Quantcast
Viewing all 118561 articles
Browse latest View live

REMEMBERING THE LATE Dr. WILBERD CHAGULA: THE FIRST INDIGENOUS PRINCIPAL OF THE UNIVERSITY COLLEGE OF DSM


By MZEE WA ATIKALI  ✍️✍️✍️


1. Introduction

The late Dr. WILBERD KUMALIJA CHAGULA was one of the most distinguished, most prominent and highly respected citizens of this country who trained in Medical Science and served as an Academician, a Member of Parliament, a Minister  and, eventually a Diplomat before he breathed his last.

2. Birth  Date & Place

The late Dr. CHAGULA was born on 3.2.1926 at Mondo Isulilo, Shinyanga, where his father was a prosperous farmer.

3. Dr. CHAGULA's Education

3.1 Primary Education

Dr. CHAGULA was a gifted student who was educated at Ibadakuli primary school.

3.2 Secondary Education

Dr. CHAGULA then joined Tabora Boys Government Secondary school, which has produced a high proportion of Tanzania's Cabinet ministers.

3.3 University Education

Dr. CHAGULA joined the prestigious Makerere university in 1945, graduating, in 1951, with an LMS (East Africa) degree.

4. Dr. CHAGULA Undergoes Internship

Having completed the Licentiateship in medicine at the age of 25, Dr. CHAGULA returned to Tanganyika as an Intern at the Sewa Haji hospital, Dsm where he underwent  a  mandatory internship program for one year, gaining his final qualifications to practice medicine.

5. Dr. CHAGULA Becomes a Lecturer at Makerere

As he had passed his exams with flying colours at Makerere university, Dr. CHAGULA, in 1953, returned to Makerere university college of Medical school, initially as a Tutorial Assistant and later as a full member of the academic staff, remaining there for 8 years.

However, much of that time was spent abroad studying at King's college , Cambridge UK, at West Indies, Kingston Jamaica and Yale University school of Medicine, USA.

6. Dr. CHAGULA Returns  to Tanganyika

The establishment of the University college, Dsm soon after independence drew Dr. CHAGULA back to his native country. It was a step that was to change the direction of his career forever. Although his short academic career in medicine had been full of promise, it was after this critical move that he was to record his major achievements.

7. Dr. CHAGULA Appointed Vice Principal

Dr. CHAGULA was appointed as the Vice Principal and Registrar of the then University College, Dsm in 1963.

8. Dr. CHAGULA Appointed the First Indigenous Principal

In 1965, Mwalimu NYERERE appointed Dr. CHAGULA as the first Indigenous Principal of the University college, Dsm.

9. Dr. CHAGULA Makes Unique Contribution

Dr. CHAGULA guided the College through the important growth phase that led to its emergence as the independent university of Dsm, when the College umbrella institution, the university of East Africa , was dissolved in 1970.

Dr. CHAGULA applied his strong scientific background to the wider range of activities. He was, at that time, without question, the most senior   Tanzanian scientist.

Frequently, Dr CHAGULA was called upon by the Govt to represent TZ at international conferences. The opportunity to discuss various topics with some of the world's greatest thinkers was an invaluable experience for Dr. CHAGULA.

10. Dr. CHAGULA Nominated as MP

On 10.11.1970, Mwalimu nominated 10 Tanzanians, including Dr. CHAGULA, as national MPs.

12. Dr. CHAGULA Appointed Minister for Water

After the General Elections in 1970, one of the significant Ministerial line-ups was the creation of a new ministry of Water. Dr CHAGULA was taken from the academics to head the new Ministry. Until then, the Water docket had been under different ministries.

13. Dr. CHAGULA Appointed Minister for Economic Affairs

In 1972, Dr. CHAGULA was moved to the higher profile position of Minister for Economic Affairs.

He frequently represented the Govt at international meetings, becoming very familiar with the UN & its specialised agencies, always looking for ways that TZ could derive benefit from its activities.

14. Dr. CHAGULA Appointed Ambassador

Following the demise of the East African Community in 1977, Dr. CHAGULA moved to Switzerland, in 1978, as TZ's first Ambassador to the United Nations in Geneva.

In 1986, Dr. CHAGULA was transferred, by H.E President ALI HASSAN MWINYI, to the post of Ambassador to the UN HQs in NY, US, his last career posting prior to his retirement in 1989.

15. The University Library renamed after Dr. CHAGULA

The University of Dar es Salaam Library has been renamed after Dr. CHAGULA, in recognition of his vision, ambition and leadership. This was an absolute honour by the said University.

16. Dr. CHAGULA awarded many Awards & Medals

In recognition of his distinguished service to his country and the world at large, Dr. CHAGULA, during  his life time, was awarded various awards internationally and nationally.

By MZEE WA ATIKALI  ✍️✍️✍️

April 6, 2020

Virusi vya Corona: Papa awataka watu 'kutokubali kushindwa na uoga'

Papa Francis amewataka watu kutosalimu amri kwa uoga wa virusi vya corona, na kuwataka kuwa "wajumbe wa uhai wakati wa kifo".

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alizungumza wakati wa sherehe za pasaka Jumamosi, katika kanisa la St Peter's Basilica ambalo lilikuwa na watu wachache.

Waumini wa Kikatoliki bilioni 1.3 kote duniani wana fursa ya kufuatilia ibada ya moja kwa moja mtandaoni.

Marufuku ya watu kutokutoka majumbani bado inaendelezwa katika maeneo mbalimbali nchini Italia ambako kumeathiriwa vibata na janga la Corona.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte alimsifu Papa kwa kuonyesha kuchukua majukumu yake kwa tahadhari baada ya kuadhimisha ibada ya pasaka bila ya mkusanyiko wa waumini.

Wakristo kote duniani wanasherehekea sikukuu ya pasaka, moja ya sikukuu muhimu katika kalenda ya Kikikristo licha ya hatua zilizochukuliwa katika nchi nyingi duniani zilizosababisha mamilioni ya watu kusalia majumbani

Makasisi wengi wanaendesha ibada zao makanisani bila waumini kukusanyika.
 

USHAURI KWA WANAHABARI KUHUSU KUCHUKUA TAHADHARI ZAIDI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA CORONA


 Siku ya Ijumaa Aprili 10, 2020 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitoa taarifa kwa umma juu ya mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini. Katika taarifa hiyo Waziri wa afya alieleza idadi ya watu waliothibitishwa kupata maambukizi ya COVID-19 nchini kuwa ni 32. Kati ya hao, wagonjwa 24 wanaendelea na matibabu, watano wamepona na uwepo wa vifo vya wagonjwa watatu tangu ugonjwa huu ulipoingia nchini.

Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na familia za waliopoteza ndugu zao kutokana na ugonjwa huu unaosababishwa na virusi vya corona.

Wito wetu kwa Wanahabari na Wananchi

Kutokana na kuongezeka kwa visa vya corona nchini ambavyo inaonyesha vimeanza kusambaa ndani ya nchi (Local Transmission and not imported). Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa pamoja tunatoa ushauri kwa wanahabari, taasisi mbalimbali na wananchi kama ifuatavyo:

1.      Kuchukua tahadhari zaidi na kutoa taarifa kwa wakati kwenye mamlaka husika endapo wakibaini mtu mwenye dalili za maambukizi ya virusi vya corona.

2.      Tunawasisitiza waandishi wa habari, taasisi mbalimbali na wananchi kutumia teknolojia ya kisasa katika kufanya kazi zao au mikutano, kwa mfano kutumia Skype, Zoom, kupiga simu, WhatsApp N.K.


3.      Tunashauri vituo vya habari nchini kupunguza vipindi vya kawaida na kuanza kutumia vipindi hivyo kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujikinga na virusi vya corona. Wananchi wapewe nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa kutoka kwa wataalamu.

4.      Waandishi wa habari wanapaswa kuzingatia kwa makini taratibu za kitaaluma, huku wakihakikisha kutumia vyanzo vya habari vya kuaminika kama vile Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO).

