Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 118669 articles
Browse latest View live

SIMBACHAWENE AWAAPISHA WATUMISHI WANNE, AONGOZA KIKAO CHA TUME JIJINI DODOMA

$
0
0


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi,Uhamiaji na Magereza,George Simbachawene akimuapisha Mrakibu Ali Juma Abdulkadir(kushoto) kuwa mtumishi wa tume hiyo kabla ya kuanza kwa kikao cha tume hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa wizara hiyo,Mtumba jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi,Uhamiaji na Magereza,George Simbachawene akimuapisha Naibu Kamishna Anthon Rutashubulugukwa(kushoto) kuwa mtumishi wa tume hiyo kabla ya kuanza kwa kikao cha tume hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa wizara hiyo,Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi,Uhamiaji na Magereza,George Simbachawene akimuapisha Mrakibu Msaidizi,Nicodemus Tenga(kushoto)kuwa mtumishi wa tume hiyo kabla ya kuanza kwa kikao cha tume hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa wizara hiyo,Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi,Uhamiaji na Magereza,George Simbachawene akimuapisha Afisa Utawala Mkuu,Erick Mbembati (kushoto), kuwa mtumishi wa tume hiyo kabla ya kuanza kwa kikao cha tume hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa wizara hiyo,Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Magereza, George Simbachawene (katikati), Naibu Waziri wa wizara hiyo ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Christopher Kadio(kushoto), wakiongoza kikao cha tume hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IGP SIRRO TUMEIMARISHA HALI YA USALAMA KUFUATIA VURUGU ZINAZOENDELEA NCHINI MSUMBIJI

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini vimejipanga vyema kuhakikisha vinadhibiti vitendo vya uhalifu hasa kutokana na vitendo vya vurugu vinavyoendelea katika nchi jirani ya Msumbiji.  

Aidha, IGP Sirro, amewataka Watanzaania hususan vijana kuacha kutumiwa na watu wachache  wanaowataka wajiingize kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kufanya uhalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi, nakuwataka wananchi hao wajikite katika shughuli halali za kujiletea maendeleo

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yatoa Zawadi kwa watoto

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mtoto mwenye matatizo ya moyo aliyelazwa katika Taasisi hiyo Elizabeth Omari zawadi ya Pasaka wakati wa ugawaji wa zawadi hizo kwa watoto leo Jijini Dar es Salaam


Maafisa Uuguzi wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya huduma ya Uuguzi Robert Mallya kumkabidhi zawadi ya pasaka mama wa mtoto Wilson Willium wakati wa ugawaji wa zawadi hizo kwa watoto leo Jijini Dar es Salaam

 Maafisa Uuguzi wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya huduma ya Uuguzi Robert Mallya kumkabidhi zawadi ya pasaka mama wa mtoto Silvanus Brayton  wakati wa ugawaji wa zawadi hizo kwa watoto leo Jijini Dar es Salaam
Maafisa Uuguzi wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Teresia Marombe na Rehema Bakari wakimkabidhi mtoto mwenye matatizo ya moyo aliyelazwa katika Taasisi hiyo Ikram Samari zawadi ya pasaka wakati wa ugawaji wa zawadi hizo kwa watoto leo Jijini Dar es Salaam
Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

WATUMISHI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAPATA ELIMU YA CORONA

$
0
0
 Bw. Yusuph Seif Afisa Afya kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto akitoa elimu juu ya ugonjwa wa Corona kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais hii leo Mtumba Dodoma. Katika picha ni baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo.

Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Bw. Yusuph Seif Afisa Afya kutoka Wizara Afya (hayupo pichani) wakati wa utoaji wa elimu juu ya ugonjwa corona. Elimu hii imetolewa nje ya jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba – Dodoma huku watumishi wakizingatia maelekezo ya wataalumu wa afya ya kupeana nafasi.

TUMEANZA KUPATA MAAMBUKIZI YA NDANI YA VIRUSI VYA CORONA - UMMY

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Tanzania imeanza kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ya ndani kuanzia maambukizi yaliyopatikana tarehe 08/04/2020.
Amesema kuwa tahadhari kubwa inahitajika katika kuhakikisha kuzuia kuendelea kwa maambukizi ya kijamii itasababisha kuongezekana kwa kasi ya maambukizi katika jamii.
Ameyazungumza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini katika kujadiliana namna ya kukabiliana na maambukizi ya virusi ya Corona nchini.
Ameongeza kuwa Serikali itatangaza hivi karibuni wananchi kuchukua tahadhari kwani tafiti zinaonesha virusi vya Corona vinaweza kusambaa na kuambukizwa kwa njia ya hewa hivyo maelekezo ya kutumia barakoa yatatolewa ili kuondokana na maambukizi.
“Tafiti zimeonesha kuna uwezekano wa Virusi vya Corona vinaweza kuenezwa kwa njia ya hewa hivyo tutaleta muongozo wa kuanza kutumia Barakoa (Mask) kwa jamii ili kuziua maambukizi kuenena kwa njia ya hewa” alisema
Aidha amewataka viongozi wa dini kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwalinda watoto kutowaruhusu Watoto kuzurula na kuhangaika ovyo mitaani ili kupunguza uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
“Imani ya watanzania wengi kufikiri kuwa hatuwezi kupata maambukizi ni suala sahihi tunaweza kupata maambukizi kama watu wengine wanavyopata” alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa viongozi ni watu muhimu katika kuleta mabadiliko katika Jamii yetu kwani wanasikilizwa zaidi na waumini katika sehemu za ibada.
Ameongeza kuwa lengo ni kuwashirisha viongozi wa kidini katika kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Corona yanatokomea nchini.
"Viongozi wa kidini ni watu muhimu sana katika mapambano katika kuondokana na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini tunaomba mtusaidie katika hili" alisema
Naye Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Gilbert Kamanga amewaomba vingozi wa dini kutofanya suala la virusi vya Corona kuwa la kisiasa bali waunganishe nguvu pamoja ili kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kupewa elimu kila mahali ikiwemo katika nyumba za ibada ambapo watu wengi ukusanyika pamoja kuabudu itakuwa sehemu sahihi kufikisha ujumbe kuhusu kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
"Viongozi wetu wa dini nawaomba tushikamane katika hili kwani virusi vya Corona ni hatari sana lakini tukisimama pamoja hakika tutafanikiwa katika kutokomeza virusi vya Corona" alisema
Akitoa salam za mkoa wa Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rashid Mfaume amesema mkoa umejidhatiti katika kupambana kwa kuenea na maambukizi ya Virusi vya Corona mkoani humo kwa kuzingatia maelekezo yanayotokea na wataalam wa Afya  na Serikali kwa ujumla.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Musa Salum amesema janga la Corona ni kubwa na kama watu wa imani tunaamini katika kumuonba Mwenyezi Mungu na tunaamini litatokomea.
Pia amemshukuru Rais John Magufuli kuendelea kuruhusu ibada kuendelea katika kama kawaida ni jambo ambalo litasaidia kuzidisha maombi katika kupambana na Virusi vya Corona.
Mkutano huu kati ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini umekuja wakati Tanzania ikiendelea kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona huku ikiwa na jumla ya watu 25 waliombukizwa virusi hivyo.
 aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa dini kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini katika Mkutano uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea jinsi Wizara inavyoshirikiana na wadau katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona katika Mkutano kati ya Wizara(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na viongozi wa Dini jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Gilbert Kamanga akielezea jinsi Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali katika mapambano dhidi maambukizi ya Virusi vya Corona katika Mkutano kati ya Wizara(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na viongozi wa Dini jijini Dar Es Salaam.
 Baadhi ya viongozi wa kidini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika Mkutano kati yao na Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

