HANANG' WAZINDUA JOGGING YAO
MAJALIWA AAGIZA KITUO CHA AFYA USINGE KIKAMILIKE IFIKAPO OKTOBA 2021.
*Aiagiza TFS kuyapiga mnada magogo yaliyovunwa kinyume cha utaratibu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Matiko kusimamia ujenzi wa kituo cha Afya Usinge na kuhakikisha kinakamilika ifikapo Oktoba 2021 ili wananchi wa maeneo hayo waweze kupata huduma za afya.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Agosti 28, 2021) alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kilitengewa shilingi milioni 620 za ujenzi.
Waziri Mkuu amesema kuwa amefika katika eneo la kituo hicho lakini hajaona vifaa vya ujenzi ambavyo awali aliambiwa vimenunuliwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi ikiwa tayari zimeshatumika shilingi milioni 600 lakini vifaa hivyo havipo eneo la ujenzi na kiasi hicho cha fedha kilitakiwa tayari kiwe kimekamilisha ujenzi huo.
“Sitawaelewa mkiniambia mnatafuta fedha nyingine na kuzileta hapa ili muongeze kwenye milioni 620 kukamilisha ujenzi wa majengo katika kituo hiki, na hili watu mjiande, Serikali yetu ipo makini na usimamizi wa fedha za serikali upo vilevile”
Amesema kuwa ukamilikaji wa kituo hicho cha Usinge kitakuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo kwa kuwa kitawafanya kutokusafiri umbali mrefu hadi Kaliua kufuata huduma za afya kwa kuwa kituo hicho kitakuwa na huduma zote muhimu.
“Mheshimiwa Rais, ameleta kwenye Wilaya yenu Bilioni 1 na Milioni 860 kwa ajili ya dawa, na kila mwezi Halmashauri inapokea fedha Shilingi Milioni 165, Mna vituo vya afya na Zahanati, nisisikie vituo hivyo vinakosa dawa, Madiwani naomba msimamie katika vituo hivyo kusiwe na mapungufu”
Katika Hatua nyingine, Waziri Mkuu alitembelea eneo la pori la akiba la Igombe na kushuhudia magogo yaliyokamatwa baada ya kukatwa kwa njia haramu na ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuyapiga mnada magogo hayo kwa kufuata utaratibu.
“Wizara toeni vibali vya mnada magogo haya yauzwe, na yaliyo humo ndani hifadhini TFS nendeni mkayakusanye haraka sana ili mpaka mwishoni mwa mwezi wa tisa yawe yamekusanywa na kuuzwa kupitia mnada, waambieni wanunuzi mtayapiga mnada lini ili waje hapa kila mtu ajaribu bahati yake”
Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuhakikisha wanaongeza ulinzi katika eneo la hifadhi hiyo ili kuwalinda wanyama wanaokatiza na wasisite kuwachukulia hatua kali wale watakaokamatwa wakifanya ujangili.
“Hawa lazima tuwafanyie msako tuwakamate, awe anatoka Tanzania au nje ya nchi, ana silaha, kamata aingie kwenye mkono wa sheria, tengeneza timu yako upekuzi ufanyike”
Akiongea na Wanakijiji cha Wachawaseme, Kaliua mkoani Tabora, Waziri Mkuu amewasihi kuulinda msitu ulio katika pori la akiba la Igombe kwa kuacha kukata miti ili kulinda uoto katika eneo hilo
“Tunaharibu miti, hili bonde lote ni eneo linalosaidia kutoa maji kwenda mto Malagarasi lakini pia ziwa Tanganyika, mkiacha miti iondolewe eneo hili litakuwa kavu na hakutakuwa na maji, hapa ni nyumbani kwenu, ni wajibu wenu kulinda maliasili hii”
Rais Samia apongeza jitihada za Benki ya CRDB kuchangia maendeleo katika jamii
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (watatu kulia) akikata utepe kuzindua Afisi ya Maendeleo kata ya Kizimkazi Dimbani na nyumba mbili za madaktari zilizonjengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB na kugharimu shilingi milioni 300. Wengine pichani ni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman (wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid (wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay (watatu kushoto), Mwenyekiti wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (watatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wanne kushoto).
Zanzibar, 28 Agosti 2021 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuchangia maendeleo katika jamii. Rais Samia ametoa pongezi hizo wakati wa kilele cha Tamasha la Kizimkazi alipokuwa akikabidhiwa miradi ya nyumba za madaktari na ofisi za shehia Kizimkazi Dimbani zilizojengwa kwa udhamini wa Benki hiyo.
Akipokea miradi hiyo iliyo gharimu kiasi cha shilingi milioni 300, Rais Samia alisema Serikali inajivunia ushirikiano wa kimaendeleo baina yake na Benki ya CRDB. Aliongezea kuwa Benki hiyo imekuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma (PPP) katika kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya 2025.
“Suala la kuijenga nchi yetu ni wajibu wa kila mmoja wetu na si la Serikali peke yake, niwapongeze Benki ya CRDB kwa kujitoa kwenu kutatua changamoto zilizopo katika jamii. Leo hii mmetutoa kimasomaso kwa kutusaidia kuimarisha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wa Kizimkazi Dimbani wanapata huduma bora za kijamii, ama hakika hii ni Benki ya kizalendo,” alisema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia alisifu mafanikio ya Tamasha la Kizimkazi kwa mwaka huu 2021 ambalo lililenga katika kuhamasisha jamii kudumisha utamaduni na kuongeza ujumuishaji wa kiuchumi kwa wananchi kwa kuonyesha fursa mbalimbali zitokanazo na tamaduni za Kitanzania. Tamasha hilo lilihusisha mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 500 juu ya ubunifu wa bidhaa za asili, elimu ya fedha na uendeshaji biashara, pamoja na michezo mbalimbali ya asili.