5.      Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari zaidi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa kuzingatia Miongozo iliyotolewa na



6.      Waandishi wa habari wanapaswa kuchunguza kwa makini aina ya matukio ambayo wanapanga kuhudhuria, kutokana na uwepo wa amri ya Serikali inayokataza mikusanyiko ya idadi fulani ya watu ili kujikinga na hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.

7.      Wamiliki wa vyombo vya habari wanapaswa kuwawezesha waandishi wa habari usafiri binafsi au kutumia uber, gloves ukiwa, mavazi ya kujikinga kiafya kama vile suti ya kitabibu (bodysuit) na barakoa inayofunika uso gubigubi (full face mask).

8.      Tunatoa ushauri kwa waandishi wa habari kufuata sheria na kuomba ruhusu kwa mamlaka husika endapo wanahitaji kukusanya taarifa kutoka maeneo ya karantini, hospitali na maeneo mengine yenye vizuizi vya kuingia.


9.      Tunapenda pia kuishauri serikali kutenga maeneo maalumu ya watoa huduma kwa wagonjwa wa corona ili wasirudi majumbani mwao kuepusha maambukizi kwenye familia zao.

10.Tunatoa ushauri kwa watu wote mfano viongozi, Asasi za Kiraia, wanasiasa, viongozi wa dini, watu mashuhuli watumie vipaji vyao kuelimisha umma kuhusu namna ya kujikinga na virusi vya corona kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Afya.

11.Tunawahimiza waandishi wa habari pale wanapokusanya taarifa, kutumia maikrofoni ya kushikilia (directional mic) kwa kuishika kwa mbali iwezekanavyo, badala ya kutumia maikrofoni inayoshikizwa kwenye mavazi (clip mic).

12.Meza na vifaa vyote vya kufanyia uhariri, kompyuta, vichanganyio (mixers) na vifaa vingine vya kazi lazima vifutwe na vitakasa mikono kila baada ya kipindi au shughuli ya uhariri.

13.Ni muhimu kushirikisha Asasi za Kiraia, vyombo vya habari binafsi na vya serikali katika kamati zinazoundwa kukabiliana na virusi vya corona kwa kuwa AZAKi na vyombo vya habari ni wadau wakubwa katika kutatua changamoto za kijamii.

Kwa kutambua umuhimu wa kazi za waandishi wa habari, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania utatoa mafunzo kwa waandishi wa habari mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar kwa njia ya mtandao ili kuwawezesha namna bora ya kufanya kazi za uandishi salama hasa katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.

Imetolewa kwa pamoja na:

THRDC, MCT, TEF na UTPC

Dar es Salaam, Tanzania

Aprili 12, 2020.

WAZIRI HASUNGA AWAHAKIKISHIA WATANZANIA MAVUNO YA MAZAO YATAKUWA YA KUTOSHA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua shughuli za maendeleo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na Mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya PCT Ndg John Power wakati akikagua eneo maalumu lililopemndekezwa na kampuni hiyo kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu za Pareto wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa maendeleo wakati akikagua shughuli za maendeleo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua maendeleo ya mazao shambani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua shughuli za maendeleo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imeendelea kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula ili watu wake wawe na nguvu ya kufanya kazi kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. 
Kauli hii ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Tarehe 11 Aprili 2020 mkoani Songwe wakati akikagua mashamba ya wakulima mashambani.
Akiwa katika Kijiji cha Idiwili na Iyula mkoani humo Waziri Hasunga ameridhishwa na hali ya ustawi wa mazao ya wakulima shambani hivyo kuwahakikishia wananchi kuwa kutakuwa na mavuno ya kutosha katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 kwani wakulima wengi wameitikia wito wa serikali wa kuongeza tija na uzalishaji wa mazao.
Waziri Hasunga amesema kwa miaka mitatu  sasa serikali ya imeendelea kuhakikisha nchi inazalisha mazao mengi na ya kutosha ya chakula kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wizara ya kilimo na taasisi zake.
Alibainisha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula mwaka 2019 ulishuka ikilinganishwa na mwaka 2018 ambapo nchi ilizalisha tani milioni 16.8 hivyo katika msimu huu wa mwaka 2020 nchi itazalisha mazao ya kutosha na kuwa na utoshelevu mkubwa wa chakula
Amewapongeza wakulima nchini kwa kuitikia wito na maelekezo ya serikali katika kuhakikisha uzalishaji nchini unaendelea kuongezeka hususani kwenye mazao ya chakula na biashara.
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga ameigiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha inaharakisha upatikanaji na usambazaji wa mbolea aina ya UREA ambayo imeadimika kwa wakulima.
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amebainisha mkakati wa serikali wa kuongeza uzalishaji wa zao la Pareto ambapo umeanza mkakati wa makusudi wa kuanzisha shamba la pareto katika Kijiji cha Idiwili Mkoani Songwe kwa ajili ya uvunaji wa mbegu ili kuongeza kiasi cha mbegu kwani idadi ya wakulima inaongezeka kila siku. 
Tanzania imejaaliwa kuwa na mifumo mbalimbali ya kilimo yenye misimu ya tabia nchi inayotofautiana na hali za ekolojia ya kilimo inayofaa kwa uzalishaji wa mazao.  Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni pamoja na mahindi, mtama, lulu, mpunga, ngano, jamii ya kunde (hasa maharage), mihogo, mbatata, ndizi mbichi na ndizi za kuiva.  Vyakula mbalimbali vya biashara vinavyozalishwa ni pamoja na kahawa, pamba, korosho tumbaku, katani, pareto, chai na miwa. 

Mbegu za mafuta ni pamoja na karanga, alizeti na ufuta. Kilimo cha bustani hujumuisha mazao kama vile mbogamboga, matunda, maua na viungo vya chakula. Karafuu ni zao kuu la biashara kwenye visiwa vya Zanzibar.