BrighterMonday Tanzania yazindua kampeni ya ‘Umoja Wakati wa Shida’ kusaidia Waajiri Kukabiliana na Athari za Janga la Corona

$
0
0
Kampuni ya uajiri na usimamizi wa rasilimali watu ya BrighterMonday Tanzania imeanzisha programu iitwayo ‘Umoja Wakati wa Shida’ inayotoa nafasi kwa waajiri (makampuni na watu binafsi) kutangaza kazi kwenye tovuti yao bure kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo, wakati ambao taifa linakabiliana na janga la maradhi ya virusi vya Corona.

Kampeni hii inalenga kuwezesha uendelevu wa juhudi za makampuni na biashara kwa kuziwesesha kufanya udahili na kuajiri watendaji sahihi ili kuongeza ufanisi wakati na baada ya nyakati hizi za changamoto.

‘’Kwa miezi mitatu ijayo, tutatoa fursa kwa taasisi zinazotaka kuajiri wataalamu katika sekta mbalimbali kote nchini kutangaza bure nafasi za ajira katika tovuti yetu. Hii itawawezesha hospitali, vituo vya afya na watoa huduma nyingine muhimu walio mstari wa mbele katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona (COVID-19) kuajiri wataalamu wenye vigezo kamilifu katika kipindi cha muda mfupi’’, anasema Mkurugenzi Mkuu wa BrighterMonday Tanzania, Bi. Reshma Bharmal-Shariff.

Chini ya programu hii, waajiri wataweza kuchakata kwa haraka mchakato wa uajiri kwa kutumia mbinu za kisasa zilizobuniwa na BrighterMonday Tanzania kama vile Zana ya Kupima Ufanisi wa Waajiriwa ambayo inapima ubora wa mwajiriwa na ujuzi unaohitajika kwa kazi anayoomba, zana hii hupima zaidi ya kile kilichopo kwenye wasifu (CV) ya mtahiniwa.

Vilevile, waajiri wataweza kuangalia alama za mtahiniwa pamoja kulinganisha na mahitaji ya kitaaluma na kiuzoefu kwa kutumia mfumo wa ufuatilaji wa maombi ya kazi ‘Application Tracking System’ (ATS) wa BrighterMonday Tanzania. Kupitia mfumo huu, mwajiri ataweza kulinganisha kwa urahisi ubora wa mtahiniwa, ujuzi na kiwango cha uzoefu.

‘Tupo kwa ajili yako jana, leo na hata kesho’- Timu ya BrighterMonday Tanzania inasema.

TANZANIA YATOA BIILIONI 10 KUIFUFUA UPYA TAZARA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akimsikiliza Meneja wa Karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Mbeya, Mhandisi Ezekiel Mong’ateko, wakati akimweleza hatua ya ukarabati iliyofikiwa katika karakana ya tazara mkoani Mbeya.
Muonekano wa moja ya Vichwa vya treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) vilivyokamilika baada ya kufungwa mashine ya kufua umeme (Tranction Motor), katika karakana ya Mamlaka hiyo Mkoni Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na wafanyakazi wa karakana ya maelekezo Karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mkoani Mbeya (hawapo pichani) wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa vichwa vya treni mkoani humo.
Muonekano wa vifaa vinavyofanyiwa ukarabati katika karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mkoani Mbeya.
Mafundi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mkoani Mbeya, wakiendelea na ukarabati wa vichwa vya treni katika karakana hiyo mkoani humo. TAZARA iko katika hatua za mwisho za kukamilisha ukarabati wa kichwa cha tat umara baada ya kufunga traction motor mpya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akinawa mikono kama njia ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona katika Karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Mbeya, Mhandisi Ezekiel Mong’ateko, mara baada ya kukagua vichwa viwili vya treni ya shirika hilo vilivyofungwa mashine ya kufua umeme (traction motor) mpya.

………………………………………………………………………………………………

Serikali ya Tanzania imetoa kiasi cha shilingi bilioni 10 ikiwa ni kuhakikisha inaifufua upya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuiongeza mtaji na kufikia lengo la kujiendesha kibiashara.

Akizungumza mkoani Mbeya mara baada ya kukagua vichwa viwili vilivyokamilika baada ya kufungwa mashine mpya za kufua umeme (traction motor) Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amesema kuwa kukamilika kwa ukarabati huo kutaongeza usafirishaji wa mzigo kwa mamlaka.

“Makusudi makubwa ya Serikali kuwekeza fedha hizi ni kuhakikisha mnafanya biashara na kurejesha mzigo wa tani milioni tano mnaotakiwa kuusafirisha kwa mwaka”, amesema Mhandisi Kamwelwe.

Kamwelwe amefafanua kuwa fedha hizo zilizotolewa zimeshanunua mashine mpya za kufua umeme takribani arubaini na mbili ambazo zitafungwa kwenye vichwa saba.

Meneja Karakana ya TAZARA mkoani humo, Mhandisi Ezekiel Mong’ateko, amesema mpaka sasa vichwa viwili vimeshakamilika na mwishoni mwa mwezi huu kichwa cha tatu kitakamilika ambapo kichwa kimoja kina uwezo wa kusafirisha tani laki mbili na nusu kwa mwaka.

“Kukamilika kwa vichwa hivi kutaongeza mzigo tunaotakiwa kuusafirisha kwa mwaka kwani kwa sasa mzigo tunasafirisha umepungua sana na hauzidi tani laki tatu, tunaishukuru sana Serikali kwa kuiwezesha mamlaka”, amesema Mhandisi Mong’ateko.

Mhandisi Mong’ateko ameongeza kuwa sambamba na ukarabati wa vichwa hivyo mkoani humo, Mamlaka inaendelea na ukarabati wa mabehewa katika karakana ya mamlaka jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha ukamilikaji wa vichwa hivyo unaendana na ongezeko la usafirishaji wa abiria na mizigo.

Kukamilika kwa ukarabati wa vichwa hivyo kutaongeza idadi ya vichwa kumi na tatu vilivyopo kwa sasa na kufikia vichwa 20 ambapo kila kichwa kina uwezo wa kubeba tani elfu thelathini.