Pia alieleza kwamba wakati umewadia kwa Watanzania kuacha utamaduni wa kigeni na kujivunia utamaduni wetu. Alitoa rai kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa na mikakati mbalimbali itakayosaidia kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania. Rais Samia alisema jamii pia ina wajibu wa kushiriki kikamilifu katika matamasha ya utamaduni ili kusaidia ukuzaji na uendelezaji wa mfumo wa utamaduni na sanaa katika jamii ya Kitanzania.
“Benki ya CRDB imetuonyesha kwa mfano kuwa tukiwekeza katika utamaduni wetu tutafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa kutengeneza soko kwa bidhaa zetu za asili na Sanaa yetu. Kupitia Tamasha hili la Kizimkazi niiombe Wizara iweke mikakati ya kuanzisha matamasha ya utamaduni katika kila kanda hii itasaidia kukuza tamaduni za maeneo mbalimbali na kuchochea utalii,” alisisitiza Rais Samia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamjaid Nsekela alisema utekelezaji wa miradi hiyo na uandaaji wa Tamasha hilo la Kizimkazi ambalo zamani lilikuwa likijulikana kama “Kizimkazi Day,” ni muendelezo wa utekelezaji wa Sera ya Benki hiyo ya uwekezaji katika jamii ambayo inaelekeza asilimia 1 ya faida ya Benki kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii kupitia program bunifu za uwezeshaji.
Nsekela alisema Benki hiyo imedhamiria kwa dhati kusaidiana na Serikali kujenga uchumi jumuishi na kuwa utamaduni ni moja ya eneo ambalo Taifa likiwekeza vizuri linaweza kusaidia kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Pato la Taifa kwa ujumla. “Pamoja na vijielezi vingi vya neno utamaduni, sisi Kama Benki ya kizalendo tunaamini kuwa; utamaduni ni ujasiriamali, utamaduni ni utalii, utamaduni ni ajira, utamaduni ni uchumi.”
Aidha Nsekela alibainisha kuwa Benki hiyo imedhamiria kuweka mchango wake katika pande zote za Muungano na hivyo kuchochea maendeleo ya Taifa. Akielezea mchango wa Benki hiyo katika kukuza uchumi wa visiwa vya Zanzibar, Nsekela alisema katika nusu mwaka 2021 pekee Benki ya CRDB imetoa zaidi ya shilingi bilioni 150 kuwezesha sekta mbalimbali za maendeleo ili kuwezesha ajenda ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Buluu.
Alimwambia Mheshimiwa Rais, Benki hiyo pia inajivunia zaidi kuleta mapinduzi makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mwaka 2014 Benki ya CRDB iliunganisha mfumo wake wa kielekroniki wa ukusanyaji mapato na mfumo wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, ambapo ndani ya mwaka mmoja tu makusanyo yaliongezeka kwa zaidi 600%,” aliongezea.
Wananchi pia walipata fursa ya kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo itatolewa katika viwaja vya Kizimkazi Dimbani Mji Mpya, zoezi ambalo liliongozwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Ahmed Nassor Mazrui.
Abiria waaswa kujikinga na UVIKO -19
Na Abubakari Akida, MOHA
Serikali imewataka abiria wanaosafiri mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO -19 huku wakiaswa kupaza sauti zao pindi wanapoona uvunjifu wa sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazosababisha vifo na majeruhi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo alipofanya ziara, alfajiri ya kuamkia leo, lengo ikiwa kutoa tahadhari kwa wadau wa vyombo vya usafiri juu ya tahadhari ya ajali wawapo barabarani sambamba na kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19 kwa abiria hao.
“Sasa kuna janga la UVIKO-19 nawaomba muwe makini mkiwa safarini,vaeni barakoa na tumieni vitakasa mikono lakini pia nawaomba mpaze sauti zenu pindi muonapo uvunjifu wa sheria za usalama barabarani,nchi hii inawategemea sana katika kuleta maendeleo na serikali haipendi kuona watu wake wakipoteza viungo na Maisha,askari wetu wako kila sehemu huko barabarani toeni taarifa” alisema Naibu Waziri Chilo
Akizungumzia madereva wanaoenda mwendokasi bila kufuata sheria za usalama barabarani Naibu Waziri Chilo alisema tayari serikali ishaanza utaratibu wa kuchukua leseni ya udereva kwa dereva yoyote atakaethibitika kusababisha ajali kwa uzembe wake.
“Hivi karibu mmeona jinsi dereva wa basi la Sauli linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tunduma alivyoyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari sasa ile ni hatari, ametokea Mbeya mbali kweli anakuja kupata ajali Kibaha alikuwa na haraka gani? tayari serikali kupitia mamlaka husika ikiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbrod Mutafungwa tushachukua leseni yake na tumemfungia kwa muda wa miezi sita na sasa atarudi darasani akajifunze upya udereva, kwenye kulinda maisha ya wananchi hatutaki mchezo” alisema Naibu Waziri Chilo.
