Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 118642 articles
Browse latest View live

Rais Samia azindua miradi mbalimbali ya maendeleo kizimkazi Zanzibar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Maendeleo Kizimkazi iliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB leo Agosti 28,2021 kwenye Tamasha la Kizimkazi zilizofanyika leo tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Skuli ya maandalizi Kizimkazi katika Tamasha la Kizimkazi Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi zilizofanyika leo tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.



ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kwa ajili ya kupokea rasmi Ambules iliyotolewa kwa ufadhili wa Benki ya NBC kwa ajili ya kutoa huduma katika Kijiji cha Kizimkazi kwenye Tamasha la Kizimkazi lililofanyika tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Vyakula vya Asili vya aina mbalimbali kwenye Tamasha la kizimkazi lililofanyika leo tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Nyumba za Madaktari na Jengo la Ofisi ya Maendeleo Kizimkazi katika Tamsha la Kizimkazi zilililofanyika leo tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifurahia mashindano ya mchezo wa kuvuta Kamba kati ya Timu za Vijana Wanawake na Wanaume katika Kijiji cha Kizimkazi, kwenye Tamasha la kizimkazi lililofanyika tarehe 28 Agosti 2021 katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja. PICHA NA IKULU.

KAMATI YA USALAMA SHINYANGA YARUHUSU WAFANYABIASHARA KUCHUKUA DENGU ZAO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamati ya Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa shinyanga Dr. Philemon Sengati (PhD) imewaruhusu wafanyabiashara wa mazao ya dengu kuchukua dengu katika maghala ya chama cha Ushirika (SHIRECU) kuanzia Jumatatu Agosti 30,2021.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa mkoa Dkt. Philemon Sengati kufanya kikao na wanunuzi wa dengu leo Agosti 28, 2021 kikao ambacho pia kimehudhuriwa na Kamati yote ya Ulinzi na Usalama mkoa,Wakuu wa wilaya, Waendesha ghala, Wakili wa Serikali, Mwanasheria wa Makampuni yaliyofungua kesi mahakamani na wawakilishi wa Makampuni ya ununuzi wa dengu.

Dkt. Sengati amesema amefanya maamuzi na kutoa agizo baada ya kupokea Waraka kutoka kwa Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda unaoelekeza kwamba mazao jamii ya mikunde ikiwemo dengu hayapo katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwa sasa.

Amesema Waraka huo umeondoa mfumo wa Stakabadhi ghalani kwa zao la dengu kwa mikoa inayolima dengu mpaka pale serikali itakapotoa maelekezo mengine.

“Jana Agosti 27,2021 nimepokea Waraka kutoka Wizara ya Kilimo wa tarehe 26,2021 ukielekeza kuwa mazao jamii ya dengu hayatatumia mfumo wa stakabadhi ghalani na soko la bidhaa (TMX)”, amesema Dkt. Sengati.

“Hapakuwa na Waraka rasmi kutoka wizarani lakini baada ya kupokea Waraka nimekutana na wadau wa dengu na tumekubaliana utaratibu wa kuondoa dengu ghalani. Dengu hizi zitoke kwa utaratibu ambao hautaleta mgogoro”,amesema Dkt. Sengati.

Amesema kutokana na hali hiyo sasa Walanguzi watanunua dengu moja kwa moja kwa wakulima.

Vile vile Dkt. Sengati amewaomba wanunuzi hao kufuta kesi waliyoifungua mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga kupinga amri ya kukamata mazao hayo ya Dengu kiasi cha tani 400 ambapo Wanunuzi hao wamekubali kuifuta kesi hiyo bila gharama yoyote kupitia kwa wakili wao Paul Kaunda.

“Tumekubaliana utaratibu wa kuondoa dengu ghalani uanze Siku ya Jumatatu hadi Ijumaa ambapo wanunuzi wa dengu watakuja kuchukua dengu zao bila masharti yoyote",amesema.

MWENGE WA UHURU WAHITIMISHA WIKI YA MALIKALE MIKINDANI MTWARA

$
0
0

Maadhimisho ya wiki ya Malikale Mikindani yamehitimishwa rasmi na Mwenge wa Uhuru uiliokabidhiwa leo Mkoa wa Mtwara ukitokea Mkoa wa Lindi.

Akitoa ujumbe wa Mwenge kwa maelfu ya watu waliokusanyika kwenye viwanja vya Mjimkongwe Mikindani, Mkimbiza Mwenge Kitaifa CPL Rehema Ally Haji ameeleza mafanikio makubwa yaliyo tokana na maendeleo ya TEHAMA nchini yakiwemo ya urahisi wa kuhamisha taarifa za waajiriwa, uombaji wa mikopo kwa wanafunzi, uduma za afya nk.

CPL Haji, ameongeza kwa kuwataka wananchi kuchukuwa taadhari dhidi ya janga la UKIMWI kwani limekuwa likitekeza nguvu kazi ya Taifa hususan vijana pamoja na kuendelea kupambana na Janga la UVIKO 19 kama inavyo shauriwa na wataalam wa afya.

Mratibu wa Wiki ya Malikale Mikindani Bi Frida Kombe amesema Maadhimisho hayo yamekuwa na mwitikio Mkubwa wa watu na wameweza kutoa elimu kwa jamii juu ya uhifadhi wa majengo ya kale. 

"Mwenge wa Uhuru umetuletea Baraka katika hitimisho la Maadhimisho haya, hivyo naupongeza uongozi wa Wilaya ya Mtwara Mjini kwa  kuishirikisha  Makumbusho ya Taifa katika ratiba ya Mwenge". Alisema Bi Kombe. 

Maadhimisho ya Wiki ya Malikale Mtwara yaliyozinduliwa rasmi tarehe 25 Agosti 2021 yamehitimishwa rasmi leo tarehe 28 Agosti 2021 na Mwenge wa Uhuru ambao umebeba ujumbe wa "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji".
Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani Mtwara

iongozi mbalimbali wakiwa na Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani



Wananchi wakiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Malikale Mtwara, ambapo Mwenge wa Uhuru uliwasili kwenye viwanja hivyo vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani.

BAKWATA MWANZA YASHAURI WATENDAJI WA MAHAKAMA KULINDA AMANI YA NCHINI

$
0
0

NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA),Mkoa wa Mwanza,limewaasa watumishi wa Idara ya Mahakama na vyombo vya dola,kutenda haki kwenye kesi zinazohusu taasisi za dini ili kuondoa migogoro inayoweza kusababisha taharuki na uvunjifu wa amani.

Pia amewaonya waislamu mkoani humu wasiruhusu chokochoko zinazolenga kuwarudisha nyuma kwenye suala la maendeleo yao na uwe wimbo wa kila mmoja katika kufikia malengo waliyojiwekea lakini kwenye baadhi ya taasisi za kiislamu, kumeibuka jambo ambalo analiona, kadiri wanapofanya vizuri wapo watu wanazuia mazuri yasiendelee kufanyika.

Kauli hiyo imetolewa jana na Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke, wakati akifunga maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu ulioanza Agosti 10 mwaka huu na kutoa mwelekeo wa nini wanakihitaji katika mwaka mpya wa 1443 wa kiislamu.

Alisema baadhi ya watumishi wa Idara ya Mahakama waliokosa maadili na uaminifu wakiwemo wa vyombo vingine vya dola, wanapokea na kusikiliza mashauri yenye sura ya migogoro inayohusu taasisi za kidini kwa hila na kuwataka wawe makini ili wasijiingize kwenye migogoro hiyo na kuwa sehemu ya kuvunja amani.

Sheikhe huyo wa Mkoa wa Mwanza alidai baadhi wanapokea kesi zenye sura ya migogoro ya kidini na kusikiliza upande mmoja bila wadaiwa kuitwa kujitetea ilhali inahusu taasisi za kiimani,wamekosa maadili na uaminifu, wawe makini wanapotoa maamuzi bila kuathiri amani ya nchi.

“Niviombe vyombo vinavotoa haki mfano mahakama,kumekuwa na hila na ujanja ujanja unaotumika, mtu anawahi mahakamani,akifika baadhi ya watendaji waliokosa maadili na uaminifu,wanapokea kesi za aina hiyo na wanaambiwa tuiendeshe na isikilizwe upande mmoja,huyo Bakwata haambiwi,haitwi na hafahamishwi,na huyo hakimu anasikiliza kesi upande mmoja kwa siku moja wakati ni jambo linagusa hisia za umma,linaweza kuhatarisha uvunjifu wa amani,” alisema na kuongeza kuwa;

“Kwa unyenyekevu mkubwa nikiwa kiongozi wa waislamu Mkoa wa Mwanza, niwaombe baadhi ya watendaji wa mahakama,wawe makini na amani ya nchi,chonde chode na ni vizuri tukafahamiana amani hailindwi na mhimili mmoja tu wa serikali,kama jeshi,usalama wa taifa,polisi kwamba hao ndio wanahakikisha amani ya nchi inakuwepo au Rais, Waziri Mkuu,mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya,hapana, amani ya nchi inalindwa na vyombo vyote.”

Alisistiza kuwa taasisi za dini zinawajibu wa kulinda amani ya nchi, lakini alikwenda mbali zaidi kuwa Mahakama na Bunge pia vinawajibu huo,hivyo wanapopelekewa mashauri ya aina hiyo na watu kuwa Bakwata imeingia kwenye misikiti yao, hawaulizwi imeingiaje,Bakwata haihitwi na kuulizwa imekuwapo na inasimamia misikiti hiyo tangu lini, kunakuwa na walakini.

