Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 118927 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUFUTA LESENI VITALU VYA MADINI NDANI YA SITINI

$
0
0

 Na Anthony Ishengoma-Shinyanga

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema ndani ya siku 60 atafuta leseni za uchimbaji madini za wale wamiliki ambao wameodhi maeneo ya madini bila kuyafanyia kazi kwa muda mrefu lakini wamekuwa wakijitokeza kuzuia wachimbaji wadogo kutumia maeneo hayo kwa kigezo cha kumiliki leseni.

Doto Biteko amesema kuna baadhi ya watu wanaleseni nchi nzima na inapotokea wachimbaji wadogo wakagundua eneo hilo lina madini watu  hao  anajitokeza kudai tayari wana leseni za eneo hilo na kujiuliza mtu huyo muda wote anakuwa wapi.

Kufuatia hali hiyo Biteko amesema sio tu kwamba atafuta leseni zinazomolikiwa kwa kipindi kirefu bali pia atahakikisha wamiliki hao wanalipa kodi ya serikali kwani mpaka sasa serikali inadai jumla ya Tsh Bil.9 ambazo amesema lazima zilipwe kwa serikali kutoka kwa wamiliki hao.

Bw. Biteko amesema hayo jana wakati wa akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini ambayo yamefanyika kwa takribani wiki moja sasa na kuongeza kuwa anashangaa kuwa bado kuna watanzania wanaangaika kutorosha madinio nje ya Nchi.

Biteko amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa kulipa kodi ya serikali badala ya kutorosha madini kwani Tanzania ina masoko ya madini 50 hapa nchini na kuna wafanyabiashara ya madini kutoka Congo ambao wanekuwa wakifika Tanzania kwa ajili ya kuuza madini uku akisema kuwa kutorosha madini ni sawa na kuchoma kuni kwa kutumia mwanga wa tochi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa upande wake amesema yuko tayari kupambana na watoroshaji madini hao na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani ikiwa watabainika atahakikisha wanafirisika na kutaifisha madijni yote watakayokuwa nayo.

Dkt. Sengati amewataka watanzania kutanguliza uzalendo mbele kwa ustawi wa uchumi wa wana Shinyanga na watanzania kwa ujumla na kwamba atakuwa mkali sana kwa wale wote ambao wataendelea na ukosefu wa uzalendo kwa kuendelea kutolosha madini hapa Nchini.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya madini nchini Prof. Idris Kikula ameongeza kuwa serikali inalazimika kufuta leseni izo ndani ya siku sitini zijazo huku akijua maamuzi hayo hayatawafuraisha watu lakini hamna namna lazima uamzi huo ufanyike na kodi izo zilipwe kwa manufaa ya Taifa.

Prof. Kikula ameongeza kuwa kuhusu suala hilo tayari Tume ya madini imeshatoa tangazo ikiwemo mikutano ya vyombo vya habari na kuwataka wamiliki waleseni hizo kuwa tayari na zoezi hilo na kuwataka kuwa tayari kulipa kodi inayodaiwa na serikali.

Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini yamefanyika katika viwanja vya Zainab Telack nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga na yamehitimishwa jana na yanatarajia kuendelea tena mwakani kwa kipindi kama hiki ili kutoa fursa kwa wananchi kujua soko la madini lakini pia kujipatia elimu ya teknolojia ya madini.   


Waziri Biteko akikagua madini aina ya Almasi alipotembelea banda hilo wakati wa siku ya kufunga maonesho ya Biashara na Teknolijia ya madini jana Mkoani Shinyanga.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuena Omary akipokea cheti cha ushiriki maonesho baada ya Ofisi yake kushiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini yalifungwa jana Mkoani Shinyanga.

.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati hakitoa hotuba yake kwa wananchi walioshiriki  Maonesho katika Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini jana Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Marryprisca Senyemule hakitoa salamu ya Mkoa wa Geita  kwa wananchi walioshiriki  Maonesho katika Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini jana Mkoani Shinyanga.
 

Wanawake Watayarishwe katika Uongozi kabla ya Uchaguzi Mkuu

$
0
0

 

Vyama vya siasa vimeshauriwa kuwatayarisha wanawake katika nafasi ya uongozi mapema kabla ya kufikia kipindi cha Uchaguzi Mkuu ili waweze kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.

Ushauri huo umetolewa leo na wajumbe wa Kamati ya Wanaume wa Mabadiliko (Male change agent) katika kikao cha pamoja na maafisa wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) kilichofanyika Tunguu kwenye ofisi ya chama hicho kutathmini hali ya ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Wanaume zaidi ya 22 kutoka Unguja na Pemba wakiwemo wafuasi wa vyama mbali mbali, wataalamu wa masuala ya jinsia na viongozi wa dini  wameanzisha mtandao miaka mitatu iliyopita ili kuhamasisha  jamii kumpokea mwanamke kama kiongozi halali kama walivyo wanaume.

Mwenyekiti wa kamati ya wanaume wa mabadiliko bw, Mohammed Jabir Makame amesema mifumo mibaya ya vyama vya siasa  inapelekea wanawake kushindwa majimboni kwasabu hawajatayarishwa na vyama vyao kwa kuwapa nafasi ya kuongoza ndani chama.

 “ Wanawake wanapewa nafasi ya kugombea jimbo wakati wa uchaguzi mkuu bila ya kumtayarisha kwanza ndani ya chama chake hivyo sio rahisi kushinda jimboni. Kwanza chama kimtayarishe kwa kipindi cha miaka minne nyuma kabla ya kufika uchaguzi mkuu, kwa kumpa nafasi ya kuongoza ndani ya chama chake” Alisema Makame.

Pia amesema awali wanawake walikuwa na woga wa kugombea nafasi ya majimboni lakini baada ya kuhamasishwa wanawake wengi walijitokeza kugombea katika majimbo katika uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo wanawake 435     waliweza kutia nia na wanawake 216  waligombea.

Kwa upande Pemba mwanaume wa mabadiliko bwana Omar Mjaka Ali amesema mbali na utayari wa wanawake lakini pia wamekabiliwa na kikwazo cha kiuchumi hivyo kinapelekea kukosa kushinda nafasi za majimboni kwasababu harakati za uchaguzi zinahitaji fedha kuanzia uchukuwaji wa fomu na mzunguuko mzima wa kampeni.

Aidha wanaume wa mabadiliko wamesema wamejifunza mengi kutokana na harakati hizo za kutoa elimu kwa jamii kumkubali mwanamke kua kiongozi ikiwemo ulinganisho wa sheria, Quran na Hadithi za dini ya kiislam. Wamesema katika juhudi hizo walikua wakitembea na viongozi wa dini ili  jamii ifahamu kwamba dini ya kiislam haikukataza mwanamke asiwe kiongozi.

Takwimu zainaeleza kuwa hadi sasa wanawake katika vyombo vya maamuzi hasa kupitia nafasi za kugombea ni wachache sana ambapo kwa mujibu wa uchaguzi wa mwaka 2020, kwenye udiwani wanawake ni 25 sawa na asilimia 22.72%,  Baraza la wawakilishi ni 8 sawa na asilimia  16%  ubunge ni  4 sawa na asilimia 8% na Uraisi ni 0.