Akizungumza kwa niaba ya madereva wengine, Dereva wa Basi la Al Saedy, Alex Emmanuel aliomba elimu itolewe kwa madereva wa malori kwani ndio wamekua chanzo cha ajali nyingi za barabarani hali inayopelekea kutokukoma kwa matukio ya ajali huku Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Boniface Mbao akiweka wazi kuwepo kwa utaratibu wa wa utolewaji wa elimu na ukaguzi wa mabasi kabla ya kuanza safari na basi linalokutwa na hitilafu basi huzuiwa lisiondoke.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo akizungumza na abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini wakati wa ziara aliyoifanya alfajiri ya leo lengo ikiwa kuwakumbusha wasafiri kupaza sauti waonapo viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani huku pia akiwaasa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO-19. Ziara hiyo imefanyika leo,Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo akizungumza na dereva wa basi la Kimbinyiko juu ya kufuata sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepukana na ajali hizo wakati alipofanya ziara leo alfajiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Boniface Mbao akizungumza na abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo aliyoifanya alfajiri ya leo lengo ikiwa kuwakumbusha wasafiri kupaza sauti waonapo viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani huku pia akiwaasa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO-19. Ziara hiyo imefanyika leo,Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo akitoka ndani ya Basi la Kimbinyiko ambako alikuwa akizungumza na abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini wakati wa ziara aliyoifanya alfajiri ya leo lengo ikiwa kuwakumbusha wasafiri kupaza sauti waonapo viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani huku pia akiwaasa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO-19. Ziara hiyo imefanyika leo,Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma
ASASI ZA KIRAIA ZATAKIWA KUHAKIKISHA ZINAZINGATIA HAKI ZA WATOTO
Na Mwandishi Wetu,Michuzi Tv Moshi
Wito umetolewa kwa Asasi za kiraia hususani zile zinazopigania haki za binadamu nchini kuhakikisha kuwa wanazingatia haki za watoto wakati wanapotekeleza majukumu yao ili kulinda usalama na usiri kwa watoto.
Hayo yamezungumza hivi karibuni mjini Moshi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Tusonge, Aginatha Rutazaa wakati wa kuandaa washiriki katika maandalizi na utekelezaji wa majukwaa ya jamii kwa Asasi 17 kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Akielezea maana ya Jukwaa la Jamii amesema ni mkusanyiko wa kundi (jamii) wenye lengo la kujadili jambo lililopo ndani yao kwa lengo la kupata suluhu au muafaka ambapo lengo ni kujadili masuala mazima yanayohusu ukatili wa kingono ndani ya jamii.
Amewataka washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili kuwa ni vema wakati wa kuandaa majukwaa hayo kuelezea sheria na taratibu zilizopo katika kusaidia wahanga wa ukatili, kuelezea taratibu zilizopo katika kufanya kazi na watoto na kuzingatia usalama na usiri wao ikiwa ni pamoja na kuielimisha jamii ili iweze kuzungumzia masuala ya ukatili wa kingono kwa uhuru na haki.
"Ni vema tuhakikishe tunatengeneza usiri katika mahojiano baina ya waathirika wa masuala ya ukatili wa kingono wakiwemo watoto kila tunapotekeleza majukumu yetu, tuzingatie miongozo na taratibu zilizopo ili tuleta tija kwa kile tunachokifanya" alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Kukuza Usawa kwa Kutumia Elimu ya Haki za Binadamu kutoka katika Shirika hilo, Consolata Kinabo aliwaambia washiriki hao kuwa lengo la Jukwaa la Jamii ni kutoa nafasi ya majadiliano jumuishi, salama na shirikishi kwa wanawake, wanaume, wasichana, vijana na watu muhimu kutafakari masuala ya ukatili wa kingono na kubainisha mikakati ya msingi ya kutatua.
"Umuhimu wa kutumia mbinu hii shirikishi ni ili kupata matokeo chanya ikiwemo kuongeza kujiamini, kujiheshimu kwa wanawake, wasichana na wavulana ili wajione wenye tija ndani ya jamii, lakini pia serikali kuongeza ulinzi kwao" Alisema Consolata.
Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo wanatarajia kujenga uelewa wa Haki za Binadamu na msingi wa maadili, kujenga uelewa wa Usawa wa kijinsia, kujenga uelewa wa ukatili wa kingono pamoja na utambuzi wa fursa na vizuizi kwa wanajamii katika kutatua ukatili wa kingono.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Community Economic Development and Social Transformation (CEDESOTA) Jackson Muro amesema kupitia mafunzo yanayotolewa na Tusonge kwa Asasi hizo, wanatarajia kuwa na jamii inayozingatia haki za binadamu isiyokuwa na vitendo vya ukatili wa kingono na yenye kuheshimu Usawa na kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Tusonge lenye Makao makuu yake mjini Moshi, Aginatha Rutazaa akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka Asasi 17 kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Washiriki wakiwa katika vikundi vya majadiliano
WANAFUNZI SOMENI ACHENI KUIGA MASUALA YA UTANDAWAZI-DIWANI LIDYA MGAYA
DIWANI wa viti Maalum Kibaha Mjini ,Lidya Mgaya amewaasa wanafunzi wilayani hapo ,kuachana na masuala ya utandawazi na kuiga mambo yasiyo na maadili na badala yake watumie TEHAMA kupata uelewa wa masuala mbalimbali ya kielimu.