Utoaji wa fedha hizo ni utekelezaji wa makubaliano ya nchi Mbili ya Tanzania na Zambia ambazo kwa pamoja zilikubaliana kutoa bilioni 20 ambapo kila nchi ilitakiwa kuchangia bilioni kumi ili kuifufua upya mamlaka hiyo na kuiwezesha kujitegemea mara baada ya kushuka kwa usafirishaji kutokana na upungufu wa vichwa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU WATOTO MINADA YA MIFUGO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara wa mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara ndogo ndogo wa matunda na nyanya kando ya mnada wa   mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora ya kunawa wa Mikono kabla ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu kitachotumika kuhudumia wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa huo Wilayani Kishapu jana alipofika katika kituo hicho  kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora ya kunawa wa Mikono kabla ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu kitachotumika kuhudumia wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa huo Wilayani Kishapu jana alipofika katika kituo hicho  kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara ndogo ndogo wa matunda na nyanya kando ya mnada wa   mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

…………………………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma- Sinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack amewataka wazazi na walezi mkoani Shinyanga kutowaruhusu watoto wadogo kwenda katika mikusanyiko hususani minada ya mazao na mifugo kama hatua muhimu ya kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati alipotembelea mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko katika Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwa lengo la kujionea utekelezaji wa agizo la serikali linalowataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na  ugonjwa wa corona ikiwemo kuweka maji na sabuni katika maeneo yanayokutanisha watu wengi pamoja na kukaa  umbali wa mita moja.
Bi. Tellack ameonya kuwa huu si wakati wazazi kutembea na watoto wao kutokana na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kuwataka kusubiri mpaka wakati ugonjwa huu utakapokuwa umedhibitiwa kwani uwezo wa watoto kujikinga ni mdogo sana.
Pamoja na agizo hilo la Mkuu wa Mkoa kwa wakazi na wafanyabiashara katika minada ya mifugo pia hakuridhishwa na hatua za zuinazochukuliwa na uongozi wa mnada huo za kuhakikisha wale wote wanaoingia mnadani hapo wanasafisha mikono yao baada ya kujionea mnada huo ukiwa na njia zaidi ya moja ya kuingia mnadani hapo na kutoa nafasi kwa baadhi ya watu kujipenyeza ndani ya eneo hilo bila kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona.
Bi. Tellack amewataka wafanyabiashara mnadani hapo kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo kwa kila mmoja kunawa mikono yake kila mara na kuhakikisha wanakuwa na vitakasa mikono (sanitizers) kwa vile wanao uwezo wa kuvinunua kama hatua muhimu ya kujikinga na hatari ya maambukizi hayo.
‘’Nunueni vitakasa mikono kwa ajili ya usalama wenu kwa sababu hamuwezi kukosa fedha ya kununua ya kiasi cha shilingo elfu nne na miatano na hata kama ni shilingi elfu kumi kwa ajili ya kujikinga na kuwakinga wengine.’’Aliendelea kusema kiongozi huyo wa Mkoa.
Agizo kama hili pia lilitolewa na Mkuu wa Mkoa kwa wafanyabiashara ndogo wanaofika eneo la mnada kwa lengo la kujipatia kipato tofauti na mifugo inayouzwa mnadani kuhakikisha wanakuwa na maji na sabuni vinginevyo watozwe faini kwa kushindwa kutekeleza agizo hilo muhimu la Serikali.
Pamoja na kutembelea mnada huo Bi. Tellack pia alitembelea Kituo cha Afya cha Wilaya ya Kishapu kilichoandaliwa kama sehemu maalumu ya kupeleka wagonjwa wa corona endapo watabainika Wilayani humo kama hatua muhimu ya kujionea ni namnagani Wilaya ya Kishapu imejipanga kukabiliana na ugonjwa huo.
Akiwa katika kituo hicho cha Afya Mkuu wa Mkoa amejionea vifaa vnitakovyotumiwa na waudumu wa Afya kujikinga na kuwahudumia wagonjwa na kuwataka wahudumu hao kuwa tayari kwa lengo la kukabiliana na kuhudumia wagonjwa hao kwa tahadhari kubwa.
Mnada huo unaowakutanisha wafanyabiashara wa mifugo kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Shinyanga na mikoa jilani ufanyika kila Siku ya Alhamisi na kuvuta wafanyabiashara wa aina nyingine nje na ndani ya mnada huo ambao pia wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuweka vitakasa mikono katika maeneo yao ya biashara.

ISAAC NEWTON; PROFESA ALIYETUMIA VYEMA MUDA WAKATI WA JANGA LA TAUNI KUGUNDUA NADHARIA ZA KISAYANSI

$
0
0

 Leandra Gabriel, Michuzi TV

MWAKA 1665 kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Tauni uliojulikana zaidi kama "Black Death" nchini Uingereza hali iliyopelekea shule, vyuo na huduma mbalimbali za kijamii kuzuiliwa kwa muda kwa lengo la kupunguza kasi ya maambukizi ya Tauni kama inavyofanyika sasa ambapo dunia inakabiliwa na mlipuko wa virusi vya Corona (Covid-19.)

Wakati huo Isaac Newton alikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cambridge na hakuwa Profesa na alilazimika  kurudi nyumbani kati ya mwaka 1665 na 1666 baada ya Cambridge kufungwa kutokana na janga hilo.

Newton alirejea Cambridge 1667 na nadharia zinazodumu hadi sasa hiyo ni baada ya kutumia vyema muda huo ambapo janga hilo lilitokea.

Wakati huo wa janga la  Tauni "Babonic Plague", Newton akiwa nyumbani alishuhudia tufaa likianguka toka mtini kwenye bustani ya familia huko Woolsthorpe (maili 50 kutoka Cambridge). Hapo alijiuliza maswali yaliyopelekea ugunduzi wa nadharia ya nguvu ya uvutano(Gravity).

Newton alifanya majaribio kadhaa ya mwanga ambayo pia yaliyopelekea kugundua nadharia ya Optiki.Vilevile Newton aliandaa njia na kanuni mpya katika fani ya hisabati na zikawa chimbuko la Calculus.

Janga hilo lilipelekea robo ya wakazi wa Uingereza kufariki kutokana na tauni iliyopiga kati ya miaka ya 1665 na 1666. 

Newton alirudi chuoni Cambridge mwaka 1667, akiwa na nadharia alizoziandaa akiwa nyumbani, ndani ya miezi 6 tu alifanywa kuwa mtafiti na miaka miwili alitunukiwa shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Cambridge.
Wakati huu ambao shule na vyuo vimefungwa ni vyema wanafunzi wakatumia kufanya kazi za ziada ambazo zitaleta matokeo chanya baada ya dunia kurejea katika hali yake ya kawaida.