Mwisho wanaume hao wa mabadiliko wameiomba Chama Cha Waandishi wa Habari  Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,ZNZ) na wadau wengine kuendelea kutoa fursa za kuwajenga uwezo  wanawake, vijana wakike na kuwapa  hamasa kuingia katika uongozi pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii imkubali mwanamke kwamba wanaweza kuongoza na dini sio kikwazo cha kumzuia asiwe mbunge, mwakilishi wala diwani.

Wanaume wa mabadiliko walifanya kazi  kupitia mpango  wa kuwainua wanawake katika siasa na uongozi (WPEL) unaosimamiwa na Chama Cha Waandishi wa Habari  Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,ZNZ)kwa mashirikiano na  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mambo ya wanawake(UN Women).

WAZIRI BITEKO ATOA SIKU 60 LESENI ZISIZOFANYA KAZI KUFUTWA

$
0
0


Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza wakati Agosti 1, 2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyoanza Julai 23 katika uwanja wa Zainab Telack Kijiji cha Butulwa Manispaa ya Shinyanga



Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula, akizungumza wakati Agosti 1, 2021 wakati Waziri wa Madini Doto Biteko akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga Agosti 1, 2021



Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa katika banda la kampuni ya Barrick kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyoanza Julai 23 katika uwanja wa Zainab Telack Kijiji cha Butulwa Manispaa ya Shinyanga.

***********************

Na. Steven Nyamiti – Shinyanga

Waziri wa Madini Doto Biteko, ametoa siku 60 za kufuta leseni za uchimbaji wa madini zilizohodhiwa na wawekezaji kwa muda mrefu bila kuzitumia.

Biteko amesema hayo Agosti 1, 2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Zainab Teleck kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Amesema, kumekuwepo na tatizo kwa baadhi ya wawekezaji wa madini kuhodhi leseni kwa muda mrefu na kutozitumia na pale yanapovumbuliwa madini na wachimbaji wadogo ndipo hujitokeza na kudai eneo hilo ni lao.

“Tutafuta leseni na mahakamani utakwenda, utatulipa kutoka mahakamani, kama una leseni endeleza leseni yako, hatutaki tuwasumbue wachimbaji wakubwa lakini vilevile wakubwa wasiwasumbue wachimbaji wadogo,’’ ameeleza Biteko.

Kufuatia hali hiyo, Biteko amesema wametoa siku 60 za kutaifisha leseni za uchimbaji wa madini zilizohodhiwa na wawekezaji kwa muda mrefu bila kuzitumia huku akibainisha kuwa Serikali imedhamiria kuinua Sekta ya Madini, pamoja na kumaliza migogoro yote ambayo hujitokeza baina ya wachimbaji wadogo na wakubwa.

“Naomba mfikishe salamu kwa wawekezaji wa madini ambao wana leseni za uchimbaji na hawazitumii, tumetoa siku 60 tu zianze kutumika, zaidi ya hapo tutazitaifisha na kutoza gharama ambazo Serikali imeingia kutokana kutolipiwa kodi kwa muda mrefu na kusababisha Serikali kukosa mapato na fedha hizi lazima zilipwe hatutakuwa na msalia mtume, hatutaki migogoro ya uchimbaji wa madini,’’ amesema Biteko.

“Tumeondoa kila aina ya kikwazo kilichokuwa kinawafanya watu watoroshe madini, tumeondoa kodi peke yake zaidi ya asilimia 23, tunaona watu kutoka Nje ya nchi Congo, Zambia na Msumbiji wanaleta madini kuja kuuza hapa, unashangaa kumuona Mtanzania na yeye anatorosha madini kupeleka mahali kwingine,” amesisitiza Biteko.

Aidha, amewataka wachimbaji wenye leseni walipe kodi na waepuke vitendo vya utoroshaji madini huku akibainisha kuwa atakayetorosha madini atakuwa anachoma madini kwa tochi, hivyo akikamatwa hatabaki salama na kuwataka wapeleke madini yote kwenye masoko.

“Tumefungua masoko, leo Tanzania tuna masoko ya madini 39, tuna Vituo vya kuuza madini 50, na hata Shinyanga masoko yapo mengi, Mwaka 2019 tulifungua soko la kwanza la madini na hili limetuletea faida kubwa, tuone fahali kulipa kodi, tuone fahali kupeleka madini kwenye masoko yetu, kama Wizara ya Madini tutaendelea kuwahudumia watanzania wanaohitaji kuchimba,’’ ameongeza Biteko

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula ameunga mkono kauli ya Waziri Biteko kwa kutoa siku 60 kwa wawekezaji ambao wanamiliki leseni za uchimbaji madini na kutoziendeleza kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria, pamoja na kufidia fedha ambazo zilipaswa kulipwa kwa kipindi chote walichohodhi leseni hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati amesema maonesho hayo yamesaidia kuutatangaza Mkoa huo na kuonyesha fursa za biashara hasa katika sekta ya madini.

Pia, kama mkoa utaendelea kuboresha maonesho hayo na kuwaunganisha wafanyabiashara na wajasiriamali akiongeza kuwa maonesho hayo ni muhimu kwa sababu Mkoa wa Shinyanga una madini mengi na una madini ya pekee ya Almasi ambayo yanaendelea kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

“Kupitia maonesho haya washiriki wamepata fursa ya kutambulisha biashara zao, kuuza bidhaa na kujifunza teknolojia ya kisasa na kujua wapi wapate mitaji,’’ amesema Sengati.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini mkoa wa Shinyanga (SHIREMA) Hamza Tandiko amezishukuru Taasisi za kifedha kwa kuanza kuwapatia mikopo wachimbaji wa madini huku akiomba Serikali kupeleka umeme wenye nguvu ya kuendesha mitambo kwenye maeneo ya machimbo kwani umeme uliopo sasa ni kwa ajili ya mwanga tu.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui ambao ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa Maonesho hayo, amesema taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya CRDB zimeanza kuwezesha mikopo kwa vikundi vya wachimbaji wa madini na wajasiriamali hivyo kuwakaribisha kupata huduma katika Benki yao ambayo pia inatoa Bima za aina mbalimbali zitakazowasaidia wachimbaji.

Maonesho hayo yaliyokwenda kwa kauli mbiu ya Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu yaliyoanza Julai 23 na kufungwa Agosti 1 na Waziri wa Madini Doto Biteko.

RAIS SAMIA AWASILI NCHINI RWANDA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali Nchini Rwanda kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Paul Kagame leo Agosti 02,2021.


 

MGANGA MKUU HOSPITALI YA MT MERU AELEZA SABABU ZA WATOTO KUTOPATA UGONJWA WA CORONA

$
0
0

MGANGA wa Hospitali ya Mount Meru Hospitali jijini Arusha Sunday Wanyika  ameeleza kuwa kufa na kuzaliwa kwa cell mara kwa mara kwa watoto ndio sababu inayopelekea watoto kutoshambuliwa na Virusi vya UVIKO 19 vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya Mapafu.

Ametoa maelekezo hayo jijini Arusha leo wakati akitoa mada Kuhusu mlipuko wa Virusi vya UVIKO 19 kwenywe mkutano wa wadau Kuhusu masuala ya msaada wa kisheria na upatikanaji haki kwa wananchi katika kipindi cha matumizi ya lugha ya kiswahili.