Aidha amewaasa kusoma kwa bidii ili kujiinua kitaaluma .
Akigawa taulo za kike na sabuni za unga za kufulia kwa msaada kutoka KEDS TANZANIA COMPANY LIMITED na kisha kuwapatia baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kibaha na Tumbi sekondari kwa wavulana, Lidya Mgaya alisema ,lengo ni kuongea na wanafunzi kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na yasiyo na maadili wakati wanasoma.
Aliwasisitiza wasimame kuitafuta elimu kwa bidii na wafauru kusiwe na sifuri wala mimba za utotoni wakiwa wanasoma hivyo wajikite kuzingatia masomo na kuepuka mambo mabaya yatakayowarudisha nyuma kitaaluma.
Diwani huyo alielezea, amejipanga kuanza kampeni ya MWANAFUNZI WA KIKE KATAA MIMBA ZA UTOTONI KATAA ZERO hali itakayosaidia kupunguza changamoto ya kukatisha masomo kwasababu ya mimba, kufeli ama utoro.
Lidya aliishukuru halmashauri ya Mji wa Kibaha, ofisa elimu taaluma na sekondari pamoja na halmashauri na KEDs TANZANIA COMPANY LTD ambao wamemuunga mkono katika zoezi hilo la kupata taulo za kike.
TradeMark East Africa Women in Trade Project Bears Fruits, That Produces Positive Results, More Women Better Products, TWCC Wins Award.
By Pascal Mayalla.
TradeMark East Africa (TMEA) funding for the Tanzania Women Traders' Association (TWCC) has begun to bear fruit, with more than 200 women entrepreneurs being empowered to produce quality products, assisted with the TBS brand logo and barcode, and enabled to participate in the 45th Dar es Salaam International Trade Fair to showcase their products, promoting then, and opens their access to national and international markets.
This was revealed by the TradeMark East Africa, Tanzania Country Director, Monica Hangi, during the evaluation of TWCC's participation in the 45th Dar es Salaam International Trade Fair, where TWCC, Clinched one among the top awards.
Monica Hangi, congratulated TWCC for the victory and for the good job it’s doing to women traders.
"Congratulations to TWCC Chairperson, Mercy Silla and TWCC Executive Director, Mwajuma Hamza for a job well done. Many of them now have the TBS logo, they can sell it abroad, they have reliable markets that is a big deal for us, TradeMark East Africa because the goal is now being fulfilled, to be able to support and help Tanzanian women traders to do business not only locally, but cross borders and international as well as securing permanent reliable markets, that is the key because sometimes you can find a market but you no longer have enough products to continue producing, but most are sustainable, some we see who trained four years ago and are here continue to grow and they have more products, better products, with TBC stickers and barcodes, for us that really is a very good issue. We are happy, we are relieved, Mama Silla and Mwajuma, congratulations ”- concluded Monica Hangi.
On his part, TradeMark East Africa Women in Trade Project Manager, Elibariki Shammy, said “we are really happy, because we have supported TWCC, and they have proved to be very effective, especially in reaching out rural women, we have now reached about 20 thousand women, we had the first phase of the project, now in the second phase. It is very interesting, to see many products now. At the beginning when we started, and these people had no TBS quality mark so these TBS quality marks, now help them reach larger markets that are global. For example, there are women who now export cashew nuts to Uganda; there are women there who we are exporting batik to Kenya. There are many women who have soap products or similar, they can sell them at super markets, because through this training, not only TBS, there is also a barcode issue, initially they did not have a barcode, but our training has enabled them to have TBS and a barcode, so the main goal is to help them reach the big markets, TradeMark is here to make sure that happens ”, said, Elibariki.
For her part, TWCC Chairperson, Mercy Silla said “I would really like to take this opportunity on behalf of the directors of TWCC, all members, and business women in our country to thank TradeMark, East Africa, for their great support. they have thrown us. As you can see the number of women traders is increasingly, we are formalizing their businesses, we teach them to produce quality products, branding, we help then get TBS, and barcodes. There are many others, they are still behind. So our duty and responsibility is to reach all women at all levels. And to enable them to formalize their businesses, but we also believe that by doing so; we contribute to the economy of our country, but also the economy of their families. We are walking along President, Samia foots steps, she argues, women to dare, rise, and do everything. “Every thing a man can do, a woman can do”. “I really want to thank you very much Trade Mark East Africa. I believe everyone coming here, gets a lesson, and these when they all return, they will tell their colleagues great things, and today you have come to visit us, I believe they will tell you we have seen those who brought us here, so I thank you very much ”concluded Mama Silla.
On her part, TWCC Executive Director, Mwajuma Hamza, thanked TradeMark East Africa, “Thank you TradeMark East Africa, we have reached many women, since we started working with TradeMark East Africa, this project is 5-year project, now is just 2nd year we have reached thousands of women, we hope to reach tens thousands of women, but also to help them access business information, build their capacity, their businesses to meet the international standards, but also to address the challenges of the business environment. For us through Trademark, we believe we will continue to benefit, and these women will continue to do well locally and internationally, and right now TradeMark are creating a system for us to sell online, so due to the Covid 19 pandemic, we believe, women will continue to do their businesses online. Thank you very much ”concluded Mwajuma.
On their part, the women traders thanked TWCC and TradeMark East Africa for empowering them by providing them with training, on how to produce quality products, packaging, providing TBS and barcode logos, sponsoring them to participate in various local and international exhibitions to the country including a trip to China, to market their products and open up opportunities for domestic and international markets.