Alisema watu au mtu huyo aulizwe amekuwa kiongozi toka lini, kwa muda gani,aliwekwa na nani,lakini hakimu kuhukumu kesi hiyo bila kuzingatia hoja za pande mbili,inaweza kuleta athari na matatizo gani kwenye jamii, na kwamba baadhi ya taasisi za kiislamu wapo watu wanazuia maendeleo,pia wamechukua mali za BAKWATA na kuzikabidhi kwenye taasisi zingine kinyume.

Sheikhe Kabeke alisema kufanya hivyo wanazua mtafaruku,wanaleta mpasuko na migogoro,hivyo BAKWATA haitaki kuona mali za waislamu zinahamishiwa taasisi nyingine baada ya kuondoa mitafaruku,ugomvi baina ya waislamu, makundi na taasisi zote za kiislamu zimesimama pamoja,waislamu wamerudisha imani na wametoa mali na viwanja vyao na kuleta wakfu, wamejenga misikiti, kuisajili na kuikabidhi BAKWATA.


Mwenyekiti Mwenza huyo wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini aliviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuwa makini na matukio hayo,ni ukweli usiopingika kuwa wana baraza au viongozi wa BAKWATA hawatakubali kuona misikiti yao inachukuliwa na taasisi nyingine,hilo likiachwa bila kuangaliwa kwa macho makini litaleta mgogoro mkubwa.

“Mtu anakuja kusema msikiti huu ama kiwanja hiki hakina mtu,hakina mmiliki hivyo navikabidhi kwenye taasisi fulani ya kiislamu, wakati anafahamu kiwanja hicho au msikiti huo kwa muda wa zaidi miaka 30 kiko chini ya Baraza Kuu la Waislamu,sasa ukifanya hivyo maana yake wewe hauleti tu matatizo madogo,bali mtafaruku na mpasuko kati ya waislamu,”

“Bakwata inayosimamiwa na Mufti,tulijiwekea utaratibu,hatuko tayari kuona mali za waislamu kurudi tuliko toka,zinamilikiwa na watu wachache,mali na vitu vya waislamu vitaendelea kumilikiwa na kusimamiwa na waislamu lakini mtu anakwambia nataka kuusajili msikiti ndani ya taasisi yako,wewe kiongozi wa taasisi hiyo unakubali,unasema karibu unausajili,aha jambo ambalo humwulizi kwa miaka 15 msikiti huu upo ulikuwa chini ya taasisi gani?” alihoji Sheikhe Kabeke.

Aliziomba baadhi ya taasisi akisema mwaka 1442 walikwenda vizuri sana katika hali ya umoja na kuyashika maelekezo ya Mufti, basi wanaotaka kuvuruga wasiwalazimishe waislamu kuingia kwenye mitafaruku na ugomvi kwa kuwa waislamu ni kitu kimoja,na wanafahamu wakiingia kwenye mizozo isiyo ya lazima wanaweza kujenga kitu kibaya sana kikaharibu mazuri yote yaliyokwisha kufanyika.

Aidha alilishukuru jeshi la polisi kusimama imara kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa kwa kuwadhibiti wakorofi wanaoleta chokochoko katika baadhi ya maeneo,Mwanza imetulia na kuwaasa mwaka 1443 wasizue chokochoko na ugomvi wa kurudisha tena waislamu nyuma kwa yale yaliyosemwa zamani na kuonyooshewa vidole,kwani ndani ya Quran Mwenyezi Mungu amesema Shikamaneni katika dini ya Mwenyezi Mungu msifarakane.

Hivyo, mali ikiwa ya taasisi fulani ibaki ilivyo na iwe na ushahidi,ikiwa chini ya BAKWATA vivyo hivyo,asije mtu akasema nakuja kusajili msikiti kwenye taasisi yako na wewe kiongozi ukakubali bila kutafakari na kufanya utafiti, huko ni kusababisha chokochoko na uvunjifu wa amani. Aliongeza kiongozi wa dini ameamua kupaza sauti kulinda amani ya yetu nchi, waislamu na viongozi wa serikali,iwe mahakama na polisi wasikubali kuingia kwenye migogoro ya kuhatarisha amani na kuleta machafuko kwenye jamii,wasipokuwa makini wanapotoa maamuzi ya kesi zenye sura ya migogoro ya kidini, Bakwata haiko tayari kuona hata dhiraa moja ya mali yao inachukuliwa na taasisi zingine kinyume.

 

Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akihitimisha siku ya mwaka mpya wa 1443 wa Kiislamu.Picha na Baltazar Mashaka

TANZANIA YASIKITISHWA NA DENMARK KUFUNGA SHUGHULI ZA UBALOZI WAKE

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesikitishwa na hatua ya Serikali ya Denmark ya kuamua kufunga shughuli za Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ameeleza masikitiko ya Serikali kufuatia hatua hiyo ya Denmark hasa ikizingatiwa jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita za kufufua na kuimarisha diplomasia na uhusiano na nchi rafiki ikiwemo Denmark, kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini pamoja na kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria.

Waziri Mulamula ameyasema hayo jijini Washington, D.C. nchini Marekani tarehe 27 Agosti 2021 wakati wa mazungumzo kwa njia ya mtandao (Video Conference) na Mhe. Flemming Moller Mortensen, Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark kufuatia ombi la Waziri huyo kuzungumza na Waziri Mulamula. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula yupo nchini Marekani kwa ziara ya kikazi.

Kwenye mazungumzo hayo, Waziri Mulamula amemueleza Waziri Mortensen kwamba, pamoja na hatua hiyo iliyochukuliwa na Denmark, ni matarajio ya Tanzania kuwa Serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono ajenda za Tanzania katika Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na majukwaa mengine ya kimataifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen amesema kwamba uamuzi wa kufunga shughuli za Ubalozi wake Tanzania ni wa kisiasa na haukuwa rahisi na kwamba umefikiwa kutokana na vipaumbele vipya vya Serikali ya Denmark kwenye ushirikiano wa maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye mkakati wake mpya uitwao “The World We Share”.

Kwa mujibu wa Waziri Mortensen, mkakati huo mpya unaitaka nchi ya Denmark kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na nchi zenye machafuko na migogoro (fragility countries in conflict or crisis, displacement and irregular migration) hususan katika ukanda wa Sahel, Pembe ya Afrika na Nchi jirani ya hizo ambazo zina matatizo ya kisiasa.

Kadhalika, Waziri huyo amesema kwamba kutokana na Tanzania kufikia hatua nzuri ya maendeleo, Denmark imeamua sasa kufanya kazi kwa ukaribu na nchi tajwa ambazo ameeleza kwamba ndizo zenye uhitaji zaidi na kwamba hatua hiyo haimaanishi uhusiano na urafiki kati ya Denmark na Tanzania unakufa au kufifia. Amemhakikishia Balozi Mulamula kuwa Denmark itaendelea kutekeleza makubaliano ya ufadhili (financial commitments) iliyokwishayafanya kwa Tanzania na itaendelea kuunga mkono jitihada za kuimarisha biashara, ukuaji wa uchumi, demokrasia na Sekta binafsi.

Tanzania sasa itakuwa inahudumiwa na Ubalozi wa Denmark uliopo Kenya.

Mwisho, Waziri Mortensen ameeleza azma yake ya kufanya ziara nchini baadaye mwaka huu.

WAZIRI BASHUNGWA AWAPIGANIA WANAMICHEZO KUPATIWA CHANJO DAR

$
0
0




Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa akizungumza

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa aliyevalia jezi ya timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mpira wa soka na wachezaji wa timu za taifa za wanawake (Twiga Stars na Tanzanite) alipowatembelea wakiwa mazoezini katika viwanja vya Kidongo chekundu maarufu kama JK Park jijini Dar es Salaam.



Na John Mapepele, WHUSM

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya leo Agosti 28, 2021 imeratibu zoezi la hiari la siku mbili kwa timu za Taifa za michezo na wadau wote wa michezo upatiwa chanjo ya Uviko-19 jijini Dar es Salaam ili kujikinga na ugonjwa huo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa amesema makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya kazi zao, wako katika hatari ya kuambukizwa.

“Ninapenda tena leo kuendelea kusisitiza na kuhamasisha wanahabari, wanautamaduni, wasanii na wanamichezo wenzangu kuendelea kupata huduma ya chanjo. Sekta zetu zinahudumia wananchi na hivyo kulazimika kukutana na makundi ya watu mara kwa mara. Kutokana na hivyo tuna hatari kubwa ya kuambukizwa, ama sisi wenyenyewe au kuambukiza wananchi ambao ndio wadau wetu wakubwa tunaowapa huduma. Kwa vyovyote vile ni lazima tujikinge lakini pia tuwakinge wadau wetu”. Amefafanua Mhe. Bashungwa

Amesema ili kufanikisha zoezi hilo vimefunguliwa vituo maalum ndani ya uwanja wa Mkapa na Uhuru vitakavyokuwa vikitoa huduma ya chanjo hiyo kuanzia saa 3 asubuhi kwa siku zote mbili ili kutoa fursa kwa wadau wote kupata huduma ya chanjo.

Ameushukuru Uongozi wa Klabu ya Simba kwa kuwapa chanjo wachezaji wao.