TUSHEREKEE PASAKA TUKICHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA: RC MTAKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi Mjini (hawapo pichani), wakati alipofika kanisani hapo kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao leo Aprili 12, 2020 kushoto ni Mchungaji wa Kanisa hilo, Greyson Kinyaha na kulia ni Mchungaji Sarah Kimaro.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
aadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi Mjini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  wakati alipofika kanisani hapo kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao leo Aprili 12, 2020.Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akipokea ekaristi takatifu katika misa takatifu Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini, wakati aliposhiriki katika misa hiyo na kutoa salamu za pasaka kwa waumini wa Kanisa hilo waumini hao leo Aprili 12, 2020.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akizungumza na waumini wa Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini wakati alipofika kanisani hapo kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao leo Aprili 12, 2020.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini,Peter Mkunya akitoa mahubisri ya neno la Mungu katika misa Takatifu leo Aprili 12, 2020.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi Mjini wakiimba wakati wa ibada ya kwanza  leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka   ameshiriki katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka kwa waumini na wananchi.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara baada ya kuwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Bariadi Mjini ambapo ameshiriki ibada ya Pasaka na kutoa salamu za Pasaka za Mkoa leo Aprili 12, 2020 kwa waumini wa Kanisa hilo.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Waimbaji wa Kwaya kutoka Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini wakiimba wakati wa ibada leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka   ameshiriki katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mchungaji wa Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini, Amosi Ndaki akitoa mahubiri ya neno la Mungu wakati wa ibada leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka   ameshiriki katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Kwaya ya Mtakatifu Johh kutoka Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini  wakiimba wakati wa misa takatifu  leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka   ameshiriki katika misa hiyo na kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Baadhi ya wanakwaya na Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Luka Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Pasaka za Mkoa kwa waumini wa kanisa hilo leo Aprili 12, 2020.
……………………………………………………………………………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka leo ameshiriki ibada ya Pasaka katika makanisa tofauti mjini Bariadi na kuwasisitiza waumini na wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu kutulia, kuepuka safari zisizo za lazima na kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali.
Mtaka ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akitoa salamu za Pasaka za Mkoa aliposhiriki ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John, Parokia ya Mtakatifu Luka, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Bariadi Mjini na Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania (AICT) leo Aprili 12, 2020.
“Nimeona watu wananawa mikono utaratibu huu usiishie kwenye nyumba za ibada na maeneo ya kutolea huduma, uende mpaka nyumbani,tunapokuwa kwenye nyumba za ibada pia tuzingatie umbali katika ukaaji wetu na wakati wa kupokea huduma za kiroho: pasaka hii tutulie majumbani tuepuke safari zisizo lazima na tufuate maelekezo ya Serikali.” alisema Mtaka.
Aidha, pamoja na kuwasisitiza wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima Mtaka ametoa wito kwa jamii kuona namna ya kuwasaidia zaidi wazee, watoto  na watu wenye magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu kuepuka zaidi mikusanyiko hiyo ili kuwaondolea hatari ya kupata maambukizi kutokana na hali ya kinga zao za mwili.
Katika hatua nyingine Mtaka amewataka wazazi kuwasimamia watoto wao kujisomea kwa bidii kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona hususani wale wa madarasa ya Mitihani ya Kitaifa kwa kuwa mitihani hiyo bado ipo na itafanyika.
Sambamba na hayo Mtaka amewaasa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kutunza chakula ambacho kimepatikana mwaka huu na kutokiuza kwa matumizi ambayo si ya lazima hususani katika kipindi hiki ambacho chakula kinauzwa kwa bei ya chini huku akiwasisitiza kujiunga na Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii ili waweze kupata unafuu katika huduma za matibabu.
Kwa upande wao viongozi wa makanisa akiwemo Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John, Peter Mkunya, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Luka, Martine Jilala, Mchungaji wa KKKT Bariadi, Greyson Kinyaha na Mchungaji wa AICT, Amosi Ndaki wamesema wametumia Maadhimisho ya Kufufuka kwa Yesu Kristo(Pasaka) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na Janga la Corona na kuendelea kuwakumbusha waumini kuzingatia maelekezo ya viongozi wa Serikali na wataalam wa afya.
Koga Mihama na George Lyimo ni miongoni mwa waumini waliohudhuria ibada ya pasaka wameishukuru Serikali kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa kujikinga na Maambukizi ya CORONA huku wakitoa wito kwa wananchi wote kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali ili Maambukizi ya Virusi vya Corona yaishe nchini Tanzania.

JUMUIYA YA MABOHORA YAENDELEA KUPELEKA MISAADA HOSTELI YA MAGUFULI KUPAMBANA NA UGONJWA WA CORONA

Matarajio ya Hali Mbaya ya Hewa kwa siku Tano

Dkt.Kijazi:Ongezeko la joto duniani,limesababisha mabadiliko ya hali ya hewa

Na Karama Kenyunko-Michuzi TV

KILA ifikapo Machi 23 kila mwaka,dunia mzima huadhimisha siku ya hali ya hewa duniani. Ni siku ambayo Mkataba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ulisainiwa mwaka 1950. Kwa kawaida siku hii huadhimishwa na kila nchi mwanachama wa shirika hilo. 
 
Taasisi za Hali ya Hewa, zikiwa ni Mamlaka zilizopewa jukumu la kutoa na kusimamia huduma za hali ya hewa katika nchi wanachama wa WMO,hutumia siku hii kuonesha na kueleza huduma wanazotoa katika kuhakikisha usalama wa watu na mali zao dhidi ya athari zitokanazo na hali mbaya ya hewa. Kwa hapa nchini, shughuli zote zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa husimamiwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
 
 TMA ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2019 kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. TMA iko chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya uchukuzi na imepewa jukumu la kutoa na kudhibiti huduma za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, TMA ikiwa miongoni mwa Taasisi 192 za nchi wanachama wa WMO inaungana na Jumuiya ya hali ya hewa duniani kote kusherehekea Siku ya Hali ya Hewa duniani (WMD). 
 
Katika kusisitiza na kuhamasisha umuhimu wa huduma za hali ya hewa katika mipango na maamuzi kwenye sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii, sherehe za WMD zimekuwa zikiadhimishwa kwa kaulimbiu maalumu. Ambapo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema kaulimbiu ya mwaka huu ni “Hali ya Hewa na Maji (Climate and Water)”, ambapo kauli hiyo inaenda sambamba na kaulimbiu ya Siku ya Maji Duniani kwa mwaka 2020, ambayo imejikita katika athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye sekta ya maji. 
 
Dkt.Kijazi ambae pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), amesema hewa na Maji inafafanua uhusiano uliopo kati ya hali ya hewa na rasilimali maji, pamoja na umuhimu wa kutumia huduma za hali ya hewa katika maendeleo ya sekta ya maji.
 
 Aidha,Dkt.Kijazi amesema kupitia siku hii ni vyema awafahamishe wadau wa huduma za hali ya hewa hapa nchini kwamba kwa mujibu wa taratibu za mgawanyo wa majukumu katika Umoja wa Mataifa,Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limepewa jukumu la kusimamia masuala ya hali ya hewa na maji. 
 
Amesema Taasisi za Hali ya Hewa na Maji (NMHSs) katika nchi wanachama wa WMO hufanya uangazi wa hali ya hewa na maji na data za hali ya hewa na maji hutumika katika kutoa taarifa za mwelekeo wa hali ya hewa na maji ili kusaidia maamuzi katika vikao vya Umoja wa Mataifa vinavyohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi. 
 
Mkurugenzi huyo anasema ongezeko la joto duniani (global warming) linasababisha changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na limeathiri kwa kiasi kikubwa mifumo ya mzunguko wa maji kutokana na kubadilika kwa mifumo ya mikondobahari, mvukizo wa anga, ufanyikaji wa mawingu na mtiririko wa maji kwenye uso wa dunia. "Athari hizo zinatokana na uhusiano uliopo wa moja kwa moja wa mifumo ya hali ya hewa na mzunguko wa maji.
 
Changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa imeathiri pia upatikanaji na ubora wa maji na kusababisha upungufu wa maji yanayohitajika kwa matumizi mbalimbali,"amesema Dkt.Kijazi Amesema mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha mabadiliko ya mfumo wa mzunguko wa maji kwa namna tofauti tofauti, mfano, maeneo yenye joto zaidi hupata mvukizo zaidi wa maji kutoka baharini, ziwani, ardhini na kwenye mimea.
 
 "Anga ililopo katika eneo lenye joto zaidi lina uwezo wa kuhifadhi unyevunyevu kwa asilimia nne zaidi kwa kila ongezeko la nyuzi joto moja katika kipimo cha Celcius, na kusababisha kufanyika kwa mawingu ng’amba ambayo huambatana na mvua kubwa na ngurumo",anasema Dkt. Kijazi Mkurugenzi huyo amesema kuongezeka kwa joto husababisha mvukizo wa maji kutoka udongoni na kufanya ardhi kuwa kame zaidi na udongo kuwa mgumu, hali hiyo husababisha maji kushindwa kuingia udongoni pindi mvua inaponyesha, badala yake maji hutiririka kukimbilia kuelekea mitoni, ziwani au baharini, na kuiacha ardhi kuendelea kuwa kame. 
 
Amesema matokeo yake ni uwezekano wa kuongezeka kwa matukio ya ukame na upungufu wa maji safi na salama. Aidha,ongezeko la joto katika maji ya mito,maziwa, bahari na mabonde ya maji husababisha uhaba wa hewa safi ya oksijeni katika maji na kupelekea vifo kwa viumbe hai wanaoishi kwenye maji.
 
 "Matukio ya mvua kubwa na ongezeko la mtiririko wa maji pia husababisha usafirishwaji wa udongo, vijidudu vya magonjwa na kemikali kama vile mabaki ya mbolea na pembejeo kutoka maeneo mbalimbali yakiwemo mashamba, viwanda na mashimo ya maji taka kuelekea kwenye vyanzo vya maji,"amesema Aidha, miongoni mwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa, Dkt. Kijazi amesema ni ongezeko la kina cha bahari duniani kote, husababishwa na mambo makubwa mawili,kutanuka kwa maji ya bahari kutokana na kuongezeka kwa joto la maji na pili ni kuyeyuka kwa barafu katika maeneo yenye barafu, hususan katika uzio wa actic na antaktika. 
 
