubwa na zile zenye mapato kidogo ili baadaye kuja na muongozo wa namna bora ya matumizi ya fedha za uendeshaji.
“Tumeangalia gharama za posho za kamati za kudumu za Halmashauri, vikao na ufuatiliaji wa miradi, posho za mwezi kwa zile Halmashauri zinazolipa, uendeshaji wa ofisi za kata na vijiji, wenyeviti mitaa, posho za wenyeviti wa halmashauri, kata pamoja na matumizi mengineyo.
“ Pia posho za wakuu wa idara na vitengo, posho za watendaji wa kati, watumishi wa mikatataba, vikao vya kisheria na mabaraza hivyo tunakuja na muongozo wa utakaobainisha kiasi cha fedha za kuendesha Halmashauri zenye mapato ya chini sambamba na zile zenye mapato makubwa.
Maana unaweza kuangalia ukakuta Halmashauri inakusanya Shilingi Bilioni 5 gharama sa uendeshaji ni shilingi Bilioni 2 lakini kuna halmashauri inayokusanha shilingi Mil 600 na gharama ya uendeshaji ni shilingi Mil 360 tu unajiuliza hawa wanawezaje kundesha Halmashauri kwa milioni mia tatu ili hali wengine wanaendesha kwa bilioni mbili hivyo lazima tutoe muongozo hata kama una mapato makubwa tufahamu hizo fedha zinatumikaje alisisitiza Waziri Ummy.
Ummy aliongeza:” Tunataka kuona fedha za mapato zinakwenda kuleta maendeleo, shida za wananchi zinatatuliwa, lakini pia tutahakikisha maslahi yenu yanazingatiwa na wakati huo huo fedha zinarudi kwa wananchi kwa njia ya maendeleo.
Alisema ni muhimu kwa Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi kuhakikisha wanakusanya mapato ipasavyo na kusisitiza kuwa endapo halmashauri haitafanya vizuri katika eneo la ukusanyaji wa mapato basi Mkurugenzi atakuwa hatoshi katika hiyo nafasi.
Pia aliwataka kuhakikisha wanaongeza usimamizi wa fedha zinazopelekwa kwenye maeneo yao kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na elimu, afya, barabara na kuwezesha wananchi kiuchumi kuanzia ngazi ya chini.
Aidha Ummy amesisitiza wakurugenzi, wenyeviti na mameya wa halmashauri kuhakikisha wanatekeleza maagizo na maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati awakati alipofungua mkutano huo.
VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE ICGLR SECRETARIAT
SINGIDA DC YAPONGEZWA KWA UELEWA WA UHAMASISHAJI CHANJO YA UVIKO 19
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MWAKILISHI kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Idara ya Jamii na Lishe, Dinah Atinda amewapongeza wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya ya Singida DC kwa kuwa na uelewa mpana wa uhamasishaji wa chanjo ya Uviko 19 ambao unaendelea nchini kote.
Atinda alitoa pongezi hizo jana kwa niaba ya wenzake katika semina ya siku moja iliyokuwa ikitolewa kwa wajumbe hao wilayani humo.
" Tunapita katika Halmashauri zote kuangalia namna kinavyofanyankazi hiki kikao cha PHC lakini napenda kusema kikao hiki ni tofauti kidogo na vikao tulivyo vipitia ndugu mwenyekiti wa kikao 'Mkuu wa wilaya' inaonekana wajumbe wa kikao hiki wamepata elimu ya kutosha na wapo vizuri kabisa hivyo tunawapongeza sana,". alisema Atinda.
Alisema Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na TAMISEMI na wadau mbalimbali baada ya kuona hali ya nchi sio nzuri ugonjwa wa Uviko 19 unaendelea na watu wanakufa tukaona kuna haja ya kuanzisha mpango mkakati shirikishi na harakishi kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha jamii ili wote waweze kupata chanjo na kupunguza madhara yanayotokana na ugonjwa huo.
Alisema zoezi la mtu kuchanja ni la hiyari hivyo lifuate maagizo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuwa vituo vya chanjo sasa vimeongezwa hadi kufikia zaidi ya 6,500 na vinatoa huduma.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Muragili alisema changamoto kubwa iliyopo kwa Watanzania ni kuwa hawajapewa elimu ya kutosha kuhusu chanjo na hawajui umuhimu wa chanjo hiyo lakini wanauelewa mkubwa wa mambo mbalimbali hivyo ni wajibu wa kamati hiyo kwenda kuwaelimisha na wakielewa watachanja.
Wakizungumza baada ya kupata mafunzo hayo wajumbe wa kamati hiyo walisema sasa wanakwenda kufanya uhamasishaji wa nguvu wakianzia kwenye familia zao.
Walisema uhamasishaji huo wataufanya kwenye nyumba za ibada, magulio, mashuleni, na kwenye mikusanyiko ya watu.
Wajumbe hao walisema wataenda kutoa elimu hiyo kwa viongozi mbalimbali wa vijiji wakiwemo wa Serikali na vyama vya siasa lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wana elewa na kujitokeza kwa wingi kwenda kupata chanjo hiyo.