Aidha, amepongeza Klabu ya Yanga ya kutumia wiki yao ya wananchi kuhamasisha na kupata chanjo na kulifanya zoezi hilo la uchanjaji kuwa miongoni mwa shughuli zao muhimu watakazo zifanya siku hiyo ambapo pia ametoa wito kwa vilabu vingine vya soka nchini kuhamasika na kuwapatia chanjo wachezaji na watumishi wao.

Mkurugenzi wa Michezo nchini Yusuph Singo Omary amemhakikishia Mhe. Waziri kuwa maandalizi yote ya zoezi la chanjo yamekamilika na tayari wadau mbalimbali wa michezo wamepongeza hatua ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea kuwapa kipaombele wadau ili wajikinge.

Ametoa wito kwa Wasanii, Wanahabari na Wachezaji kwa hiari yao kujitokeza na kutumia fursa hii kipata chanjo ili kujikinga na kuwakinga wengine na ugonjwa wa UVIKO 19

MAJALIWA: RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUTOA FURSA KWA WANAFUNZI KUTIMIZA NDOTO ZAO

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikari inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikiisha sekta ya elimu inapata muelekeo mpana na kutengeneza fursa kwa watoto wa kitanzania kutimiza ndoto zao za kusoma katika ngazi zote mpaka vyuo vikuu.

Amesema kuwa katika kufanikisha hilo Serikali imeendelea kuboresha miundombinu kwa shule za msingi, Sekondari pamoja na kuongeza idadi ya vyuo vikuu nchini lengo likiwa ni kuwaandaa watoto kutimiza ndoto zao.

Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumamosi, Agosti 28, 2021) alipokuwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoani Tabora, ambapo ametembelea Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Tabora na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tabora ambako pia amefurahishwa na matokeo ya ufaulu wa shule hizo kimkoa na kitaifa sambamba na maboresho ya miundombinu yaliyofanywa katika shule hizo kongwe.

“Mheshimiwa Rais kaleta fedha nyingi sana za sekta ya elimu, kaleta Bilioni moja, akaleta tena Milioni 500 na fedha nyingine Bilioni saba ambazo naamini zimeshafika na zitajenga madarasa 590 ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea watoto wa kidato cha kwanza, Hii Bilioni saba ni sehemu ya Bilioni 29 ambazo zimesambazwa kwa ajili ya sekta ya afya na elimu makusanyo ambayo yametokana na miamala.”

Aidha, Waziri Mkuu amesema hivi karibuni Rais Samia, ametoa kibali cha kuajiri walimu wa masomo ya sayansi, ili kukabiliana uhaba wa walimu katika masomo ya sayansi ili kuweka uwiano sawa wa ufundishaji baina ya walimu na Wanafunzi.

“Tumefurahi sana kuona kuna Watanzania wenzetu wanajitolea tunajua wanafanya kazi, napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inalitazama suala hilo kwa umakini mkubwa na ninaiagiza Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha walimu hawa wanapewa kipaumbele katika ajira, wameonesha uzalendo wa hali ya juu.”

Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tabora, Mheshimiwa Majaliwa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha shule zote kongwe zinakarabatiwa na kuzirudisha katika ubora na ili kuwa na mazingira rafiki ya ujifunzaji na ufundishaji.

Hali kadhalika, Waziri Mkuu ameliomba Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Tabora kuweka utaratibu na kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule hizo.





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ukarabati wa majengo ya Shule ya Sekondari ya wavulana Tabora wakati alipotembelea Shule hiyo,



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ukarabati wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora wakati alipotembelea Shule hiyo, Agosti 28, 2021. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Deogratias Mwambuzi.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kitabua ambacho Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alisajaliwa kuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora kwa nambari 590 wakati alipokagua ukarabati wa majengo ya shule hiyo,



Muonekano wa sehemu ya bweni la Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora baada ya ukarabti uliofanywa na serikali. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ukarabati huo, Agosti 28, 2021. (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)

IGP SIRRO - WANANCHI WASHIRIKIANE NA VYOMBO VYA DOLA

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini pindi wanapoona jambo lisilo la kawaida ili kuweza kuchukuliwa hatua za haraka kabla ya kuleta madhara kwa jamii.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa gwaride maalum la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Jeshi hilo akiwemo Balozi Valentino Mlowola, Robert Boaz aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini, Dare s salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kumalizika kwa gwaride hilo pia IGP Sirro amezungumzia suala la mtu aliyewashambulia askari Polisi kwa risasi na kuwaua na baadae mtu huyo nae kuuawa amesema Jeshi hilo limemaliza taratibu zake hivyo familia inaruhusiwa kuuchukua mwili wa kijana huyo kwa ajili ya taratibu nyingine.

Kwa upande wake Kamishna Mstaafu Robert Boaz amesema licha ya kustaafu utumishi wa umma lakini bado ataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea kutenda kazi zake kwa weledi na kwa kufuata misingi ya kanuni na taratibu zilizopo.



DCI MSTAAFU ROBERT BOAZ AAGWA KWA HESHIMA

$
0
0

 Matukio mbalimbali pichani ya kionesha namna Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini Kamishna Mstaafu Robert Boaz akiagwa kwa gwaride maalum la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake baada ya kumaliza utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria, hafla ya kumuaga ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini, Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.







 

WAKULIMA WA MBAAZI TUNDURU WAENDELEA KUVUNA FEDHA KUFUATIA KUPANDA KWA BEI YA ZAO HILO

$
0
0

  Na Muhidin Amri,Tunduru


WAKULIMA wa mbaazi katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameendelea kuvuna  fedha kufuatia kupanda kwa bei ya zao hilo kutoka shilingi 1,294 katika mnada wa kwanza hadi shilingi 1,428 mnada wa tatu.

Wakizungumza, wakati wa mnada wa tatu uliofanyika katika kijiji cha Lukumbule wilayani humo,baadhi ya wakulima wamefurahi  mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umewezesha  kupanda kwa bei ya mbaazi  kwa kila mnada.

Hadija Mitete amesema, kabla ya zao hilo kuingizwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani hawakuwa na manufaa yoyote licha ya kutumia nguvu kubwa katika uzalishaji kutokana na wafanyabiashara kununua mbaazi kwa bei ndogo tofauti na sasa tangu Serikali ilipoanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani.

Ameipongeza Serikali kwa kusimamia mfumo  huo, ambao umewasaidia kumaliza unyonge wa muda mrefu wa kukosa soko la uhakika wa zao hilo ikilinganisha na wakulima wa mazao mengine.
Hata hivyo,amewaomba wanunuzi kulipa fedha kwa wakati ili  ziwasaidie kusomesha watoto na kununua pembejeo za kilimo hususani dawa(Salphur)kwa ajili ya kupulizia korosho.

Daimu Kalambo amesema, mfumo wa stakabadhi ghalani ni nzuri kwa kuwa umeleta tija  kwa wakulima kwa kupata bei  kubwa ya mazao yao tofauti na soko hulia ambapo wafanyabiashara walinunua mazao kwa bei wanayopanga wao jambo lililosababisha umaskini mkubwa kwa wakulima.

Ameiomba Serikali, kuendelea kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani hata kwa mazao mengine ya biashara ikiwemo mpunga ili kuwasaidia wakulima kupata soko la uhakika na bei nzuri.Kwa upande wake Afisa Ushirika wa wilaya ya Tunduru George Bisani amesema,  katika mnada huo jumla ya kilo 1,324.886 zimeingizwa mnadani  na wanunuzi saba walijitokeza katika mnada huo.

Bisani amesema, kampuni ya Export Trading Co Ltd imeshinda  ambayo imenunua mbaazi zote kwa bei ya Sh.1,428 kwa kilo moja na kufanya jumla ya Sh. 1,891,937,208.00 kuingia katika mzunguko wa fedha katika wilaya ya Tunduru kupitia zao la mbaazi.

Amesema, mpaka sasa  mwenendo wa  minada ni nzuri kwa bei  ya mbaazi inaendelea kupanda tokea mnada wa kwanza ambayo ilikuwa Sh 1,294 kwa kilo moja.

Kwa mujibu wa Bisani,katika mnada wa pili bei ilikuwa Sh 1,341 kwa kilo moja ikiwa ni ongezeko la Sh. 47 na katika mnada wa tatu bei imefikia Sh 1,428 sawa na ongezeko la Sh 87.

Bisani, amewashukuru wakulima wote ambao wameamua kupeleka mazao yao kwenye Vyama vya msingi ili wakutanishwe na  wanunuzi  wenye bei ya juu(kubwa) ambayo itahamasisha wakulima wengi zaidi kupeleka mbaazi zao kwenye vyama vya ushirika na kuongeza uzalishaji katika msimu ujao.

Amewatoa hofu wakulima juu ya  kukosekana kwa vifungashio(mifuko) na kusema kuwa,tayari Serikali kupitia Chama Kikuu cha Ushirika imeshaleta kwa wingi na vinatosheleza mahitaji ya wakulima wa zao hilo.

Aidha amesema kuwa,malipo ya wakulima  waliopeleka mbaazi katika mnada wa tatu wataingiziwa fedha  kwenye akaunti zao ndani ya siku saba tokea  siku ya mnada.

Akifunga mnada huo, Kaimu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wilayani humo(Tamcu Ltd) Pino Chikojola, ameishukuru Serikali kwa kuwadhibiti wanunuzi na walanguzi holela wa mazao ambao wanapenda wapate faida kubwa na kumuacha mkulima akiendelea na umaskini.