PAPPY TSHISHIMBI RASMI SASA KUBAKI JANGWANI

$
0
0
Yassir Simba,Michuzi TV

Klabu ya Yanga imethibitisha kumalizana na kiungo wake mkabaji ambaye ni nahondha wa klabu hiyo raia wa Congo DRC Pappy Kabamba Tshishimbi ambaye mkataba wake ulikuwa unaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara.

Kiungo huyo ambaye siku za karibuni alikuwa akitajwa kuwaniwa na baadhi ya vilabu vya ligi kuu ikiwemo wekundu wa msimbazi Simba, rasmi sasa atasalia kwa wananchi hao wa jangwani mpaka 2022 kutokana na taarifa za awali kuwa ameingia kandarasi ya miaka 2 na mabingwa hao wa kihistoria.

Kupitia Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM Hersi Said amesisitiza kuwa, "Tshishimbi ni mali ya Yanga kwa sasa na haendi popote labda wanaomuhutaji wasubiri mpaka mkataba huu wa sasa utakapo malizika."
 

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA CHINA

$
0
0





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Nchini, Wang Ke, Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 10, 2020.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Nchini, Wang Ke, Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 10, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………………………………………..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Wang Ke na ameishukuru Serikali ya nchi hiyo kwa misaada ambayo imetoa katika kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaotokana na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

“Tunaishukuru Serikali ya China kwa misaada ambayo imetupatia hadi sasa vikiwemo dawa na vifaa tiba. Na leo umesema kwamba kuna asasi za kiraia na wafanyabiashara bado wanakusanya vifaa vingine ili viletwe hapa nchini vitusadie kuzuia maambukizi, tunawashukuru sana.”

Waziri Mkuu ametoa shukrani hizo leo (Ijumaa, Aprili 10, 2020) ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma alipokutana na Balozi huyo. “Mchango wenu ni muhimu sana kwetu, kwa sababu tunaanza kupata uzoefu wa namna ya kupambana na ugonjwa huu,” amesema.

Amesema Tanzania Bara na Zanzibar zinapata wagonjwa kwa sababu ni vituo vya biashara lakini wageni wote wanaoingia nchini kwa sasa wanawekwa sehemu maalumu ambako wanapatiwa huduma zote wakiwa hukohuko.

“Tunashukuru Watanzania wa pande zote mbili wanaendelea kupokea maelekezo wanayopewa, wanaendelea kujikinga na kuchukua tahadhari za kutozunguka ovyo ili wasisambaze maambukizi,” amesema.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa China kwa niaba ya Serikali ya nchi hiyo kwa jinsi ambavyo waliwahudumia wanafunzi wa Kitanzania zaidi ya 500 wanaosoma China katika kipindi chote cha kupambana na ugonjwa huo.

“Balozi Mbelwa Kairuki amekuwa akitupa taarifa za mara kwa mara kuhusiana na jinsi mlivyowasaidia wanafunzi wetu walioko huko na kuhakikisha wanakuwa salama tangu maambukizi yasambae nchini China.”

“Leo hii Tanzania tumeanza kupitia tatizo lile lile ambalo liliwapata ninyi. Tuna wagonjwa wachache lakini tuna kundi kubwa la wale waliokutana na wagonjwa na bado tunaendelea kuwafuatilia na kuwapima kila siku.”

“Tunaendelea na jitihada za kuzuia maambukizi mapya, tunatoa elimu kwa wananchi wetu na kuwaelimisha kuhusu kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono. Tunaendelea kufanya tathmini kila siku ya watu wanaopimwa. Tumezuia mikutano na mikusanyiko yote, tumefunga shule na vyuo, tumezuia michezo ili tusisambaze maambukizi.”

Waziri Mkuu amemweleza Balozi huyo kwamba kwa sasa Tanzania imefunga mipaka yake kwa sababu hata nchi jirani zimefunga mipaka yao na endapo kuna wageni wanaingia nchini, ni lazima waende kwenye isolation centres ambako wanalazimika kukaa kwa siku 14.

Kwa upande wake, Balozi Wang Ke alimfikishia salamu za shukrani Mheshimiwa Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu wa China, Mhe. Li Keqiang. “Waziri Mkuu wetu anashukuru kwa barua ya pole uliyomtumia wakati nchi yetu inapitia janga kubwa la ugonjwa wa virusi vya corona,” alisema.

Alimweleza Waziri Mkuu Majaliwa kwamba nchi yake sasa hivi haina maambukizi na kwamba hivi sasa wamelenga kuzuia maambukizi mapya kutoka nje ya nchi yasiingie nchini mwao.

“Kwenye baadhi ya miji tumefungua viwanda na vimeshaanza uzalishaji wa bidhaa ili kufufua uchumi wetu. Mwaka huu ni muhimu sana kwetu kwa sababu nchi yetu ilijipangia kuwa uwe ni mwaka wa kuhakikisha kuwa hakuna kabisa umaskini (zero poverty). Kwa hiyo, tunapambana kurejesha shughuli za kiuchumi zilizoathirika kutokana na ugonjwa huu,” alisema.

Balozi Wang Ke alisema nchi yake imechagua baadhi ya nchi za Afrika ambazo inazisaidia kwa kubadilishana nazo uzoefu kupitia mikutano kwa njia ya video (video conferencing) ili ziweze kukabiliana na ugonjwa huo.

“Zaidi ya hayo, kuna misaada ya vifaa tiba kwa ajili ya Serikali ya Zanzibar na Tanzania Bara ambayo inakusanywa na asasi za kiraia na wafanyabiashara. Hii iko njiani, na ile ya Tanzania Bara itawasili wiki ijayo.”