The Country Director of TradeMark East Africa, Tanzania, Monica Hangi, signing the guest book, during the Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Special Entrepreneurship Fair, to evaluate TWCC's participation in the just ended 45th DITF (Saba Saba) Exhibition. The evaluation took place last, Saturday, outside the TWCC Offices located inside the Saba Saba Exhibition Grounds in Dar es Salaam which was attended by more than 200 traders who also participated in the just ended 45th DITF exhibition through the TWCC pavilion sponsored by TradeMark East Africa.
The Country Director of TradeMark East Africa, Tanzania, Monica Hangi, center, inspecting products during the Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Special Entrepreneurship Fair, to evaluate TWCC's participation in the 45th DITF (Saba Saba) Exhibition. The evaluation took place last, Saturday, outside the TWCC Offices located inside the Saba Saba Exhibition Grounds in Dar es Salaam which was attended by more than 200 traders who also participated in the 77th exhibition through the TWCC pavilion sponsored by TradeMark East Africa. Left is the TradeMark East Africa Project Manager, Supporting Women Entrepreneurs, Elibariki Shammy, and right is TWCC Executive Director, Mwajuma Hamza.
TWCC Entrepreneur, Rehema Patrick of Eden Products from Morogoro presenting her products to the Country Director of TradeMark East Africa, Tanzania, Monica Hangi, (right) during the Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Special Exhibition, to evaluate TWCC's participation in the 45th DITF (Saba Saba) Exhibition. The evaluation took place last Saturday, outside the TWCC Offices located inside the Saba Saba Exhibition Grounds in Dar es Salaam that was attended by more than 200 traders who also participated in the just ended exhibition through the TWCC pavilion sponsored by TradeMark East Africa. In the center is TWCC Executive Director, Mwajuma Hamza.
TWCC Entrepreneur, Jane Simon Ndettoe of Jesano Batik Company from Mwanza, presenting her products to The Country Director of TradeMark East Africa, Tanzania, Monica Hangi, (right) during Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC), to evaluate TWCC's participation in the 45th Saba Saba Exhibition. The evaluation took place yesterday, Saturday, outside the TWCC Offices located inside the Saba Saba Exhibition Grounds in Dar es Salaam that was attended by more than 200 traders who also participated in the 77th exhibition through the TWCC pavilion sponsored by TradeMark East Africa. In the center is TWCC CEO, Mwajuma Hamza.
TWCC Entrepreneur, Judith Lugembe (Left) of Lubasu Soap Factory, located in Musoma in Mara region, producing Just Soap brand name, presenting its products to the Resident Director of Trade Mark East Africa Tanzania Branch, Monica Hangi, (right) during the Special Entrepreneurship Fair of Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) to evaluate TWCC's participation in the 45th Saba Saba Exhibition. The evaluation took place yesterday, Saturday, outside the TWCC Offices located inside the Saba Saba Exhibition Grounds in Dar es Salaam that was attended by more than 200 traders who also participated in the 77th exhibition through the TWCC pavilion sponsored by TradeMark East Africa. In the center is TWCC Chairman, Mercy Silla
TWCC Entrepreneur, Marriam Zapoka of Mary Foods in Dar es Salaam (left) presenting her products to The Country Director of TradeMark East Africa, Tanzania, Monica Hangi, (second right) during a special product exhibition Entrepreneurs of the Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC), to evaluate TWCC's participation in the 45th DITF, (Saba Saba) Exhibition. The evaluation took place yesterday, Saturday, outside the TWCC Offices located inside the Saba Saba Exhibition Grounds in Dar es Salaam that was attended by more than 200 traders who also participated in the 45th DITF exhibition through the TWCC pavilion sponsored by TradeMark East Africa. Right is TWCC Executive Director, Mwajuma Hamza.
WANAFUNZI WA SEK CHANGARIKWA WALIOSHINDWA KULIPIA CHAKULA WARUDISHWA SHULE-MSONDE
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE ASIA AKAMILISHA MBAO ZA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU UVCCM HANANG'
TASAF YAANZA UJENZI WA UKUMBI KATIKA SHEHIA YA KIZIMKAZI UTAKAOWEZESHA WANAFUNZI KUFANYA MITIHANI NA SHUGHULI ZA KIJAMII
Na. James K. Mwanamyoto-Kizimkazi
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeanza ujenzi wa ukumbi utakaogharimu shilingi milioni 149 katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani, Zanzibar ili kutatua changamoto ya kukosekana kwa darasa la kufanyia mitihani kwa wanafunzi wa eneo hilo, ambapo ukumbi huo pia utatumika kwa shughuli za kijamii kwa wananchi wa shehia hiyo iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa ukumbi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema dhamira ya ofisi yake kutumia fedha za ruzuku zinazotolewa na TASAF ni kuwasaidia wanafunzi wa eneo la Kizimkazi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihangaika kutafuta maeneo ya kufanyia mitihani.
“Mradi huu utawasaidia wanafunzi ambao wakati wa kipindi cha mitihani wamekuwa wakitafutiwa maeneo mengine ya kufanyia mitihani kutokana na kukosa darasa ya kufanyia mitihani na utawasaidia pia wakazi wa Kizimkazi kupata ukumbi wa mikutano kwani ni muda mrefu wamekabiliana na changamoto hiyo,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.