Amesema, mfumo wa stakabadhi ghalani katika wilaya ya Tunduru umewezesha kupandisha  uzalishaji na thamani ya mazao yao.

Amewataka wakulima kujitahidi kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara ili kutatua changamoto ya umskini kwenye kaya zao kwa kuwa Serikali imeonesha dhamira ya kuwasaidia wakulima.

Afisa Ushirika wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma George Bisani akisoma taarifa ya mnada wa tatu wa zao la mbaazi uliofanyika katika kijiji cha Lukumbule ambapo zaidi ya kilo milioni 1.3 zimeingizwa katika mnada huo.
Baadhi ya wakulima na wananchi wa kijiji cha Lukumbule wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakimsikiliza jana Afisa Ushirika wa wilaya hiyo George Bisani(hayupo pichani)wakati wa mnada wa tatu wa zao  la mbaazi  zinazouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani. Picha zote na Muhidin Amri,

MCHUNGAJI KABONAKI KANISA LA BAPTIST KINONDONI AONGOZA IBADA KULIOMBEA TAIFA, ASISITIZA KUMTUMAINIA MUNGU KWA KILA JAMBO

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WAUMINI wa Kanisa la Baptist Kinondoni mkoani Dar es Salaam  wakiongozwa na  Mchungaji wa kanisa hilo Samweli Kabonaki wamefanya ibada maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Akizungumza wakati wa Ibada hiyo ,Mchungaji Kabonaki amesema Watanzania na Dunia wanajua kipindi tunachopitia kutokana na uwepo wa janga la Corona ambalo limeleta madhara katika mataifa mbalimbali,hivyo wameona ni vema Kanisa hilo likafanya maombi maalum kuliombea taifa la Tanzania.

Amesema kwamba katika kukabiliana na janga la Corona pamoja na hatua ambazo zinachukuliwa, ni vema kila mmoja wetu akamtanguliza Mungu zaidi na yvema ikajulikana Mungu ndiye mwenye majibu yote na  ni mponyaji mkuu.

Amefafanua hilo kwa kunukuu maandiko matakatifu kutoka Neno lilitoka 1 Wafalme 18:35-40 na ijulikane kwamba katika Tanzania kuna Mungu wa pekee ndiye Mungu aponyaye.

Katika hatua nyingine Mchungaji Kabonaki amewaomba waumini wa kanisa hilo wafuate maelekezo kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na watalaam wa afya kuhakikisha kila mmoja anajikinga na kumkinga mwingine dhidi ya maambukizi ya Corona.

"Watumishi wa Mungu tunalo jukumu la kuliombea Taifa na watu wake wakiwemo viongozi wetu, lakini kwa nafasi ya kila mmoja wetu tunatakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia watalaam wake wa afya,"amesema Mchungaji Kabonaki.

Amesisitiza kuwa utawala wa Awamu ya Sita umekuwa ukimtanguliza Mungu mbele ,hivyo amewaomba Watanzania kuendele kuwaombea viongozi wote ili watekeleze majukumu yao licha ya kuwepo kwa vikwazo mbalimbali.

Mchungaji Kabonaki pia amewaomba waumini wa dini ya Kikristo kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira kwani bila kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata nafasi katika jamii."Kwa nafasi yetu tutahakikisha tunaendelea kufanya Maombi kuiombea Serikali ya Awamu ya Sita na viongozi wake."

Pia amewaomba wananchi wote kuhakikisha hawawapi nafasi watu ambao wamekuwa na roho za uadui,kusema vibaya na kukatisha tamaa wengine."Tusivunjike moyo kwa maneno ya watu wenye roho za uadui,chuki,usenganyaji na wenye kukatisha tamaa.Sisi sote tujikite kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi yetu."

Mchungaji wa Kanisa la Baptist Kinondoni ,Samweli Kabonaki (kulia) akiongoza ibada ya maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kipindi hiki cha janga la Corona  leo mkoa wa  Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel wa Michuzi TV)

Ibaada ya kuliombea taifa ikikendelea.
Waimbaji wa kwaya ya Shalom wakiimba wakati wa ibaada ya maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kipindi hiki cha janga la Corona leo  Mkoa wa Dar es Salaam.




Waumini wa Kanisa la Kanisa la Baptist Kinondoni mkoani Dar es Salaam wakiendelea na maombi ya kuliombea Taifa.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG TV)

IAA YAJENGA MIRADI YA BILIONI 15

$
0
0

Na Pamela Mollel, Arusha

Chuo cha uhasibu Arusha IAA kimeanza ujenzi wa miradi ya zaidi ya bilioni 15 kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji elimu chuoni hapo.

Akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua miradi hiyo naibu waziri wa fedha na mipango  Hamad Yussuf Masauni, alisema ameona majengo kadhaa yakiwa yamekamilika na mengine yakiwa yanaendelea kujengwa yakiwemo ya maktaba, mabweni, sehemu ya chakula na sehemu ya kujisomea (Vimbweta).

kwa upande wa jengo la chakula  litagharimu zaidi ya Sh.bilioni 1.3 na linatarajia kukamilika Oktoba mwaka huu.

Alisema katika majengo mengine kutakuwa na kituo cha ukuzaji  na uendelezaji wa biashara na kitengo cha TAHAMA ambayo yapo katika hatua nzuri ya ujenzi.

"Miradi hii muhimu kwa wanafunzi wetu kama ujenzi wa mabweni, utakapokamilika  utasaidia wanafunzi hususani watoto wa kike, kuendelea  na masomo, lakini pia kwa chuo watapata kipato cha pango watakazolipa na  kujiletea maendeleo ya chuo"alisema.

Aidha alisema  serikali iko tayari kuongeza nguvu  kwa  yale maeneo ambayo watahitaji msaada ili  kuongeza kasi  ya  kuwaandaa wanafunzi kuwa tayari kwaajili ya maisha yao  na wahitimu wanaomaliza fani mbalimbali chuoni  waweze  kujiajiri  na kujiendeleza wenyewe, badala ya kusubiri kuajiriwa.

"Tuna waunganisha wanafunzi wetu na makampuni ya umma pamoja na Taasisi binafsi za masuala ya kodi, masuala ya benki kwa sababu soko lake ni zuri  nchini, kwani maeneo haya mazuri yanatengeneza   fursa kwa vijana wetu wa  kitanzania za kujiajiri,"alisema.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka alisema  kwasasa chuo kinatekeleza  miradi itakayowezesha wanafunzi kupata elimu kwa ufanisi zaidi, mbali na madarasa, maktaba, sehemu za kulia chakula na mabweni lakini pia utengenezaji wa vimbweta vyenye mfumo wa umeme lakini pia uwepo wa mtandao(Internet) vita waweze kusoma kwa urahisi.

"Tunatarajia Oktoba mwaka huu wanafunzi wataongezeka kutokana na chuo kuongeza baadhi ya fani lakini pia uboreshaji huu tunaoufanya,"alisema.

Prof.Sedoyeka alisema  ujenzi wa  bweni unoendelea chuoni hapo, kwa awamu ya kwanza ambao utakamilika mwezi oktoba mwaka huu unakadiriwa kubeba  wanafunzi 2000 huku matarajio ni kufikisha wanafunzi 5000 ifikapo mwakani.

"Tunaalika wenye nyumba karibu na chuo chetu ambao wanania ya kugeuza majengo yao kuwa mabweni, kwani tutayakagua na tukijiridhisha tutawaweka wanafunzi wetu huko" aliongeza.

Sambamba na hilo alisema kitengo Cha  ubunifu kwa wanafunzi, ni mpango endelevu  na   wanafunzi wote  watalazimika kuja na wazo la kibiashara Ili  kuwaandaa wataalamu wabobezi watakaoendana na soko la ajira.
Picha ya pamoja ya watendaji wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Mhandisi Hamad Yussuf Masauni mara baada ya kutembelea ujenzi wa miradi mbalimbali chuoni hapo.

Naibu waziri wa fedha na mipango Hamad Yussuf Masauni akimwagilia maji mti Mara baadaye ya kuupanda ikiwa ni sehemu ya  ishara ya kumbukumbu alipotembelea ujenzi wa miradi chuo cha uhasibu Arusha (IAA).
 
Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) Prof.Eliamani Sodoyeka akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Mhandisi Hamad Yussuf Masauni namna miradi miradi mbalimbali inavyotekelezwa chuoni hapo wakati wa ziara yake.(Picha na Pamela Mollel)

WAKALA PLUS YAWAFIKIA WANA RUVUMA.

$
0
0

Benki ya NBC imeendelea kuongeza juhudi za kuwafikia Watanzania katika kila kona ya nchi kwa dhumuni la kujenga jamii yenye uchumi shirikishi, juhudi zinazoenda sambamba na malengo Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma za kibenki.

Benki  hiyo imefanya hivyo kupitia huduma yake ya NBC Wakala Plus kwa kufungua tawi ya wakala mkuu katika Mtaa wa Mama Madaba, Mji wa Mbinga, Mkoani Ruvuma katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbali mbali.

Hatua hii imefanyika miezi kadhaa baada Benki ya NBC kuzindua tawi kama hilo la NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi na kuleta manufaa kwa wajasiriamali na wananchi wa mkoa huo.