Mganga huyo ameeleza kuwa hali hiyo ndio imekuwa ikisababisha watoto kutoshambuliwa n Virusi hivyo mana vinapotaka kushambulia vinakuta cell zimekufa na kuanza kuzalishwa nyingine hivyo wao wakijikuta wanakuwa sugu na kuwa na uwezo wa kupokea na kuambukiza na kuathiri watu wazima.

"Zaidi ya aslimia 50 ya wagonjwa hawaonyeshi dalili na wanaongoza kwa kusambaza Virusi vya ugonjw huo hivyo wakati wa kujikinga usiwahofia ambao wameshaugua na kuonyesha dalili tu, muwe makini pia na kundi hilo, mpaka sasa watubmilioni 199 wameshapimwa na kukutw na maambukizi huku watu milioni 4 wakifariki na ugonjwa huo ulimwenguni,"amesema.

Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa makini kwa kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo kwa kuchukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanachoma chanjo ambalo ni lazima kutokana na hali halisi ilivyo sasa, kutokwenda kwenye mikusanyiko isiyo ya lazima na kutulia majumbani, kuvaa barakoa ambazo zinakinga, kutumia vitakasa mikono na kunawa maji tiririka.

"Simu za mkononi zinaongoz kwa mambukizi kutokana n kushikwa mara kwa Mara nawasii wannachi muwe nazo makini kw kutumia vitakasa mikono mara kwa Mara,"amesisitiza.

Akizungumzia Virusi vya UVIKO 19 awamu ya sasa amesema viko tofauti sana na vile vya awmu ya kwanza  vinasambaa kwa haraka zaidi na ni rahisi kusababisha kifo huku akitaja dalili namba moja kuwa ni kifua kuuma na kuwa kizito wakati awali ilikuwa ni kupta mfua, kukohoa na kushindwa kunusa.

Akifungua mkutano huo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Godfrey Mizengopinda amewataka mawakala wa sheria kwenye maeneo yao wapambanie afya za watu wao suala la chanjo ni muhimu Sana kwa maisha ya watanzania hivyo amewaasha washiriki wote wajitokeze kuchoma chanjo katika zoezi la uzinduzi wa changjo litakalofanyika kesho jijini Arusha ili kujikinga.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru akitoa mada kuhusu mlipuko wa virusi vya UVIKO 19 kwenye mkutano wa wadau kuhusu masuala ya msaada wa kisheria .

Ecobank Group and Microsoft upskill Africa’s Small and Medium Enterprises to succeed in a digital economy

$
0
0

 

 

The leading pan-African banking group, Ecobank Group, in partnership with Microsoft, LinkedIn, GitHub and Ecobank Academy is set to provide training to equip Small and Medium-sized Enterprises (SMEs) across sub-Saharan Africa. This training will provide SMEs digital skills and knowledge to succeed in today’s digital world.

SMEs have been significantly impacted by the COVID19 pandemic with its attendant lockdowns and disruptions to supply chains, plummeting sales, lost revenue and operational challenges. In response to feedback from our customers, Ecobank through its Commercial Banking Segment is helping business owners close the digital skills gap within their chosen fields and improve the digital capabilities of their employees.

Josephine Anan-Ankomah, Group Executive, Commercial Banking for the Ecobank Group said: “The COVID-19 pandemic has turbocharged the shift towards digital. It is essential that businesses adapt so that they are able to compete effectively in today’s rapidly changing landscape. Ecobank’s Commercial Banking is committed to supporting SMEs across our pan-African footprint. Through this partnership with Microsoft, LinkedIn, GitHub and Ecobank Academy we are offering training to equip business owners  and their employees with the digital skills that they need to stay connected to their customers. We are intent on ensuring that our SME customers remain relevant, grow and succeed in the post COVID-19 era.”

SMEs have been  invited to register here for the upcoming webinar  taking place on July 26. The Global Skilling initiative program is available on an online portal where SMEs can register, and start their learning journey for any of the 10 in-demand skill sets (Customer Services; Digital Marketing; Financial Analysis; Graphic Design; IT Support/Help Desk; Project Management; Sales; Data Analysis; IT Administration; And Software Development). They can complete the virtual programme at their own pace and at times that work best for them. The programme runs until 31st of December 2021.

Ibrahim Youssry, Regional General Manager, Middle East and Africa – Multi market region at Microsoft said, “we are committed to building digital talent pipelines to support the workforce of the future, and our Global Skilling Initiative is an important part of this process. But beyond the future workforce, digital talent will also support more local innovation, as developers and entrepreneurs are empowered to create locally relevant solutions that best address the challenges and needs of African countries. Startups and SMEs play a critical role in innovation, economic growth and job creation, and expanded access to digital skills is one of the key steps needed to foster a successful economic recovery.

The Global Skilling Initiative is just another example of how Ecobank wants to help SMEs reach their full potential and play a vital role in driving Africa’s economic resurgence. Other support initiatives for SMEs include:

·       The Ecobank Marketplace eCommerce solution for businesses to grow their sales on digital marketplaces

·       And the Ellevate programme to provide women-led/owned/focused businesses with loans, cash management solutions, training and mentoring opportunities.

Mapato ya EABL yaendelea kukua pamoja na mazingira magumu ya biashara

$
0
0

Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) imepata ongezeko la mapato la aslimia 15 kufikia shilingi za Kenya bilini 86.0 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2021. Faida kabla ya kodi iliongezeka kwa aslimia 2 kufikia shilingi za Kenya 10.9 bilioni. Ukuaji wa faida usioridhisha umechangiwa na gharama za mfumuko wa bei, ubadilishaji wa fedha na gharama za kodi

Mafanikio haya yameweza kufikiwa wakati kukiwepo mazingira magumu ya biashara. Kampuni iliweza kufanya mabadiliko yaliyoendana na tabia zilizobadilika za wateja ikiwa ni pamoja na biashara kwa njia ya mtandao, kuwapelekea wateja bidhaa sehemu walipo na kuweka vifungashio vya kuondoka na bidhaa

Dondoo za masoko kwa mwaka huu wa fedha:

➢ Kenya: Kenya Breweries Limited (KBL) imeweza kupata ukuaji wa mapato wa 10% mwaka baada ya mwaka. Mafanikio haya yametokana na kuweza kuangalia mahitaji kwa wakati husika na kutumia njia mpya kuwafikishia bidhaa wateja wakati uwekezaji ukiendelea kufanyika kwenye bidhaa za kimkakati zaidi.

➢ Uganda: Uganda Breweries Limited (UBL) mapato yamekua kwa asilimia 33 mwaka baada yam waka wakati bia na pombe kali zionyesha ukuaji mzuri zaidi. Ukuaji huo ulitokaa na kuendesha biasahara kulingana na mazingira mapya ikiwa ni Pamoja na kubadilisha mbinu za kufikisha bidhaa sokoni. Uganda iliwekeza kwenye upanuzi katika uzalishaji kusaidia mauzo yanayokua ikiwa ni sehemu ya mkakati wa EABL

➢ Tanzania: Serengeti Breweries Limited (SBL) mapato yake yamekua kwa asilimia 15 huku bia na pombe kali vikionyesha ukuaji mzuri wa namba mbili (double digit). Ukuwaji huo mzuri umetokana na uwekezaji kwenye bidhaa pamoja na upanuzi katika uzalishaji kwa bia pamoja na uzalishaji wa pombe kali.