ZUNGU AMEWATAKA WATAALAMU KUFANYA TATHMINI YA MAZINGIRA KUJUA MADHARA YATOKANAYO NA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa maelekezo alipotembelea eneo la bahari kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu (mwenye kofia) akiwa ameambatana na wataalamu wa mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akiwa katika ufukwe alipofika kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa. 
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka akimpa maelekezo Afisa Sheria na Utawala kutoka hoteli ya Wellworth, Saimon Nguka kuhusu kufanya Tathmni ya Athari za Mazingira (EIA) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu katika eneo hilo jijini Dar es Salaam alipofika kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka apofika eneo la ufukwe wa bahari jijini Dar es Salaam wakati alipofika kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa.  
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amewataka wataalamu wa mazingira kufanya tathmini ya mazingira katika maeneo ya bahari kupata dawa ya madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Zungu alitoa kauli hiyo alipofanya ziara katika eneo la bahari lenye mgogoro kati ya Motison wanaomiliki hoteli ya Whitesand wakituhumiwa na wamiliki wa hoteli ya Wellworth Kunduchi kwa kujenga ukuta baharini hatua iliyosababisha maji kujaa hotelini kwao.
Akizungumza katika eneo hilo akiwa ameambatana na watendaji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) waziri huyo aliwataka kuwa wavumilivu kusubiriwa wataalamu wa sayansi ya bahari wafanyie kazi na kutoa majibu wiki ijayo.
Hata hivyo Waziri Zungu aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwani ndio sababu kubwa ya maji ya bahari kujaa isivyo kawaida na kuingia katika maeneo yao.
“Leo tunatazama mgogoro wa watu wawili kesho tutakuwa na wa watu watano au sita, tupeni muda nimekuja hapa na mkurugenzi wa NEMC na wataalamu wake kutazama na dawa ya changamoto tunayo kwa hiyo wiki ijayo tutawaita na tutawaambia tulichofanya kuhakikusha kila mtu ana amani ndiyo kazi ya Serikali,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka aliwataka wawekezaji wote kufanya tathmni ya athari za mazingira (EIA) ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima,
Alisema kuwa binadamu tunaishi kwa kutegemeana kwenye mazingira na ndiyo maana NEMC haitoi cheti hadi ifanyike tathmnini hiyo kubaini madshara yanayoweza kutokea kwa wananchi kupitia uwekezaji unaofanyika.
“Natoa rai kwa wawekezaji wote wawe wa viwanda ama htoeli katika fukwe zetu kufanya tathmni na kupitia tathmini hiyo tutapata maoni kutoka kwa watu wanaokuzunguka kujua je uwekezaji wako unawaathiri vipi na kama kuna athari ndogo tunajua namna ya kuzitatua ili kuepusha migioogoro,” alisisitiza.
Akitoa maoni yake kuhusu changamoto hizo Mtaalamu wa Sayansi ya Bahari Rose Mtui alisema kuwa suluhisho ni kuotesha mikoko ambayo inalunda fukwe zikibomoke kutokana na mmomonyoko wa udongo.
Aliongeza kuwa uchimbaji mchanga holela katika kingo za miti na uvuvi haramu unachangaia changamoto za kimazingira katika fukwe za bahari kwani unaharibu matumbawe ambayo yakiharibika mawimbi ya bahari higonga moja kwa moja na kwa kasi fukwe na hivyo maji kujaa kupita kiasi. 

MAFUNDI BINAFSI WA UJENZI WAIPONGEZA SERIKALI KUWAPATIA FURSA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE

MAFUNDI binafsi wa ujenzi katika Kitongoji cha Mbukwa Kijiji cha Lugoba, Kata ya Lugoba na Kijiji cha Mbwewe Kata ya Mbwewe Chalinze ,Bagamoyo Pwani, wamesema serikali imewapatia fursa ya ujenzi wa miradi mbalimbali,hali inayowasaidia kujiongezea kipato.

Wakizungumza katika Kitongoji cha Mbukwa na Changarika wilayani hapo, mafundi Rajabu Mdoe na Haruni Mohamed walisema ,hatua hiyo imewapatia pia nafasi ya kuonyesha uwezo na ujuzi wao katika kujenga vyoo na vyumba vya madarasa.

"Serikali ya awamu ya tano inatekeleza mengi na kutetea wananchi wanyonge ,na kwa hili sisi kupewa nafasi kuinua maisha yetu inatusaidia na familia zetu,"

Mdoe anayejenga matundu ya vyoo shule ya Sekondari Changarikwa alieleza kuwa, licha ya hayo, mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha kuchelewesha kufika vifaa vinavyotumika kwa ujenzi, lakini wanatarajia kukamilisha kwa wakati.

Nae Haruni alieleza,anajenga vyumba viwili vya madarasa katika shule mpya ya Mbukwa, na kwamba mbali ya vyumba hivyo tayari ameshakabidhi chumba kimoja alichokikamisha miezi michache iliyopita.
 

RC Wangabo Awataka Wananchi Kulinda Mipaka Huku 49 Wakiwekwa Karantini Mkoani Rukwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo akizungumza na viongozi mbalimbali wa vijiji na vitongoji (hawapo pichani) vinavyopaka na mwambao wa ziwa Tanganyika katika kata za Korongwe na Kabwe Wilayani Nkasi
Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo akizungumza na viongozi mbalimbali wa vijiji na vitongoji vinavyopaka na mwambao wa ziwa Tanganyika katika kata za Korongwe na Kabwe Wilayani Nkasi.

Afisa Afya wa Mkoa wa Rukwa Kennedy Kyauke akitoa elimu ya hatua za kunawa mikono kwa viongozi mbalimbali wa vitongoji, vijiji na kata (hawapo pichani) wakati wa Kikao kifupi baina ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa na viongozi hao. 
Kamanda wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi Elizeus Mushongi akitoa elimu viongozi mbalimbali wa vitongoji, vijiji na Kata wakati wa kikao kifupi baina Mkuu wa mkoa wa Rukwa na viongozi hao. 