Pamoja na kusogeza  huduma za kibenki kwa wananchi, NBC Wakala Plus pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa mbali mbali za kibiashara pamoja na kuinua uchumi wa wafanyabiashara, waajiriwa na wakulima wa mkoa huo.

Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudh weee uria hafla ya uzinduzi wa NBC Wakala Plus, Mgeni rasmi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Grace  Quintine ameipongeza Benki ya NBC kwa kuona fursa kubwa wilayani humo zinazotokana na shughuli mbali mbali za kiuchumi zinazofanywa na wananchi.

Grace amesema benki hiyo imefanya  uwekezaji wake na kutoa elimu kwa wakulima na wajasiriamali wa wilaya ya Mbinga na  kwamba Benki ya NBC imeonyesha mfano wa kuigwa wa kutoa elimu kwanza kabla ya kuleta huduma hali inayopelekea wakazi wa Mbinga kutumia huduma za kibenki kikamilifu ili kuwaletea maendeleo.

Aidha, Grace pia ameishukuru benki hiyo kwa msaada wa  mabati 240, mifuko 120 ya saruji na kilo 30 za misumari ya bati katika kuchangia juhudi za kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Nazareth iliyopo Wilaya ya Mbinga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Elibariki Masuke amesema kuwa uzinduzi wa Wakala Mkuu wa NBC Mbinga ni moja ya mikakati ya benki hiyo ya kupanua na kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi kwa wananchi hasa katika maeneo yanayokua kiuchumi.

“NBC inaamini kwamba mpango wa upandaji wa mawakala wakuu katika maeneo yenye uchangamfu wa kiuchumi utaongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa wananchi na kuinua kipato cha wajasiriamali. Mchakato wa NBC Wakala Plus unaenda sambamba na malengo ya serikali yetu ya kusogeza huduma bora kwa wananchi  kwani mawakala wetu wakuu watatoa huduma kama zile zinazotolewa katika matawi yetu yalioenea nchi nzima.” amesema Masuke.

Aidha kwa upande wake, mmiliki wa ofisi hiyo ya NBC Wakala Plus, Agasto James ameishukuru Benki ya NBC kwa kumpa fursa hiyo ya kipekee itakayomuongezea kipato pia kuwa wakala mkuu inampa  fursa mbali mbali kwa wakazi wa Mbinga hasa wale watakaotumia ofisi yake kupata huduma mbali mbali zikiwemo kuweka, kutoa, kupokea na kuhamisha fedha, kufungua akaunti mbali mbali na kupata kazi mbali mbali za kibenki pamoja na kufanya malipo na kodi za serikali kupitia mfumo wa GePG.

Kabla ya uzinduzi wa NBC Wakala Plus Wilayani humo, Benki ya NBC iliendesha semina kwa makundi mbali mbali ya wajasiriamali kwa dhumuni la kutoa mafunzo ili kuwasadia wajasiriamali hao kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi. Kupitia semina hizo, Benki ya NBC pia ilipata fursa ya kutambulisha bidhaa zake na kuwaelimisha wajasirimali hao juu ya faida na manufaa ya bidhaa hizo.

Pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa semina hizo pia zililenga viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika (AMCOS) Wilaya na Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kwa lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni  pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi. Mafunzo kwa wakulima yalilenga kufafanua  zaidi huduma ya #NBCShambani inayowalenga wateja wanaoshughulika katika sekta ya kilimo


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Grace  Quintine (wanne kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa  o fisi ya Wakala Mkuu wa huduma ya Benki ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Wilaya ya Mbinga mkoani  Ruvuma yenye lengo yakuwafiki a na ku wa sogeza huduma za kibenki kwa wananchi   na wateja wake .   Wengine kwenye picha ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC  Elibariki Masuke (w anne kulia )  na  Wakala wa Ofisi hiyo , Nd. Agasto James (watatu kulia )  na wengine ni maofisa kutoka Benki hiyo.

SERIKALI YAANZA NA BILIONI 149/- KUFANIKISHA BIMA YA AFYA KWA WOTE, YAIPONGEZA NHIF KUTIMIZA MIAKA 20

$
0
0

Na Karama Kenyunko,Michuzi TV .


SERIKALI imetenga sh.bilioni 149 kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa Bima ya Afya kwa Wote ambapo Muswada unatarajiwa kupelekwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Septemba mwaka huu ili kuwa sheria rasmi.

Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa mkutano wa sita kati ya Wahariri na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao mwaka huu unasherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema wakati Watanzania wakijiandaa kuingia kwenye utaratibu wa bima ya afya kwa wote, Serikali imeona ni vema ikaanza kwa kutenga fedha hizo kufanikisha azma hiyo.

“Itaanza na wananchi wasio na uwezo kwa kugharamia matibabu na baadae itaendelea kupanua hadi itakapoweza kuwafikia watanzania wote. Ni matarajio yangu kuwa wahariri tutaibeba dhamira hii ya Serikali na kuhakikisha waandishi wetu wa habari wanaandika habari za kuhakikisha ajenda hii inafanikiwa ili watanzania waendelee kunufaika na huduma za bima ya afya,”amesema Msigwa.

Aidha ameipongeza NHIF kwa kupanua huduma za mfuko huo ambapo sasa pamoja na wafanyakazi , hata mtu moja mmoja ana uwezo wa kujiunga na mfuko. Pia amepongeza NHIF kwa kuviwezesha vituo mbalimbali vya kutolea tiba kuboresha huduma kwa kuvipatia mikopo ambayo inalipilika kwa urahisi.

Amesisitiza hilo ni jambo muhimu kwasababu mwisho wa siku nchi inakuwa na huduma bora za matibabu na kwa pamoja tutaweza kuokoa maisha ya wananchi walio wengi.Aidha amewaomba wahariri kuendelea kushirikiana na mfuko kutoa mchango wowote ambao wataona unafaa ili kuimarisha mfuko huo.

“Tunapokutana na taarifa zinazohusu huduma za afya tuwakumbuke watanzania wenzetu ambao wanataabika kupata huduma za matibabu kutokana na kukosa uwezo wa kulipia gharama za matibabu.Tutumie kalamu zetu kuhakikisha huduma za mfuko huu zinaimarika na zinaswanufaisha watanzania wengi zaidi”amesema Msigwa.

Akifafanua zaidi kuhusu mfuko huo  amesema yeye ni mwandishi wa habari hivyo anafahamu wahariri na waandishi wa habari wakiamua nchi hii iimbe wimbo wa bima ya afya wanaweza , wakiamua viongozi watoe umuhimu wa pekee kwa mfuko wa bima ya afya wanaweza.Wakiamua wadau wajitokeze waunge mkono mfuko huo wanaweza.“Wahariri ni muhimili imara ndani ya nchi na Serikali inawahaheshimu.”

Aidha amesema Serikali inatambua kazi kubwa na nzuri ambayo imefanywa na mfuko huo tangu kuanza kwake mwaka 2001 katika kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa kila mtanzania licha ya kupitia changamoto lukuki lakini mfuko umeendelea kuimarika siku hadi siku.

“Kwa dhati ya moyo wangu naomba mniruhusu nikupongeze Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Benard Konga ,watumishi wa NHIF na Serikali kwa ujumla kwa kusimama kidete kuhakikisha mfuko huu unasonga mbele hadi leo hii unatimiza miaka 20 tangu uanzishwe.Tuliopita katika mapambano haya leo tunafarajika sana kuona mfuko huu sasa umekuwa kimbilio , kila mtanzania anataka kujiunga kwasababu sasa faida za mfuko zinaonekana dhahiri,”amesema Msigwa.

Amefafanua kwa wale ambao wamesahau ama hawakuwepo wakati mfuko huo unaanzishwa miaka 20 iliyopita amewaambia kuwa haikuwa rahisi .”Upinzani ulikuwa mkubwa sana , shukrani kwa msimamo thabiti uliowekwa na serikali kuwa ni lazima uanze , nakumbuka vyama vya wafanyakazi vilivyokuwa vikipinga watumishi kukatwa fedha kwa ajili ya kuchangia mfuko.

“Kuna wakati hata sisi waandishi wa habari tuliokuwa tunaandika kuhamasisha mfuko huu tulikuwa tunakata tamaa lakini tunashukuru leo tuko hapa tukifurahia mafanikio ya mfuko,”amesema Msigwa.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Benard Konga amesema mfuko huo ulipoanzishwa mwaka 2001 changamoto kubwa ilikuwa ni kukubalika hasa kwa sababu unahusisha kuchangia fedha lakini pia namna ulivyoanzishwa ,hivyo ilihitajika nguvu kubwa ya kuelimisha umma kuhusu dhana ya bima ya afya na umuhimu wake. Historia inaonesha mchango mkubwa uliofanywa na Wanahabari na Wahariri katika kuelimisha umma na hasa kwa sababu Mfuko uliwashirikisha sana.

Hivyo amesema lengo la kukutana na wahariri kwenye mkutano huo ni kutaka kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa kwa taasisi hiyo kwa miaka 20 ya uhai wa NHIF na kwamba itaendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha mfuko unaendelea kusonga mbele kwa mafanikio makubwa ya kutoa huduma za afya kwa watanzania wote.