Faida ya EABL baada ya kodi katika kipindi hiki imeshuka kwa asilimia 1% kufikia shilingi za Kenya Bilioni 7 kutokana na kuathiriwa mfukumo wa bei, kodi na atahri za ubadilishaji wa fedha za kigeni. Unafuu wa kodi uliotolewa Kenya kutokana na ugonjwa wa COVID-19 uliishia Disemba 2020 na kupelekea kurudi kwa kodi iliyokuwepo kabla ya Covid-19


Katika kipindi hiki kipaumbele cha kampuni kilikuwa ni kuhakikisha afya na usalama wa watu kwa kuwapatia vifaa vilivyowawezesha kufanya kazi katika mazingira salama. 


Mkurugenzi mtendaji wa EABL Group Jane Karuku, alisema: “Mwaka wa fedha 2021, umekuwa mgumu kutokana na ugonjwa wa Covid-19 kuathiri biashara katika eneo lote la Afrika Mashariki. Kenya na Uganda ziliweka hatua kali za udhibiti na watu walipunguza matumizi yasiyo ya lazima jambo ambalo lilituathiri. Tuliweza kukabliana na hali hii kwa kuwekeza kwenye bidhaa, kuongeza uzalishaji na kuendeleza jitihada za ili kupunguza matumizi na kuhakikisha tunaendelea kuwa imara,”

Akizungumzia kuhusu mipango ya mbele Jane alisema “tunafahamu kuwa athari zinazoletwa na Corona zitaendelea. Hata hivyo, tuna uhakika kuwa mkakati wetu wunafanya kazi vizuri na tutaendeleza jitihada za kuimarisha biashara,”


TANZANIA YAPIGA HATUA UNYONYESHAJI WATOTO MAZIWA YA MAMA

$
0
0

Jamii imeaswa kuwajibika katika ngazi zote ili kutetea, kulinda na kuendeleza utaratibu sahihi wa unyonyeshaji watoto maziwa ya mama kwa kuwajengea mazingira wezeshi kwa kina mama ili waweze kunyonyesha watoto maziwa ya mama.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Cosmas Nshenye kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani ambapo kitaifa yamezinduliwa mkoani Songwe na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa lishe ya watoto wachanga na wadogo.

“Unyonyeshaji watoto maziwa ya mama ukifanyika ipaswavyo familia, jamii na taifa kwa ujumla watoto wachanga watakuwa na hali nzuri ya lishe itakayoboresha ukuaji na maendeleo yao kimwili na kiakili na kasi ya itapunguza vifo na kasi ya magonjwa ya kuambukizwa.” Amesema Mhe. Nshenye

Amesema kuwa twakimu za hali ya ulishaji watoto nchini Tanzania kwa mwaka 2018 zinaonyesha kuwa Tanzania imepiga hatua katika unyonyeshaji wa maziwa ya mama ambapo 98% wanachagua kuwanyonyesha watoto wao, 92% watoto wanaendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee ndani ya miezi 6 ya mwanzo huku 87% ya watoto wanaanzishiwa vyakula vya nyongeza katika umri sahihi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania TNFC Dkt. Germana Leyna amesema kuwa takribani vifo 823,000 vya watoto na 20,000 vya wanawake vinatokea wakati wa kujifungua duniani kila mwaka vinaweza kuzuiwa kutokana na unyonyeshaji na madhara ya kutonyonyesha maziwa ya mama kwa mtoto mchanga yanahusishwa na uwezo mdogo kiakili na kusababisha hasara za kiuchumi kwa kiasi cha dola bilioni 301 kwa mwaka.

Dkt Leyna anasema Tanzania imechukua jitihada mbalimbali za kulinda unyonyeshaji wa maziwa ya mama zikiwemo upitishwaji wa kanuni kuu 2 zinazolenga kulinda muda wa mama kuweza kunyonyesha na kumlinda mama na jamii, vilevile kutoa elimu kwa jamii yote ya watanzania ili itambue umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto.
“Jukumu kubwa la Taasisi ya Chakula na Lishe katika muktadha huu unyonyeshaji ni kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi za lishe ikiwemo suala zima la uhamasishaji maziwa ya mama kwa mtoto kupitia njia mbalimbali za upashaji habari”
Akitoa ushuhuda wa faida ya aliyoipata kwa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza Bi. Modesta Kayuni Mkazi wa kata ya Mlowo Mbozi mtoto hajawahi kuumwa tumbo kabisa na anakuwa na akili ambayo inaonekana iko vizuri na kushukuru wizara ya afya kwa kutuoa elimu ya umuhimu ya maziwa ya mama kwa mtoto mchanga.

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani kwa mwaka huu2021 yamebebwa na kauli mbiu inayosema kulinda unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni jukumu letu sote.



Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Cosmas Nshenye akinywa uji wa Lishe wakati wa kufungua Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.


TFRA yawaomba wakulima kutumia mbolea mbadala kujikwamua na ghalama sokoni

$
0
0

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kutokana na kupanda kwa gharama ya mbolea ya kupandia DAP na kukuzia UREA hapa nchini iliyosababishwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa Corona duniani.

Mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini (TFRA) imetoa wito kwa wakulima kutumia mbolea mbadala ikiwemo NPC pamoja NPC ZINK zinazouzwa kwa bei naafuu huku uwezo wake wa kufanya kazi  unatajwa kufanana na DAP au kuzidiana.

Wito huo umetolewa na Stephan Eliuth Ngailo ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania alipokuwa mkoani Njombe kwa lengo la kufanya tathmini ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

“Hizi mbolea zinauzwa kwa bei naafuu lakini uwezo wake zinaweza zikafanya vizuri zaidi ya DAP au sawa na DAP nimeuliza gahalama kwa mkoa wa Dar es salaam zinauzwa elfu 61 na hapa ni elfu 64.Na hii NPS ZINK ambayo ina virubish vinne nimeona inauzwa kwa shilingi elfu 68 hapa Njombe kwa hiyo mkulima akishindwa kununua DAP basi aweze kununua hii mbolea ya NPS”Alisema Ngailo

Vile vile ameongeza kuwa “kuna mwenzetu pia mzalishaji wa ndani wa kampuni ya Minjingu naye tumemsisitiza kuleta mbolea zake za kupandia na kukuzia kwasababu nazo zina bei naafuu,kuna mbolea zingine ambazo zinasambazwa na kampuni ya YARA zinaitwa YARA mira kuna otesha pia kwa hiyo mkulima anaelimishwa kuwa na uwanja mkubwa wa kuweza kuchagua kwa hiyo na sisi tupo ili kuchagiza hiyo.Kwa UREA unaweza ukatumia CAN au SA zenye bei naafuu  kwa hiyo mkulima ana uwanja mkubwa” Alisema Ngailo

Katika hatua nyingine bwana Ngailo amesema licha ya kupanda kwa bei ya mbolea katika soko la dunia lakini upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya nyanda za juu kusini unaridhisha.