Ameongeza kuwa, ofisi yake kupitia TASAF imekuwa na utamaduni wa kutoa mchango kwenye jamii kwa kutoa fedha zinazotumika kuboresha huduma kwenye sekta ya elimu, afya na miundombinu kwa lengo la kuwa karibu na jamii, kushiriki utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na hatimaye wafurahie mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amesema kuwa, mradi huo wa ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii ulikuwa ni hitaji la wananchi wa Shehia ya Kizimkazi, hivyo TASAF ikaamua kufadhili ili kukidhi mahitaji ya wananchi hao.
“Ujenzi wa mradi huu unahusisha wananchi kufanya kazi za ajira ya muda ambapo kaya za walengwa 107 wa TASAF zinafanya kazi kwenye mradi huo,” Bw. Mwamanga amefafanua.
Bw. Mwamanga amesema, mradi huo umehusisha ushiriki wa wananchi ili waweze kutoa mchango kwenye eneo la ujenzi na kupata ujira, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kujiona ni sehemu ya mradi kwa kuchangia nguvu kazi yao.
Dhamira kuu ya ujenzi wa ukumbi huo ni kuunga mkono azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo kwa wananchi wote ikiwemo wa Shehia ya Kizimkazi ambako ndiko alikozaliwa.
Muonekano wa mradi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akipokea maelezo ya ujenzi wa mradi wa ukumbi wa kufanyia mitihani na shughuli za kijamii unaogharamiwa na TASAF katika Shehia ya Kizimkazi Dimbani iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YAKAGUA MAENDELEO YA MAFUNZO YA UANAGENZI NA MIRADI ILIYOZINDULIWA NA MBIO MAALUM ZA MWENGE WA UHURU MKOANI SINGIDA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Najma Giga (wa tatu kutoka kushoto) wakisikiliza maelezo ya kijana Idd Ramadhani mnufaika wa mafunzo ya Uanagenzi fani ya Umeme katika Chuo cha VETA wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kukagua miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Mkoani Singida.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Najma Giga (wa tano kutoka kushoto) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiangalia zulia walipotembelea vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu waliowezeshwa na Mikopo ya Asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani wakati wa ziara yao Mkoani Singida.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Najma Giga (wa tano kutoka kushoto) wakisikiliza maelezo ya vijana wanufaika wa mafunzo ya Uanagenzi fani ya Ufundi Bomba katika Chuo cha VETA Mkoani Singida.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Najma Giga akiwa pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiangalia bidhaa za nguo na mapazia yanayotengenezwa na vijana wenye ulemavu walipotembelea Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu Sabasaba Mkoani Singida kwa lengo la kukagua maendeleo ya Mafunzo hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Najma Giga (Mb.) akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua Mafunzo ya Uanagenzi yanayotolewa kwa vijana kupitia Vyuo vya Ufundi stadi mbalimbali vilivyopo nchini pamoja na kukagua miradi iliyozinduliwa na mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Singida. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Kirumbe Ng’enda.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akifafanua jambo kuhusu mafunzo ya Uanagenzi yanayoratiwa na Ofisi hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kukagua miradi inayosimamiwa na Ofisi hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(SERA, URATIBU, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
*************************
Na: Mwandishi Wetu – Singida
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imetembelea na kukagua miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Mafunzo ya Uanagenzi yanayotolewa kwa vijana kupitia Vyuo vya Ufundi stadi mbalimbali vilivyopo nchini pamoja na kukagua miradi iliyozinduliwa na mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Singida.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe Najma Giga (Mb.) imetembelea Chuo Cha VETA na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu ambavyo vinatoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana. Pia kamati hiyo imetembelea Maabara ya Mafunzo ya Kompyuta, Karakana ya Umeme katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Ofisi ya udhibiti wa Ubora wa Elimu na mradi wa maji uliopo Nguka Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, miradi hiyo ilizinduliwa wakati wa mbio maalum za mwenge wa Uhuru.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Najma Giga (Mb.) alieleza kuwa kamati hiyo imekuwa ikisimamia miradi mbalimbali inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na wameridhishwa namna ofisi hiyo imekuwa ikitekeleza mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakishauriwa na kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.
“Tumefurahi kuona mafunzo haya ya Uanagenzi wanayopatiwa vijana wakiume, wakike na wenye ulemavu kupitia ufadhili wa Serikali yao yamewasaidia kupata fani mbalimbali za ufundi stadi ambazo zitawasaidia kukuza ujuzi na kuwawezesha waondokane na tatizo la ajira na hivyo kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wenzao,” alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Najma Giga (Mb.)
Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga alisema kuwa Mafunzo hayo ya Uanagenzi yanayoratibiwa na ofisi hiyo awamu ya tatu ilianza rasmi Juni 2021 katika mikoa yote ya Tanzania Bara ambapo jumla ya vyuo 72 vinashiriki kutoa mafunzo hayo.