Amesema mfuko huo kwa kipindi chote cha uwepo wake umekuwa na mchango mkubwa katika sekra ya afya kwani umefanikiwa kujenga majengo ya kutolea huduma za fya, umejenga hospitali na kununua vifaa tiba na kwamba mafanikio yote ambayo yanaonekana kwenye hospitali zote kubwa zikiwemo zile za rufaa nyuma yake kuna mkono wa NHIF katika mafanikio hayo.

Akifafanua zaidi sababu ya kikao hicho, Konga amesema lengo moja la kukutana siku ya leo ni katika kuadhimisha miaka 20 ya Mfuko tangu kuanzishwa kwa Mfuko pamoja na wahariri, aidha kama ilivyo ada  katika mkutano huo pia watapeana mrejesho ya yaliyofanyika katika kipindi chote hicho na kupata mrejesho kutoka kwa wahariri wa nini umma unapata kutoka kwao na kipi ambacho bado hakijakidhi mahitaji ya Watanzania.

Aidha Konga amesema mfuko huo umetoka mbali kiutekelezaji wa majukumu yake na  umeendelea kushirikiana na wadau wake katika kutekeleza hayo.”Kwa kuwa yataongelewa zaidi kwenye mada mimi nagusia kidogo tu. Tunapoongelea tulipotoka na tulipo tunaweza kuongelea haya: Wote sasa wamewekewa utaratibu wa kujiunga na Mfuko tofauti na hapo awali ambapo makundi machache na hasa watumishi ndio waliwezeshwa kujiunga.

“Tumewezesha vituo mbalimbali kuimarisha huduma za matibabu na miundombinu kupitia mikopo nafuu inayotulewa na NHIF. Vituo kama MNH, MOI, KCMS, BMH na vingine ni wanufaika,Malipo kwa Watoa huduma yamewezesha vituo kuwa na mapato ya uhakika ambayo yanawezesha vituo kuimarisha huduma,”amesema Konga.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akikata keki huku akishudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya (NHIF), Bernard Konga (katikati) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ikiwa ni ishara ya kudumisha ushirikiano wakati wa mkutano wa sita kati ya Wahariri na NHIF ambao mwaka huu unasherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 28, 2021 jijini Dodoma.


Msemaji Mkuu wa Seikali ambaye ni Mgeni rasmi katika mkutano huo, Msigwa (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Konga (kushoto) na Mwenyekiti wa TEF, Balile wakibadilishana keki kabla zingine kuzigawa kwa wahariri na waandishi wa habari waliokuwepo wakati mfuko huo unaanzishwa mwaka 2001.


Baadhi ya wahariri waliokuwepo wakati NHIF inaanzishwa mwaka 2001 wakikagawiwa keki


Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini wakionesha keki hizo baada ya kugawiwa. Baadaye wahariri wote waliohudhuria mkutano huo walikula keki hiyo.
Meneja Uhusiano wa NHIF, Anjela Mziray akizungumza neno la utangulizi wakati wa kuanza mkutano huo.


Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga akielezea historia ya mfuko huo ulioanzishwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu mwaka 2001.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
 

Sehemu ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa makini kusikiliza yaliyokuwa yanajiri mkutanoni.

 

Baadhi ya maafisa wa NHIF wakiwa katika mkutano huo ambapo baadhi walijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wahariri kuhusu mfuko huo.

Ummy aifanya Kahama Shamba darasa, Awapeleka RC’S, RAS’S kujifunza

$
0
0

 

 

Na Atley Kuni – KAHAMA.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amelazimika kuigeuza Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kuwa sehemu ya Shamba darasa kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kote nchini.

 

Hatua hiyo ya Waziri Ummy imewafikisha viongozi hao katika miradi ya uwezeshaji ya wananchi kiuchumi kwenye eneo la Chapulwa, lenye ukubwa wa hekari 2000 huku hekari 90 zikiwa zimetolewa kwa mwekezaji, na  katika eneo la Zongomera  lenye hekari 2100, Hekari 500 zimegawanywa kwa wajasiriamali ili waendeshe shughuli za kibiashara na ufundi.

 

Wakionekana kuguswa na hatua zilizochukuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, yakuwawezesha wanachi kujikwamua kiuchumi, Wakuu hao wa Mikoa wameaahidi kutumia fursa ya maarifawaliyopokea kwaajili ya Mikoa yao.

 

Akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa wenzake, Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa John Mongella, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amesema ziara hiyo imewafungua macho, hivyo watachukua hatua za haraka katika kufanikisha azma hiyo kwakuwawezesha wananchi kwenye maeneo yao.

 

“Mhe. Waziri, Mimi kwa niaba ya viongozi wenzangu hatuna lakusema kwa sasa, ila tumuahidi Mhe. Rais kwamba, tunakwenda kuishi viapo vyetu, moja ikiwa nikuhakikisha maarifa haya ambayo wenzetu wa Kahama tumevuna kwao, sisi tutakwenda kufanya vizuri zaidi” alisema Mongella.  

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adamu Malima, hakusita kuonesha hisia zake mbele ya Waziri Ummy na kutoa maelekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo, kuhakikisha manunuzi ya Jozi tatu za Masofa ambazo zilikuwa zimepangwa kununuliwa na Ofisi hiyo ya Mkuu wa Mkoa kwenye maeneo mengine, sasa manunuzi hayo yafanyike kwenye kampuni ya  *Wahitime Furniture* ya Kahama Shinyanga ilioanzisha kiwanda cha Furniture katika eneo hilo la biashara ikiwa ni jitihada zakuunga Mkono shughuli hiyo inayofanywa na vijana wazalendo wa kitanzania.

 

Awali akitoa maelezo Mbele ya Waziri wa Nchi na Ujumbe wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba, alisema wao kama Manispaa walikaa na kuamua kutoa Hekari 500 bure kwa wananchi, lakini mara baada ya Mradi kuanza, sasa Halmashauri inakusanya  shilingi Milioni. 80 kila mwaka, fedha inayoingia kama sehemu ya mapato ya ndani.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakati wa ziara hiyo yakikazi kwenye Manispaa ya Kahama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakati wa ziara hiyo yakikazi kwenye Manispaa ya Kahama, huku wakijionea bidhaa za makochi zinazo zalishwa na Wahitime Feniture
Eneo la Chapulwa kama linavyo onekana kwa juu, ambapo Zaidi ya Hekari 900 zimegaiwa kwa mwekezaji.
 
Fundi akiendelea na kazi katika kiwanda cha Wahitime cha Manispaa ya Kahama


OCEAN CITY COMMUNITY MARATHON WASHINDI KUONDOKA NA GARI, WANARIADHA WATAKIWA KUJITIMA

$
0
0

 

Mwanariadha wa zamani na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Mbio za Ocean City Community Kanali Juma Ikangaa akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yatakayofanyika Oktoba 3 mwaka huu.

Mwakilishi kutoka Jan International Basilisa Biseko akizungumzia ushiriki wa kampuni yao katika mashindano hayo ambayo leo wametiliana saini makubaliano ya zawadi ya gari kwa washindi wa upande wa wanaume na wanawake kwenye mbio za Ocean City Community zitakazofanyika Oktoba 3 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Jan International Muhamad  Chishti (katikati), Mwenyekiti wa Riadha Dar es Salaam Catherine Nyamko, Mwakilishi kutoka One Plus Event Bakari Ramadhan (wa kwanza kushoto) , mwanariadha wa zamani Kanali Juma Ikangaa (wa pili kulia)  wakikata utepe kuashirikia uzinduzii wa Mashindano ya  Ocean City Community Marathon zitakazohusisha Mbio za Km 21.1, km 10 na Km 5 na   Zitafanyika Oktoba 3 mwaka huu katika Viwanja ya The Green Oysterbay.
Mkurugenzi wa Jan International Muhamad  Chishti (kulia) na Mwakilishi kutoka One Plus Event Bakari Ramadhan wakitia saini makubaliano ya zawadi ya gari  kwa washindi wa Ocean City Community Marathon zonazotarajiwa kufanyika Oktoba 3 mwaka huu katika Viwanja ya The Green  Oysterbay.



Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

WANARIADHA nchini wametakiwa kuongeza juhudi,kujituma na kufanya mazoezi ili waweze kuiwakiliasha nchi kwenye mashindano makubwa ya kimataifa.

Hayo yanesemwa na Mwanariadha wa zamani Kanali Juma Ikangaa wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya zawadi ya magari ya washindi wa Mbio za Ocean  City Community kati ya Kampuni ya One Plus na Jan International yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Kanali Ikangaa amesema, ili taifa la Tanzania liweze kufika mbali katika mchezo wa riadha haina budi kwa wanariadha kufanya mazoezi kwa bidii zote ili wapate nafasi ya kuwa wawakilishia wa mashindano makubwa ikiwemo Jumuiya madola, Olimpiki na kurudi na medali.

“Kwanza nimefurahi kuona zawadi ya gari kwa upande wa Wanawake na upande wa wanaume ambapo zitakabidhiwa kwa wale watakaoshinda kwenye mbio za Km 21.1 na cha ziada ni kuwa fedha zitakazopatikana zitaenda kwa watoto yatima 200 ambao watatengenezewa bima za afya,” amesema 

Kwa upande wa Mwakilishi kutoka Jan International Basilisa Biseko amesema mbio Katika kuhakikisha michezo inaendelea hapa nchini, kampuni ya Plus one imeweza kuandaa  mashindano ya riadha, yakiwa na lengo kuu la kukusanya kiasi cha fedha kuweza kusaidia Watoto yatima takribani 200 kupatiwa huduma ya bima ya Afya.