“Upatikanaji wa mbolea unaridhisha kwa kiasi kikubwa,katika mikoa yote mitatu tuna tani zaidi ya elfu nane.Mbinga kuna zaidi ya tani elfu moja,Ruvuma kuna zaidi ya tani elfu mbili,na hapa Njombe kuna zaidi ya tani elfu tano.Na kwa bahati nzuri hawa wanaosambaza mbolea wametueleza bado kuna mbolea inakuja”alisema Ngailo

Kwa upande wake Sad Mwang’onda meneja wa kampuni ya Mtewele General Traders ambao ni wasambazaji wa mbolea mkoani Njombe amewahikishia wakulima upatikanaji wa mbolea wakati wote.

“Tutaendelea kuhakikisha pembejeo zinakuwa karibu na wakulima na kama mnavoona sasa hivi tunajiandaa na msimu wa kilimo lakini maghala yetu yana mbolea ya kutosha na nyingine bado iko barabarani inakuja na tutaendelea kuhakikisha mkulima hapati changamoto kwenye upatikanaji wa mbolea na pia tutajitahidi kuhakisha bei kutokuwa ya kumuumiza mkulima”alisema Sad Mwang’onda

Stephan Eliuth Ngailo mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) akiwaeleza waandishi wa habari hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini pamoja na kutoa wito kwa wakulima kutumia mbolea mbadala zenye bei naafuu sokoni.
Baadhi ya mbolea zilizopo kwenye moja ya ghala la msambazaji wa mbolea mkoani Njombe Mtewele General Traders zikionekana wakati mkurugenzi wa TFRA alipofika mkoani humo kukagua upatikanaji wa mbolea.

 

SERIKALI KUTUMIA BILIONI NNE KUKAMILISHA UJENZI WA MAABARA NA MADARASA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

$
0
0

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga (mwenye kofia ya kijani) akipokea maelekezo ya ujenzi wa jengo la kliniki kutoka kwa Meneja Uzalishaji na Usimamizi wa Miradi, Injinia Faraji Magania wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo hilo linalojengwa katika Chuo cha Ufundi Arusha.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga (mwenye kofia ya kijani) akifafanua jambo mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la madarasa na maabara linalojengwa katika Chuo cha Ufundi Arusha.
Hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la madarasa na maabara linalojengwa katika Chuo cha Ufundi Arusha.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga akiangalia mmoja wa wanafunzi wa ufundi magari katika Chuo cha Ufundi Arusha akiinua gari kwa kutumia jeki ya umeme.



SERIKALI inatarajia kutumia zaidi ya Shilingi bilioni 4.2 katika mwaka wa fedha 2021/22 kukamilisha ujenzi wa jengo la madarasa na maabara katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akiwa ziarani Jijini Arusha ambapo amesema jengo hilo litakuwa na ghorofa tatu lenye maabara, madarasa, ofisi na stoo.

Amesema mpaka sasa ujenzi wa jengo hilo umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 2.6 na kwamba hadi kukamilika litatumia jumla ya Shilingi bilioni 6.8.

 "Lengo la Serikali ni kuhakikisha inaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuweza kuzalisha wataalamu watakaokuwa na umahiri unaohitajika katika soko la sasa la ajira," amesisitiza Mhe. Kipanga.

Awali akitoa taarifa ya miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Musa Chacha amesema chuo kimepokea jumla ya Shilingi bilioni 1.499 kutoka Serikalini kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 420 likikamilika na kwamba ujenzi wake umefikia asilimia 15.

Amesema chuo pia kina mradi wa ujenzi wa kliniki itakayogharimu takribani Shilingi bilioni moja ambazo zitatokana na mapato ya ndani na kwamba ujenzi wake umefikia asilimia 30.

Aidha Dkt. Chacha amesema  chuo kupitia maabara zake kimetafiti na kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya jamii ikiwemo vipukuswa vyenye ubora, barakoa na dawa ya kunywa kwa waathirika wa UVIKO-19 ili kupambana na janga la ugonjwa huo.

Naibu Waziri Kipanga yupo Jijini Arusha kwa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi katika vyuo na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Wataalamu waeleza umuhimu wa 4G kuboresha elimu Zanzibar

$
0
0

 
· Walimu na wanafunzi watakiwa kutumia fursa za kimtandao kuendana na kasi ya kidigitali


Zanzibar.Wataalamu mbalimbali wa masuala ya elimu wameeleza nafasi ya mtandao wa 4G katika kuendeleza sekta ya elimu ikiwamo walimu na wanafunzi kutumia fursa ya elimu mtandao kama nyenzo muhimu ya kufundishia na kujifunzia ili kuendana na kasi ya ulimwengu wa kidigitali.

Hayo yalibainishwa jana katika warsha maalumu iliyoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kujadili juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuboresha elimu visiwani humo na kuhudhuriwa na wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali na kufanyika katika Ukumbi wa Taasisi uliopo Vuga.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Meneja Chapa wa Zantel kwa niaba ya Mkuu wa Zantel-Zanzibar,David Maisori alisema warsha hiyo ililenga kujadili kiundani namna gani wadau wa elimu wanavyoweza kutumia intaneti kuendeleza na kuboresha utendaji kazi katika sekta hiyo.

“ Kampuni yetu ya Zantel imefanya kazi kubwa sana ya kujenga miundombinu ya mtandao wenye kasi wa 4G hapa Zanzibar. Tuna minara zaidi ya 100 inayotoa huduma ya mtandao wa 4G kote Unguja na Pemba hivyo kazi ni kwenu sasa wanafunzi, walimu na wahadhili, serikali, taasisi na wadau wengine wa elimu kutumia miundombinu iliyopo ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia,” alisema.

Alisema wanafunzi wana uwanja mpana zaidi wa kuendeleza taaluma zao kwani kupitia mtandao wanaweza kufanya mambo mengi zaidi ya kuwanufaisha kielimu mbali na kutumia katika mitandao ya kijamii pekee.

“Kwa kutambua hilo, Zantel tuna simu za bei nafuu zaidi aina ya SMARTA inayouzwa kwa Sh39,999/= tu pamoja na vifurushi vya wanafunzi ili tu kuhakikisha wanafunzi wanapata intaneti ya uhakika kwaajili ya kujisomea na kupeana taaraifa mbalimbali,” alisema.

Naye, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Omari Saidi Ali alisema Serikali imefanya juhudi kubwa kuboresha miundombinu ikiwamo kujenga mkongo wa Taifa mawasiliano na minara ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma zinakuwa za uhakika na nafuu.

“Tumefanya jitihada hizi ili nchi yetu iendane na karne ya maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na kuanzisha tume mbalimbali za usimamizi.Lakini pia tumeweka sera ikiwamo sera ya Serikali mtandao ili kuchochea matumizi ya mtandao,”

Alitolea mfano kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo mtandao umegeuka kuwa nyenzo muhimu ya mawasiliano hasa kwa kufundishia kutokana na shule kufungwa hivyo kufanya intaneti kuwa mkombozi mkubwa katika kuendeleza elimu.

Aliipongeza Zantel kwa jitihada za kuhakikisha mtandao wa 4G unawafikia watu wengi zaidi pamoja na unafuu wa huduma zake ikiwamo kwa wanafunzi.

Kwa upande wake, Mhaddhiri wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere-Zanzibar, Dk.Venance Kalumanga alisema mbali na kujifunza, wanafunzi wanaweza kutumia mtandao kujiendeleza kibishara ili kuepukana na tatizo la ajira mara baada ya kuhitimu.