Viongozi mbalimbali wa vijiji na vitongoji vinavyopaka na mwambao wa ziwa Tanganyika katika kata za Korongwe na Kabwe Wilayani Nkasi, wakisikiliza kwa makini elimu na maelekezo wanayopewa ili kuilinda mipaka ya nchi na kujilinda dhidi ya ugonjwa wa Corona. 
……………………………………………………………………………………….
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka viongozi wa vitongoji, vijiji pamoja na watendaji wao wa kata za Korongwe na Kabwe kuhakikisha wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao kuwa mstari wa mbele katika kuilinda nchi kutokana na ugonjwa wa Corona kwa kuzuia uingiaji holela wa wageni wanaoweza kuuleta ugonjwa huo kutoka nchi za jirani.
Mh Wangabo amesema kuwa hadi sasa mkoa wa Rukwa umewaweka Karantini watu 49 ambapo kati ya hao watanzania 36 na wageni 13 ambao walipita katika bandari na mipaka rasmi ya mkoa huo na kusisitiza kuwa katika utekelezaji wa kuwaweka watu Karantini hauangalii uraia wa mtu wala hadhi yake, na kuongeza kuwa inachokijali serikali ni usalama wa wananchi wake dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona.
Hivyo amewataka viongozi hao kuwaelimisha wananchi kuwakataa wageni wasiotumia mipaka na bandari rasmi kuingia katika nchi kwani kutofanya hivyo kutailetea nchi maafa makubwa na hivyo na hivyo kuwataka viongozi na wananchi kuacha matumizi ya bandari bubu zilizopo katika vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika.
“Waende wakapite katika maeneo ambayo ni rasmi, waje hapa kwenye bandari ya Kabwe, wapite hapo na taratibu nyingine za kiafya zitafanyika, lakini sio kwenye bandari bubu huku, bandari bubu ni marufuku kutumika, ndani ya wilaya hii ya Nkasi kuna bandari bubu 46, Nkasi peke yake na katika kata zenu mbili hizi, ya Korongwe na Kabwe kuna bandari bubu 13, ndio maana nikasema viongozi ninyi wa kata mbili hizi mje hapa, ili muone umuhimu wa kuzuia watu kiholela holeal kuja kwenye bandari hizi bubu,” Alisisitiza.
Mh. Wangabo ameyasema hayo wakati wa kikao na wenyeviti wa vitongoji na vijiji vyenye bandari bubu pamoja na watendaji wa kata Kabwe na Korongwe zinazobeba vijiji hivyo katika kikao kilicholenga kutoa elimu ya ugonjwa wa Corona kwa viongozi hao pamoja na kutoa maelekezo ya serikali dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi Elizeus Mushongi alitahadharisha matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi hao ambao huwapokea wageni hao na kuwaruhusu kuingia katika nchi bila ya kufuata utaratibu wa serikali na kuongeza kuwa matumizi ya bandari bubu ni haram una hivyo atakayekamatwa anahalalisha matumizi ya bandari hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
“Wageni kutoka nje ya nchi, iwe Kongo, iwe Burundi, iwe Zambia, mnawapokea kule na nyinyi ndio mnakuwa maafisa uhamiaji, mnakuwa maafisa forodha, kila kitu mnamaliza wenyewe kule, sasa kama mtampokea mtu anaumwa ule ugonjwa, ninyi ndio mtakaoanza kuupokea ule ugonjwa kabla ya wote na bila ya kujua mtaenda kuambukiza familia na familia kama dokta alivyosema, niwaombe sana msipokee watu kutoka nje ya nchi kama hawajapita katika vituo vilivyoainishwa kisheria,” Alisema.
Aidha wakati akitoa salamu zake kwa mkuu wa mkoa, Diwani wa Viti Maalum Mh. Christina Simbakavu alisema kuwa kuna baadhi ya watu wenye ndugu zao nchi ya jirani ya Kongo huwa na kawaida ya kuingia katika vijiji hivyo nyakati za usiku na ndugu zao huwapokea katika utaratibu ambao unaweza kuhatarisha maisha yao.
“Kuna boti zinazoingia usiku kama alivyotamka mjumbe wa Kijiji cha Kalila, zile boti zinaingia lakini wenyeji wenye ndugu zao kutoka nchi jirani ya kongo wanawapokea katika mazingira ambayo sio Rafiki sana na hawatoi taarifa, na hili nalo linafukuta lakini hatujapata uhakika uliowazi, tunajaribu kuongea na wananchi kuwa tusipokee wageni wa aina yoyote na nawaomba viongozi wangu tuhamasishe utumiaji wa maji na sabuni kunawa na katika nyumba zetu tuweke vifaa hivyo,” alisema.
Naye Diwani wa Kata ya Korongwe Mh. Venus Bamilitwaye wakati akitoa neno la shukurani ka mkuu wa mkoa wa rukwa aliwasisitiza viongozi wa kata hizo kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika kulinda bandari bubu pamoja na kuzuia uingiaji wa kiholela wa wageni jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wananchi wa mkoa wa Rukwa na Tanzania. 

WATENDAJI SEKTA YA ARDHI OFISI ZA MIKOA WATAKIWA KUEPUKA URASIMU

$
0
0



Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa watendaji wa sekta ya Ardhi wa ofisi za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma jana.





Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Nhonge akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Watendaji wa sekta ya ardhi wa ofisi za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma jana.



Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Watendaji wa sekta ya ardhi wa ofisi za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma jana.



Watendaji wa sekta ya Ardhi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo (Hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo kwa Watendaji wa sekta ya ardhi wa ofisi za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma jana (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA).

……………………………………………………………………………………………………..

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka watendaji wa sekta ya ardhi katika ofisi za mikoa kuepuka urasimu na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ili kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi.

Alisema, pamoja na kutenda kazi kwa kuzingatia sheria, watendaji hao pia wanapaswa kuhakikisha wanashughulikia kero za wananchi kwa kukaa nao pamoja hasa pale wananchi wanapokosea kwa lengo la kuwasaidia badala ya kuwakatisha tamaa.

‘’Urasimu uishe, lengo hapa ni kumhudumia mwananchi na cha msingi ni kukaa pamoja na mteja na kumueleza alipokesea badala ya kumkatisha tamaa kwa kumzungusha, tuwaonee huruma na kuacha urasimu usio wa lazima’’. Alisema Mary.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Maofisa wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Morogoro, Manyara, Singida na Dodoma katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma jana, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu na kutenda kazi kwa kasi na kusisitiza kuwa kazi katika maeneo wanayotoka ni nyingi na zinahitaji kushughulikiwa.

Kwa mujibu wa Mary Makondo, watendaji hao ambao ni Makamishna na Wasajili Wasaidizi wa ofisi za ardhi za mikoa wahakikishe wanatoa kipaumbele katika kushughulikia migogoro ya ardhi kwa haraka pamoja na kutilia mkazo mafunzo ya ndani kwa watumishi.

Aidha, alihimiza utoaji huduma nzuri kwa wateja wanaokwenda kupata huduma katika ofisi za mikoa na kubainisha kuwa suala hilo linahitaji uvumilivu mkubwa na wakati mwingine kushirikisha wataalamu wengine wa ofisi moja ili kuja na uamuzi utakaohusisha mawazo ya wengi.

Akigeukia utoaji hati za ardhi, Mary Makondo aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanaongeza idadi ya utoaji hati miliki za ardhi kwenye maeneo yao zikiwemo hati za kimila, urasimishaji na leseni za makazi sambamba na kuhakikisha fidia zinalipwa kwa wakati hususan maeneo yaliyotwaliwa kwa shughuli mbalimbali.

Vile vile, katibu Mkuu Wizara ya Ardhi aliwataka watendaji hao wa sekta ya ardhi kuhakikisha wanapata taarifa zote za makampuni ya urasimishaji na mikataba yao na wakati huo makampuni hayo kufuata miongozo ikiwemo bei elekezi ya urasimishaji.

Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha alieleza kuwa mafunzo hayo ya watendaji wa sekta ya ardhi kutoka ofisi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yatawawezesha watendaji wa ardhi wa mikoa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na aina ya mafunzo waliyoyapata ikiwemo namna ya kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi ya ardhi.

Alisema, watendaji hao walipatiwa mafunzo katika masuala ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, upimaji na ramani, mipango miji sambamba na masuala ya maendeleo ya makazi aliyoyaeleza kuwa watakuwa wakikutana nayo katika utendahji wa kazi za kila siku.