Amesema ongezeko hilo la kina cha bahari linahatarisha miundombinu, mazingira na maisha ya jamii zinazoishi maeneo ya fukwe za bahari na visiwa, na kuathiri ubora wa maji kwa kusababisha mwingiliano wa majichumvi na vyanzo vya maji baridi hali inayopelekea hitaji la kutumia teknolojia yenye gharama kubwa kusafisha maji hayo. 
 
Kutokana na shughuli mbalimbali zinazotegemea maji kwa namna moja au nyingine, Dkt. Kijazi amesema mabadiliko hayo katika mifumo ya maji yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya viumbe katika uso wa dunia katika siku za usoni. "Hali hii inaonesha kwamba hali ya hewa ina mchango mkubwa na wa pekee katika mtawanyiko na upatikanaji wa maji katika uso wa dunia, pamoja na ubora wa maji yanayohitajika kwa shughuli za kiuchumi na kijamii kwa maendeleo endelevu,"amesema .
 
Amesema kwa msimu wa mvua za Oktoba hadi Desemba (vuli), 2019 kulikuwa na mvua nyingi zaidi katika mwezi Oktoba na Desemba. Aidha, katika mwaka 2020 matukio ya mafuriko yametokea katika maeneo mbalimbali ya nchi hususan mkoani Lindi. "Inatazamiwa kuwa, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, matukio ya mafuriko na ukame yataongezeka kwa wingi na ukubwa na hivyo kusababisha athari katika sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo sekta ya maji, nishati, usafirishaji na kilimo,"amesema. 
 
Dkt.Kijazi amesema pamoja na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, na athari zake katika mfumo wa mzunguko na upatikanaji wa maji, taarifa za hali ya hewa za sehemu husika zitasaidia katika kupanga shughuli za kiuchumi na kijamii zinazotegemea upatikanaji wa maji. Mkurugenzi huyo amesema taarifa hizo ni pamoja na data za hali ya hewa za kipindi kirefu ,utabiri wa hali ya hewa na matazamio ya mabadiliko ya hali ya hewa. 
 
Hivyo, ni muhimu kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu hali ya hewa ya eneo husika na kutumia taarifa za hali ya hewa. Mkurugenzi huyo amesema katika ngazi ya kidunia, Programu ya Kidunia ya Huduma za Hali ya Hewa inayoongozwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani “Global Framework for Climate Services (GFCS)” ndiyo programu inayoongoza jitihada za matumizi ya huduma za hali ya hewa katika mipango ya maendeleo. 
 
Katika kutekeleza programu hiyo kwenye ngazi ya kitaifa kwa nchi wanachama wa WMO, Dkt. Kijazi amesema TMA inatekeleza Programu ya Kitaifa ya Huduma za Hali ya Hewa “The National Framework 6 for Climate Services (NFCS)”, ambayo ina malengo ya kuboresha huduma za hali ya hewa katika sekta zilizoathiriwa zaidi na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo sekta ya maji. Amesema katika kutimiza mahitaji ya wadau na matakwa ya programu ya NFCS pamoja na sheria iliyoanzisha TMA, mamlaka hiyo hufanya shughuli za uangazi wa masuala ya hali ya hewa. 
 
Amesema TMA hufanya uangazi kupitia mtandao wake wa vituo vya hali ya hewa vilivyopo nchi nzima, ambavyo vinajumuisha vituo vilivyopo kwenye uso wa dunia nchi kavu, vilivyopo bandarini na vilivyopo katika anga la juu ambavyo vinajumuisha mtando wa RADAR (upper air stations). Aidha, Dkt. Kijazi amesema TMA hutoa utabiri wa hali ya hewa unaotumika katika mipango kwaajili ya shughuli za kijamii na kiuchumi, utabiri unaotolewa na TMA ni pamoja na utabiri wa kila siku (saa 24), siku tano, siku kumi (dekadal forecast), mwezi, msimu na tahadhari za hali mbaya ya hewa (severe weather warnings and alerts).
 
 "Tabiri hizi za hali ya hewa ni kwa jamii yote kwa ujumla, zikiwa na ushauri unaolenga sekta ambazo shughuli zake hutegemea zaidi hali ya hewa na maji. Hutoa taarifa mahsusi kwa sekta mahsusi kama vile sekta ya usafiri wa anga na usafiri wa kwenye maji,"amesema. Utabiri huo husambazwa kwa njia mbalimbali zikiwemo tovuti ya TMA (www.meteo.go.tz), radio, runinga, mitandao ya kijamii (facebook, twitter, Youtube, na WhatsApp), magazeti na mfumo wa kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa njia ya simu za mkononi (FarmSMS). TMA imeendelea kupata mafanikio zaidi katika kutekeleza mpango mkakati wake. 
 
Aidha, Dkt. Kijazi amesema TMA imefanikiwa kuzindua jarida la huduma za hali ya hewa, ambalo ni mahsusi kwa kuwafikia wadau na jamii yote kwa ujumla ikiwemo sekta ya maji. Katika eneo la vifaa vya hali ya hewa, TMA imeendelea na mkakati wake wa kuboresha vifaa kwa kununua vifaa vya kisasa na kuondoa vifaa vinavyotumia zebaki. Amesema katika kuhakikisha TMA inaboresha huduma zake na kuchangia katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, TMA imeendelea kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa ambazo zimechapishwa katika machapisho mbalimbali ya kisayansi ya kimataifa. 
 
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika taarifa yake amesema kwa upande wa Tanzania, TMa ina jukumu la kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa utabiri wake ambao huchangia kulinda vyanzo vya maji na hivyo kuboresha upatikanaji wa rasilimali maji. Amesema upatikanaji wa rasilimali maji ni muhimu katika kuchangia maendeleo ya Taifa na malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu. 
 
Huduma za hali ya hewa ni muhimu katika malengo hayo hususani lengo namba saba la SDG7 ambalo linahusiana na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi. "Tanzania inaendelea kutekeleza maridhiano ya kimataifa katika sekta ya hali ya hewa kwa kuhakikisha Mamlaka ya Hali ya Hewa inatoa huduma za hali ya hewa katika viwango vinavyokubalika kimataifa,"amesema Mhandisi Kamwelwe. 
 
Mhandisi Kamwelwe amesema utekelezaji huo ni pamoja na kuijengea uwezo Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa upande wa vifaa na wataalamu ili kuhakikisha wanafuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazohitajika nchini, kikanda na kimataifa kwa matumizi ya sekta zote ikiwa ni pamoja na sekta ya maji. Amesema, 2019 Serikali ilipitisha sheria ya kuhuisha Wakala wa Hali ya Hewa nchini kuwa Mamlaka kwa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa namba mbili ya 2019. 
 
Sheria hiyo inaiwezesha mamlaka kutekeleza majukumu yake kitaifa, kikanda na kimataifa na kutoa huduma za hali ya hewa kwa jamii. Pia, amesema sheria iliyounda Mamlaka hiyo inaipa nguvu za kisheria za kudhibiti huduma za hali ya hewa hapa nchini na kukusanya mapato yanayotokana na matumizi ya huduma za hali ya hewa zinazotumiwa kibiashara. Aidha, amesema Sheria hiyo inaitambua Serikali kama mdau mkubwa wa huduma zinazotolewa kwa matumizi ya wananchi (Public Good) hususan tahadhari za hali mbaya ya hewa. 
 
"TMA inatarajiwa kuboresha zaidi huduma za hali ya hewa nchini, hivyo sheria hii imehakikisha uwakilishi,ushirikishwaji, mabadiliko ya kimtazamo na uwajibikaji wa wadau wote ikiwa ni pamoja na sekta binafsi na jumuiya za kijamii,"amesema Mdandisi Kamwelwe.
 