Mtaalamu wa masuala ya mitandao, Dk.Venance Kalumanga ambaye pia ni Muhadhiri wa Chuo Cha Mwalimu Nyerere-Zanzibar, akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kujiendeleza kielimu na kibiashara wakati wa warsha iliyoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kujadili matumizi ya 4G kwenye sekta ya elimu.


Baadhi ya wanafunzi wa vyuo Vikuu Visiwani Zanzibar, wakifuatilia mjadala juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuendeleza sekta ya elimu katika warsha iliyoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu pamoja na Serikali uliofanyika jana katika ukumbi wa Taasisi Vuga.

Hakuna taarifa ya 'Level Seat' kutoka vyombo vya usafiri-Kamanda Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni

$
0
0


Kamanda  wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa Kipolisi Kinondoni Notker Kilewa akizungumza na Madereva wa Daladala katika Kituo cha Mawasiliano jijini Dar es Salaam.


 *Asema Mechi ngumu kazi  kubwa ni kutoa Pasi 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

KIKOSI Cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa hakuna taarifa rasmi ya daladala kuwa idadi ya abiria kuendana na idadi viti (Level Seat.)

Askari akipata usumbufu wa Dereva kazi hiyo apewe aweze kuifanyia kazi kwani Mechi ngumu kazi kubwa ni kutoa Pasi ili mwingine aweze kucheza.

Akizungumza na Madereva na Abiria katika Kituo cha Daladala Mawasiliano Kamanda  wa Polisi wa Usalama Barabarani  Mkoa wa Kinondoni Notker Kilewa amesema kuwa taarifa hizo hutolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) au Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani na sio vinginevyo.

Amesema kuwa viongozi wa juu wakitangaza kinachofanyika ni  utekelezaji wa agizo hilo kuwa na level seat.

Amesema kuwa Daladala  mbovu hazitakiwi atakayekamatwa ni dereva pamoja na mmliki wa Daladala wote watawekwa ndani.

Kilewa amesema  dereva wa daladala akirudisha  Daladala mbovu kwa mmiliki, anajitokeza dereva mwingine kulitaka Daladala hiyo licha ya kuwa na ubovu akikamatwa  dereva atawekwa ndani kazi ya mmiliki kuchukua Daladala yake na kufanya matengenezo.

Aidha amewataka  Madereva na makondakta kuwa na ustaarabu wa kuvaa na kuoga kwani hakuna makosa yaliyoanishwa juu ya mtu aliyemchafu kuchukuliwa hatua.

Kilewa amezitaka Daladala zote katika Mkoa huo kuwa na Jacks Mwanga  sheria ambayo ilitungwa mwaka 2015 hivyo ni lazima itekelezwe.

Amewataka makondakta kuacha tabia ya kukimbilia Askari wa  Usalama  Barabarani pale anapokamatwa kwa kuwa ni  ni kosa, Askari anawajibu  wa kumfuata dereva wa gari na kusisitiza kuwa akiwakuta dereva na askari wote ndani.

NEWZ ALERT: CCM YASHANGAZWA MBUNGE WAKE KUJIUZULU UBUNGE

TAASISI YA BENJAMINI ,SERIKALI MKOA WA MTWARA WATOA MAFUNZO YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA KWA WAHUDUMU NGAZI YA JAMII 194

$
0
0


Na Mwaandishi Wetu Mtwara

TAASISI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mtwara chini ya ufadhili wa Shirika la UNICEF imetoa mafunzo kwa wahudumu wa ngazi ya jamii 194 kutoka Newala na Nanyamba Mji ili waweze kuwa kiungo katika utoaji wa huduma za afya kati ya jamii na vituo vya afya vilivyopo maeneo yao.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku 16 kwa wahudumu hao, Ofisa Miradi kutoka Taasis ya Benjamin Mkapa Zawadi Dakika amesema wahudumu hao wamepewa mafunzo ambayo yatawawezesha kutoa elimu ya afya katika jamii yao ili kusaidia kuimarisha afya ya jamii hususani katika afya ya lishe na uzazi.

“Tumechagua  Newala na Nanyamba kwa sababu ilionekana kwamba kuna tatizo kubwa la udumavu na ‘malnutrition’ kwa watoto katika halmashauri zote mbili, kwa hiyo tumewaweka wahudumu hawa ili waweze kusaidia kuelimisha jamii namna bora wanaweza wakatumia vyakula vilivyopo kwenye jamii kuimarisha afya zao,” amesema.

Ameongeza kwa siku 16 wahudumu hao wamefundishwa jinsi ya utoaji wa elimu ya afya katika ngazi ya jamii, jinsi ya kutoa elimu ya afya ya lishe na kutoa rufaa kwa wagonjwa pale wanapoona wanahitaji kwenda kituo cha afya.

Amesema mafunzo hayo yanafanyika katika mikoa takribani kumi nchini ambapo Taasis ya Benjami Mkapa inatekeleza miradi ya kuimarisha afya ya lishe katika jamii.

Kwa upande wakeaimu Mnganga Mkuu wa Halmashauri ya Newala Mji Kidei Mzerela ameishukuru Taasis hiyo ya Mkapa kwa kuchagua Mji wa Newala ambayo amesema yatasaidia kuibua wahitaji wa hudumu za lishe kama vile watoto, wajawazito na wazee.

“Tumekuwa tunapata changamoto ya kuwafikia wahitaji wa huduma za afya kwenye upande wa lishe kama vile watoto na wajawazito, watoto wengi wanakuja kupata huduma za afya wakiwa tayari wana viriba tumbo, tatizo limeshakuwa sugu na inakuwa ngumu kuwatibu,” amesema.

Mzerela amesema kupitia mradi huu wa Mkapa wahudumu waliopewa mafunzo wataweza kuwaibua watoto wenye tatizo la lishe na wajawazito ambao hawaji kiliniki kwa wakati.

Amesema pia kupitia hiyo program ya Taasis ya Mkapa, wahudumu waliopewa mafunzo katika Mji wa Newala wataweza kuwaibua wagonjwa wenye tatizo la TB ambao pia imekuwa ngumu kuwafikia katika jamii.

Aidha Ofisa Lishe wa Mkoa wa Mtwara Harriet Kipuyo amesema Mkoa umekuwa ukifanya jitihada za kupunguza tatizo la lishe ambapo kwa sasa wameweza kupunguza udumavu kwa watoto kutoka asilimia 44 na kufikia asilimia 30 kwa mwaka 2020/2021.

Amesema kwa Newala na Nanyamba bado kuna changamoto kubwa ambapo kwa Newala tatizo la udumavu kwa watoto lipo kwa asilimia 10 na Nanyamba asilimia 11.

Amesema mafunzo wahudumu waliochaguliwa na kupewa mafunzo watasaidia jamii kujikita zaidi katika kuhakikisha lishe bora kwa watoto na jamii nyinging ili kufikia lengo la mkoa huo kupunguza tatizo mpaka kufikia asilimia 5 kwa Newala na Nanyamba TC.

Amesema sababu kubwa inayochangia udumavu kwa Mkoa wa Mtwara ni mila na desturi ambapo watu wazima wanakula pamoja na watoto bila kufahamu kuwa watoto wanahitaji chakula chao maalum chenye lishe bora.