SERIKALI KUUPATIA MUAROBAINI MGOGORO WA ENEO LA ITUHA MBEYA-WAZIRI HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila wakikagua ramani ya eneo la Ilomba lenye mgogoro kati ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI Uyole na wananchi kabla ya kufanya ziara kugagua maeneo hayo wakiambatana na wananchi jana Tarehe 9 Aprili 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila wakiambatana na wananchi wakikagua eneo la Ilomba lenye mgogoro kati ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI Uyole na wananchi jana Tarehe 9 Aprili 2020. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI Uyole Dkt Tulole Bucheyeki akimuonyesha Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila mipaka ya eneo la Taasisi hiyo na wananchi  wa eneo la Ilomba wakati wa ukaguzi wa mashamba hayo jana Tarehe 9 Aprili 2020. 
Sehemu ya wakazi wa eneo la Ilomba wakifatilia ziara ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ukaguzi wa mipaka ya eneo lenye mgogoro kati yao na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI Uyole jana Tarehe 9 Aprili 2020. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila wakisikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu mgogoro wa eneo la Ilomba Mkoani Mbeya jana Tarehe 9 Aprili 2020. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mbeya

Serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kuumaliza mgogoro wa eneo lililo ndani ya Taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI UYOLE) lililopo kata ya Ilomba mkoani Mbeya.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) jana Tarehe 9 Aprili 2020 ametangaza hatua za serikali katika kutatua mgogoro huo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Mbeya akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Albert Chalamila na kulikagua eneo hilo na kuzungumza na wananchi husika.

Waziri Hasunga ameiagiza Taasisi ya TARI Uyole kutoendelea na shughuli za utafiti mpaka hapo kesi ya mgogoro huo iliyopo mahakamani itakapotolewa uamuzi.

Kwa upande wa wananchi, Waziri Hasunga amewataka kusitisha shughuli zote za kilimo ili kusubiri maamuzi ya mahakama. Kuhusu mazao ambayo yalishalimwa na wananchi hao amesema kuwa wataruhusiwa kuvuna lakini hawataruhusiwa kuendelea na kilimo.

Wananchi hao wapatao 200 kwa mujibu wa orodha waliyoiandika na kusaini kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko yao kwa katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Januari 1, 2020 wanailalamikia serikali kwa kutowalipa fidia kwa wakati hivyo kuiomba kuwalipa fidia ama kuwarudishia eneo hilo.

Eneo hilo lenye ukubwa wa Hekta 8.52 limekuwa likitumiwa na wananchi hao kwa ajili ya shughuli za kilimo pamoja na ufugaji.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amewasihi wananchi hao kadhalika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Uyole kuitikia maelekezo ya Waziri wa Kilimo kwani serikali itafanya maamuzi ya busara na kila mtu atapata haki yake inayostahili.

Na endapo mahakama itabaini kuwa wanastahili kurudishwa eneo hilo watapatiwa kwa mujibu wa sheria na kama itabaini hawana haki kadhalika itafanya maamuzi.

JESHI LA POLISI SHINYANGA LAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI WA HABARI KUTOKOMEZA VITENDO VYA UHALIFU

$
0
0


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.

Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama. Kulia ni Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus Sulle , Kushoto ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi.


Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi akizungumza katika kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.

Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus Sulle akizungumza katika kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga limeahidi kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari kuhakikisha vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji,ajali za barabarani na ukatili wa kijinsia hususani mimba na ndoa za utotoni vinatokomezwa mkoani humo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Aprili 10,2020 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga.

Kamanda Magiligimba amesema suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mtu katika jamii huku akibainisha kuwa Waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa zaidi kuielimisha jamii kuachana na vitendo viovu ndiyo maana Jeshi la polisi limekuwa likishirikiana bega kwa bega na waandishi wa habari kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.

“Naomba waandishi wa habari tuendelee kushirikiana katika kuufanya mkoa wetu unakuwa mahali salama pa kuishi kwa kuhakikisha tunapunguza ajali za usalama barabarani,mauaji kuepuka vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto”,amesema Kamanda Magiligimba.

Katika hatua nyingine ameitaka jamii kuachana na tabia ya kupeleka watoto wa kike/wasichana wadogo kwa waganga wa kienyeji kwenda kuoshwa dawa za mvuto/nyota maarufu ‘Samba’ ili wapendwe na wanaume kwani inachangia kuwepo kwa matukio ya mimba na ndoa za utotoni.

"Mkoa wa Shinyanga ulikuwa unakabiliwa na matatizo ya mauaji ya wazee na watu wenye ualbino lakini sasa yamepungua kwa asilimia kubwa na kubaki tatizo la mimba na ndoa za utotoni ambalo linasababishwa na mila na desturi za kuogesha watoto wao wa kike dawa za mvuto wa mapenzi hasa katika wilaya ya Kishapu",amesema Magiligimba.


Amewaomba waandishi wa habari kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kuandika habari ambazo zitatoa elimu kwa wazazi na walezi kuachana na mila potofu za kuogesha watoto wao wa kike dawa za mvuto wa mapenzi ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.

Kamanda Magiligimba ametumia fursa hiyo kuwasihi wakazi wa Shinyanga kuzingatia maagizo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu Ugonjwa wa Corona ikiwemo kuepuka, Mikusanyiko isiyo ya lazima, kuepuka kukumbatiana , kunawa mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara na kutumia Vitaka Mikono 'Sanitizer'.

Kwa upande wake,Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi amewashukuru wadau mbalimbali wa masuala ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na jeshi la polisi kupunguza matukio ya mauaji ambapo katika Kipindi mwezi Januari hadi Machi 2020 kuna matukio 6 yametokea ukilinganisha na matukio 23 yaliyotokea Mwezi Septemba hadi Desemba 2019.

Naye Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus Sulle amesema katika Kipindi hiki ambapo kuna Ugonjwa wa Corona Jeshi la polisi limeendelea kutoa elimu kwa waendeshaji wa vyombo kuhakikisha hawajazi abiria kupita kiasi ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa Corona.

“Tunaendelea kukabiliana na ujazaji abiria kwenye magari yanayoingia mjini na yanayokwenda vijijini ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Kwa upande wa magari madogo mfano Hiace tunaondoa viti vya nyuma ya dereva ili abiria wasiangaliane”,ameeleza Sulle.

Hata hivyo amesema jeshi la polisi halitasita kuwachukulia hatua za kisheria madereva bodaboda wanaoendesha kwa mwendo kasi Mjini Shinyanga huku akibainisha kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa waendesha bodaboda kupitia kwenye vituo vyao kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuhakikisha wananawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kutumia Sanitizer.


“Barabara kuwa salama ni lazima,nami nitahakikisha nasimamia Sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuhakikisha tunapunguza ajali za barabarani ambazo zinasababisha vifo,ulemavu na uharibifu wa mali”,ameongeza Sulle.



Ahukumiwa maisha jela kwa kosa la kubaka na kulawiti

$
0
0


Na Amiri kilagalila,Njombe

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe imemuhukumu Hezron Ndone ( 44) mkazi wa joshoni kata ya mji mwema mjini Njombe kwenda jela kifungo cha maisha kwa kosa kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kumzaa ambaye ni mwanafunzi darasa la tano mwenye umri wa miaka 10.

Akisoma hukumu ya kesi namba 14 ya mwaka 2020 hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa Njombe Hassan Mkakube alisema mtuhumiwaalishtakiwa kwa makosa manne mawili ya kuzini na maalimu kinyume na kifungu cha sheria namba 158 kifungu kidogo cha kwanza na makosa mawili ya kulawiti kinyume na kifungu namba 54 kifungu kidogo cha pili na cha kwanza vikisomwa pamoja na kifungu namba 185 cha sheria ya mtoto.