Biseko amesema wao kama Jan International waliweza kupokea maombi kutoka One Plus ya kuweza kuwa moja ya wadhamini na walilipokea hilo kwa mikono miwili kwa sababu linahusisha jamii.

“Jan tumetoa magari mawili aina ya Passo na tutayakabidhi kwa washindi wa mbio za Km 21.1. na tumefurahia sana ushirikiano huu kwani tunaamini huu ni mwanzo kikubwa tutaendelea kusaidia jamii kwa njia mbalimbali’l amesema Biseko.

“Kampuni ya Jan International inafuraha sana juu ya ushirikiano huu, na inaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa waandaaji, na jamii kwa ujumla , ikiwa pia ni mpango mkakati wa kampuni katika kurudisha kwa jamii ambayo ndio wateja wetu,”


Naye Bakari Ramadhan mwakilishi kutoka Plus One amesema Kampuni ya Plus one inajihusisha  na uaandaaji wa matukio, imeeleza kuwa ni jukumu la kila mwanajamii kufanya jambo kwa jamii yake, na ndio sababu kuu iliyopelekea wao kuja na wazo la kuandaa mashindano haya ya riadha.

Amesema, mashindano hayo ya Ocean City Community Marathon yatahusisha wakimbiaji na wanariadha na yatafanyika Oktoba 3 mwaka huu katika Viwanja vya The Green Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

“Mbio zetu tumeziboresha na kwa washiriki wote ikitokea umeshinda na umegundulika umetumia dawa za kuongeza nguvu hatuna budi kukunyang’anya zawadi uliyopatiwa na pia tutakuwa na zawadi kwa washindi wa pili hadi wa kiume kwa upande wa wanaume na wanawake,” amesema 

Ramadhan amesema,” fedha zitakazopatikana zitaenda kuhudumia watoto yatima 200 ili kuwakatia huduma ya bima ya afya na huu ni mwanzo tutaendelea kuboresha kila tutakapokuwa tunaandaa mashindano mengine”

Mashindano hayo yatahusisha mbio za  umbali wa Km 21.2, Km 10 na Km 5 na zitafanyika Oktoba 3 mwaka huu.

MAJALIWA AJIONEA MAGOGO YALIYOVUNWA KINYUME CHA UTARATIBU KATIKA PORI LA AKIBA LA IGOMBE WILAYANI KALIUA

$
0
0

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja  (kushoto) wakitazama magogo  katika  kijiji cha Wachawaseme ambayo yamevunwa kinyume cha utaratibuna watu wasiojuliakana kutoka katika Pori la Akiba  la Igombe wilayani Kaliua mkoa wa Tabora,  Agosti 28, 2021. Waziri Mkuu aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania (TFS) kuyapiga mnada magogo hayo kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mipaka ya Hifadhi ya Iswima  katika Pori la Akiba la Igombe wilayani Kaliua ambako aliagiza pori hilo lilindwe baadwe baada  ya kushuhudia uharibifu unaofanywa na watu wanokata miti, kuendesha shughuli za kilimo, uvuvi na makazi kinyume cha sheria, Agosti 28, 2021.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mipaka ya Pori la Akiba la Igombe wilayani Kaliua ambako aliagiza pori hilo lilindwe baada ya kujionea uharibifu unaofanywa na watu wanokata miti, kuendesha shughuli za kilimo, uvuvi na makazi kinyume cha sheria, Agosti 28, 2021. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Balozi. Dkt.  Batilda Burian. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mipaka ya Pori la Akiba la Igombe wilayani Kaliua ambako aliagiza pori hilo lilindwe baada ya kushuhudia uharibifu unaofanywa na watu wanokata miti, kuendesha shughuli za kilimo, uvuvi na makazi kinyume cha sheria, Agosti 28, 202. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt.  Batilda Burian. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MPANGO WA USIMAMIZI WA MAZINGIRA WILAYA ZA SINGIDA MBIONI KUKAMILIKA

$
0
0

Mratibu wa Sera kutoka Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai nchini (TOAM), Paul Chilewa, akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara ya Kilimo, TAMISEMI, na Mashirika ya kuendeleza Kilimo Hai nchini (TOAM, GIZ na Helvetas), ambacho kilifanyika juzi mkoani hapa lengo likiwa ni kutathmini na kuweka mikakati ya kuhakikisha ajenda ya 'Kilimo Himilivu' na 'Mabadiliko ya Tabianchi' vinaingizwa katika Mpango wa Mazingira wa miaka mitano ndani ya halmashauri za wilaya za Singida.

Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Mradi wa Kilimo Himilivu cha Pamba kutoka GIZ kwa mkoa wa Singida, Leonard Mtama, akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Mkalama,  Seleman Musunga, akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Mazingira kutoka Wilaya ya Iramba, Yohana Dondi,akizungumza kwenye kikao hicho.

Washiriki wa kikao hicho wakiwa katika picha ya pamoja,




Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida.


WATAALAMU mbalimbali wamekutana kutathmini na kuweka mikakati ya kuhakikisha ajenda ya 'Kilimo Himilivu' na 'Mabadiliko ya Tabianchi' vinaingizwa katika Mpango wa Mazingira wa miaka mitano ndani ya halmashauri za wilaya za Singida ili kuwezesha kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kuongeza tija katika kilimo.

Kupitia kikao hicho wataalam hao kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara ya Kilimo, TAMISEMI, na Mashirika ya kuendeleza Kilimo Hai nchini (TOAM, GIZ na Helvetas), pamoja na mambo mengine, walijikita katika kuziwezesha halmashauri mkoani hapa kutengeneza mipango inayoweza kuratibu na kusimamia uharibifu wa mazingira kwenye maeneo yao.

Mratibu wa Sera kutoka Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai nchini (TOAM), Paul Chilewa, alisema wamekutanisha  wilaya nne za Manyoni, Ikungi, Iramba na Mkalama ndani ya mkoa wa Singida ili kuzisaidia kitaalamu kutengeneza mipango hiyo ambayo inakwenda kuanza kutumika katika kipindi cha miaka 5.

Alisema lengo la TOAM ni kuhakikisha kwenye mpango huo masuala yote ya Kilimo Himilivu  na Mabadiliko ya Tabianchi yanaingizwa kikamilifu ili kuongeza tija kwenye kilimo katika muktadha chanya wa ongezeko la uzalishaji, ubora na zaidi kuifanya ardhi kuwa endelevu kwa matumizi ya kizazi cha sasa na baadaye.

Chilewa ambaye anatoka kwenye shirika hilo ambalo ni mwamvuli wa mashirika yenye lengo la kuendeleza kilimo hai nchini alisema mathalani kama taifa litajikita kwenye kuzalisha zao la Pamba kwa mfumo wa 'Kilimo Hai' na kuweka sera madhubuti sio tu litapata faida kubwa lakini pia wananchi wote wanaolima zao hili na mengine ya chakula kwenye eneo hilo watakuwa na uhakika wa kupata ithibati ya kuuza mazao yao kwenye soko la dunia kutokana na matokeo ya ubora wake.

"Uzalishaji wa pamba ya kilimo hai kwenye maeneo mengine duniani zikiwemo nchi za Afghanistan na India kwasasa kuna changamoto,  hivyo kama tutazalisha pamba hii (Organic Cotton) tutapata faida kutokana na kuwa na mahitaji makubwa kwenye soko," alieleza Chilewa.

Alisema lengo la kikao hicho, pamoja na mambo mengine ni kuhakikisha kunakuwa na mkakati ambao utahakikisha kilimo kinazingatia taratibu zote za kilimo himilivu kwenye mabadiliko ya tabianchi.

"Hapa tupo kimkoa lakini TOAM kwa kushirikiana na wenzetu GIZ Tanzania, Helvetas na wadau wengine ndani ya wilaya hizi za mkoa wa Singida tunataka kuzisaidia halmashauri kutengeneza mpango huu na kuchukua hatua ya kuwa na miradi mbadala ikiwemo kupanda miti na kuanzisha mashamba darasa ya kujifunzia hizi teknolojia kwa ustawi na tija," anasema.

Hata hivyo Chilewa alishauri kuangalia baadhi ya teknolojia na shughuli nyingine za kibinadamu zinazotumika katika kilimo hususani suala la matumizi makubwa ya mbolea za viwandani ambayo kwa kiasi kikubwa zinachangia kufanya mazingira yasiwe himilivu.

Katika hilo, alisema Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa wingi wa mifugo, lakini kitu cha kushangaza wakulima wake walio wengi hawatumii hizo mbolea za mifugo hususani ng'ombe katika kurutubisha ardhi.

Alisema hata zile teknolojia na aina nyingine za mbolea ambazo zinaweza kurutubisha ardhi kwa kiwango cha kutoathiri- kwa maana ya kuifanya ardhi iendelee kuishi na kuzalisha nazo bado hazitiliwi mkazo wala kutumika ipasavyo.