“Kuna tatizo la mila na desturi linachangia sana, mtoto hapewi kipaumbele, wanakula na watu wazima bila kujua mtoto anatakiwa kula nini,” amesma.



Wahudumu ngazi ya jamii Wilaya ya Newala wakiwa wanajifunza jinsi ya kuandaa chakula cha Lishe Bora Kwa watoto na wajawazito ikiwa ni sehemu ya mafunzo waliopewa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Kwa kushirikiana na mamlaka ya Mkoa wa Mtwara


Vifaa vya kazi mbalimbali ambavyo vilitolewa na Taasisi ya Benjamin Kwa ajili ya kuwawezesha wahudumu hao wa afya ngazi ya jamii kutekeleza majukumu Yao katika utoaji wa Elimu ya Lishe na Afaya ya Uzazi kwenye maeneo yao
Wahuduma wa afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri ya Newala wakiwa kwenye mafunzo ambayo yalilenga kuwawezesha kutoa Elimu kwenye maeneo Yao ilo kusaidia jamii kuimarisha afya ya Lishe na Afya ya uzazi. Mafunzo hayo yalitolewa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Kwa kushirikiana na mamlaka ya Mkoa wa Mtwara chini ya Ufadhili wa Shirika la UNICEF.

 

SPIKA ACHOMA CHANJO YA UVIKO-19

$
0
0

 

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Mb) akichoma chanjo ya UVIKO 19  Agosti 2, 2021 Jijini Dar es Salaam

PICHA NA OFISI YA BUNGE

WANANCHI KIJIJI CHA KINGO’MBE WALILIA UFINYU WA ARDHI KUTOKANA NA HIFADHI YA MSITU WA MTO LOASI

$
0
0

 Wananchi wa Kijiji cha King’ombe Kata ya Kala Wilayani Nkasi wameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwaongezea ardhi ya kijiji ili waweze kufanya shughuli za maendeleo kama kilimo na ufugaji kwani wanashindwa kufanya shughuli hizo kutokana na kubanwa na Hifadhi ya Msitu wa Mto Loasi.

Hayo yamesemwa wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akizungumza na wananchi hao leo.

“Shida tuliyonayo wananchi wa King’ombe ni ardhi kuwa finyu, tuna hekta zisizopungua hekta 6,260 na wakazi wa mahali hapa ni zaidi ya kaya elfu 10 na pia tuna Sekondari ya Kata hapa” amesema Titus Pius ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha King’ombe.

Naye Mkazi mwingine wa kijiji hicho Maria Mpoli ameiomba Serikali iwasaidie kuongeza ardhi ili wanakijiji waweze kulima kwa nafasi.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na wataalamu wa ardhi itaunda kamati itayoainisha mipaka mipya ya Hifadhi ya Msitu wa Mto Loasi.

“Hii kamati itapitia mipaka ya hifadhi upya na haitapita mwezi wa nane, tutarekebisha ramani yetu ya mwaka 1957 kwa kuviondoa hivo vijiji ambavyo viliingia mwaka 1974 na baada ya hapo tutaangalia uhitaji wa wananchi kama tunatakiwa kuwaongezea ardhi au kuwapunguzia” Mhe. Mary Masanja amefafanua.

Mhe. Masanja amewaasa wananchi wa kijiji hicho kuwa waangalifu kwa kuepuka kuvamia maeneo ya hifadhi ili kuepuka migogoro ya wanyamapori wakali na waharibifu kama tembo.

“Lengo la Serikali sio kun’gang’ania maeneo bali ni pamoja na kuwakinga wananchi wasikutane na wanyama wakali na waharibifu na changamoto ya tembo itaendelea kuwepo kama sisi tutayasogelea maeneo ya wanyama wakali na waharibifu ” Mhe. Masanja amesisitiza.

 Amesema Serikali inayahifadhi baadhi ya maeneo kwa ajili ya kulinda maeneo ya wanyama kwa ajili ya kutangaza utalii ambao unaongeza mapato, kwa Serikai kwa ajili ya kujenga vituo vya afya, shule n.k.

“Unaweza ukaomba eneo lakini kumbe ni hatarishi ni mapito ya tembo, baada ya mwaka mmoja utaanza kuilalamikia Serikali kwamba tembo wamekula mazao yako hivyo, msisogelee maeneo ya wanyama hawa”Mhe. Masanja ameweka bayana.

Awali , Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mhe. Peter Lijuakali amewaambia wananchi hao kuwa mkutano huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM inayosema itatatua kero za wananchi na kuwapunguzia wananchi nafuu ya maisha.

Mkutano huo ni mwendelezo wa ziara za kikazi za Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja za kusikiliza changamoto za wananchi zinazohusiana na sekta ya maliasili na utalii katika maeneo mbalimbali nchini.

 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi wa kijiji cha King’ombe alipofanya ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu mipaka ya Hifadhi ya Msitu ya mto Loasi katika Kata ya Kala Wilaya ya Nkasi leo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, Mhe. Vicent Mbogo na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mhe. Peter Lijuakali (kushoto).
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha King’ombe wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu mkakati wa Serikali wa kupima upya mipaka ya Hifadhi ya Msitu ya mto Loasi katika mkutano uliofanyika Kata ya Kala Wilaya ya Nkasi leo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mhe. Peter Lijuakali akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) katika kijiji cha King’ombe Kata ya Kala Wilaya ya Nkasi leo.
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, Mhe. Vicent Mbogo akimshukuru Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa ziara ya kikazi katika kijiji cha King’ombe Kata ya Kala Wilaya ya Nkasi leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, Mhe. Vicent Mbogo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha King’ombe Kata ya Kala Wilaya ya Nkasi leo.

 

 

Serikali kupeleka Chanjo ya UVIKO 19 Makambi ya Wakimbizi

$
0
0

 

Na Abubakari Akida,MOHA

Serikali imesema iko katika mpango wa kupeleka Chanjo ya UVIKO 19 katika Makambi na Makazi ya Wakimbizi katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi ikiwa ni mpango mkakati wa kukabiliana na wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Katumba kinachotumiwa na wakimbizi na raia wapya wanaokadiriwa kufikia 86,233  toka nchini Burundi ambao walikimbia mapigano ya kikabila yaliyotokea nchini kwao 1974.

“Katika kukabiliana na janga la UVIKO 19 tayari Wakuu wa Makambi washaanza  kutambua idadi ya watu ambao wanauhitaji wa hiari wa kupata chanjo hiyo ili jamii ya wakimbizi wanaokaa katika makambi yaliyopo nchini ili muda ukifika tuwe na takwimu sahihi za wanaohitaji kuchanjwa na tayari kama mnavyoona tayari zoezi la chanjo lishaanza baada ya siku chache kuzinduliwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu,wito pekee naotoa kwa wakimbizi kufuata ushauri wa wataalamu wa afya katika kujikinga na maradhi hayo ambayo dunia sasa inapitia” amesema Naibu Waziri Chilo

Akizungumzia idadi ya wagonjwa wa UVIKO 19 katika Kituo cha Afya Katumba, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,Dkt.Veneranda Msati amesema hawana mgonjwa aliyefika kituoni huku akielezea utolewaji wa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwa wagonjwa na mama wajawazito wanaofika katika kituo hicho kupata huduma.