Hakimu Makube alisema kupitia mashahidi watatu kati ya sita wa upande wa mashtaka akiwemo shahidi namba moja ambaye ni mke wa mshtakiwa , shahidi namba mbili ambaye ni mtoto aliye athirika pamoja na shahidi namba tatu ambaye ni daktari aliyefanya vipimo vya mtoto mahakama imejiridhisha kuwa mshtakiwa kwa nyakati tofauti alizini na kumwingilia kinyume na maumbile mtoto wake mwenye umri wa miaka 10.

Hakimu Hassan Makube alisema shahidi namba moja ambaye ni mke wa mshtakiwa Valentina Mkorongo aliieleza mahakama kuwa awali alikuwa na mgogoro na mume wake na ikatokea akawa analala jikoni na mtoto wake mdogo huku watoto wake wengine wanne wakilala chumbani na baba yao akiwemo binti yake wa kike.

Shahidi namba mbili ambaye ndiye muathirika aliieleza mahakama kuwa akiwa na wadogo zake watatu baba yake alikuwa anawalaza wadogo zake kitandani na yeye alikuwa akilala na baba yake kwenye godolo lililokuwa likitandikwa chini na hapo ndipo baba yake alipokuwa akimvua nguo na kumwingilia kwa zaidi ya mara saba.

Makube alisema shahidi namba sita ambaye ni mdodgo wake na muathirika aliieleza mahakama kuwa yeye alikua akilala na wadogo zake kitandani lakini dada yao mkubwa alikua akilala chini na baba yao.

Hakimu Hassan Makube alisema mahakama ilisikiliza ushahidi wa daktari aliyemfanyia uchunguzi muathirika na kuthibitisha kuwa mtoto hakuwa na bikira na sehemu yake ya nyuma ilikuwa imeingiliwa na baadaye akajaza fomu namba tatu kwa ajili ya hatua nyingine.

Mshtakiwa ambaye alikuwa akitetewa na wakili Emmanuel Chengula alipewa nafasi ya kujitetea ambapo alikataa kutenda kosa na kuieleza mahakama kuwa huenda waliomwingilia binti yake ni vijana ambao amewahi kuwahisi kuwa na uhusiano na binti yake.

Hata hivyo wakili wa serikali Andrew Mandwa akiwa naye Happines Makungu,Nura Minja waliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wanaothubutu kufanya vitendo vya namna hiyo.

Baada ya mahakama kuridhika na maelezo ya mashahidi imemkuta mtuhumiwa na makosa na kumhukumu miaka 30 kwenda jela kwa kosa la kuzini na binti yake na kifungo cha maisha kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile pamoja na kutoa fidia ya shilingi milioni 10 ikiwa ni fidia kwa muathirika.
 

TAKUKURU YAOKOA MILIONI 7 ZILIZODHULUMIWA

$
0
0
Na Woinde Shizza,SIHA

Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni saba laki tano na elfu tisini na mbili (7,592,000/= )kwa watumishi wa idara ya afya halmashauri ya siha,walinzi wa shamba la miti West Kilimanjaro na shule ya sekondari Magnifikacant na mama lishe Fatuma Athumani,zilizokuwa zimedhulumiwa na kufanyiwa ubadhirifu na watuhumiwa ambao ni mhasibu wa halmashauri na mlinzi mkuu wa shamba.

Zoezi la kukabidhi fedha hizo limefanyika mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Onesmo Buswelo, akiwemo pia mtuhumiwa aliekuwa meneja wa shamba la miti West Kilimanjaro Christopha Ngonyani,watumishi waliodhulumiwa fedha zao na wahusika wote waliofujiwa fedha zao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo kamanda wa Takukuru wilaya ya Siha Deo Mtui alisema baada ya kuletewa malalamiko hayo taasisi hiyo ilianza uchunguzi ambapo baada ya kuwahoji watuhumiwa wote walikiri kufanya makosa hayo hivyo kuamuriwa kurudisha fedha hizo.

Mkuu wa wilaya ya Siha Onesmo buswelo licha ya kuipongeza TAKUKURU kwa kazi hiyo ameonekana kukerwa na kitendo hicho na kuamuru mtuhumiwa Christopha nyonyani na Namson Fisso licha ya kurudisha fedha hizo kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo.

"Pamoja nakurudisha fedhahizo lakini watumiwa Hawa wachukuliwe hatua hatua za kinithamu ili iwefundisho kwa wengine wasijaribu kufanya vitendo Kama hivi" alibainisha buswelo

Baadhi ya wananchi na watumishi ambao walidhulumiwa fedha zao kwa hila na udangayifu wameishuruku TAKUKURU kwa kufanikisha zoezi hilo huku wakiwashauri wananchi wengine kutoogopa kuitumia taasisi hiyo

Watu waliodhulumiwa fedha zao ni watumishi 126 wa idara ya afya,walinzi 8 wa shamba la miti West Kilimanjaro,shule ya sekondari Magnificant na mama lishe Embassy Tea room zote za wilayani Siha zilizokuwa zimefanyiwa ubadhirifu na watuhumiwa Namson Fisso aliyekuwa mhasibu halmashauri ya siha na Mlinzi mkuu wa shamba la misitu la West Kilimanjaro Christopha Ngonyani.

 Mkuu wa wilaya ya Siha Onesmo Buswelo anamkabidhi Meneja wa shamba la miti la West kilimanjaro fedha za walinzi waliodhulumiwa kwa hila na udanganyifu kiasi cha shs 499000/= na mlinzi mkuu christopha Ngonyan
 Kamanda wa Takukuru wilaya ya Siha Deo Mtui akionyesha fedha walizofanikiwa kurejesha  kiasi cha shilingi milioni saba laki tano na elfu tisini na mbili (7,592,000/= )kwa watumishi wa idara ya afya halmashauri ya siha,walinzi wa shamba la miti West Kilimanjaro na shule ya sekondari Magnifikacant na mama lishe Fatuma Athumani,zilizokuwa zimedhulumiwa na kufanyiwa ubadhirifu na watuhumiwa ambao ni mhasibu wa halmashauri na mlinzi mkuu wa shamba.(picha na Woinde Shizza,SIHA)
 

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA IJUMAA KUU KANISA LA MTAKATIFU YOHANA- MARIA MZEYI PAROKIA YA MLIMANI CHATO MKOANI GEITA.

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita leo tarehe 10/04/2020.
Padre Innocent Sanga akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita leo tarehe 10/04/2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita leo tarehe 10/04/2020 katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Padre Innocent Sanga watatu kutoka kushoto mara baada ya Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chatomkoani Geita leo tarehe 10/04/2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka Kanisani katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita leo tarehe 10/04/2020. PICHA NA IKULU

Viewing all 118669 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>