 Katika kuhakikisha kuwa TMA inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi ili kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini, Kamwekwe amesema Serikali inaendelea kuijengea uwezo mamlaka hiyo ili iweze kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kuboresha utabiri wa hali ya hewa. 
 
"Taarifa za hali ya hewa ni za muhimu sana katika kutoa maamuzi na kuweka mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, taarifa na huduma za hali ya hewa husaidia na kuongeza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na vilevile kuchangia katika maendeleo endelevu,"amesema Waziri huyo amesema huduma za hali ya hewa zitolewazo husaidia watumiaji wa huduma hizo kupanga vyema shughuli zao ambazo ni pamoja na mipango ya utoaji wa huduma za maji mijini, kilimo, mifugo, maendeleo ya uvuvi, uzalishaji wa nishati na uratibu wa maafa miongoni mwa sekta nyingine. 
 
Aidha, katika jitihada za kuboresha huduma za hali ya hewa nchini, Serikali imeendelea kuongeza uwezo wa TMA kwa kuboresha mtandao wa Taifa wa vituo vya upimaji wa hali ya hewa ili kuboresha upatikanaji wa data na usahihi wa utabiri wa hali ya hewa. Amesema Serikali inaendelea kuongeza uwezo wa TMA kufuatilia na kupima hali ya hewa na kuboresha utabiri wa hali ya hewa kwa matumizi katika sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kufanya maamuzi ya mipango ya maendeleo katika sekta hizo. 
 
"Kwa kuzingatia hatua kubwa ya maendeleo iliyopigwa katika nyanja ya teknolojia na mahitaji yake katika sayansi ya hali ya hewa, Serikali inaipongeza TMA kwa kuendeleza ubunifu na matumizi ya teknolojia katika kuboresha huduma wanazotoa hapa nchini'"Kwa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli ambapo imeboresha utendaji wa TMA katika utoaji wa huduma bora za hali ya hewa, hatuna budi kutumia huduma hizi ili kuboresha shughuli zetu za kila siku na vilevile kufanya kazi kwa pamoja ili kuendelea kuboresha huduma hizi kwa siku zijazo,"amesema.
 
 Amesema uwekezaji wa Serikali katika utoaji wa huduma za hali ya hewa hususani katika kuboresha miundombinu ni pamoja na ununuzi wa Rada 4 za hali ya hewa kwa lengo hilo hilo la kuboresha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa nchini. 
 
Amesema Rada hizo zimefungwa Mwanza na Dar es Salaam na zingine tatu ziko katika hatua ya ununuzi ambazo zitafungwa Mtwara, Mbeya na Kigoma, ili kukamilisha mtandao wa Rada zitahitajika Rada zingine mbili ambazo zitafungwa Dodoma na Kilimanjaro. Pia, amesema kwa kutambua ongezeko la uhitaji wa huduma za hali ya hewa na changamoto zinazotukabili ambazo zinahitaji kutatuliwa, Serikali itaendelea kuwekeza ili kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa na maji kwa kuongeza uwezo wa wataalamu na miundombinu. 
 
"Kwa kuzingatia maboresho yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini, ni vyema kuongeza juhudi katika kutumia huduma hizi katika mipango ya sekta zote za kiuchumi na kijamii na utekelezaji wa miradi ya kitaifa kama vile ujenzi wa miundombinu, uendelezaji na uzalishaji wa nishati inayotokana na maji, kilimo na rasilimali maji,"amesema.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuelezea tathmini ya hali ya Hewa kwa mwaka 2019. Pichani chini Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi akiwa katika mkutano huo.


WAGONJWA WENGINE 14 WA COVID-19 WAONGEZA NCHINI NA KUFIKIA 46.

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMDA) YASHIKA NAFASI YA NNE KUREKODI KIASI CHA MVUA NYINGI KWA ZAIDI YA MIAKA 40

Na Karama Kenyunko globu ya jamii.

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mwaka 2019  umechukua nafasi ya nne na kuweka rekodi ya kuwa na kiasi cha mvua nyingi kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita tangia mwaka 1970

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akitoa uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya hali ya hewa wakati wa kikao cha Bodi ya TMA kilichofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TMA Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

 Akizindua ripoti hiyo, Dkt. Kijazi amesema mwaka 2019 umechukua nafasi ya nne kwa kurekodi kiasi cha mvua nyingi tangu mwaka 1970 kiwango ambacho ni kikubwa sana kutokea.

 Amesema, kiwango cha mvua kwa mwaka 2019 kilikuwa na wastani wa milimita 1283.5 sawa na asilimia 125 ya wastani wa mvua ya muda mrefu, 1981-2010, na kuongeza kuwa  kiwango hicho ni cha  zaidi ya wastani wa mvua ya muda mrefu kwa milimita 256.5.

Amesema kuwa,  Katika historia, mvua ya mwaka 2019 imechukua nafasi ya nne kwa wingi kati ya miaka iliyopata mvua nyingi zaidi tangu mwaka 1970 ambapo miaka iliyokua na mvua nyingi zaidi tangu mwaka huo ni 1982, 1997 na 2006.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza joto la nchi limeendelea kuongezeka kwa kiwango cha juu kuanzia mwaka 1995, ambapo joto la usiku limeongezeka zaidi ilikilinganishwa na joto la mchana ambapo kwa wastani joto kubwa kupita viwango vya kawaida (35 °C) limekuwa
likiripotiwa katika miezi ya Januari, Februari na Machi hasa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa nchi ambayo ni pwani ya kaskazini na maeneo ya
nyanda za juu kaskazini mashariki huku Joto la chini kupita kawaida (5 °C) limekuwa likiripotiwa zaidi katika maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi hasa miezi ya Juni, Julai

Pamoja na hayo taarifa za ripoti zitolewazo zimekuwa zikitumika pia kuchangia ripoti za namna hii zinazoandaliwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Aidha, Dkt.Kijazi amewashauri wadau wa sekta wa mbali kutumia taarifa zilizopo kwenye ripoti hiyo kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya nchi katika kukuza nchi na jamii kwa jumla katika tabza kilimo, ujenzi Maendeleo ya viwanda na nyingine.

Mapema kabla ya kuwasililishwa kwa ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema ripoti hizo zimekuwa zikitolewa tokea mwaka 2011 hadi 2019 ambapo lengo kubwa ni kukuza ufahamu na uelewa kwa jamii, wadau na watoa maamuzi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.

“Tathmini za ripoti hizi huonesha taarifa za kina za uchambuzi wa hali ya hewa na madhara yake na kuziweka katika mtazamo wa kihistoria”. Alisema Dkt. Chang’a.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Buruhani Nyenzi aliipongeza Menejimenti ya TMA kwa kutoa taarifa hiyo kwani ilielezwa kwamba ni nchi mbili tu Afrika ambazo zinatoa taarifa hizo ikiwemo Tanzania na Ivory Coast.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuelezea tathmini ya hali ya Hewa kwa mwaka 2019. Pichani chini Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi akiwa katika mkutano huo.

UGONJWA WA CORONA (COVID-19) WASITISHA MIKUTANO YA WAANDISHI WA HABARI IKIWEMO SHUGHULI NYINGINE ZITAKAZOWAFANYA WAKUSANYIKE

Kampuni ya FAMM (AMTL) yawakumbuka watoto yatima sikukuu ya Pasaka

Kampuni ya FAMM (AMTL) ya jijini Dar es salaam, mapema wiki hii ilitembelea Kituo cha Kulelea Watoto wenye uhitaji cha Huruma kilichopo Goba, Jijini Dar rs Salaam na kuwapatia zawadi mbalimbali za Sikukuu ya Pasaka ili na wao waweze kusherekea Sikukuu hiyo, ambapo walikabidhi mahitaji mbalimbali kama mchele, mafuta, sabuni maji n.k.

Aidha, Kampuni ya FAMM (AMTL) ilipeleka vifaa mbalimbali vya kujikinga na Virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na Sanitizer na Sabuni na mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kujikinga na kujiweka salama na Virusi vya Corona yalitolewa kwa watoto hao.