“Kwasasa katika kituo chetu hatuna mgonjwa yoyote wa Corona tunachofanya ni kutoa ushauri wa kujikinga na maradhi hayo kwa wagonjwa wanaofika hapa kupata huduma za afya ikiwemo na akina mama wajawazito lakini pia tunatuma wataalamu wetu wa afya kwenda kuwafundisha wananchi katika makazi yao jinsi ya kunawa kwa maji safi tiririka na kukaa umbali unaoshauriwa ili kuepuka maambukizi ya UVIKO”amesema Dkt. Veneranda

Awali akisoma taarifa ya makazi hayo,Mkuu wa Makazi ya Katumba,John Mwita amesema hali ya usalama ni shwari huku wakiendelea kutoa elimu na kufuata sheria za kuishi katika makazi kwa wakimbizi hao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo akizungumzia Hatua ya Serikali kupeleka Chanjo ya UVIKO-19 katika makazi na makambi mbalimbali ya wakimbizi yaliyopo nchini wakati alipofanya ziara ya kikazi leo katika Kituo cha Afya cha Katumba mkoani Katavi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA RAIS KAGAME IKULU KIGALI, RWANDA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mhe. Rais Paul Kagame wa Rwanda Ikulu Kigali Nchini Rwanda leo Agosti 02,2021. Mhe. Rais Samia ameanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili Nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais Kagame.
 

Jinsi Bolt inavyoboresha maisha kupitia usafiri wa mtandao.

$
0
0

 

“Nilijiunga na Bolt miaka miwili iliyopita kwa sababu nilitaka kufanya kitu tofauti. Nilikuwa nikitumia Bolt sana kama abiria katika safari zangu za mjini. Nilipata ushawishi mkubwa kutoka kwa madereva kuhusu uhuru wa masaa yao ya kazi wakiwa dereva wanaotumia mfumo wa Bolt. Hivyo nikaamua kujiunga.  

Ukitumia Bolt, lazima uone mafanikio. Ni nafuu kwa abiria na yenye faida kwa madereva. Leo nina uwezo wa kujikimu na kuchangia matumizi ya nyumbani. Najisikia mwenye furaha. Nashauri vijana wenzangu wajiunge Bolt ili waweze kujikimu na kujitegemea”. – Dereva wa Bolt, Maximillian George (25), Tegeta - Dar es Salaam.



Benki ya NBC yaendelea kuwagusa wakulima kupitia bima ya Afya

$
0
0

 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano rasmi  na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) yanayolenga kuwawezesha wakulima walioko ndani ya vyama vya ushirika nchini kuingia kwenye mfumo wa huduma za matibabu kupitia mpango wa bima ya afya kwa wakulima unaojulikana kama Ushirika Afya.

Mpango huo utatekelezwa na  benki ya NBC  kwa kuwasilisha michango ya  Bima ya afya moja kwa moja  katika Mfuko  wa Taifa wa Bima ya afya  kwa niaba ya wakulima watakaokuwa na Akaunti Benki ya NBC na kuchukua mikopo ya kilimo kupitia benki hiyo.

Wakizungumza kwenye hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw Bernard Konga walisema mpango huo unalenga kuongeza wigo  wa wananchi hususani wakulima katika mfumo wa Bima ya afya na hivyo kutekeleza kikamilifu majukumu yao ya kujenga uchumi imara wakiwa na afya njema.

“Sisi kama benki ili tuweze kuendelea kufanya vizuri zaidi tunahitaji kuwa na uchumi imara ambao kimsimgi pia unategemea nguvu kazi yenye afya njema. Suala la huduma  afya ya uhakika kwa wateja wetu wakiwemo wakulima na moja ya vipaumbele vyetu na ndio sababu hatukusita kuunga mkono mpango huu wa Ushirika Afya,’’ alisema Bw Sabi.

Kwa mujibu wa Bw Sabi, kupitia mpango huo mkulima atachangiwa  kiasi cha sh 76,800 kwa mwaka na ikiwa  mkulima ana mwenza wake  nae atachangiwa kiasi cha sh 76800 ambapo pia kila mtoto atachangiwa sh 50,400 kwa mwaka.

“Bima hii itatolewa na NHIF na itapatikana kwenye matawi yote ya NBC nchi nzima hivyo naomba wakulima wachangamkie fursa hii. Kwa upande wetu maofisa wa benki wamejipanga kuwatembelea wakulima wanachama wa ushirika kuhakikisha wanawapatia habari hii njema kupitia benki ya NBC,’’ aliongeza Bw Sabi.

Kwa upande wake Bw Konga aliwahakikishia wakulima wote watakaojiunga na mpango huo kwamba  watapata huduma bora kwa urahisi  zaidi huku akibainisha kuwa taasisi hiyo imejipanga kurahisisha huduma  kupitia maboresho  ya mfumo wake wa TEHAMA.

“Nina imani kupitia ushirikiano wa kihuduma baina ya NBC na wakulima kote nchini mpango huu utakuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa lengo haswa ni kuwafikia wakulima popote walipo ili tuweze kuongeza wigo wa wanufaikaji wa mfuko huu,’’ alisema Bw Konga ambae alibainisha kuwa hadi kufikia sasa ni asilimia 8 tu ya watanzania ndio wanatumia huduma hiyo ya bima ya afya kupitia mfuko huo.

Kwa upande wake Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Tanzania Dk. Benson Ndiege pamoja na kuzipongeza taasisi hizo mbili kwa makubaliano hayo muhimu alisema ili mpango huo ufanikiwe vizuri ipo haja ya kuhakikisha vyama vya ushirika nchini vinajiimarisha zaidi ili wakulima waendelee kuwa katika mfumo rasmi ambao ndio nguzo ya  mpango huo.

“Zaidi pia napenda kusisitiza kwamba kupitia mpango huu wakulima wahakikishiwe wanapata huduma bora kama ilivyokusudiwa ili kuwavutia wakulima wengine wengi zaidi. Hata hivyo sina hofu na ufanisi wa mpango huu kwa kuwa nafahamu vema uimara wa taasisi hizi mbili yaani NBC na NHIF,’’ alisisitiza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi  (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw Bernard Konga (Kulia) wakionesha hati za makubaliano baina ya taasisi hizo mbili yanayolenga kuwawezesha wakulima walioko ndani ya vyama vya ushirika nchini kuingia kwenye mfumo wa huduma za matibabu kupitia mpango wa bima ya afya kwa wakulima unaojulikana kama Ushirika Afya. Anaeshuhudia ni Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Tanzania Dk. Benson Ndiege (Katikati)


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi  (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw Bernard Konga (Kulia) wakisaini hati za makubaliano baina ya taasisi hizo mbili yanayolenga kuwawezesha wakulima walioko ndani ya vyama vya ushirika nchini kuingia kwenye mfumo wa huduma za matibabu kupitia mpango wa bima ya afya kwa wakulima unaojulikana kama Ushirika Afya. Anaeshuhudia ni Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Tanzania Dk. Benson Ndiege (Katikati)


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi  (Kushoto) akimkabidhi zawadi kutoka benki hiyo  Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Tanzania Dk. Benson Ndiege (Kulia) wakati wa hafla hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi  (Kushoto) akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi  (Kushoto) akimkabidhi zawadi kutoka benki hiyo  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw Bernard Konga (Kulia) wakati wa hafla hiyo.




Viewing all 118927 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>