“Hadi sasa jumla ya Vijana 14,440 wamenufaika na mafunzo ya Uanagenzi na mafanzo hayo yanagharamiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia fedha zilizopitishwa na Bunge letu Tukufu kwa lengo la kuwasaidia vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa kupata ujuzi stahiki utakaowawezesha kujiajiri, kuajiri wenzao ama kuajiriwa,” alisema Naibu Waziri Ummy
Alifafanua kuwa Mkoa wa Singida fursa hiyo ya mafunzo ya Uanagenzi imetolewa kwa vijana 395 ikiwa ni sawa na asilimia 91.9, vijana ambao hawajaripoti ni 35 ikiwa ni saw ana asilimia 8.1 ambapo jumla ya vijana 430 walipaswa kupatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kuhakikisha fursa zilizotolewa kwa mkoa wa singida hazipotei.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Ng’wasi Kamani (Mb.) alitoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali na waachane na dhana ya kufikiria kuwa mafanikio yanapatikana kwa njia rahisi au kupitia “connection”.
“Ninawasihi vijana wanaopatiwa mafunzo haya ya Uanagenzi watakapo maliza mafunzo yao wachangamkie fursa ya mikopo inayotolewa na halmashauri pamoja na mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ili waweze kuanzisha miradi ya kuichumi,” alisema
Akitoa neno la Shukrani Mnufaika wa Mafunzo hayo ya Unangenzi Bi. Elizabeth Charles ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendelea kukumbuka vijana na kundi la Watu wenye Ulemavu kwa kuwapatia ujuzi ambao utawasaidia kuanzisha shughuli zao binafsi za uzalishaji mali.
ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA KUANZA AGOSTI 30
Zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa vyenye usajili kamili linatarajiwa kuanza kesho tarehe 30 Agosti, 2021. Kwa mujibu wa barua na ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kusainiwa na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, zoezi hilo litaanza kwa kuhakiki vyama vyenye ofisi zake Jijini Dar-es-salaam. Vyama vitakavyofungua zoezi hilo ni AAFP kuanzia saa mbili asubuhi na NRA saa sita na nusu mchana.
Siku ya Jumanne zoezi hilo litaendelea kwa kuhakiki vyama vya UDP na NLD, vikifuatiwa na vyama vya UMD na ADC siku ya Jumatano ya tarehe 1 Septemba, 2021.
Siku ya Alhamisi ya tarehe 2 Septemba, 2021 vyama vya CCK na Demokrasia Makini vitafanyiwa uhakiki. Siku ya Ijumaa itakuwa zamu ya chama cha CHADEMA na UPDP.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo zoezi la uhakiki litaendelea wiki inayoanza tarehe sita kwa kuhakiki vyama vya NCCR na CHAUMA kuanzia saa mbili na nusu asubuhi. Vyama vingine vitakavyohakikiwa wiki hiyo ni pamoja na vyama vya ACT-Wazalendo, CUF, TLP, SAU, ADA TADEA na DP. Uhakiki wa Chama cha Mapinduzi (CCM) utafanyika Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dodoma siku ya Ijumaa ya tarehe 10 Septemba, 2021.
Baada ya kuhakiki ofisi za Dar-es-salaam na Dodoma zoezi la uhakiki litahamia ofisi za Zanzibar kuanzia tarehe 13 Septemba kwa kuhakiki vyama vya AAFP na NRA. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa kila chama chenye usajili kamili kinatakiwa kuwa na ofisi pande zote mbili za Muungano.
Zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa ni takwa la kisheria kuhakikisha vyama 19 vyenye usajili kamili vinatekeleza masharti ya usajili kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa na kanuni zake.
Mutta Rwakatale ahimiza maadili mema kwa watoto
Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa shule za St. Mary’s Mutta Rwakatale ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwasimamia watoto na kuhakikisha kuwa wanakuwa katika maadili mema sambamba na kuwapatia elimu ikiwa ni haki yao kwa mujibu wa sheria.
Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa wamahafali ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo yaliyofanyika kwenye shule ya St Mary’s Mbagala mkoani Dar es Salaam, ambapo alisema kumpatia elimu mtoto kunamsaidia asiwe tegemezi baadae.
Amesema kila mzazi anajukumu la kuhakikisha kuwa anamuelimisha mwanaye kwa hali yoyote ile ili atakapokuja kuwa mkubwa aweze kumsaidia na kusisitiza kuwa watoto wanahaki ya kusikilizwa katika mahitaji yanayowasaidia kutimiza malengo yao.
“Mtoto anapokuomba umpeleke kwenye masomo ya ziara wakati wa likizo, umnunulie daftari, kalamu na vitu vingine vinavyomsaidia katika masomo yake jitahidi umpatie kwani mafanikio yake ni furaha kwetu sisi walimu kwenu wazazi na kwake pia, watoto ndio viongozi, madaktari, marubani walinzi na nguvukazi ya taifa kwa baadae tuwalinde na kuwarithisha elimu bora.
“Tuwe na tabia ya kuwajenga watoto watu kiimani tukifanya hivyo watakuwa na hofu, wengine ni wakorofi lakini tukiwa na kawaida ya kuongea nao kwa kuwaelekeza taratibu watakuelewa,” alisisitiza.
Aliwataka wazazi pia kuwasisitiza wanafunzi hasa wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu wiki mbili zijazo kuhakikisha kwamba wanasoma kwa bidii ili watimize malengo yao.
Aidha,, watoto wanategemewa na familia na taifa kwa ujumla hivyo wanapaswa kujilinda na kuwa na tahadhari wasijihusishe na makundi mabaya mitaani wanaporudi nyumbani kwaajili ya mapumziko mafupi.