Kwa kutambua kuwa Dunia ipo kwenye janga la Virusi vya Corona, tahadhari mbalimbali zilichukuliwa ili kuhakikiasha kila aliyeshiriki anakuwa salama ikiwa ni pamoja na Watoto wa Kituo cha  Huruma.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
FAMM (AMTL) ni Kampuni inayojihusisha na Uchimbaji wa Madini, Usafirishaji na Kilimo cha Biashara. Vilevile, kwa kushirikiana na Emmanuel Shija (President of World Boxing Council Muay Thai Tanzania and World Muaythai Federation Tanzania) ipo tayari kukuletea Elimu ya Michezo na kuwa Imara kuimarisha afya kwenye jamii


POLISI ECUADOR YAKUSANYA MIILI 800 MAJUMBANI

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

ECUADOR imesema kuwa polisi wameondoa karibu miili 800 katika wiki za hivi karibuni kutoka  majumbani huko Guayaquil ambako ni kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona (Covid -19) na hiyo ni baada ya ugonjwa huo kuzidi huduma za dharura, hospitali na huduma za mazishi, Shirika la utangazaji la Al-jazeera limeripoti.

Kiongozi wa timu iliyoundwa na serikali ya nchi ili kusaidia katika mapambano dhidi ya Covid -19  yenye polisi na wanajeshi, Jorge Wated amesema kuwa miili iliyokusanywa kutoka majumbani imezidi mia saba.

Mapema jumapili Wated kupitia ukurasa wake wa Twitter alichapisha taarifa iliyoeleza kuwa katika operesheni hiyo kwa wiki tatu zilizopita miili 771 ilikusanywa kutoka majumbani na miili 631 kutoka hospitali ambapo mochwari zilikuwa zimejaa.

Wated hakueleza kwa kina sababu zilizopelekea vifo hivyo na takribani miili 600 ilizikwa chini ya mamlaka nchini humo.

Ecuador imeripoti visa 7,500 vya Covid -19 tangu kiripotiwe kisa cha kwanza mapema Februari 29 huku ukanda wa Pwani wa Guayas ukiwa na maambukizi kwa asilimia 70 na visa 4,000 na hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali.

Majeshi na polisi walianza kuondoa miili kutoka majumbani wiki tatu zilizopita baada ya mifumo ya mochwari huko Guayaquil kupata hitilafu.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na video zikionesha miili iliyopo barabarani pamoja na jumbe za kuomba msaada wa kuzikwa kwa ndugu zao na serikali ikachukua jukumu hilo.

Mapema Aprili Wated alieleza kuwa vifo vitikanavyo na Covid -19 kwa mwezi huu vinategemewa kufikia 2,500 hadi 3,500 katika eneo la Guayas. 

#Covid19 #CoronaVirus

IYANNA FLOYD KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA HADI MIAKA 99 JELA

Na Irene Mwidima,Michuzi TV.

 Iyanna Floyd ambae ni binti wa Floyd Mayweather huwenda akahukumiwa kifungo cha hadi miaka 99 jela kwa kosa la kumchoma mtu kisu mara mbili binti ambae ni mzazi mwenzake na NBA Youngboy. Iyanna Floyd ambae ana miaka 20 aliwasili nyumbani kwa mpenzi wake, rapper NBA Youngboy ambapo alimkuta na mzazi mwenzake aitwae Lapattra Lashai Jacobs. 

Iyanna alianza kumwambia Lapattra aondoke hapo nyumbani kwani NBA Youngboy ni mchumba wake. Tukio hilo lilitokea jumamosi ya wiki iliyopita April 4 ambapo mkasa ulianza baada ya iyanna kuwasili nyumbani kwa mpenzi wake. 

Baada ya kuzozana sana walifikishana hadi jikoni ambapo iyanna alichukua visu viwiwli, na pale ambapo Lapattra alipozidisha hatua tu, Iyanna alimchoma kisu kimoja na kasha kumchoma tena nba kisu cha pili. Akiwaambia polisi, Lapattra alidai hakusikia kisu cha kwanza kilivyoingia na ndipo Iyanna alimshindilia tenaImage may be NSFW.
Clik here to view.

 

TAAnet YAISHAURI SERIKALI BAR NA VILABU VYA POMBE KUFUNGWA WAKATI HUU WA MAPAMBANO NA MARADHI YA COVID-19

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mtandao wa Wadau wanaopambana na unywaji pombe kupita kiasi–TAAnet wameishauri serikali kutoa tamko la kufunga bar na klabu zote za pombe ili kudhibiti unywaji wa pombe na kuleta madhara makubwa kwa
binadamu ikiwemo kushusha kinga za mwili.

Hayo yamesemwa na mtandao huo wa TAAnet wakiungana kwa pamoja na serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya korona na kutambuliwa kama covid-19.

Katibu wa TAAnet Gladness Munuo amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa umma juu ya madhara ya unywaji pombe kupita kiasi ambapo Jamii imekuwa ikisumbuka na magonjwa mbalimbali yanayoletwa na matumizi ya pombe kupita kiasi kama vile maradhi ya moyo, ini, saratani n.k.


Amesema,hali kadhalika katika mapambano dhidi ya janga la gonjwa la covid-19 hawana budi kuweka mkazo kwa kuiomba serikali ya
Tanzania kuangalia upya utengenezaji, usambazaji na unywaji wa pombe nchini kwa wananchi wake ikiwa ni moja wapo ya kujikinga na maambukizi ya ungonjwa wa homa ya mapafu (covid-19).

"Taarifa pamoja na tafiti mbali mbali zimeshaeleza kuwa, mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini awe kijana au mzee ni rahisi kupatwa na virusi vya korona vinavyoleta ungonjwa wa covid-19 kwa maana ya kupata homa kali ya mafua, kwa kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi moja wapo ya madhara makubwa kwa binadamu ni kushusha kinga za mwili ambapo athari yeyote ya magonjwa ikiwepo huu wa covid-19 huweza kumpata mtu wa aina hiyo na kuleta maafa makubwa," amesema.

Munuo amesema, TAAnet ikiwa ni muungano wa mashirika zaidi ya 20 yanayopinga matumizi mabaya ya pombe nchini, kwa pamoja wanaiomba Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto kutambua na kubainisha
aina za pombe ambazo katika kipindi hiki cha maradhi yanayoambukizwa na virusi vya korona kusitishwa kabisa kutengezwa na kusambazwa nchini ikiwa ni hatua ya kuunga mkono serikali yetu katika kukabiliana na gonjwa la covid-19.

"Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopambana na kudhibiti unywaji pombe  kupita kiasi nchini Tanzania, kwa ujumla tuna sababu ya kuhakikisha Wa Tanzania wote mijini na vjijini, Wazee kwa vijana wanakuwa salama ki Afya, Kiuchumi na hata katika maendeleo yao kimazingira n.k. Hivyo basi, tunatoa RAI kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa katika kipindi hiki cha mapambano na ugonjwa wa covid-19 vilabu vya pombe, bar na ‘pub’ zinazojihusisha na biashara za pombe nchini kufungwa au kuwekewa utaratibu mpya mara moja.
Katika kuhakikisha kuwa wa Tanzania wanakuwa salama,"

Aidha, ametolea mfano kwa baadhi ya nchi za Afrika zilizozuia uuzwaji wa Pombe katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya kukabiliana na gonjwa la Covid -19.

"Zipo baadhi ya nchi zimechukua hatua kuhakikisha kuwa matumizi ya pombe zote yanadhibitiwa, nchi kama Zimbabwe, South Africa, Zambia na nchi nyingine kama Uganda zimepiga marufuku uendeshaji wa vilabu vya pombe na Kenya wako katika harakati za kupinga usambazaji
wa bidhaa ya pombe.,"

Katika hali kama hii Tanzania haiko katika kisiwa, na kutokana na mipaka kuwa wazi inasemekana kuwa baadhi ya walevi huvuka mipaka kuja Tanzania kunywa pombe. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO- Septemba,2018), Watu zaidi ya milioni 3 hufariki duniani kote kutokana na matumizi mabaya ya pombe. Zaidi ya robo tatu (3/4) ya vifo hivi vilikuwa ni vya wanaume. Kwa ujumla, matumizi mabaya ya pombe husababisha zaidi ya asilimia 5 ya mzigo wa magonjwa duniani. Taarifa kama hii pia inapatikana katika Taarifa ya hali ya Dunia kuhusu unywaji pombe na afya 2018(Global status report on alcohol and health 2018).

Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini Tanzania, na linapaswakudhibitiwa kwa haraka iwezekanavyo hasa katika wakati huu Taifa letu na mataifa mengine duniani yako katika mapambano na ugonjwa unaoletwa na virusi vya korona.

Aidha, tafiti zimeonyesha kuwa wanaotumia pombe za kienyeji ambao kwa takwimu Tanzania Jamii ni wengi, wao huathirika zaidi kwa ajili ya mazingira ya utengenezaji na hata unywaji. Kutokana na athari za covid-19 TAAnet inazikumbusha taasisi husikapamoja na Serikali kuangalia kwa haraka namna ya kudhibiti UTENGENEZAJI, USAMBAZAJI NA UNYWAJI WA POMBE katika kipindi hiki cha mapambano na covid-19ili kunusuru maisha ya vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa pamoja na wazee
yanayoendelea kuharibika kila siku.



POLISI AKATWA MKONO AKIWA DORIA YA KUDHIBITI CORONA INDIA


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

POLISI mmoja nchini India amekatwa mkono kwa upanga na maafisa wengine sita kujeruhiwa vibaya mara baada ya kushambuliwa wakati wa kutekeleza zuio la watu kutoka nje (Lockdown) ikiwa ni sehemu ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona (Covid -19) huko Punjab kaskazini mapema leo asubuhi, Shirika la kimataifa la utangazaji la CNN limeripoti.

Imeelezwa kuwa sehemu ya mkono (kiwiko) wa kushoto wa Harjit Singh, mkurugenzi msaidizi wa Polisi wa Punjab ulijeruhiwa vibaya na baadaye ilirudishiwa kwa kufanyiwa upasuaji uliodumu takribani masaa nane.

Shambulio hilo lilitokea wakati gari lililokuwa limebeba watu saba  waliosadikika kuwa ni wanakikundi cha wapiganaji wachache wa Sikh kinachojulikana kama Nihangs waliosimama katika uwanja wa biashara nje ya soko la mboga wilayani Patiala na polisi walipowauliza wanaume hao hati halali za kusafiri, mmoja wao akatoa upanga kumkata mkono Singh.

Aidha maafisa wa polisi wameonesha silaha zenye ncha kali zilizopatikana huko Patiala, India, Aprili 12.

Maafisa wengine waliojeruhiwa, mmoja akiwa na majeraha ya upanga mgongoni walipelekwa katika Taasisi ya Uzamili ya Mafunzo ya Utabibu na Utafiti huko Chandigarh.

Kiongozi wa Serikali nchini humo  Amarinder Singh kupitia ukurasa wake wa Twitter amechapisha taarifa inavyoeleza namna upasuaji wa kurudisha sehemu ya mkono (kiwiko) ulivyochukua  takribani masaa manane na amewashukuru  madaktari na wafanyakazi kwa msaada na kumtakia Harjeet Singh ahueni ya haraka.

Aidha  imeelezwa kuwa hatua kali  zitachukuliwa kwa yeyote ambaye atakiuka taratibu na muda uliopangwa.

Kufuatia operesheni ya saa moja katika gurdwara ya eneo hilo (hekalu la Sikh) polisi waliwakamata watu hao saba waliotuhumiwa na  uchunguzi zaidi unaendelea.

 Kwa mara ya kwanza  India imefunga reli zake katika miaka 167 na sasa treni zimegeuzwa kuwa hospitali.

India kwa sasa iko chini ya kizuizi cha kitaifa hadi Aprili 30 huku Punjab likiwa jimbo lililoripoti jumla ya kesi 151 zilizothibitishwa za virusi vya  Corona, wagonjwa waliopona 5 pamoja na vifo 11.
Image may be NSFW.
Clik here to view.

COVID-19 a threat to SADC regional economy

By Kumbirai Nhongo


The economy of the Southern African Development Community is at risk as the number of COVID-19 cases continue to increase.

Figures from the Africa Centres for Disease Control and Prevention show that as of 10 April, the SADC region had 2,831 confirmed cases of COVID-19, accounting for 22 percent of the 12,973 cases registered on the continent as of the same day.

Within the first 10 days of April, fatalities attributed to the virus in the region more than doubled from 24 to 65.

Described as the most serious health emergency in generations, the World Health Organisation (WHO) confirms that COVID-19 has had adverse effects on economies and livelihoods.

“The restrictions many countries have put in place to protect health are taking a heavy toll on the income of individuals and families, and the economies of communities and nations,” said Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, Director General of the WHO.

“We are in a shared struggle to protect both lives and livelihoods,” he added.

In the SADC region unprecedented measures such as nationwide lockdowns have been put in place by some Member States to restrict the movement of people and contain the spread of the virus.

Malawi has become the latest Member State to announce such restrictive measures, which take effect from 10 to 23 April.

In South Africa and Botswana, lockdown periods have been extended until the end of April as Member States intensify efforts to combat the spread of the disease.

The SADC Business Council, a regional association of private sector organisations, notes that such measures, though necessary, have had unintended consequences on the regional economy, particularly on intra-regional trade.

In a statement released after its online meeting on 1 April, the SADC Business Council noted the challenges businesses are facing in moving imports and exports, given the travel restrictions obtaining in some jurisdictions.

“Landlocked countries are failing to access ports, with truck drivers failing to pick and drop cargo because they do not have visas to travel to countries with port infrastructure,” read the statement.

Following the Council of Ministers meeting held in March, SADC has since issued guidelines to manage the inter-state movement of goods, services and people during this period.

However, indications are that not all Member States have adopted these guidelines, resulting in bottlenecks in the regional supply chain.

The SADC Business Council notes that delays in the movement of cargo have led to increases in both storage and transport costs.

Apart from the challenges of intra-regional trade, SADC Member States face external risks associated with the slowdown of the economies of trading partners in the rest of Africa, Europe, Asia and the Americas due to the negative effects of COVID-19 in those regions.

Information from the SADC Directorate of Industrial Development and Trade shows that the region is more exposed to exogenous shocks given its reliance on the production and export of unprocessed commodities.

Angola, the main petroleum producer in SADC, has had to revise its national budget figures downwards due to the sharp decline in oil prices; COVID-19 contributing to reduced global demand.

In fact, Brent crude oil prices declined by 66 percent in the first quarter of this year – its biggest ever quarterly loss.

“Oil has fallen drastically and everyone knows the weight of oil in terms of financing the state budget,” noted Vera Daves, the Angolan Minister of Finance.

Other commodities have not been spared, with diamonds, copper, nickel, cobalt, coal and platinum trading at reduced prices.

In countries where lockdowns have been effected, some agricultural markets have had to be closed, a situation that has affected farmers and impacted the livelihoods of those in downstream industries.

The SADC Secretariat notes that about 70 percent of the population within the region depends on agriculture for food, income and employment.

The tourism sector, which accounts for about eight percent of the gross domestic product of the SADC region, has been among the worst affected following a slow-down in global travel.

Prime regional destinations in the Seychelles, Mauritius, Zimbabwe, Namibia, Botswana and South Africa are currently inaccessible due to lockdowns in the respective Member States.

The World Tourism Organisation (WTO) estimates that at the global level tourist arrivals will be down by between 20 and 30 percent in 2020 when compared with 2019, on account of COVID-19.

WTO Secretary-General Zurab Pololikashvili says such a decline translates to a reversal of the growth built over the past five to seven years.

South Africa, the largest and most diverse economy in the region, is already in recession, with indications that it will contract further than the 0.2 percent decline projected by the central bank for this year.