Chilewa zaidi aliainisha baadhi ya viashiria vya uharibifu huo wa mazingira kuwa ni pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya maji, wingi wa mifugo isiyozingatia tija, ukataji miti hovyo na uchomaji mkaa sambamba na matumizi makubwa ya viuatilifu ambavyo vina athari kwa udongo na afya za watu

"Hivyo kusanyiko la wadau na wataalamu hawa linalenga kutengeneza mpango wa miaka 5 utakaojibu changamoto hizi kwa kizazi cha sasa na kijacho katika muktadha wa kuwa na ufugaji endelevu na kilimo endelevu ambavyo vitazingatia utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi," alisema Chilewa.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Kilimo Himilivu cha Pamba kutoka GIZ kwa mkoa wa Singida, Leonard Mtama, kupitia kikao hicho anasema lengo lao hasa ni kusimamia na kuratibu utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

"GIZ tunaratibu tu hizi shughuli kwa pamoja na wenzetu wa TOAM, Helvetas, Tari, Kampuni ya Biosustain, Bodi ya Pamba na wadau wengine, lakini pia tunasimamia uboreshaji wa AMCOS kwa kushirikiana na Chuo cha Ushirika Moshi na tawi lake la Singida," alisema Mtama.

Alisema majukumu mengine ya shirika hilo, pamoja na mambo mengine, ni kuangalia kwa namna gani vikundi vya akinamama kupitia Helvetas vinaweza kujiongezea kipato kwa kuzalisha pamba hai na mazao mengine.

Kwa mujibu wa Mtama jukumu lingine la GIZ ni kuunganisha wazalishaji wadogo waliopo mkoa wa Singida na masoko ya ndani na nje lakini masharti ni kwamba mazao husika yatokane na kilimo hai.

"Hivyo sisi tunaratibu hayo mambo mawili uzalishaji wa mazao ya wakulima yaani pamba hai na mengine ya chakula kama Dengu, Choroko, alizeti na ufuta ili kuhakikisha uzalishaji wake unakuwa wa tija," anasema Mtama.

Katika hatua nyingine, alihimiza kuwa na azma ya pamoja ya kudumisha suala la ushirikiano kwa Idara, Taasisi na wadau wote kwenye kutunza mazingira huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kila mmoja kwa nafasi yake mahali alipo kuchukua hatua katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

"Unapotaka kufuga pia unapaswa kuangalia tija mfano badala ya kufuga ng'ombe 10 wenye kilo 50 kila mmoja ni bora ufuge kisasa ng'ombe mmoja mwenye kilo 500," alisisitiza Mtama.

Naye Afisa Maliasili na Mazingira mkoa wa Singida, Charles Kidua, alisema kama mkoa wamenufaika vilivyo na uwezeshaji wa wataalamu hao katika kutengeneza mipango hiyo ya usimamizi wa mazingira, na anaamini pale itakapoanza kutumika itasaidia kwenye usimamizi thabiti mazingira.

"Kikao hiki kimetuwezesha kutengeneza mipango mtambuka ya usimamizi mzuri wa mazingira kwenye eneo la misitu, kilimo, afya na maeneo mengine mengi kwa kuzingatia suala la mazingira ni jambo mtambuka," alisema Kidua. 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA MIRADI SINGIDA

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheriaya hiyo Najma Murtaza Giga (katikati) akizungumza na Wanachuo cha Ufundi Veta Mkoa wa Singida na wadau wengine baada ya Wajumbe wa kamati hiyo kutembelea chuo hicho jana. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Selemani Mwenda na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Jamal  Katundu.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea karakana ya mitambo mbalimbali chuo cha Veta Singida.
Wajumbe wa kamati hiyo wakinunua bidhaa za wajasiriamali waliowezeshwa na Serikali.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea banda la Mjasiriamali aliyetengeneza majiko kwa kutumia teknolojia ya udongo na mabati.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu.
Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani akizungumza na Wanafunzi wa SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu wanaojifunza kushona nguo.
Wanafunzi wa SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu wakiwa kwenye hafla ya kuwapokea wajumbe hao.
Wanafunzi wa SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu wakiwa kwenye hafla ya kuwapokea wajumbe hao.
 Mkuu wa chuo hicho, Fatma Malenga akisoma taarifa ya chuo hicho kwa wajumbe wa kamati hiyo. 
Wanafunzi wa Chuo cha FDC wakiwa kwenye hafla ya kuwapokea wajumbe hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wakitoka kukagua jengo la TEHAMA la Chuo cha FDC.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua Ofisi ya  Udhibiti Ubora wa Shule Manispaa ya Singida.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imekagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya vijana iliyopo mkoani hapa.

Wakati huo huo Wajumbe wa kamati hiyo wamewataka vijana kuchangamkia fursa ya program ya kukuza ujuzi kwa vijana inayofadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwani itawakomboa kiuchumi.

Ombi hilo limetolewa jana kwa nyakati tofauti na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ziara yao ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo ya vijana iliyopo Manispaa ya Singida.

Wajumbe hao waliwasihi vijana hao kujikita zaidi kwenye mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kujiajiri na kuondokana na dhana ya kutaka kuajiriwa.

 Mafunzo wanayojifunza ni ya fani za umeme, ushonaji nguo, mapambo,useremala,ujenzi na kupaka rangi.

Miradi waliyoitembelea ni  ile ya vijana waliowezeshwa na Serikali  kupitia asilimia nne  ya mapato ya ndani.

Awali akitoa neno la utangulizi  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu Wenye Ulemavu,  Profesa Jamal  Katundu alisema nia ya kamati hiyo kwenda Singida ni kutokana na kazi nzuri ya miradi walioifanya kwa asilimia 100 na kupitishwa bila ya kukataliwa kufuatia usimamizi mzuri wa vikundi vya vijana mkoani hapa.

Katika ziara hiyo wajumbe hao walipata fursa ya kuzungumza na vijana wanaopata mafunzo mbalimbali ya ufundi katika vyuo vya Veta, FDC, na SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu  ambapo pia walitembelea miradi yote iliyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru na kukagua bidhaa za vijana hao kwenye Maonyesho yaliyofanyika Chuo cha Veta yaliyo andaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliokuwa kwenye ziara hiyo ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Watu Wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Jamal  Katundu na Mwenyekiti wa kamati hiyo Najma Murtaza Giga.

SERIKALI YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MATUMIZI YA TIBA ASILI NCHINI.

$
0
0

Na WAMJW- DOM

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  imeendelea na zoezi la kutoa Elimu kwa wananchi katika maeneo ya kutolea huduma za Afya juu ya umuhimu wa matumizi ya tiba asili/mbadala katika mapambano dhidi ya magonjwa mbali mbali, ikiwemo UVIKO-19.

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya tiba asili ya mwafrika Wadau wa tiba asili wakiongozwa na kitengo cha Tiba asili na Baraza la tiba asili kutoka wizara ya afya wameweza kutembelea na kutoa elimu katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma, kituo cha Afya cha Makole na Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Akiongea wakati wa utoaji elimu hiyo Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asili/Mbadala  Dkt. Vumilia Liggyle alisema kuwa, Wataalamu wa Tiba asili na tiba mbadala kutoka Wizarani wameongozana na Waganga wa tiba hizo kutembelea vituo vya Afya katika sehemu ya wagonjwa wa nje wa Hospitali (OPD) ambapo wameweza kuzungumza na wagonjwa na kuwapa elimu kuhusu umuhimu wa tiba asili katika mapambano dhidi ya magonjwa mbali mbali nchini.

"Kwa siku ya leo tumetembelea vituo vya Afya vitatu, tumetembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma General kama kituo cha kwanza, ambapo tumeenda sehemu ya wagonjwa wa nje wa Hospitali ambapo tumeweza kuzungumza na wagonjwa na kuwapa elimu kuhusu tiba asili." Alisema.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali tuna Baraza la tiba asili na tiba mbadala ambalo linatekeleza Sheria namba 23 ya mwaka 2002 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza hili ndio linasajili dawa, Waganga wa tiba asili, na kuwajua wako wapi na wanafanya nini, na kuhakikisha dawa hizo ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Baraza la tiba asili na tiba mbadala linafanya kazi kwa kushirikiana na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maabara ya TMDA, maabara ya taasisi ya dawa asili pamoja na Maabara ya Shirika la viwango Tanzania, Alisisitiza Dkt. Liggyle.

Naye, Katibu Mkuu wa Shirika la dawa asilia na ulinzi wa mazingira Bw. Boniventura Mwalongo ameeleza zaidi ya asilimia 93 ya dawa zinaagizwa kutoka nje ya nchi, hivyo Serikali imelenga kuboresha tafiti za ndani, kuongeza uzalishaji wa ndani ili kutoa fursa za ajira, hususan kwa vijana, hivyo kupitia kuikuza tiba asili nchini yote yanawezekana.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Waganga wa tiba asili katika zoezi hilo Dkt. Elizabeth Lema alisema kuwa, wiki hii ya maadhimisho inatoa fursa kwa Waganga wa tiba asili na tiba mbadala kuonesha bidhaa zao mbali mbali ambazo tayari zimesajiliwa kupitia Baraza la tiba asili na tiba mbadala na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi kuhudhuria maonesho hayo yatayofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ili kujifunza, kuelimishwa na kupata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kuhusu tiba asili na tiba mbadala kisha kufahamu namna ya kuzipata na kuzitumia.

Wiki ya tiba asili na tiba mbadala ya Mwafrika inaongozwa na Kauli mbiu ya "Mchango wa tiba asili katika mapambano dhidi ya UVIKO-19 " ambapo mwisho wa kilele ni Agasti 31, huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akitarajiwa kuwa mgeni rasmi kufunga maonesho hayo yanayofanyika kila mwaka.





Viewing all 118642 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>