“Mnapomaliza mitihani na kurudi nyumbani kunawatu wengi watawatazama na wengine wanaweza kujaribu kuwashawishi ili mjiunge nao hakikisheni mnawaepuka kwani watasababisha mshindwe kutimiza malengo yenu, “ alisema
“Simamieni na myaendeleze maadili mliyopatiwa na wazazi pamoja na walimu wenu hapa shuleni bado mnasafari ndefu ya kimasomo msije mkabweteka,” alisema.
Pia amewataka kutumia elimu waliyoipata kupambana na changamoto za maisha kwani kunachangamoto nyingi na aliwataka wasikubali kukatishwa tama na wakashindwa kutimiza malengo yao.
Mkurugenzi wa shule za St Mary's Mutta Rwakatale akifurahia jambo na wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo upande wa Mbagala wakati wa mahafali yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki
Wanafunzi wa shule ya St Mary's Mbagala wakionyesha umahiri wa kucheza nyimbo mbalimbali kwenye mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika Jumamosi shuleni hapo
Waziri Ummy Aagiza Kata ya Kinaga- Kahama kuwekwa katika Orodha ya Kata za Kimkakati itakayojengewa Kituo cha Afya
Muonekano wa Nyumba za Walimu ( 6 in 1) zilizofunguliwa na Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake kwenye Manispaa ya Kahama.
Junior Scholar kuwagharamia mahitaji muhimu watakaochaguliwa shule za vipaji


MATUKIO SIKU YA WANANCHI, RANGI ZA KIJANI, NJANO ZA TAWALA
Matukio Mbalimbali ya Siku ya Yanga maarufu kama siku ya Wananchi leo Agosti, 29,2021, sherehe ya siku ya Yanga inayoendelea kufanyika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam rangi za njano na Kijani zimetawala katika uwanja huo.
Rais Samia aanza rasmi kurekodi kipindi kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Msanii Mkongwe wa Taarab Asilia Nchini Bibi Mariam Hamdani, alipokutana nae katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, kabla ya kuanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi mbalimbali Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, alipokua akianza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Utalii na mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, wakati wa kuanza kurekodi rasmi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,202. PICHA NA IKULU.
RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK.HUSSEIN ALI MWINYI ASHIRIKI MAZIKO YA MJUMBE WA NEC CCM LEO.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiwa katika Sala ya Maiti ya Marehemu Semeni Khamis Vuai Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), iliyoongozwa na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Mfaume (mbele) katika Masjid Jamii-Attqwa Dunga na kuzikwa katika Kijiji cha Tunguu Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja leo.[Picha na Ikulu] 29/08/2021.

Baadhi ya Viongozi na Waislamu mbali mbali wakimswalia Marehemu Semeni Khamis Vuai Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC),Sala iliyoongozwa na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Mfaume (mbele) katika Masjid Jamii-Attqwa Dunga na kuzikwa katika Kijiji cha Tunguu Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja leo.[Picha na Ikulu] 29/08/2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatana na Mkuu wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid alipowasili katika Masjid Jamii-Attqwa Dunga aliposhiriki katika maziko ya Marehemu Semeni Khamis Vuai Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) aliyefariki jana na kuzikwa leo katika Kijiji cha Tunguu Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu] 29/08/2021.

Vijana wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) Wilaya ya Kati Unguja wakibeba Mwili Marehemu Semeni Khamis Vuai Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Tunguu Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi pamoja na Viongozi mbali mbali na Wananchi walihudhuria.[Picha na Ikulu] 29/08/2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akitia udongo katika kaburi la Marehemu Semeni Khamis Vuai Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), wakati wa Maziko yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Tunguu Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu] 29/08/2021.
KATIBU NENELWA MWIHAMBI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE JIJINI DODOMA

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Jane Kajiru akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakati wa Mkutano wa pamoja uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Agosti 29, 2021

Mwenyekiti wa TUGHE Ofisi ya Bunge, Bw. Chacha Nyakega akitolea ufafanuzi maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakati wa Mkutano wa pamoja uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Agosti 29, 2021

Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi (katikati) akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakati wa Mkutano wa pamoja uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Agosti 29, 2021, Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Jane Kajiru na Mwenyekiti wa TUGHE Ofisi ya Bunge, Bw. Chacha Nyakega
Haji Manara awa Kivutio, Ashukuru Yanga kwa kumpokea
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Msemaji wa Yanga Haji Sunday Manara amewashukuru Mashabiki wa Yanga kwa kumpokea na kumkubali kama msemaji wao mpya.
Akitoa maneno hayo, Manara amesema mashabiki na wanachama wa Yanga wamempa heshima na anawaahidi kuwapa furaha katika kipindi chote.
“Najiuliza kwanini baba yangu aliniacha niende kule, Yanga kuna raha na nawaahidi mashabiki wa Yanga kuwapa furaha na nitakuwa nanyi bega kwa bega,” amesema
Manara akiwatambulisha wachezaji wa Yanga kabla ya kuanza mechi, amesema msimu huu Yanga ni ya Makombe na sio vingine.
Katika tukio la kipekee, Manara alimfunga kamba za viatu Kiungo mahiri wa Yanga Feisal Salum ‘ Fei Toto’ na kumsifia kwa uwezo wake mkubwa uwanjani.
Aidha, katika sherehe hizo zilizomalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Zanako, Yanga iliwatumia wachezaji wake wapya na kuangalia tathmini ya kila mmoja.
Kwenye mchezo huo Yanga imekubali kichapo cha goli 2-1 goli kwa upande wa Yanga likifungwa na Heritier Makambo.