The country has the highest number of coronavirus cases in the region, accounting for 71 percent of the total.

To manage the impact of COVID-19 on their respective economies, a number of Member States have announced policy measures in mitigation.

These include tax concessions, temporary waivers on loan repayments, reduced interest rates, and social security measures for vulnerable communities.

In the Democratic Republic of Congo for example, the Central Bank of Congo announced a rate cut from 9 to 7.5 percent to reduce the cost of borrowing.

Similarly in Eswatini the government has reduced the price of fuel and suspended the increase of electricity tariffs for two months, among other measures aimed at cushioning businesses and consumers.

As of 10 April, Lesotho and the Comoros were the two remaining SADC Member States without any reported COVID-19 cases.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 13.04.2020

MTANZANIA ATOA USHUHUDA HALI ILIVYO NCHINI ITALIA BAADA YA MLIPUKO WA VIRUSI VYA COVID-19 ‘WAPO LOCKDOWN’

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Hali ya Maambukizi ya Virusi vya COVID-19 imetajwa kuwa si shwari nchini Italia kwa Wananchi wengi nchini humo kujifungia ndani (Lockdown) kutokana na kasi ya maambukizi ya virusi hivyo vilivyosambaa sehemu nyingi duniani kwa sasa.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Parma (Parma Unniversity) kilichopo nchini Italia, Mtanzania Frank Charles amezungumza na Michuzi Blog, Michuzi TV ameeleza hali si shwari nchini humo kutokana na Wananchi wengi kujifungia ndani muda wote kuogopa Maambukizi ya Virusi hivyo.

Frank ameeleza kipindi cha Sikukuu za Pasaka, Wananchi hao wengi wamesheherekea sikukuu hiyo wakiwa majumbani wakihofia maambukizi. Amesema kuna udhibiti mkubwa wa Askari wa nchi hiyo kusambaa sehemu mbalimbali kuzuia mikusanyiko ya watu.

“Hata kama kuna Mgonjwa nyumbani kwako kuna namba zimewekwa ili upige na wahudumu wa masuala ya afya waje kufanya matibabu, Wagonjwa kwenye vituo vya afya ni wengi kuliko Madaktari na Vifaa Tiba, ndio maana wameweka namna ya kufanya matibabu nyumbani,” amesema Frank.

Amesema Wanafunzi wa Tanzania wapo katika hali shwari, isipokuwa changamoto ni kufungwa maduka mengi, hivyo kufanya foleni katika sehemu za Maduka ya Vyakula na Dawa za Matibabu ya kawaida. Ameeleza Serikali ya nchi hiyo imejitahidi kuwafadhili baadhi ya Wanafunzi kujikimu Kiuchumi katika kipindi hiki.

“Chuo chetu cha Parma kimeweka namna ya kusoma kupitia Mitandao ‘Online’ ili kuzuia kutoka nje, kiukweli kuna baadhi ya vitu vinakuwa vigumu kusoma kupitia mtandao, kutokana na kufanya kitu Mtandaoni sio sawa na kama upo Chuoni, lakini hakuna jinsi tunasoma hivyo hivyo,” ameeleza Frank.

Kwa upande mwingine, Frank ameeleza kuwa tayari wameonana na Ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo Mjini Rome, mwanzoni tu baada ya virusi hivyo kusambaa, “Tayari tumeujulisha Ubalozi wetu wa Tanzania kuwa sisi tupo Chuo Kikuu cha Parma, wanajua kuna Watanzania huku”, amesema

Frank amewaasa Watanzania kuzingatia maagizo yanayotolewa na Mamlaka husika ili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi hivyo vya COVID-19 vinavyoisumbua Dunia na kuchukua tahadhari mapema, amesema endapo kama watafuata maagizo hayo itasaidia sana kupunguza Maambukizi hayo yanasumbua dunia kwa sasa.
 Baadhi ya Miji iliyopo nchini Italia, muonekano katika Kipindi hiki cha Mlipuko wa Maambukizi ya Virusi vya COVID-19.




WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA KUTOKA TAASISI YA MILELE ZANZIBAR FOUNDATION

Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 13/04/2020.

NAIBU Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amewataka wananchi na Taasisi za kiraia kushirikiane na Serikali katika mapambano dhidi ya maradhi ya Corona.

Amesema mashirikiano ya pamoja kati ya wananchi na viongozi na kufuata maekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya yatasaidia kushinda vita dhidi ya maradhi hayo.  

Naibu Waziri wa Afya alitoa kauli hiyo baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na maradhi ya Corona kutoka Taasisi ya Milele Foundation Zanzibar kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano hayo.

"Wananchi tukijidhatiti kushirikiana na Serikali kupiga vita janga hili la Corona kama tulivyoshirikiana wakati wa maradhi ya kipindupindu na tukashinda," alisisitiza Naibu Waziri wa Afya.

Harusi Said Suleiman alitoa shukrani kwa Jumuiya ya Milele Foundation Zanzibar kwa kuunga mkono Serikali kupitia Wizara ya Afya na amesema vifaa hivyo  vitasambazwa katika sehemu zenye mahitaji ikiwemo vituo vya afya mijini na vijijini.

Amezitaka Jumuiya na Taasisi nyengine zikiwemo za kiraia kuiga mfano ulioonyeshwa na Milele Foundation katika kuhakikisha janga la Corona linaondoka nchini.

Mkuu wa Miradi wa Milele Foundation Zanzibar Khadija Mohamed Sharif amesema msaada wa vifàa vya kujikinga na maambukizi ya Corona ni hatua ya awali na wataendelea kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu na Jumuiya ya gari za Daladala kutoa elimu kwa madereva na abiria juu ya maradhi hayo.

Ameitaka jamii kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima pamoja na kukosha mikono kwa maji ya kutitirika mara kwa mara.

Nae Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Shirika la Msalaba Mwekundu Mwatima Kombo Said, amesema wataendelea kutoa elimu  kwa jamii kwa njia mbali mbali pamoja na kugawa vipeperushi  vyenye muongozo wa kujiepusha na maambukizi ya maradhi ya corona mjini na vijijini.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya gari za Daladala Zanzibar Said Abdalla Suleiman amewataka abiria kabla ya kuingia ndani ya gari kuhakikisha kuna nafasi ya kukaa kwani ipo sheria ya abiria anaezidi ndani ya gari kupelekwa mahakamani kama wanavyopelekwa madereva na makonda .

“Abiria usipande gari kama hakuna nafasi ya kukaa, sheria za kupelekwa mahakamani kwa abiria aliekosa nafasi ya kukaa zipo na ingefaa zitumike hasa kipindi hichi cha mapambano dhidi ya Corona,“alishauri Mwenyekiti huyo .

Vifaa vilivyotolewa na Milele Foundation Zanzibar ni pamoja na vifaa vya kupima joto la mwili, ndoo, sabuni za kukoshea mikono, tishu, glavzi, Sanitizer na mafuta ya gari lita 1,500 kwa ajili ya kufuatilia wagonjwa wa Corona vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 32.
 :Mwenyekiti wa Jumuiya ya Daladala Zanzibar Saidi Abdalla Sleiman akizungumzia  kuhusu uingiaji wa abiria kwenye gari  katika kujiikinga  na maradhi ya Corona huko Wizara ya afya  Zanzibar.
 Mjumbe wa Halmashauri kuu wa shirika la Msalaba Mwekundu Zanzibar Mwatima Kombo Said akieleza mikakati yao ya kutoa elimu kuhusiana na mapambano dhidi ya  Corona huko Wizara ya afya Mnazi mmoja Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said Suleman akipokea msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Corona kutoka Taasisi ya Milele  Foundation Zanzibar hafla iliyofanyika katika Wizara ya Afya Mnazi mmoja  Zanzibar.PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO
Mkuu wa Miradi wa Taasisi ya  Zanzibar  Milele Foundation Khadija Mohammed Bakar akitoa maelekezo  juu ya matumizi ya chanja maalum ya kunawa mikono wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na Corona katika Wizara ya Afya Zanzibar .
Viewing all 118561 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>